MASWALI
Maagizo: Jibu maswali yote katika nafasi zilizoachwa baada ya kila swali.
Sehemu A (Alama 20)
- Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya maneno yafuatayo: (alama 2)
- bali
- mbali
- Taja aina mbili za mofimu na utolee mfano kwa kila moja. (alama 2)
- Andika kwa wingi: (alama 1)
Gaidi alipigwa risasi na askari aliyekuwa akilinda doria. - Taja aina nne za nomino. (alama 2)
- Ni nomino gani isiyochukuana na nyingine? (alama 1)
Kumbi, paa, kubeta, kuta, mlango. - Tegua vitendawili vifuatavyo: (alama 2)
- Abeba mishale kila anapoenda.
- Ana meno lakini hayaumi.
- Tumia kivumishi cha sifa katika mabano kukamilisha sentensi ifuatayo. (alama 1)
Bei ya meli ni ………… mno (ghali). - Jaza pengo kwa kiulizi mwafaka: (alama 1)
Ni muundo ………………… uliotumiwa? - Ziandike upya sentensi zifuatazo ukitumia kiwakilishi cha pekee –ote. (alama 2)
- ……………………. Kilivunjika kilipoanguka.
- …………………….. ulipasuliwa.
- Geuza sentensi hii iwe katika wingi: (alama 2)
Mwanzi alioupanda karibu na mto umeshikana ukawa msitu mkubwa. - Tumia vitenzi vishirikishi vipungufu kukamilisha sentensi zifuatazo: (alama 2)
- Kipya kinyemi …………… kidonda.
- Mungu …………. wa kuabudiwa milele.
- Taja aina mbili za vielezi namna. (alama 2)
SEHEMU B
ISIMUJAMII
- Fafanua sifa tano za rejista ya kituo cha polisi. (alama 5)
FASIHI SIMULIZI - Taja njia tano za kumalizia hadithi. (alama 5)
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA
Maagizo: Jibu maswali yote katika nafasi zilizoachwa baada ya kila swali.
Sehemu A (Alama 20)
- Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya maneno yafuatayo: (alama 2)
- bali
- mbali
Wasafiri walinyeshewa bali waliendelea na safari hiyo ya mbali.
(mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi)
- Taja aina mbili za mofimu na utolee mfano kwa kila moja. (alama 2)
- Mofimu huru- baba
- Mofimu tegemezi- mtoto
(mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi)
- Andika kwa wingi: (alama 1)
- Gaidi alipigwa risasi na askari aliyekuwa akilinda doria.
Magaidi walipigwa risasi na askari waliokuwa wakilinda doria.
- Gaidi alipigwa risasi na askari aliyekuwa akilinda doria.
- Taja aina nne za nomino. (alama 2)
- Nomino za kawaida
- Nomino za pekee
- Nomino za wingi
- Nomino dhahania
- Nomino za wingi
- Nomino za vitenzi jina.
- Ni nomino gani isiyochukuana na nyingine? (alama 1)
- Kumbi, paa, kubeta, kuta, mlango.
Kubeta
- Kumbi, paa, kubeta, kuta, mlango.
- Tegua kitendawili vifuatavyo: (alama 2)
- Abeba mishale kila anapoenda- nungunungu
- Ana meno lakini hayaumi- kitana
- Tumia kivumishi cha sifa katika mabano kukamilisha sentensi ifuatayo. (alama 1)
- Bei ya meli ni ghali mno.
- Jaza pengo kwa kiulizi mwafaka: (alama 1)
- Ni muundo …gani/ upi……………… uliotumiwa?
- Ziandike upya sentensi zifuatazo ukitumia kiwakilishi cha pekee –ote. (alama 2)
- …………chote…………. kilivunjika kilipoanguka.
- ……………wote……….. ulipasuliwa.
- Geuza sentensi hii iwe katika wingi: (alama 2)
- Mwanzi alioupanda karibu na mto umeshikana ukawa msitu mkubwa.
Mianzi waliyoipanda karibu na mito imeshikana ikawa misitu mikubwa.
- Mwanzi alioupanda karibu na mto umeshikana ukawa msitu mkubwa.
- Tumia vitenzi vishirikishi vipungufu kukamilisha sentensi zifuatazo: (alama 2)
- Kipya kinyemi ……ki……… kidonda.
- Mungu ……yu/ni……. wa kuabudiwa milele.
- Taja aina mbili za vielezi namna.
- Vielezi namna hali
- Vielezi namna halisi
- Vielezi namna vikariri
- Vielezi namna viigizi
- Vielezi ala/ vitumizi (alama 2)
SEHEMU B
ISIMUJAMII
Fafanua sifa tano za rejista ya kituo cha polisi. (alama 5)
- Msamiati maalumu- afisa
- Lugha legevu- hii kijana
- Lugha ya unyenyekevu- samahani
- Lugha ya kuamuru- njoo hapa
- Lugha ya kudadisi- ulikuwa wapi?
(mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi)
FASIHI SIMULIZI
Taja njia tano za kumalizia hadithi. (alama 5)
- Hadithi yangu imeisha hapo.na wakaisha raha mustarehe.
- Na huo ndio mwisho wa hadithi yangu.
- Na hiyo ndiyo hadithi yangu.
- Hadithi yangu ni hiyo.
- Na wakaishi raha ustarehe.
(mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi)
Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Mid-term Exams Term 1 2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students