Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 1 Exams 2023

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU (ALAMA15)
    Soma kifuatacho kisha ujibu maswali.

Lugha inaweza kuelezwa kwa jumla kuwa ni mfumo wa kueleza chanzo au kiini cha mawasiliano na sote tunakubaliana kuwa matumizi yake yameanza tangu kuumbwa kwa binadamu kwani ni vigumu kukisia kuwepo kwa jamii ya watu bila lugha ya mawasiliano yoyote ile. Katika taifa lolote,huwepo na lugha moja au hata zaidi ya moja ambayo huwa ndicho chombo zatika cha mawasiliano ya taifa katika nyanja za:elimu, maandishi, siasa na biashara.Kwa mfano mataifa ya Kanada hutumia lugha mbili kwa usawa kama lugha za taifa na za kikazi. Maana ya lugha ya taifa ni lugha moja ambayo huteuliwa kutumika katika shughuli zote za taifa hasa katika nchi yenye lugha nyingi za kikabila. Lugha ya taifa ni muhimu sana kwa maisha na maendeleo ya taifa lolote lile.Lugha hii huwa ndiyo kiungo cha kueneza umoja na uelewano miongoni mwa jamii nyingi tofauti na huwa kama kitambulisho kwao kwa kuwa wao ni ndugu wa jamii moja kubwa, yaani taifa lao.

Kenya ni mfano mzuri wa taifa lenye lugha nyingi zinazozidi 40 za vikundi vidogo vidogo vya kikabila.Hapo kabla ya miaka mia moja hivi iliyopita kila kimojawapo cha vikundi hivi kilijitambulisha kama taifa huru.Baada ya kuja kwa serikali ya kikoloni na hasa baada ya Kenya kujinyakulia uhuru,haja ya kuunganisha raia wote chini ya taifa moja lenye uongozi na shabaha moja lilikuwa ndilo jambo lililozingatiwa sana.Kwa hivyo utamaduni wa taifa la Kenya ni mchanganyiko wa tamaduni za watu wengi wenye mila,desturi,imani na itikadi tofauti. Utamaduni humaanisha jumla ya amali na tabia za watu wa jamii fulani. Amali hizi zinafungamanisha fikira, ustaarabu, mila, taasisi na sanaa za aina zote za jamii inayohusika. Ili kujieneza na kujiimarisha,taifa huhitaji chombo hicho kuwasiliana na kuwaunganisha watu wake wenye asili mbalimbali.Chombo hicho huwa ni lugha ambayo siyo tu kwamba ni sehemu ya utamaduni wa jamii bali pia ni njia muhimu sana ya kutawanyia na kustawishia ule utamaduni.

Katika taifa lenye lugha nyingi kama Kenya kwa mfano,lugha ya taifa inayozungumzwa na kueleweka na idadi kubwa ya raia ambayo imekiuka mipaka na tofauti za kikabila ni njia muhimu sana ya kueneza maongozi ya taifa, bendera ya taifa, ndicho kielelezo cha taifa lolote lile lililo huru. Lugha kama hiyo huvunja na hukomesha hisia za kibinafsi na kikabila na badala yake kuunda moyo wa uaminifu wa kitaifa.

Zaidi ya kuwa chombo cha mawasiliano, lugha ni kielelezo cha fikira na hisia za binadamu.Lugha ya watu fulani haituelezi tu ujuzi au maarifa yao bali pia mtazamo wao kimaisha, falsafa na mawazo yao. Kwa ufupi lugha hutufahamisha namna akili za watu waizungumzayo ile lugha zinavyofikiri na kutafanya maazimio.Lugha ni sehemu ya utamaduni wa taifa ilimozaliwa na lazima lugha hiyo ifunzwe katika muktadha wa maisha ya jamii ihusikayo.Utamaduni wa jamii havitenganiki na lugha yake.

MASWALI

    1. Ni nini fasiri ya neno lugha? (alama 2)
    2. Tofautisha baina ya lugha ya taifa na lugha ya kikazi. (alama 2)
    3. Kwa nini lugha ya taifa huhitajika sana katika nchi kama Kenya? (alama 2)
    4. Taja kazi tatu kuu zinazotekelezwa na lugha ya taifa. (alama 3)
    5. Eleza maana ya msamiati ufuatao kulingana na taarifa. (alama 1)
      • Haiyamkiniki:
  1. MATUMIZI YA LUGHA.(Alama 30)
    1. Taja kikwamizo hafifu cha ufizi. (Al 1)
    2. Tambua aina za vitenzi katika sentensi hii. (Al 2)
      1. Wale waliokuwa hapa sio wagenu wetu.
    3. Alama ya Nukta mbili huweza kutumika kuorodhesaha vitu. Tunga sentensi mbili tofauti kuonyesha namna alama hiyo inaweza kutumiaka. (Al 2)
    4. Yakinisha sentensi ifuatayo . (Al 2 )
      1. Usipopita mtihani hutakuwa shujaa mapema.
    5. Sahihisha sentensi hii kwa njia mbili mwafaka. (Al 2)
      1. Dereva ambaye aendeshaye kwa uangalifu husalimika.
    6. Tunga sentensi sahihi huku ukitumia kihusishi cha wakati. (Al 1)
    7. Ainisha aina za maneno katika sentensi ifuatayo. (Al 3)
      1. Mwanafunzi mtundu ameadhibiwa vikali na mwalimu.
    8. Eleza ‘po’ ilivyotumika katika sentensi hizi. (Al2)
      1. Alipofika waliposimama, waliondoka.
    9. Tumia kiunganishi kifaacho kuunganisha sentensi hii. (Al 2)
      1. Juma hakusoma kwa bidii. Amefuzu mtihani.
    10. Geuza sentensi hii iwe katika usemi wa taarifa. (Al 3)
      1. “ Nimekuwa nikija kwenu kila siku lakini nimeamua kulikata guu langu,” Hamisi akamweleza Amina.
    11. Andika sentensi hii kwa ukubwa. (Al. 1)
      1. Mwizi aliiba kikapu na ng’ombe.
    12. Eleza matumizi ya “ KI” iliyopigiwa mstari katika sentensi hii. (al 3)
      1. Ukirusha kipira hiki kitapotea.
    13. Andika maana tatu zitokanazo na sentensi hii. (Al 2)
      1. Mama alimpigia mtoto mpira.
    14. Tunga sentensi moja kuonyesha maana ya vitate vifuatavyo. (Al 2)
      1. Chaka
      2. Shaka
    15. Tunga sentensi sahihi ukitumia kiwakilishi kisisitizi cha mbali kidogo ngeli A- wA katika hali ya wingi . (Al 2)
  2. FASIHI SIMULIZI (Alama 5)
    1. Eleza maana ya vitanza ndimi. (Al 2)
    2. Eleza umuhimu wa jamii kutumia vitanza ndimi. (Al 3)
  3. ISIMU JAMII (Alama 5)

Ali: Wee kuja hapa. Wewe ni nani? Sema haraka!

Ebo: Mimi……ni….afande ni Ebo

Ali: Unatoka wapi saa hii? Hapa hakuna sheria?

Ebo: Samahani mkubwa. Mimi niku……

Ali: Mkubwa wa nani? Wakubwa wako ofisini

Ebo: pole mzee

Ali: Mzee gani? Hii mtu lazima niiweklw store. Yaani Self contained. Toa viatu.

Ebo: Tafathali Bwana Askari, nilichelewa…..

Ali: Mimi sitaki hadithi. Hizo pelekea nyanya yake,eh. Fanya haraka!

Ebo: Naomba mkubwa…..

Ali: Hapa si kanisani. Unaomba! Hata…….

Fafanua sifa tano za sajili hii. (al 5)



 



 



MAKIZO

  1. UFAHAMU (ALAMA 15)
    1. Ni mfumo wa mawasiliano katika jamii yoyote ile. (alama 2)
    2. Lugha ya taifa na ile inayoteuliwa kutumia katika shughuli zote za taifa ambayo hueneza umoja na uelewano katika jamii ilhali lugha ya kikazi ni ile inayotumiwa kuendesha shughuli rasmi za taifa. (alama 2)
      1.   Huhitajika ili kueneza maongozi ya taifa ya kuleta ufahamikiano kote nchini.
      2.  Ili kuvunja na kukomesha hisia za kibinafsi na kikabila. (alama 2)
      1.  Ni chombo cha mawasiliano katika nyanja za elimu, biashara, maandishi na siasa.
      2. Ni kiungo cha kueneza umoja na maelewano miongoni mwa jamii tofauti.
      3. Ni kitambulisho cha utaifa. (alama 3)
      1.   Haiwezekani.
      2. Matendo na hulka za binadamu.
  2.  MATUMIZI YA LUGHA.(Alama 30)
    1. Taja kikwamizo hafifu cha ufizi. (Al 1)
      • /S/
    2. Tumia kiiunganishi kifaacho kuunganisha sentensi hii. (Al 2)
      • Juma hakusoma kwa bidii. Amefuzu mtihani
        1. Japo, ijapokuwa, ingawaje,ingawa, lakini, ila,
    3. Tambua aina za vitenzi katiak sentensi hii. (Al 2)
      1. Wale waliokuwa hapa sio wagenu wetu
        • Waliokuwa – Kitenzi kishirikishi kikamilifu.
        • Sio – Kitenzi kishirikishi kipungufu
    4. Alama ya Nukta mbili huweza kutumika kuorodhesah vitu. Tunga sentensi mbili tofauti kuonyesha namna alama hiyo inaweza kutumiaka. (Al 2)
      1. Kutenganisha saa na dakika.Amefika 7:00asubuhi.
      2. Kutenganisha tarakimu. Alisoma mathayo 7:6 – 10.
      3. Katika mazungumzo ya kitamthilia; Baba: unaenda wapi?
    5. Yakinisha sentensi ifuatayo . (Al 2 )
      1. Usipopita mtihani hutakuwa shujaa mapema.
        • Ukipita mtihani utakuwa shujaa mapema.
    6. Sahihisha sentensi hii kwa njia mbili mwafaka. (Al 2)
      1. Dereva ambaye aendeshaye kwa uangalifu husalimika.
        • Dereva ambaye anaendesha kwa uangalifu husalimika
        • Dereva aendeshaye kwa uangalifu husalimika .
    7. Tunga sentensi sahihi huku ukitumia kihusishi cha wakati. (Al 1)
      • Baada ya, kabla ya, tangu, hadi, toka, mpaka
    8. Ainisha aina za maneno katika sentensi ifuatayo. (Al 3)
      1. Mwanafunzi mtundu ameadhibiwa vikali na mwalimu.
        KSWFRM2QNH
    9. Eleza ‘po’ ilivyotumika katika sentensi hizi. (Al2)
      1. Alipofika waliposimama, waliondoka.
        • Wakati Mahali
      2. Geuza sentensi hii iwe katika usemi wa taarifa. (Al 3)
        • “ Nimekuwa nikija kwenu kila siku lakini nimeamua kulikata guu langu,” Hamisi akamweleza Amina.
        • Hamisi alimweleza Amina kuwa alikuwa akiwnda kwao kila siku lakini aliamua kulikata guu lake
    10. Mofimu ni nini? (Al 1)
      • Sehemu ndogo sana ya maneno inayowasilisha maana kisarufi.
    11. Andika sentensi hii kwa ukubwa. (Al. 1)
      1. Mwizi aliiba kikapu na ng’ombe.
        • Jizi liliiba jikapu na gombe
    12. Eleza matumizi ya “ KI” iliyopigiwa mstari katika sentensi hii. (al 3)
      1. Ukirusha           kipira    hiki kitapotea.
        • Masharti    Udogo    Ngeli
    13. Andika maana tatu zitokanazo na sentensi hii. (Al 2)
      1. Mama alimpigia mtoto mpira.
        • Kwa sababu
        • Kuelekeza kwa mtoto
        • Kwa niaba
        • Kutumia mpira
    14. Tunga sentensi moja kuonyesha maan aya vitate vifuatavyo. (Al 2)
      1. Chaka
      2. Shaka
        • Chaka lile bila shaka, limechomeka
    15. Tunga sentensi sahihi ukitumia kiwakilishi kisisitizi cha mbali kidogo ngeli A- wa katika hali ya wingi . (Al 2)
      • Watoto wao hao wameitwa na mwalimu.
  3. FASIHI SIMULIZI (Alama 5)
    1. Eleza maana ya vitanza ndimi. (Al 2)
      • Vitanza ndimi ni vifungu vya maneno vyenye sauti tatanishi. Ulimi hutatizika wakati wa kutamka sauti ambazo aghalabu hukaribiana sana.
    2. Eleza umuhimu wa jamii kutumia vitanza ndimi. (Al 3)
      1. Hutumika kuchemsha bongo
      2. Hutumika kuburudisha na kufurahisha
      3. Hutumika kuimarisha matamshi bora
      4. Hukuza kiwango cha kufikiria
      5. Kupitisha wakati
  4. ISIMU JAMII (Alama 5)
    • Sajili kituo cha polisi
      Sifa za sajili
      1. Matumizi ya kauli za kuamrisha – fanya, haraka
      2. Kuma kuchanganya ndimi – yaani self – contained, toa viatu
      3. Matumizi ya msamiati maalum – afande
      4. Kauli za ukali – mimi sitaki hadithi
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 1 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest