Kiswahili Karatasi ya 2 Form 3 Questions and Answers - End Term 2 Exams 2021

Share via Whatsapp

Kiswahili Karatasi ya 2 Form 3 End Term 2 Exams 2021 with Marking Schemes

 1. UFAHAMU

  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

  Habari kuwa watoto chini ya miaka mitatu ‘huwindwa’ kitandani na kuraushwa na wazazi wao waende shuleni mwendo wa saa kumi na moja asubuhi ni za kusikitisha.

  Kwa mujibu wa ripoti za wataalamu wa elimu ya watoto wachanga (ECD), watoto hao hutakikana kuwa darasani kabla ya saa kumi na mbili asubuhi.

  Wanapowasili wao huanza kufukuza ratiba ya masomo ambayo huwapatia muda mfupi mno wa kula, kucheza, kupumzika na hata kuchunguza afya na usalama wao.

  Badala ya kuondoka mapema kuelekea nyumbani, wengi wao hufika saa za usiku pamoja na wazazi wao wakitoka kazini. Wanapowasili nyumbani wanapaswa kuoga na kupata chakula cha jioni kwa pupa ili wafanye mazoezi waliyopewa na walimu wao.

  Mazoezi hayo huwa ya masomo yote matano huku kila somo likiwa na zaidi ya maswali thelathini. Badala ya kupumzika mwishoni mwa juma, watoto hao huhitjika kuhudhuria shule siku nzima ya Jumamosi. Jumapili wanatakiwa Kanisani na hali hii hujirudia mpaka muhula umalizike. Ikiwa ulidhani watapewa nafasi ya kupumzika wakati wa likizo , umekosea kwa sababu watoto hao huhitajika kuhudhuria shule. Hili limekuwa likiendelea hata baada ya Wizara ya Elimu kupiga marufuku kusomesha wakati wa likizo.

  Wazazi-hasa wale wanaofanya kazi mijini- wamekuwa wakiunga mkono mtindo huu kwa sababu unawaondolea mzigo wa malezi na gharama ya kuwaajiri walezi.

  Wataalamu wanasema matokeo ya hali hii ni watoto wakembe wenye afya na maadili mabaya kutokana na kuchanganyishwa akili na walimu wanaowataka wajue kila kitu wakiwa na umri mdogo.

  Kuwashinikiza watoto wakembe wahudhurie shule na zaidi ya hayo wajue kila kitu kuna madhara mengi. Kwanza kabisa, kuraushwa kwa watoto macheo waende shule kunawanyima fursa ya kulala na kupumzika. Utafiti unaonyesha kuwa watoto wanahitaji kulala na kupumzika kwa zaidi ya saa 12 kwa siku. Hii ina maana kuwa mbali na muda mfupi wanaolala na kupumzika mchana kutwa, watoto wanapaswa kutumia usiku mzima kwa usingizi.

  Hii huwasaidia kukua wakiwa na afya nzuri hasa kiakili. Matokeo ya kuwarausha watoto hao waende shule saa hizo huwafanya wakose furaha mbali na kuwafanya wachanganyikiwe kiakili.

  Pili, kuwalazimisha watoto wakae darasani kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni huwa kunawanyima fursa ya kucheza na kutangamana. Wataalamu wa afya ya watoto wanapendekeza kuwa watoto wachanga wanapaswa kucheza ili viungo vya miili yao kama moyo, akili, mapafu na kadhalika vifanye kazi vizuri.

  Kinyume na watu wazima ambao hufanya kazi nzito nzito na kuwawezesha kufanya mazoezi, watoto huwa hawafanyi kazi hizo. Wazazi na walimu wanapaswa kufahamu kuwa kazi ya watoto ni mchezo na wana kila haki ya kupewa furaha ya kucheza wakiwa shuleni na hata nyumbani.

  Tatu, wazazi wengi ambao hufurahia kuwaachia walimu jukumu la kuwalea watoto wao huku wao wakiwa kazini huwa wanasahau kuwa sio kila mwalimu ana maadili yanayopaswa kuigwa na mwanawe. Ingawa tunawatarajia walimu wawe mifano bora ambayo inaweza kuigwa na kila mtu, ukweli ni kwamba baadhi ya walimu hawajui maana wala hawana maadili. Hatari ni kwamba watoto wakembe husoma kwa kuiga wakubwa wao na ikiwa walimu wanaoshinda nao shule wamepotoka kimaadili, kuna uwezekano mkubwa wa watoto hao kupotoka pia. Hii ndiyo sababu wazazi wengi wamekuwa wakilalamika kuwa wanawao tabia mbaya ambazo hawaelewi zilipotoka.

  Kila mzazi anayejali maisha ya mwanawe anapaswa kutekeleza jukumu lake la kumlea na kumwelekeza jinsi anavyotaka akue. Ni kinaya kuwa wanawatarajia wanawao wawe na tabia na maadili kama yao ilhali hawachukui muda wa kukaa nao na kuwaelekeza.

  Nne, kuwawinda, kuwaamsha, kuwaosha na kuwalazimisha watoto waende shule kila siku hata ingawa hawataki huwa kunawafanya wawe wategemezi wasioweza kujipangia na kutekeleza mambo kivyao. 

  MASWALI.
  1. Ipe taarifa anwani mwafaka. (alama 2) 
  2. Mwandishi anatoa maoni gani kuhusu ratiba ya masomo? (alama 2)
  3. Eleza athari za mfumo wa elimu unaoangaziwa hapa. (alama 3)
  4. Ni ushauri upi unaotolewa kwa wazazi ? (alama 2)
  5. Taja mbinu zozote mbili za lugha alizotumia mwandishi (alama 2)
  6. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika taarifa. (alama 4) 
   1. ‘huwindwa’ kitandani 
   2. Maadili 
   3. Kuwashinikiza… 
   4. Wakembe…
 2. UFUPISHO

  Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yafuatayo. 

  Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kutoka kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo. Ubongo wa mwanadamu hutekeleza shughuli hii kwa namna tatu. Kwanza ubongo hunasa jambo kisha huliihifadhi. Baadaye huanzisha mfumo wa kutoa kilicho hifadhiwa. Ubongo ukiathirika kwa namna yeyote katika moja wapo ya njia hizi, basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika.

  Ingawa inaaminika kuwa uwezo wa kukumbuka hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine, wataalamu wa maswala ya kiakili wanabaini kuwa uwezo huu unaweza kuimarishwa. Uimarishaji huu huhitajika mikakati madhubuti.

  Njia mojawapo ya kustawisha uwezo wa kukumbuka ni kupitia kwa lishe. Vyakula vilivyosheheni vitamini B vyenye amino asidi husaidia kuimarisha uwezo wa kukumbuka. Vyakula kama hivi ni mboga, nyama (hasa maini), bidhaaa za soya, matunda, maziwa, ,bidhaa za ngano, samaki, pamoja na mayai. Vyakula vingine muhimu katika ustawishaji huu ni vile vyenye madini ya chuma. Madini haya huwezesha usambazaji wa hewa katika ubongo kwa wepesi. Vyakula ambavyo vina madina haya ni mboga za kijani, mawele, ndengu, soya, matunda kama maembe, ufuta (simsim) pamoja na nyama, hasa maini na mayai.

  Ubongo wa mwanadamu aliye hai hufanya kazi kila wakati awe macho au amelala. Utendaji kazi wake huendeshwa na glukosi mwilini. Kwa hivyo, vyakula vyenye sukari hii ni muhimu kuliwa. Hata hivyo, lazima mtu awe mwangalifu na kuhakikisha kuwa mwili una kiwango cha sukari kisicho hatarisha maisha. Haya yanawezekana kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mboga na matunda.

  Njia ya pili ni kupiga marufuku vileo kama pombe na nikotini. Vileo hivi huathiri utaratibu wa kunasa, kuhifadhi na kutoa yaliyo ubongoni.

  Iwapo mtu ana tatizo la kuyakumbuka majina ya watu, ni muhimu kufanya mazoezi ya kusikiliza kisha kurudia majina hayo wakati wa mazungumzo. Ni bora kulihusisha jina na sura ya mtu. Kwa njia hii ubongo utanasa jina na kile kinacholengwa.

  Woga na kuvurugika kiakili ni mambo mengine tunayopaswa kuepuka kila wakati. Ni kawaida mtu kupata woga wakati anapokabili jambo asilokuwa na uhakika na matokeo yake kama mtihani au mahojiano. Lakini anapaswa kuwa makini. Woga huo usikiuke mpaka na kumvuruga kiakili. Vurugu hizi huathiri kilichohifadhiwa ubongoni na pia namna ya kukitoa.

  Halikadhalika, mwili wenye siha nzuri huhakikisha kuwa ubongo ni timamu. Wataalamu wengi wa siha wanakubali kuwa na mazoezi ya kunyoosha viungo hustawisha ubongo na hivyo kuhakikisha kuweko kwa uwezo wa kukumbuka mambo. Ni muhimu kuwa na taratibu ya kunyoosha viungo kila wakati. Fauka ya hayo, mazoezi ya kiakili, kama vile kusoma makala yanayovutia, kujaza mraba na michezo mingine kama mafumbo, vitenzi ndimi ni muhimu katika kustawisha uwezo wa kukumbuka.

  Jamii ya watu wenye uwezo kuyakumbuka mambo ni ya jamii iliyopiga hatua kimaendeleo. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuimarisha uwezo wa kukumbuka kila wakati.

  Maswali:
  1. Kwa maneno 60 – 65 fupisha mchango wa chakula katika uimarishaji wa uwezo wa kukumbuka.(alama 6 , 2 mtililiko)

   Matayalisho

   Nakala safi
  2. Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno 80 – 90 (alama 7)

   Matayarisho

   Nakala safi
 3. MATUMIZI YA LUGHA
  1. Andika sifa bainifu za sauti. (alama 2) 
   1. e:- 
   2. n:- .
  2. Eleza maana ya :- (alama 2) 
   1. Kiimbo.
   2. Shadda.
  3. Tunga sentensi moja moja kudhihirisha ngeli zifuatazo:- (alama 2) 
   1. U-U
   2. Pokomo /Pa-ku-mu
  4. Unda kitenzi kimoja kutokana na nomino ‘Mtubia” (alama 2)
  5. Eleza matumizi mawili ya kiambishi ‘ku’ (alama 2)
  6. Tunga sentensi ya maneno manne ambayo ina sehemu zifuatazo. Kielezi cha namna, kivumishi,kitenzi na jina (alama 2)
  7. Yakinisha sentensi ifuatayo; (alama 2)

   Mvua haijanyesha vizuri msimu huu.
  8. Onyesha matumizi mawili mawili ya alama zifuatazo:- (alama 2) 
   1. Alama ya mshangao
   2. Mshazari
  9. Tunga sentensi sahihi ukitumia –wa- katika kauli ya kutendeana (alama 2)
  10. Andika udogo wa sentensi:- (alama 2) 
   Ndama wa ng’ombe yule ameuzwa.
  11. Onyesha tofauti ya vitate vifuatavyo kwakuvitungia sentensi (alama 2) 
   1. Dhamani
   2. Thamani
  12. Kanusha sentensi ifuatayo katika wingi (alama 2) Ningalikuwa na pesa ningalinunua gari
  13. Tumia neno “shujaa” katika sentensi kama:- (alama 2) 
   1. Kivumishi
   2. Kielezi.
  14. Huku ukitumia mifano mwafaka, eleza tofauti ya sentensi sahili na ambatano (alama 4)
  15. Onyesha aina za viambishi katika sentensi hii: (alama 2) Nitajisomea
  16. Andika katika usemi wa taarifa:- (alama 2) Tutaanza mashindano kesho, Mwalimu alimwambia mwanafunzi.
  17. Eleza maana mbili ya sentensi:- (alama 2) 
   Tumetengeneza barabara
  18. Tumia mifano mwafaka kueleza aina za mofimu (alama 2)
  19. Changanua kwa njia ya mishale
   Mama analima shambani.
 4. ISIMU JAMII 

  Soma mzungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali :

  A : Ohh, dada Naomi
  B : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!
  A: Asifiwe sana
  B: Ehh dadangu, miezi ...mingi...sijakuona
  A: dada wee...Nilitumwa huko kusini ...Kuwahubiria watu injili (mtuo mdogo)singeweza kukata...
  B: Ehh, usiwe kama Yona
  A: Habari ya siku nyingi?
  B; Nzuri Mungu bado ameendelea kunibariki
  A: Amen!
  B: Nimeendelea kuiona neema yake
  A: Amen! Asifiwe Bwana
  B: Halleluya
  A: Ni Mungu wa miujiza!
  B: Amen. Hata nami nimeona neema yake
  Bado niko imara katika wokovu katika siku hizi za mwisho
  A: Amen !
  B: Ni Mungu wa ajabu kweli !
  A: Nilikumbana na matatizo lakini nikategemea sala
  Kama Paulo na sila… Na nikashinda (anatua). Sikuweza kumpa shetani nafasi…maana ameshindwa
  B: Ameshindwa kabisa

  Maswali:- 
  1. Hii ni sajili ya wapi ? Fafanua [alama 2]
  2. Taja na ueleze sifa za sajili hii [alama 6]
  3. Taja mambo mawili muhimu yaliyosaidia katika maenezi ya Kiswahili Afrika mashariki na kati. [Alama 2]

USAHIHISHO

 1. UFAHAMU
  1.  
   • Sera ya elimu na athari zake
   • Sera ya kusimamia elimu iwepo
   • Mfumo hasi wa elimu
   • Masomo ya ziada  
    *Mada ilenge Elimu ;maneno yasizidi 6
   • Ina dosari/dosari
   • Haiwapi wanafunzi muda wa kutosha wa kula,kucheza,kupumzika na hata kuchunguza afya na usalama  wao  
  2.  
   • Watoto kukosa maadili mema `
   • Watoto kukosa furaha na kuchanganyikiwa akili .
   • Watoto kukosa nafasi ya kucheza na kutangamana hivyo kuathiri viungo vya miili yao kama  moyo,mapafu na akili.
   • Watoto kuwa wategemezi wasioweza kujipangia na kutekeleza mambo kivyao. 
   • Wazazi kutotekeleza majukumu yao ya kuwalea na kuwaelekeza watoto kwani mfumo huu huwaondolea  mzigo wa malezi na gharama ya kuwaajiri walezi.
   • Wanapaswa kutekeleza majukumu yao ya kuwalea na kuwaelekeza wanao jinsi wanavyotaka wawe.
   • Wawashinikize wanao wahudhurie shule maana kutawafanya wawe wategemezi wasioweza kujipangia  na kutekeleza mambo kivyao
  3.  
   1. Tashhisi - kufukuza ratiba.
   2. Msemo  – Wakiunga mkono
                - Kupiga marufuku
   3. Takriri –Kazi nzito nzito 2*2
  4.  
   1. - Huwindwa kitandani
    -Kuondolewa kitandani/usingizini bila ana yeondolewa kupenda
    -Kulazimishwa kuamka
   2. Maadili-  Tabia njema /matendo mema
   3. Kuwashinikiza - Kuwalazimisha /kuwashurutisha
   4. Wakembe-Wadogo/wachanga


 2. UFUPISHO
  1. Vyakula vyenye vitamini B, vyenye amino asidi na vile vyenye madini ya chuma kuimarisha uwezo wa kukumbuka.
   - Vyakula vyenye glukosi husaidia kuendesha viungu vya mwili na ubongo. Lakini mtu anatakiwa kutahadhari asizidishe kiwango cha sukari mwilini, kwani kinaweza kuthiri uwezo huu.
   - Ni muhimi kutotumia  vileo na vyakula vyenye nikotini kwani huzorotesha uwezo wa kukumbuka (Kila hoja na maelezo al. 2 na mbili za mtiririko).
  2. Ni muhimu kuepuka woga na kuvurugika akili kulikozidi haya huathiri uwezo wa kukumbuka. 

   Halikadhalika, lazima mtu awe na ratiba kuonyesha viungo. Hili ni kwa kuwa unyooshaji wa  viungo huimarisha ubongo pamoja na uwezo huu. Uimarishaji wa uweza huu ni muhimu kwa   maendeleo ya jamii na unahitaji mchango wa kila mmoja kila wakati.
 3. MATUMIZI YA LUGHA
  1.  
   1. e – Irabu ya mbele – hutamkwa kutumia sehemu ya mbele ya ulimi
    - Irabu ya midomo – hutamkwa midomo ikiwa imetandazwa
   2.  n – sauti ya ufizi
    - Nazali
  2.  
   1. Kiimbo – Ni upandaji na ushukaji wa sauti unaofanyika wakati mtu anapozungumza 
   2. Shadda – Ni mkazo katika nenoau maneno
  3.  
   1. U – U – Nomino za dhaharia zitumiwe    
   2. Pokomo/ Pakumu k.m Mahali humu ndimo alimoingia
  4. Tubu
  5.  - Kudhihirisha vitenzi vya silabi moja – kula, kuja n.k
   • Mwanzo wa vitenzi
   • Wakati wa ukanusho k.m haku, hatuku……
   • Kuonyesha mahali k.m kuliko na miti
   • Kiwakilishi cha nafsi k.m anakuita
  6. Mfano: Msichana yule anasoma barabara
  7. hakiki majibu ya wanafunzi
  8.  
   1. Mshangao
    • Kuonyesha hisia
    • Kuamrisha
    • Kutahadharisha/ kuonya
   2. Mshazari
    • Katika uandishi wa kumbu 2 
    • Kuonyesha maneno Fulani yana maana sawa
    • Kuonyesha ‘au’
  9. Mfano: majirani waliwiana radhi baada ya utesi wa siku nyingi  
  10. Kijdama cha kijigombe kile kimeuzwa
  11.  
   1. Dhamani – mwezi wa mwisho wa kusi (demani)
   2. Thamani – Gharama / ubora wa kitu/ bei
  12. Tusingalikuwa na pesa tuingalinunua magari
  13. hakiki majibu ya wanafunzi
  14. Sahili – sentensi ya wazo moja/ kitenzi kimoja
   Ambatani – sentensi mbili au zaidi zilizounganishwa
  15. Ni-ta-ji   ----- awali
   som—mzizi
   e-a------tamati
  16. Mwalimu alimwambia mwanafunzi kuwa wangeaza masshindano kesho yake/ siku itakayofuata 
  17. – Njia
   - Vizuri/ mwafaka/ sawasawa
  18. Mofimu huru
   Mofimu tegemezi 
  19. S → KN  +  KT
   KN  →  N   
   N    → Mama
   KT  →  T  +  E
   T    →  Analima 
   E    →  shambani
 4. ISIMU JAMII
  1. Sehemu za kuabudu/ ibada / mzungumzo ya Kristo
  2.  
   • Matumizi ya lugha iliyojaa upole/ unyenyekevu
   • Msamiati maalum unaohusiana na dini Fulani. Kwa mfano ‚Yesu“ okoka, ‚
    Mungu asifiwe’ ‚  Halleluya, ‚ Amen’ dini ya kikikristo
   • Huweza kuwapo matumizi ya maneo au makuu kutoka kwa Bibilia m.f. usiwe kama Yona, Paulo na Si
   • Huwepo matumizi ya msamiati ambao unaeleweka tu katika muktadha huo wa mazingira yanayohusika tu. Mungu anaendelea kunibariki. ‚Amen“
   • Lugha haina matumizi ya misimu au hata lugha inayoonekana kama isiyozingatia adabu;  huwa  lugha yenye tasfida
   • Majina yanayofungamana na ibada inayohusika, injili, sala, Mungu, Bwana asifiwe
   • Matamshi au lafudhi ya utamkaji wa maneno kutegemea mazingira fulani ya ki-ibada         
  3.  
   • Dini
   • Biashara    
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Karatasi ya 2 Form 3 Questions and Answers - End Term 2 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest