Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 End Term 3 Exams 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI 102/1
INSHA
KARATASI YA 1
KIDATO CHA TATU

MAAGIZO:

  • Andika Insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobaki.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ina alama 20.

MASWALI:

  1. Wewe ni katibu wa kamati ya maslahi ya klabu ya wasanii chipukizi mtaa wa Rehema.
    Andika kumbukumbu za mkutano uliofanywa hivi karibuni kujadili suala la usalama uliozorota.
  2. Mfumo wa elimu nchini Kenya una kasoro nyingi na unafaa kufanyiwa mabadiliko. Eleza.
  3. Andika kisa kinachodhihirisha maana ya methali: Ujana ni moshi ukienda haurudi.
  4. Tunga kisa kinachomalizika kwa maneno haya: ‘……. Hapo ndipo iliponipambazukia kuwa
    nilikuwa naogelea baharini pekee, kinyume na wenzangu wote.


MAAKIZO:

  1. Wewe ni katibu wa kamati ya maslahi ya klabu ya wasanii chipukizi mtaa wa Rehema.
    Andika kumbukumbu za mkutano uliofanywa hivi karibuni kujadili suala la usalama uliozorota.
    • Hii ni insha ya kiuamilifu
    • Sura ya kumbukumbu izingatiwe:
      1. Kuwe na anwani iliyo na mahali, tarehe na saa ya kufanyika kwa mkutano
      2. Orodha ya waliohudhuria
      3. Waliotumia udhuru
      4. Waliokosa kutuma udhuru
      5. Waalikwa wengine (wageni)
      6. Ajenda
    • Maudhui yagusie yafuatayo:-
      1. Visa vya kuzorota kwa usalama kama vile ujangili, utekaji nyara, ujambazi, dhuluma mbalimbali kwa umma, uhalifu mtaani, mauaji, ubakaji, wizi km wa mifugo na mali ya watu
      2. Ataje wahasiriwa au wahusika
      3. Hatua za kudhibiti usalama k.v. mpango wa nyumba kumi.
  2. Mfumo wa elimu nchini Kenya una kasoro nyingi na unafaa kufanyiwa mabadiliko. Eleza.
    • Insha hii ina upande mmoja wa hoja. Mwanafunzi apendekeze kwa kutoa maelezo kwa nini mfumo wa elimu unafaa kufanyiwa mabadiliko.
      Hoja zinazopendekezwa:-
      1. Masomo mengi hufanyikia darasani badala ya hali halisi maishani km viwandani, shambani au biasharani.
      2. Wanafunzi hawana muda wa kutosha kupumzika kwa kuwa masomo ni mengi
      3. Karo inayolipwa ni ya juu sana na wanafunzi maskini hawawezi kuimudu.
      4. Elimu ya sasa haizingatii maadili ya kiafrika bali huegemea maadili ya kizungu km kazi za ofisi, mavazi, vyakula, lugha.
      5. Shuleni wanafunzi ni wengi na kuwafikia kila mmoja ni vigumu haswa katika shule za umma.
      6. Masomo ya sayansi hayafanywi vizuri na idadi kubwa ya wanafunzi.
      7. Watoto wengi wanfikia drasa la nane bila uwezo wa kujieleza kwa kuandika na kuzungumza.
      8. Elimu ya sasa haizingatii mahitaji ya jamii tofauti km wafugaji, wakulima, wavuvi, walemavu na wanaoishi vibandani.
      9. Wanafunzi walio na vipawa na uwezo wa kipekee hawatiliwi maanani km wakimbiaji na walio werevu zaidi au wasioelewa kwa haraka.
  3. Andika kisa kinachodhihirisha maana ya methali: Ujana ni moshi ukienda haurudi.
    • Methali hii inatufunza kwamba jambo likishapita halirudi tena. Ni sawa na methali isemayo maji yakimwagika hayazoleki.
    • Inatufunza kuwa iwapo tutapima mambo fulani maishani ambayo tunapaswa kuyatekeleza ili tunufaike maishani, tutajuta bila lolote la kufanya.
    • Mwanafunzi azingatie kisa kinachoonyesha ukweli wa methali hii.
    • Kisa kinaweza kuwa cha mtu asiyezingatia mashauri.
      1. Kusoma kwa bidii ili afaulu mtihani
      2. Kujihusisha mihadarati na baadaye kujutia madhara yake.
      3. Kijana anayeonywa na wakubwa wake aachane na vijana wapotovu lakini anapuuza.
      4. Kijana anayejihusisha na mapenzi kiholela na baadaye kupata maradhi ya zinaa au mimba za mapema.
    • Tanbihi
      • Kisa kisichooana na methali hii apewe alama 3
  4. Tunga kisa kinachomalizika kwa maneno haya: ‘……. Hapo ndipo iliponipambazukia kuwa nilikuwa naogelea baharini pekee, kinyume na wenzangu wote.
    1. Kisa lazima kimaliziwe na maneno ‘aliyopewa bila kutoa au kuongezea neno lolote.
    2. Pawe na mantiki ya kisa na maneno aliyopewa.
    3. Mnenaji asawiriwe akingangania kufanya jambo walipopatana na wenzake.
    4. Wenzake hawafanyi lile
    5. Ndiye tu anaye endelea na jambo hilo.
      • Tanbihi
        • Mtahiniwa asipomalizia maneno hayo amepotoka. Atuzwe alama 2.
        • Atachukuliwa kuwa alijitungia swali lake mwenyewe.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 End Term 3 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest