Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 3 Opener Exams 2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO

 • Jibu maswali yote.
 • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
 1. INSHA
  Wewe ni mwenyekiti wa kamati ya usalama wilayani mwenu.Andaa hotuba utakayoitoa katika kikao kinachoshughulikia usalama huku ukizingatia chanzo cha tatizo hili na hatua zinazofaa kuchukuliwa kulitatua.
 2. UFAHAMU ( alama 15)

  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yafuatayo

  Wiki iliyopita nilikuwa napanga foleni kuingia kwenye benki nilipopigwa na butwaa.Kilichonistaajabisha ni kuwa dada mmoja alikuwa aking’ang’ania kujibanza mbele pasipo kupanga foleni,bila kuwajali wateja waliokuwa mbele yake.Jambo hilo lilinikera kwani mwanamke hakuwa na wakati wa kuomba radhi kwa waliokuwa mbele yake.

  Baada ya kutafakari kwa muda niliamua sitakereka wala kumlaumu kwani ni tabia iliyokita mizizi miongoni mwa wanawake humu nchini.Ni mara ngapi umewaona wanawake wakichukulia wanaume wana muda wote wa kupoteza na kuwakaripia kuwa hawawapi nafasi kwa mujibu wa msemo “ladies first”?Ni wangapi ambao huwanunia na kuwatukana wanaume kwa kuwa hawakutambuliwa wala kuwapa nafasi ya kwanza licha ya kuwa haikuwa haki yao?Ni wangapi huwaaibisha waume wao kwa kukosekana kwa hiki na kile nyumbani licha kuwa wenyewe wana uwezo wa kifedha?
  Katika mahusiano wanaume wanapaswa kutambua ishara kama hizi mapema ambazo zitakutahadharisha kuingia katika uhusiano na dada ambaye katika siku zijazo hatakuthamini;ambaye kila kizuri kitakuwa chake.Bila shaka wanaume wengi watakubaliana nami kuwa sio rahisi kubaini tabia hizi miongoni mwa akina dada,kabla ya uhusiano kunoga.Halikadahlika,iwapo katika siku za kwanza za uhusiano utagundua kuwa dada ana mazoea ya kununa kwa sababu umeshindwa kutekeleza jambo fulani na kutupa matusi makali bila kuogopa,funganya virago kwani hii ni ishara atakukosea heshima siku za usoni.

  Wanaume wengi hawaelewi kuwa uhusiano wa kudumu ni uwili ,kila mmoja akijitahidi kumfurahisha mwenzake .Wanajitwika jukumu la kuleta raha katika uhusiano kwa jua kwa mvua.Wamejitwika madeni ya ufukara pasi kukidhi kiu cha mwenziwe kikuacho kila uchao.Mwaunaume aingiapo matatani hutupiliwa mbali kwa madharau..Haya yananikumbusha bwana mmoja aliyeoa na kuishi na mkewe mjini .Alimtumikia kwa kila njia alipokuwa mwenye mshahara mnono.Alipofutwa kazi na mali kufifia kwa mahitaji yasiyoisha ya mkewe,mkewe alimwaibisha kwa kumfuata kila mwanaume aliyekuwa nacho na hatimaye kumtoroka kwa madai mwanamke ni kama gari.

  Wanaume watakubaliana nami kuwa ni wengi wanaoishi maisha ya kunyanyaswa na wake wao bila kulalamika. Kimefika kiwango cha kupigwa,kuuawa,kutusiwa na kutishwa kupitia makundi haramu.Wengine wameendewa kwa wachawi kulainishwa wakaishia kupoteza akili zao razini.

  Licha ya kishidikizo wanaume kunyenyekea na kufuatia haki za wanawake wanastahili.

  Maswali
  1. Eleza kilichomkera mwandishi na kwa nini? Al 2
  2. Kutokana na taarifa hii ni ishara gani zinaashiria kuwa tabia kama hizi zimekita mizizi miongoni mwa wanawake. Al 3
  3. Eleza sababu mbili zinazofaa kumfanya mwanaume kuvunja uhusiano mapema kulingana na mwandishi. Al 2
  4. Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumika katika taarifa hii. Al 3
   1. Kwa jua kwa mvua
   2. Mwanamke ni kama gari
   3. Akili zao razini
  5. Wanaume wanakumbana na changamoto gani katika ndoa? Al 3
  6. Andika neno lingine lenye maana sawa na yafuatayo kulingana na taarifa. Al 2
   1. Kunoga
   2. Pasi
 3. MATUMIZI YA LUGHA
  1. Bainisha maneno katika senensi zifutazo
   1. Mama anapika ugali al 3
   2. Alifika kabla ya wote
  2. Bainisha viambishi vya neno lifuatalo. Al 2
   Ilinyesha
  3. Sahihisha sentensi hizi al 2
   1. Nilimpea mkebe hizi jana.
   2. Hizi ni zikombe za kukunywa chai.
  4. Unda vitenzi kutokana na nomino hizi. Al 2
   1. Mtukufu
   2. Mchumba
  5. Andika sentensi zifuatazo katika hali ya kutendwa al 2
   1. Mzee alimwadhibu mwana kwa sababu ya utundu.
   2. Huyu paka ndiye aliyeyanywa maziwa yote.
  6. Kanusha sentensi zifuatazo al 2
   1. Vidozo alikula wali jana akashiba.
   2. Wavulana walicheka juzi.
  7. Eleza maana ya vitate hivi. Al 4
   1. Tua
   2. Dua
  8. Yakinisha al 2
   Wasingalisoma kwa bidii wasingalipita mtihani huo.
  9. Bainisha aina za viwakilishi katika sentensi hizi. Al 3
   1. Yeye mwenyewe ni mwanafunzi.
   2. Ambao ulipotea umepatikana.
   3. Wangapi watafika?
  10. Fafanua sauti hizi.     al 2
   1. /p/ na
   2. /b/ 
  11. Eleza maana ya: al 2
   1. Kiimbo
   2. Shadda
  12. Andika sentensi zifuatazo kulingana na maagizo
   Kuku alitaga yai.(hali timilifu)   al 2
  13. Onyesha aina ya vitenzi katika sentensi ifuatayo
   Leon alikuwa akicheza uwanjani. Al 2
  14. Maneno yafutayo yamo katika ngeli gani? Al 2
   1. Ugwe
   2. Limau
  15. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao. Al 2
   W+V+T+E
  16. Andika katika kinyume:
   Msichana mzuri alifunga mlango. Al 1
 4. ISIMU JAMII (alama 10)
  Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata

  Mhudumu: Mnakaribishwa.Menyu hii hapa.Mtakula nini?
  Mteja 1: Naomba uniletee mix na ugali.Fanya haraka
  Mhudumu: Sawa mzee,Nafurahi kukuhudumia.
  Mteja 2: Mhudumu,hebu leta mboga na madodo na chemsha mbili.Pia uletee maji ya machungwa.
  Mhudumu: Sawa.Baada ya dakika moja utapata yote uliyoagiza.
  Mteja 1: (Akila).Wewe!please bring me drinking water.Yawe baridi tafadhali.
  Mhudumu: Ndiyo haya hapa mezani.Glasi nayo hii pia ,karibu.
  Mteja 2: Nina haraka mzee.Wapi toothpick?
  Mhudumu: Hizo hapo mezani na maji.
  Mteja 1: (Akila) Mhudumu ,naomba uniletee ugali saucer tafadhali.
  Mhudumu: Naam.
  Mteja 2: (Akisimama)Nimeshiba.Hizi pesa.Nilitee change haraka niondoke.

  Maswali
  1. Ni sajili gani inayohusishwa katika mazungumzo haya? Al 2
  2. Taja sifa zozote nane za sajili hii. Al 8
 5. FASIHI SIMULIZI
  1. Andika sifa nne za visasili. Al 4
  2.  
   1. Hadithi ni nini? Al 2
   2. Kwa nini hadithi hutambwa wakati wa jioni. Al 4
  3. Andika tofauti tano kati ya fasihi andishi na fasihi simulizi. Al 10

MARKING SCHEME

 1. INSHA
  Wewe ni mwenyekiti wa kamati ya usalama wilayani mwenu.Andaa hotuba utakayoitoa katika kikao kinachoshughulikia usalama huku ukizingatia chanzo cha tatizo hili na hatua zinazofaa kuchukuliwa kulitatua.
  Ni hotuba
  1. Mwanafunzi azingatie
   • Sura-kichwa
   • utangulizi
   • mwili/maudhui
   • tamati
  2. Maudhui
   1. Chanzo
    • Ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana
    • Mihadarati
    • Umaskini miongoni mwa jamii
    • Kutowajibika kwa asasi za usalama
    • Tofauti za kisiasa
    • Ongezeko la silaha haramu wilayani
    • Ongezeko la wakimbizi
    • Kudorora kwa maadili katika jamii
   2. Suluhisho
    • Serikali kubuni nafasi za kazi kwa vijana
    • Kuhamasisha wanaohusika na mihadarati kuhusu madhara yake
    • Hatua kali kuchukuliwa kwa walanguzi wa mihadarati
    • Makundi yasiyo ya kiserikali kuhusishwa kwa mfano,NACADA
    • Kuongezwa kwa maafisa wa usalama wanaoajibika.
    • Wakimbizi kutoka nchi jirani kukaguliwa kuhakikisha hawana silaha
    • Mwalimu ahakiki joja za wanafunzi.
    • Mwanafunzi akiegemea upande mmoja akadiriwe nusu.
 2. UFAHAMU
  1.  
   1. Mwanamke kung’ang’ania kujibanza mbele bila kupiga foleni
   2. Kwa sababu dada huyo hakuwa na wakati/heshima wa kuomba radhi waliokuwa mbele . 2x1=2mks
  2.  
   1. Wanawake kuchukulia wanaume wana muda wote wa kupoteza na kuwakaripia kuwa hawawapi nafasi ingawa si haki yao.
   2. Wanawake kununia na kuwatukana wanaume kwa kutowapa nafasi ya kwanza
   3. Wanawake kuwaaibisha waume wao kwa kukosa hiki na kile nyumbani licha ya kuwa wenyewe wanauwezo wa kununua 3xala1
  3.  
   1. Kununa kwa sababu umeshindwa kutekeleza jambo fulani.
   2. Kutupa matusi makali bila kuogopa2xal 1
  4.  
   1. Kwa jua kwa mvua:wakati wa changamoto na wakati mambo ni shwari
   2. Mwanamke ni kama gari :lazima umtunze kwa kutimiza kila mahitaji yake ili akufaidi
   3. Akili zao razini :akili zao timamu 3x al 1
  5.  
   1. Kupigwa
   2. Kuuawa
   3. Kutisiwa
   4. Kutishwa
   5. Kuendewa kwa wachawi /kupoteza akili zao razimi (6xal½)
   6. Kuaibishwa
  6.  
   1. Kunoga:kunawiri/kustawi/kuimarika
   2. Pasi: bila 2x1
 3. MATUMIZI YA LUGHA
  1. Bainisha maneno katika senensi zifutazo
   1. Mama anapika ugali al 3
        N         T         N
   2. Alifika kabla ya wote
      T           H          W
  2. Bainisha viambishi vya neno lifuatalo. Al 2
   Ilinyesha
   • i-ngeli
   • li-wakati
   • nyesh-mzizi
   • a-kiishio
  3. Sahihisha sentensi hizi al 2
   1. Nilimpea mkebe hizi jana.
    • Nilimpa mkebe huu jana
   2. Hizi ni zikombe za kukunywa chai.
    • Hivi ni vikombe vya kunywa chai.
  4. Unda vitenzi kutokana na nomino hizi. Al 2
   1. Mtukufu-tukuza,tukuka
   2. Mchumba-chumbia
  5. Andika sentensi zifuatazo katika hali ya kutendwa al 2
   1. Mzee alimwadhibu mwana kwa sababu ya utundu.
    • Mwana aliadhibiwa na mzee kwa sababu ya utundu.
   2. Huyu paka ndiye aliyeyanywa maziwa yote.
    • Maziwa yote yalinywewa na paka huyu.
  6. Kanusha sentensi zifuatazo al 2
   1. Vidozo alikula wali jana akashiba.
    • Vidozo hakula wali jana wala hakushiba.
   2. Wavulana walicheka juzi.
    • Wavulana hawakucheka juzi
  7. Eleza maana ya vitale hivi. Al 4
   1. Tua
    • Elekea chini
   2. Dua
    • Ombi/sala
  8. Yakinisha al 2
   Wasingalisoma kwa bidii wasingalipita mtihani huo.
   • Wangalisoma kwa bidii wangalipita mtihani huo
  9. Bainisha aina za viwakilishi katika sentensi hizi. Al 3
   1. Yeye mwenyewe ni mwanafunzi
    nafsi
   2. Ambao ulipotea umepatikana
    Kirejeshi
   3. Wangapi watafika
    Idadi
  10. Fafanua sauti hizi./p/ na /b/ al 2
   1. /p/-sauti sighuna
   2. /b/-sauti ghuna
  11. Eleza maana ya: al 2
   1. Kiimbo
    • Upandaji na ushukaji wa sauti wakati wa kutamka
   2. Shadda
    • Mkazo unaowekwa kwenye silabi za neno
  12. Andika senntensi zifuatazo kulingana na maagizo
   Kuku alitaga yai.(hali timilifu) al 2
   • Kuku ametaga yai
  13. Onyesha aina ya vitenzi katika sentensi ifuatayo
   Leon alikuwa akicheza uwanjani. Al 2
   • Alikuwa-kitenzi kisaidizi
   • Akicheza –kitenzi kikuu
  14. Maneno yafutayo yamo katika ngeli gani? Al 2
   1. Ugwe-U-ZI
   2. Limau -LI-YA
  15. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao. Al 2
   W+V+T+E
   • Wale wazuri walikimbia sana.(kadiria)
  16. Kinyume:
   Msichana mzuri alifunga mlango. Al 1
   • Msichana mbaya alifungua mlango
 4. ISIMU JAMII
  Soma mazungumzo yafuatayo kasha ujibu maswali yanayofuata
  Mhudumu: Mnakaribishwa.Menyu hii hapa.Matakula nini?
  Mteja 1: Naomba uniletee mix na ugali.Fanya haraka
  Mhudumu: Sawa mzee,Nafurahi kukuhudumia.
  Mteja 2: Mhundumu,hebu leta mboga na madodo na chemsha mbili.Pia liletee maji ya machungwa.
  Mhudumu: Sawa.Baada ya dakika moja utapata yote ulioagiza.
  Mteja 1: (Akila).Wewe!please bring me drinking water.Yawe baridi tafadhali.
  Mhudumu: Ndiyo haya hapa mezani.Glasi nalo hii pia ,karibu.
  Mteja 2: Nina haraka mzee.Wapi toothpick?
  Mhudumu: Hizo hapo mezani na maji.
  Mteja 1: (Akila) Mhudumu ,naomba uniletee ugali saucer tafadhali.
  Mhudumu: Naam.
  Mteja 2: (Akisimama)Nimeshiba.Hizi pesa.Nilitee change haraka niondoke.

  Maswali
  1. Ni sajili gani inayohusishwa katika mazungumzo haya? Al 2
   • Sajili ya hotelini.
  2. Taja sifa zozote nane za sajili hii. Al 8
   • Matumizi ya msamiati maalum
   • Lugha isiyo sanifu
   • Kuchanganya ndimi
   • Kubadili msimbo
   • Lugha amrishi
   • Lugha ya kushawishi
   • Lugha ya majibizano
   • Matumizi ya viziada vya lugha
   • Lugha ya upole na heshima
 5. FASIHI SIMULIZI
  1. Andika sifa nne za visasili. Al 5
   1. Visasili ni hadithi zinazoaminiwa kuwa za kweli
   2. Wahusika katika visasili ni binadamu miungu mashujaa,wanyama,mawe na vitu vingine.
   3. Visasili huwa na misingi ya kihistoria
   4. Visasili husimulia mambo ya kiimani au kidini kama yanavyoaminiwa na jamii.
   5. Hueleza asili ya matukio katika jamii.
  2.  
   1. Hadithi ni nini? Al
    • Ni masimulizi ya kinathari kuhusu watu,matukio na mahali mbalimbali
   2. kwa nini hadithi zilitambwa wakati wa jioni. Al 4
    • Ndio wakati watu walikuwa wamejumuika nyumbani baada ya kazi
    • Utambaji ulikuwa njia ya kupitisha wakati chakula kikingojewa.
    • Wakati huu ulihakikisha mwanajamii hapotezi wakati wa kazi.
  3. Andika tofauti tano kati ya fasihi andishi na fasihi simulizi al 10.
   1. Fasihi simulizi
    • Inawasilishwa kwa njia ya mdomo
    • Huhifadhiwa akilini
    • Huweza kubadilishwa
    • Ni mali ya jamii
    • Muundo wake ni rahisi kufuatika
    • Uzuri wake hutegemea ubingwa wa mwasilishaji
    • Sifa zake Fulani za zamani huweza kupotea
    • Hadhira ni tendi
    • Mwanzo wake ni kipawa cha usimulizi
   2. Fasihi Andishi
    • Njia ya kuwasilisha ni maandishi
    • Huhifadhiwa vitabuni
    • Maandishi hayabadiliki
    • Ni mali ya mwandishi
    • Huenda muundo ukawa mgumu kufuatika
    • Uzuri unategemea usanii wa mwandishi
    • Maandishi hubaki katika hali yalioandikwa
    • Hadhira ni tuli
    • Mwanzo wake ni kipawa cha uandishi

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 3 Opener Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest