KISWAHILI - FORM 3 END TERM 1 EXAMS 2020

Share via Whatsapp
 1.  UFAHAMU: (ALAMA 15)
  Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali

  Tukilinganisha maisha ya zamani na ya siku hizi tutaona kwamba mambo mengi sana yamebadilika. Si watu wazima, si watoto; sote tumeathirika si haba. Mitindo mipya ya kimaisha na mazingira yanayobadilika kasi ni baadhi tu ya mageuzi haya. Sio katika mavazi, lugha, mienendo, mitazamo, mawazo na mielekeo tu bali katika vipengele vingine vingi.

  Mavazi ya zama hizo yalikuwa yakitengenezwa kutokana na maganda ya mti au ngozi za wanyama kama vile mbuzi, kondoo, punda, ngamia, ng’ombe na hata pengine wanyama wa mwituni. Kwa vile kila mtu alifuga wanyama wengi, hakukuwa na shida ya kuzipata ngozi kama hizo wakati wowote ule haja zitokeapo. Magome ya miti yalipatikana mwituni- na kwa kuwa katika enzi hizo hakukuwa na hifadhi za wanyama wa mwitu wala misitu yenyewe, watu waliweza kuingia katika pori lolote na kubambua maganda au kuua wanyama kama walivyohitaji.. mavazi yalikuwa rahisi kupatikana kuliko zama zetu; licha kwa upande wa ndarama hata kwa upande wa sheria pia. Zaidi,katika enzi hizo watu hawakujali kwenda uchi au walipachika kipande tu cha vazi mwilini. Siku hizi gharama ya maisha imepanda mno.

  Siku hizi hatuwezi kuwaua wanyama wa mwituni vururu mtende eti kwa chakula, kama walivyofanya babu zetu. Enzi hizo matunda yalining’inia mitini na njaa zilikuwa si nyingi. Chakula kilikuwa bwerere zaidi ya leo. Vinywaji vilikuwa kwa mpango – wazee wa ngambi walikuwa na vinywaji vyao; wazee wa kawaida, wanawake na watoto hirimu hawakusahauliwa. Watu waliheshimiana; vijana walikuwa wenye adabu na walifahamu fika kuwa walipaswa kuwaheshimu wakubwa wao kwa vyoyote vile. Siku hizi vyakula ni haba na ghali na vingi vyazua magonjwa tata.

  Siku hizi kuna weledi wengi, hasa wa sayansi. Mja akitaka kwenda safarini huchukua kidubwasha fulani na huyoo! Kaenda zake; barabarani, angani au hata katikati ya kilindi cha bahari. Leo twajivunia ujuzi na maendeleo ya kiafya na madawa yapunguzayo mno unyofu wa binadamu lakini bado kuna pengo kubwa kati ya vikongwe na watu wa makamo, kinyume na zama hizo. Maisha ya karne hii yamekuwa kama zile nguo ziitwazo bwaga – mtwae”, ambazo hazibali kufumka au kukwajuka..

  Hivi leo, mtu akiumwa na kichwa hukimbilia daktari. Mwingine akiumwa na nyoka popote pale, hukimbilia hospitalini akapate sindano ambayo hata jina lake halijui. Zamani mtu alikuwa achimbechime mizizi ya upuzi upuzi, aitafune na alipata nafuu! Wa kisasa twapuuza wa kale eti hawakujua elimu ya usafi tuijuavyo sisi, ilhali walikuwa wakichoma miili ya watu waliokuwa wamekufa kwa ukoma au kifua kikuu. Wakati mwingine walikihama kijiji kilichoingiliwa na maafa ya ndui. Hata sasa wagonjwa kama hao hutengwa hospitalini maradhi kama vile UKIMWI bado yakikosa tiba.

  Mengi tuliyo nayo sasa mathalan tarakilishi na eropleni yalivumbuliwa au kugunduliwa na hao wa zamani. Fanaka zetu zote na ustawi tulionao asili yake ni watu hao wa zamani. Akili ni mali na kila mtu ana zake. Kuongezeka kwa watu duniani, mchanganyiko au matumizi mabaya ya madawa mengi pamoja na uchafuzi wa hali ya anga pia yameongezea kuleta hasara kubwa. Kweli sikio haliwezi kushinda kichwa.
  1. Kulingana na mwandishi, kwa nini maisha ya kale na ya sasa hayalingani? (alama 3)
  2. Kupata mavazi zama zile kulikuwa nafuu. Toa sababu. (alama 2)
  3. Kwa kusema siku hizo, ‘chakula kilikuwa bwerere zaidi ya leo,’ mwandishi anamaanisha nini?   (alama 2)
  4. Taja sababu za magonjwa na maafa kukithiri siku hizi licha ya hatua kubwa katika elimu na afya. alama 3)
  5. Fafanua usemi, ‘sikio haliwezi kupita kichwa,’ kwa mujibu wa taarifa.             (alama 2)
  6. Eleza maana ya;
   1. Magome-
   2. Vururu mtende-
   3. Hazibali-
 2. SEHEMU YA B: UFUPISHO: (ALAMA 15)
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.

  Katika safu yangu hii sina lengo la kuzishambulia dini zetu na namuomba Mungu sana asiniandikie dhambi kutokana na ninayotaka kuyaandika, lakini nashawishika kuikumbusha jamii yangu ambayo inatufanya watu tuzione dini zetu zinamkandamiza mwanamke. Dini zetu kubwa kama Uislamu na

  Ukristo zinatuelekeza mwanamke kumheshimu mumewe na kumskiliza anachosema, lakini kwa yeye kufuata maadili ya dini na sikukwambia uue ukakubali.

  Wakati dini inasema utekeleze amri ya mumeo na wao wameelezwa mambo ya kuwafanyia wanawake, ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu na kuwaridhisha kadri na uwezo wao.

  Kutokana na hilo la amri, wanaume wengi ndio wamechukua kama tiketi ya kuwanyanyaza wanawake na hata kumnyima fursa ya kujiendeleza kielimu na hata kufanya shughuli za kuongeza kipato. Unakuta familia ni ya kimaskini, baba hana fedha za kutosha kuihudumia familia yake, lakini baba huyo anataka kujishughulisha na shughuli yoyote ya kumuingizia kipato kinachoweza kuwasaidia wote na matokeo yake kuendelea kuwepo, kwenye dimbwi la umaskini. Wengine kwa hofu ya kupata changamoto kutoka kwa wake zao wanawakatalia wanawake walio wao kujiendeleza kielimu au kutafuta mwanamke asiyeelimika ili asiweeze kuhoji mambo kadhaa ndani ya nyumba.

  Hili limebainishwa hivi karibuni na shirika moja lisilo la kiserikali huko Kigoma ambapo katika utafiti wao asilimia 90% ya wanawake wa vijijini wanashindwa kutoa hoja kutokana na uelewa wao duni na kutoa sababu ya kuwa hiyo ni kutokana na ukosefu wa elimu, masuala ya kidini yanayomwelekeza mwanamke kufuata amri za mumewe, mila na desturi kadhaa.

  Dini zote zinaeleza wazi umuhimu wa mtu kupata elimu bila kubagua kama ya kiisalmu inavyosema; mtu anapata thawabu anapotafuta elimu na anatakiwa aitafute popote bila kujali umbali na hata ikiwezekana kufika China ambapo inaaminika ni mbali. Sijawahi kuona wala kusikia dini ikisema mwanamke asipate elimu lakini baba zangu na kaka zangu wanaume wanalipotosha hili kutaka kuendelea kumkandamiza mwanamke bila kufikiria kuwa mwanamke ni msaada mkubwa kwao na maendeleo ya taifa lolote; ikiwa leo tuko katika harakati za kupata maendeleo na nchi hii hivi kweli tutafanikiwa?

  Mapambano ya kuleta maendeleo yaanze katika ngazi ya familia kwa kuondoka kwa ujinga wa kumkandamiza mwanamke ili naye aelimike, aweze kujenga hoja, aweze kujitafutia kipato na mwisho kusaidia katika maendeleo ya familia ambayo kwa njia nyingine ndiyo maendeleo yenyewe ya taifa hili.
  1. Fupisha aya tano za kwanza. (Maneno 70)
  2. Mwanamke anaweza kuendelezwa vipi? Rejelea aya mbili za mwisho. (Maneno 50)
 3. SEHEMU YA TATU: MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1.  Andika katika hali ya umoja. (alama 2)
   1. Masaibu yaliyowapata yaliwafanya wapoteze matumaini.
   2. Machaka ya waridi hayazai maua meusi
  2. Tunga sentensi ukitumia neno ‘mwitu’ kama:-
   1. Kielezi           (alama 1)
   2. Nomino         (alama 1)
  3. Andika katika usemi wa taarifa   (alama 2
   Askari: Ulikuwa unaenda wapi uliposhambuliwa?
   Jirani: Nilikuwa nikienda sokoni.
  4. Sahihisha sentensi ifuatayo.      (alama 2)
   Mtu ambaye aliyechukua kitabu chenye kilikuwa hapa arudishe.
  5. Bainisha mofimu katika maneno haya                                                               (alama 1)
   1. Samaki
   2. Mtu
  6. Andika sentensi ifuatayao katika hali ya kuamrisha.                                         (alama 1)
   Tafadhali, acheni kucheka ovyo.
  7. Changanua kwa kutumia mistari. (alama 4)
   Raisi mpya aliwahutubia wananchi jana.
  8. Taja ala nne za kutamkia. (alama 2)
  9. Majina haya yako katika ngeli gani? (alama 1)
   1. Uga
   2. Huzuni
  10. Tambulisha viambishi katika kitenzi:- (alama 3)
   Kitakachotolewa
  11. Toa maana mbili za sentensi ifuatayo. (alama 2)
   Majoka alimpigia mpira
  12. Andika katika hali ya wingi. (alama 2)
   Mimi ndimi niliyepanga mkutano huu.
  13. Andika katika hali ya udogo. (alama 2)
   Mtoto amejiwa na mama yake.
  14. Andika upya kwa kuzingatia maagizo. (alama 2)
   Mbwa aliyepotelea mwituni alipatikana kidimbwini.
   (Anza: Kidimbwini…)
  15. Kinyume cha:-
   Jogoo akiwa juu ya banda aliwika na kusikika kote……………(alama 2)
  16. Fafanua matumizi matatu ya neno ‘kwa’. (alama 3)
  17. Vihisishi hivi hutumika katika hali gani? (alama 2)
   1. Makiwa
   2. Lahaula
  18. Ainisha muundo wa silabi katika maneno yafuatayo. (alama 3)
   1. Tandazwa
   2. Eua
   3. Chichiri
  19. Ainisha vitenzi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
   Babu alikuwa akitusimulia hadithi
 1. ISIMU JAMII (Alama 10)
  1. Lahaja ni nini? (alama 2)
  2. Sajili ni nini? (alama 2)
  3. Taja wahusika wawili katika rejesta ya hotelini. (alama 2)
  4. Eleza kwa kutoa mifano sifa nne za rejesta ya shuleni/darasani. (alama 4)

MWONGOZO WAKUSAHIHISHA

 1. UFAHAMU                                                        
  1. Mabadiliko ya maisha/athari za kigeni/mitindo mipya ya kimaisha, mavazi,chakula, afya nk.
   Mazingira yanayobadilika – sheria zinabadilika
   Teknolojia, tarakilishi n.k                                                                   zozote 3 x 1 = 3
  2. Wanyama walifugwa kwa wingi
   Misitu ilikuwa kocho
   Watu walikuwa huru hata kuwinda na kukata miti                            zozote 2 x 1 = 2
  3. Chakula kilipatikana kwa urahisi mno na bila malipo au gharama kubwa 1 x 2 =2
  4. Idadi kubwa/kuongezeka kwa watu duniani
   Mazingira yanayobadilika mara kwa mara
   Mchanganyiko au matumizi ya madawa mengi pamoja
   Uchafuzi wa hali ya anga                                                                       zozote 3 x 1 = 3
  5. Vijana si sawa na wazee; watu wazima wahekima, busara na tajriba ya maisha.
   Watu wa siku hizi hawashindi wa zamani kimaisha.                                         2 x 1 = 2
  6.  
   1. maganda ya miti
   2. ovyo ovyo bila uoga au vikwazo
   3. hazikawii: hazichukuimuda; hazihimili                                                     3 x 1 = 3
 2. SEHEMU B: UFUPISHO
  1.  
   1. Sina lengo la kuzishambulia dini zetu na namuaomba Mungu asiniandikie dhambi
   2. Dini za uislamu na ukristo zinatuelekeza mwnamke kumheshimu mumewe na kumsikiliz aanachosema
   3. Dini imewapa wanawake jukumu la kufuata amri ya mumeo.
   4. Wanaume wengi wamecchukua amri hii kumyanyasa n akuwanyima fursa ya elimu na hofu ya kupata kipato.
   5. 90% ya wanawake hawatoi hoja kwa sababu wao wameiamini kuwa dini
   6. Wanaume huwa na hofu ya kupata changamoto kutoka kwa wake waliojiedeleza kielimu
   7. Dini zinaelez aumuhimu wa mtu kupat aelimu bila kubagua
    (Hoja -6, mtiririko 2, jumlaalama 8)
   • Kwa kupata elimu
   • Asikandamizwe kwa vyoyote
   • Tutambue umuhimu wa mwanamke katika ujenzi wa taifa
   • Atafute kipato cha familia
   • Aweze kutoa maoni ya ujenzi wa nchi
   • Imani potovu zakidini zitupiliwe mbali. (mtiririko - 1 (alama 6)
 3. LUGHA
  1.  
   1. Masaibu aliyoyapata yalimfanya apoteze matumaini. (1x1 =1)
   2. Chaka la waridi halizai na jeusi.                                                   (1x1 = 1)
  2.  
   1. Ngombe walipotelea mwituni. (al 1)
   2. Mwitu huu umejaa samba.                                                                      (al 1)
  3. Askari alimuuliza jirani alikuwa anaelekea wapi aliposhambuliwa naye jirani akamjibu kwamba alikuwa akienda sokoni (al 2)
  4. Mtu aliyechukua kitabu kilichokuwa hapa, arudishe. (al 2)
  5. Samaki-huru
   M|tu, m-tu.Tegemezi                                                                     (1/2 x 2) = 1)
  6. Acheni kucheka ovyo! (1 x 1)
  7. S –KN+KT
   KN-N+V
   N-Raisi
   V-Mpya
   KT-T+N+E
   T-Aliwahutubia
   N-wananchi
   E-jana                                                                           (8 x ½ =4)
  8.  
   1. Ulimi
   2. meno
   3. midomo
   4.  ufizi
   5. Kakaa gumu
   6. kakalaini
   7. koromeo                                                              zozote (4 x ½ = 2)
  9.  
   1. U-ZI
   2. I-I                                                                          ½ x 2 = 1
  10. KI- Kiambishi ngeli
   ta-              wakati
   ka-             hali
   cho-           kirejeshi
   to-              (mzizi)
   lew-           kauli
   a                tamati|kiishio                                                       (½ x 6 = 3) 
  11.  
   1. Alimpiga kwa sababu ya mpira
   2. Alipiga mpira kwa niaba yake
   3. Alipiga mpira akielekeza kwake
   4. Alitumia mpira kumchapa (2 x 1 = 2)
  12. Sisi ndisi tuliopanga mikutano hii (2 x 1 = 2)
  13. Kitoto kimejiwa na kimama chake (2 x 1 = 2)
  14. Kidimbwini ndimo alimopatikana mbwa aliyepotelea musituni   (2 x 1=2)
  15. Jogoo akiwa chini ya banda aliwika na kusikika kote (2 x 1 = 2)
   1. Kwa ya sehemu ya kitu kizima
   2. Kwa ya mahali
   3. Kwa ya umilikaji
   4. Kwa ala/kifaa kilichotumiwa
   5. Kwa ya kihusishi
   6. kuonyesha pamoja na                                             zozote 3x1=3)
  16. kumpamtu pole baadayamsiba
  17.  
   1. kumpa mtu pole – baada ya msiba
   2. lahaula-mshangao (2 x 1= 2)
  18.  
   1. KIKKIKKI
   2. III
   3. KIKIKI                                                                        (3 x 1) = 3)
  19. Ts-kitenzi kisaidizi - alikuwa
   T-kitenzi kikuu-    alitusimulia

ISIMU JAMII

 1. Ni kilugha ndani ya lugha moja kuu
 2. Sajili ni matumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali
 3. Hadimu na mteja
 4.  
  1. Lugha ya heshima/adabu/samahani mwalimu
  2. lugha sanifu
  3. maswali na majibu
  4. istilahi maalum kutegemea somo
  5. lugha ya ushauri
  6. lugha ya kuelekeza
  7. lugha ya kuhimiza n.k    (zozote 4 x 1 = 4)

Download KISWAHILI - FORM 3 END TERM 1 EXAMS 2020.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest