Kiswahili Paper 1 Form 3 Questions and Answers - Term 3 Opener Exams 2021

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Andika insha mbili.
  • Insha ya kwanza ni lazima.
  • Chagua insha nyingine moja kutoka kwa tatu zilizobaki.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ina alama 20.

MASWALI

  1. Umepata habari kwamba binamu wako anayeishi Ujerumani ameanza kutumia mihadarati. Mwandikie barua ukimweleza kuhusu athari hasi za tabia hiyo.
  2. Ufisadi umekuwa tatizo sugu nchini. Jadili vyanzo vyake na upendekeze suluhu kwa uovu huo.
  3. Pang’okapo jino pana pengo.
  4. Tunga kisa kitakachoanza kwa maneno yafuatayo; Buum! Mlipuko huo ulitapakaza vifuzi kote.Wingu jeusi la moshi lilitanda..............

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. Barua
    1.  
      • Zingatia mtindo wa kuandika barua ya kirafiki
      • Anwani za mwandishi / tarehe
      • Matini/ mwili
      • Kimalizio
      • Jina la mwandishi.
    2. Mwandishi azingatie lugha ya kiwango cha juu, matumizi bora ya tamathali kama istiari, methali, semi na kadhalika.
    3.      
      • Zingatia maudhui , kama vile:
      • Kupoteza makini katika utelelzaji wa mambo
      • Husababisha uraibu
      • Huathiri uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi
      • Husababisha magonjwa ya mapafu na maini
      • muhimu sizipungue tano.
      • Husababisha matatizo ya yanayohusiana na kuona
      • Husababisha matumizi mabaya ya pesa
      • Hufanya mtu kuwa mkorofi na kutotii sheria
      • Husababisha vifo
      • Huvuruga utaratibu wa masomo
    4. Idadi ya maneno iwe kama ilivyotolewa katika maagizo.
  2. Ufisadi umekuwa tatizo sugu nchini. Jadili vyanzo vyake na upendekeze suluhu kwa uovu huo.
    • Tamaa – Hali ya kutaka kujilimbikizia mali nyingi.
      Suluhu ni kuwashauri au na kuwaonya wafanya kazi dhidi ya tamaa.
    • Mshahara duni – Wafanya kazi kupewa mshahara usiolingana na ujuzi wao.
      Suluhu ni kuwapa wafanya kazi mshahara unaofaa.
    • Kutofuata sheria – Wananchi kuvunja sheria na kisha kutafuta njia ya mkato kujitoa shidani.
      Suluhu ni kuhakikisha wanaovunja sheria wanaadhibiwa mara moja.
    • Uongozi mbaya – Viongozi hawafanyi lolote kuondoa ufisadi.
      Suluhu ni kuwachagua viongozi wanaojitoa kupigana dhidi ya ufisadi.
    • Mapendeleo – Kuna wale ambao wanapendelea wenzao wanaojuana nao.
      Suluhu ni kuondoa mapendeleo katika jamii.
    • Ukabila – Wengine wanapendelea watu wa makabila yao.
      Suluhu ni kuhakikisha ukabila umeondolewa nchini.
    • Matumizi mabaya ya mamlaka – Kuna wale wanaotumia mamlaka yao vibaya.
      Suluhu ni kuwafanya wale walio mamlakani watumie vizuri bila mapendeleo.
    • Kutoajibika kwa idara za mahakama
      Suluhu niMabadiliko katika idra za mahakama na kuwachukulia hatua kali maafisa wanaohusika.
  3. Pang’okapo jino pana pengo.
    Kisa kidhihirishe maana;
    1. Kung’oka kwa jino-jinsi mtu alivyotoweka /kufa
    2. Pengo – shida/madhila/dhiki zilizowakumba waliobaki
      Ni kawaida kuwa jino lingokapo hubakia pengo
      Hii ni methali ambayo hutumiwa kupigia mfano, mahali apoondoka au kufariki kiongozi wake, mahali hapo huwa na upungufu fulani.
      Mtahiniwa asimulie kisa kinachoashiria kuondoka kwa mtu (kiongozi) mahali fulani aliposhikilia wadhifa au kazi fulani muhimu na nafasi hiyo kubakia wazi.
      Pengo hili aidha laweza kuwa lililoachwa na baba au mama mzazi
      Aonyeshe upekee wa mhusika huyu na namna alivyokuwa tegemeo kwa wengi
      Aonyeshe namna kuondoka kwa huyu aliyetegemewa kunaishia kufungua gharika la madhila kwa jamii hii iliyomtegemea
      Kwa vyovyote vile, kisa kilenge kubaini shida zilizowakumba waliobaki kutokana na pengo lililobaki.
      Ruwaza zifuatazo zinaweza kujitokeza;
      1. Mzazi(baba au mama au wote) kufariki na kuwaacha watoto na kukosa mwelekezi au mlezi
      2. Mlezi kuondoka /kuaga na kuwaacha waliomtegemea wakihangaika kwa kukosa ; chakula,karo ya shule na mahitaji mengine
      3. Wazazi kutalikiana na hivyo familia kusambaratika na kuacha watoto bila mwangalizi, watoto kukosa mahitaji ya kimsingi kama vile elimu, chakula na ikizidi ushauri/uelekezi
      4. Kiongozi wa kidini au kisiasa kungatuka uongozini na kumpisha kiongozi mwingine ambaye kwa kiasi fulani hawezi kulinganishwa na mtangulizi wake, kimaendeleo.
      5. Meneja wa kampuni kung’atuka na kuacha kampuni chini ya usimamizi duni na hatimaye kampuni hiyo kusambaratika
      6. Mwalimu kustaafu na kuacha shule mikononi mwa mwalimu mkuu mwingine na ambaye anakosa kuwajibika kiusimamizi, hatimaye shule inadorora kimatokeo.
  4. Andika insha itakayoanza kwa maneno haya;
    Buum! Mlipuko huo ulitapakaza vifuzi kote.Wingu jeusi la moshi lilitanda.............
    • Hii ni insha ya mdokezo
    • Kisa kioane na mdokezo uliotolewa.
    • Insha iwe ya kusisimua na kuteka hisia kwa taharuki na hisia mwafaka.
    • Insha ya kukadiriwa.
      Tanbihi
      Mtahiniwa azingatie yafuatayo kuhusiana na urefu.
      1. Robo – 05/20 (upeo)
      2. Nusu – 10/20 (upeo)
      3. Robo tatu – 15/20 (upeo)

                            

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Form 3 Questions and Answers - Term 3 Opener Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest