Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 2 Opener Exams 2022

Share via Whatsapp

QUESTIONS

  1. Eleza matatizo ambayo yaliletwa na ugonjwa wa Korona (Covid -19) nchini Kenya.
    UFAHAMU
    Soma taarifa ifuatayo na ujibu maswali.
    Dini ya ulimwengu ambayo imechukua karibu kila mtu ni mchezo wa mpira wa miguu.Wafuasi wa dini hii wamesambaa dunia nzima. Wafuasi hawa huitwa mashabiki. Katika kila nchi mashabiki huwa na timu zao, hasa katika miji yao. Mara nyingi timu hizi huchukua majina ya miji yao. Hawa wauasi huwa wanatoka katika kila tabaka. Kuzungumza kinyume cha dini yao ni kama kukasiri nguzo naitikadi zao. Zahama huweza kutokea kwa sababu ya jambo hili. Timu zinapocheza, mashabiki hawawezi hata kubari mvua, wao husimama kidete wakishangilia kwa vifijo na nderemo.
    Asili ya mchezo huu haijulikani kabisa ila inaaminika ulianzia huko Uchina na Japan. Mchezo huu ulipelekwa Uingereza na Warumi walipoitawala hapo kale kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Mchezo huu ulitumiwa kuwatumbuiza wafalme na watu wengine wakwasi.Mchezo huu ulikuwa ukichezwa kwa miguu peke yake lakini siku hizi huchezwa kwa kila sehemu ya mwili isipokuiva mikono. Mchezo huu zama hižo,ulikuwa ukichezwa baina ya vijiji. Kijiji kimoja kiliünda timu moja kucheza dhidi ya kijiji kingine. Inasemekana kwamba mechi moja ilichukua hata siku tatu kumalizika. Milingoti ya goli ilikuwa mita chache hadi kilomita chache kutoka kwa nyingine.Vita viliweza kutokea baina ya timu hizo za wanavijiji. Kuusukuma mpira ufike masafa ya mbali ulihitajika ujuzi wa wanaume wa miraba minne. Kengele kubwa ilitumiwa kuwajulisha mashabiki kuwa timu yao-imeingiza bao upande ule mwingine, labda kilomita tatu kutoka walipokuwa. Ili kupunguza ütumiaji wa nguvu kwa kucheza ovyoovyo tu, mpango maalumu ulibuniwa wa kutoa pasi kwa mwenzako katika sehemu ndogo ya uwanja. Idadi ya wachezaji wa kila timu ilipunguzwa kutoka ishirini na saba hadi ya mchezo wa kisasa. Waamuzi pia walipunguzwa kutoka sita, Mchezo wa kisasa, asili yake ni Uingereza baada ya sheria zake kubadilishwa hapa na pale. Mchezo huu umechukua majina ya lakabu, kwa mfano kabumbu, ngoma, gozi, soka, kandanda na kadhalika.
    Mchezo huu unapochezwa huwa unakusudiwa uwe na manufaa kadha wa kadha, yakiwemo kujiburudisha, kujenga mwili na kutoa mazoezi ya akili, chambilecho Wayunani kuwa akili timamu hukaa katika mwili wenye atya nzuri. Mchezo huu umekuwa kama kazi katika nchi zilizoendelea ambapo wachezaji hulipwa kiasi kikubwa cha darahimu. Ushindi unachukuliwa kuwa jambo muhimu sana na nguzo ya matendo ya mwanadamu. Mshindwa huwa na kisasi cha milele juu ya mshindi, atakacholipiza wakati ukiwadia. Jambo hili huwafanya wafuasi wa timu hii kuzusha vurumai iwapo watashindwa tena. Kujipatia umahiri katika mchezo huu sio jambo rahisi, lakini ukipata sifa, jina lako litakuwa likızungumziwa na watu wa aina yote. Wimbo wako hautadidimia na sifa yako itaenea karibu na mbali hadi siku utakapoiaga dunia,
    MASWALI
    1. Fafanua umuhimu wa mchezo wa kandanda kulingana na ufahamu.[al3].
    2. Fafanua wayasemayo wayunani.(al1).
    3. Eleza jinsi mchezo huu ulivyofika Uingereza.[al2].
    4. Kwa nini ilihitaji wanaume wa miraba minne kuwa wachezaji hapo kale.[al2].
    5. Eleza maana ya msamiati ufuatao;(al2)
      1. Zahama
      2. Masafa

MATUMIZI YA LUGHA

  1.        
    1. Ainisha mofimu katika neno achezaye. [al2]
    2. Weka maneno haya katika mofimu .[al1]
      • Parafujo
      • Samaki
  2. Tunga sentensi ambayo ina kivumishi kiashiria kisisitizi cha mbali kidogo katika ngeli ya k i –vi umoja.[al2].
  3. Bainisha maneno katika sentensi hii.[al3]
    Mama amepikiwa chai na mtoto wake.
  4. Tunga sentensi ukitumia nomino dhahania. [al2]
  5. Eleza matumizi ya neno Nairobi kama vile limetumika katika sentesi zifuatazo;(al2)
    1. Mama ameenda Nairobi .
    2. Nairobi ni mji mkuu wa Kenya .[al1].
  6. Katika tanakali za sauti kuna ;(al1)
    Tulia _______________________________
    Lewa ______________________________ .
  7. Eleza maana ya sentesi zifuatazo;(al2)
    1. Wanafunzi wowote wanaitwa na mwalimu.
    2. Wanafunzi wote wanaitwa na mwalimu.
  8.        
    1. Onyesha vitenzi katika sentensi zifutazo na ueleze ni vya aina gani [al2]
      1. Mama alikuwa shambani .
      2. Mama alikuwa akilima.
    2. Tunga sentensi ukitumia kitenzi kishirikishi kipungufu[al2]
  9. Taja sifa za sauti /e/. (al 1)

ISIMU JAMII

  1. Eleza sifa za sajili ya maabadini.[al5].
  2. Eleza mambo yanayodhibiti lugha katika jamii.[al3].
  3. Eleza maana ya msamiati ufuatao;[al2]
    1. Isimujamii
    2. Sajili

FASIHI SIMULIZI

  1. Eleza tofauti tatu baina ya fasihi simulizi na fasihi andishi.[al3].
  2. Taja aina tatu za nyimbo na ueleze jukumu la kila moja.[al3].
  3. Taja aina nne za hadithi.(al4].


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA 

  1.        
    1. Kujiburudisha
    2. Kujenga mwili
    3. Kutoa mazoezi ya mwili
  2. Wayunani husema kuwa akili timamu hukaa katika mwili wenye afya nzuri.
  3. Mchezo huu ulipelekwa na warumi walipoitawala kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
  4. Ili kuusukuma mpira ufike masafa ya mbali.
  5. Zahama –Ghasia,Fujoama Vurugu.
    Masafa—Mbali

INSHA

  1. Umesababisha ,vifo
  2. Utengano wa familia na kuvunjika kwa ndoa.
  3. Kusitishwa kwa masomo.
  4. Waja wengi wamepoteza kazi.
  5. Njaa baada shughuli nyingi nchini kufungwa .
  6. Watoto wengi kuacha masomo na kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.
  7. Kufungwa kwa biashara.
  8. Safari za kimataifa kusitishwa.

MATUMIZI YA LUGHA

  1.      
    1. A-nafsi ya tatu umoja
      Chez-mzizi
      a-kiishio
      ye- kirejeshi
    2. parafujo—mofimu tegemezi
      samaki –mofimu
  2. Kicho hicho kimeraruka vibaya.
  3. Mama amepikiwa chai na motto wake
    Mama-N
    Amepikiwa-T
    Chai-N
    Na –H
    Mtoto-N
    Wake-V
  4. Mtahiniwa atumie nomin ambazo hazina mashiko ;Upepo,Ugonjwa .nk.
  5.      
    1. Nairobi –kielezi cha mahali.
    2. Nairobi-Nomino.
  6. Tulia tuli.
    Lewa chakali.
  7.      
    1. Bila kubakisha.
    2. Bila kuchagua au kubagua.
  8.        
    1.      
      1. alikuwa –kitenzi kishirikishi kika milifu.
      2. alikuwa -kitenzi kisaidizi.
        Alikuwa akilima –vitenzi sambamba.
    2. Mtahiniwa atemie vitenzi kama ;si, ni, ki, li, u, yu.
  9. /e/
    1. Mbele wastani.
    2. Midomo hutandazika itamkwapo .

ISIMU JAMII

  1. Msamiati maalum ,Mungu,Yesu ,Allah.nk.
    Lugha ya matumaini.
    Lugha ya kushurutisha .
    Nyimbo hushirkishwa .
    Mafungu ya vitabu vitakatifu hutajwa.
    Lugha ya unyenyekevu na maombi.
  2. Kaida za lugha,umri,cheo,jinsia ,mazingira nk.
  3. Isimuu jamii –Matumizi ya lugha katika jamii.
    Sajili –Matumizi ya lugha katika mazingira tofauti.

FASIHI SIMULIZI

  1.        
    1. Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali andishi nimali ya mtu binafsi.
    2. Fasihi simulizi huenezwa kwa midomo ilhali andishi huenezwa kwa maandishi.
    3. Fasihi simulimu huhifadhiwa ubongoni ilhali andishi huhifadhiwa vitabuni
  2. Bembea-nyimbo za watoto-hutumika kwa watoto kulala au kusitisha kulia.
    Nyiso-nyimbo za jandoni –huwapa watahiriwa ujasiri.
    Mbolezi—nyimbo za matanga-hutumika kuliwaza wafiwa.
  3.      
    1. Visa viini-husimulia asili ya jamii.
    2. Ngano za mtanziko husimulia visa ambapo mhusika hukabiliana na utata wa uamuzi.
    3. Mighani husimulia kuhusu majagina na sifa zao
    4. Hekaya husimulia visa vifupi ambavya wahusika wake huwa wajanja katika mambo Fulani mfano hekaya za Abunuasi. 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 2 Opener Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest