Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 End Term 3 Exams 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KIDATO CHA TATU
MUHULA WA TATU 

SEHEMU A.UFAHAMU (ALAMA 15)

Soma makala yafuatayo kisha kisha ujibu maswali:-

Waajiri wengi wanazilaumu taasisi za elimu kwa kukosa kutoa wafanya kazi wenye ujuzi tosha, hasa wa kiteknolojia za kisasa kama kutumia kompyuta kutenda kazi mbalimbali. Hali hii imekuwa ya kuhuzunisha sana.

Ujuzi wa kuweza kutumia Kompyuta unaweza kumfaa mwanafunzi hata anapokosa nafasi ya kujiunga na chuo kikuu kwa vile anaweza kuendelea na elimu yake kupitia kwa elimu mtandao. Pia anaweza kufanya utafiti wa kina kupitia intaneti na kwa njia hii akaimarisha elimu yake.

Mojawapo ya njia ya kuimarisha elimu kuhusu maswala ya teknolojia ni kuanzishwa kwa mikakati mipya ya kufunza. Somo la Kompyuta laweza kuimarika mashuleni endapo kwanza walimu watahamasishwa juu ya faida za ujuzi huu.

Kwa kutumia Kompyuta kufunza, walimu wanaweza kufunza madarasa kadhaa katika kipindi kimoja bila kulazimika kuyahudhuria. Hii itapunguza kiwango cha kazi kwa walimu kwa vile watapata muda wa kufanya utafiti mpana. Aidha, watapata habari na ufahamu zaidi wa mambo kwa kutumia mitambo ya Kompyuta kutoka kwenye intaneti, kupitia tovuti.

Hata hivyo mipango hii inakabiliwa na changamoto kama vile bei za juu za mitambo na vifaa vya Kompyuta, ukosefu wa miundo msingi itakayowezesha utumiaji wa mitambo hii na ukosefu wa walimu waliohitimu somo la Kompyuta.

Pia, kuna tatizo la ukosefu wa nguvu za umeme hasa maeneo ya mashambani; vile vile, katika maeneo yaya haya, wanafunzi na wazazi wengi huvichukulia somo la Kompyuta kuwa gumu na linalofaa wakaazi na wanafunzi kutoka maeneo ya mijini na linalofaa wakaazi muhimu kwao mashambani.

Maswali

  1. Ipe taarifa uliyoisoma anwani inayoifaa AL.2
  2.  “Hali hii imekuwa ya kuhuzunisha.” Ni hali gani inayozungumziwa katika aya ya ? AL.2
  3. Ujuzi wa kutumia Kompyuta unaweza kumfaidi vipi mwanafunzi? AL.4
  4. Mikakati mipya ya kuimarisha elimu kuhusu maswala ya teknolojia inakabiliwa na vizingiti vipi? AL.3
  5. Taja manufaa mawili ambayo mwalimu anaweza kupata kutokana na ujuzi wa teknolojia ya Kompyuta AL.2
  6. Andika msamiati mwafaka zaidi kwa maneno yafuatayo: AL.2
    1. Kompyuta
    2. Intaneti

SEHEMU B.UFUPISHO ( ALAMA 15)

Soma taarifa hii kisha ujibu maswali

Umaskini ni tatizo sugu katika jamii. Binadamu wengi hujikuta katika hali hii kwa sababu hawakubahatika kusoma. Baadhi yao huenda walijaribu kusoma wakashindwa mapema kujipandisha kielimu. Ukosaji wa elimu huchangia sana katika kukuza ukata. Elimu huweza mtu kupata tonge kwa kujipatia kazi za kumwezesha kuyakidhi mahitaji ya maisha. Hali kadhalika, elimu humsaidia binadamu kupata maarifa mengi ya kutendea shughuli zake za kimaendeleo. Kwa mfano, kama ni wakulima wanaweza kutumia pembejeo zifaazo ili kuboresha uzalishaji wa mazao. Wakulima wenye elimu hawatapendelea njia duni za kuendeleza kilimo kama vile kutumia visagilima na mbinu nyingine za kijadi. Badala yake watatumia njia za kisasa za kuvunia mazao yao.

Umaskini mwingine huwa mwiba wa kujichoma. Baadhi ya watu ni mikunguni. Kulaza damu kwao kunawafanya kuwa wategemezi katika familia na jamii kwa jumla. Kwa vile hawajazoea kuinamia cha mvunguni, hata wakifunzwa kuchakura hawawezi. Ili kujaribu kuutibu uwele wao na ufukara baadhi yao hutafuta njia za mkato kama vile upwekuzi wa vitu vya wale waliojitahidi. Wakifanikiwa huweza kufurisha vibindo vyao. Hata hivyo mkono mrefu wa walinda usalama ukiwakumbatia wao hubakia kusagika kwa dhiki isiyomithilika ndani ya magereza.

Majanga ya kimaumbile kama vile mitetemeko ya ardhi, mikurupuko ya maradhi hatari, moto, ukame na mafuriko huchangia na kuzidisha umaskini. Matukio hayo yakiandama kidindia watu wengi huhasirika. Licha ya mali nyingi kupotea, manusura huachwa wakiwa maskini hohehahe. Matumizi yao hupotea kwani wengi huhitajika kuanza maisha upya.

Vijana ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote ile. Endapo watajiingiza katika uraibu wa dawa za kulevya, wataathirika wao wenyewe na jamii kwa jumla. Pamoja na kuwa vijana hawa hufuja pesa nyingi katika ununuzi wa dawa hizi, dawa zenyewe huwadhoofisha na kuwapoka nguvu za kushiriki katika uzalishaji mali. Kutokana na hali hii,umaskini hupaliliwa na kushamiri zaidi.
Umaskini huzua matatizo mbalimbali katika jamii. Ufukara huchachawiza juhudi za serikali za kuwapa raia wake mahitaji ya kimsingi kama vile huduma za afya. Pia umaskini husababisha maovu mbalimbali ya kijamii kama vile mauaji na ukahaba.

Baadhi ya wanajamii huona kwamba njia ya kipekee ya kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na hali ya ulitima ni kupitia kwa biashara haramu. Hali hii huchochea zaidi kudorora kwa maadili ya kijamii.

Mataifa mbalimbali ulimwenguni yamezua mikakati mahsusi ya kukabiliana na umaskini. Baadhi ya mataifa yamebuni utaratibu maalum wa kupunguza mwanya mkubwa uliopo kati ya matajiri na maskini. Mojawapo ya mipango hiyo ni kupandisha viwango vya kodi inayotozwa wenye mishahara minono na wafanyibiashara wenye pato kubwa. Aidha huduma za burudani hutozwa kodi ya kiwango cha juu. Kupitia kwa kodi hizo, na njia nyinginezo, serikali za nchi hizo hupata pesa za kuwahudumia maskini.
Mataifa yanayoendelea yanaweza kuwakwamua wananchi kiuchumi kwa kuwapa wahitaji mitaji ya kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo. Mifano ya miradi hiyo ni viwanda vya ‘Jua kali’, ususi wa vikapu na uchongaji wa vinyago. Hali kadhalika, serikali inaweza kuwatafutia masoko ya nje wafanyi biashara wadogo wadogo. Aidha, serikali inaweza kupunguza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa na masoko ya nje wafanyibiashara wa aina hiyo. Mathalan, ushuru unaotozwa nguo kuukuu zinazoingizwa nchini ukipunguzwa, wauzaji wa nguo hizi watafaidika zaidi na hali ya umaskini itaendelea kupungua.

Sehemu za mashambani ni mhimili mkubwa wa uchumi. Ingawa kumekuwa na juhudi za kuzistawisha sehemu hizi kwa kusambaza huduma za umeme na maji kwa gharama nafuu, bado hali haijawa ya kuridhirisha. Ili kuimarisha sehemu hizi na kukabiliana vilivyo na tatizo la umaskini, hatuna budi kusambaza huduma hizi hasa katika sehemu kame. Sehemu hizi zikipata maji, kilimo chenye natija kitaendelezwa na umaskini utakuwa karibu kuzikwa katika kaburi la sahau. Ikiwa tutazitekeleza sehemu hizi, vijana wanaoweza kusistawisha watahamia mjini kutafuta maisha ‘bora’. Hali hii itazidisha msongomano wa watu mjini.

Umaskini ni nduli ambaye lazima aangamizwe ima fa ima. Vijana hawana budi kubadili mtazamo wao hasa kuhusu kazi za mashambani na kujitahidi kuimarisha kilimo. Fauka ya hayo, mifumo mwafaka ya elimu ibuniwe ili kukidhi mahitaji ya kiuchumi ya taifa. Badala ya kuhimiza elimu ya kinadharia, elimu tekelezi isisitizwe zaidi ili wale wanaokosa kazi za kiafisi waweze kujiajiri katika kazi za kiufundi. Ukusanyaji wa ushuru uimarishwe zaidi. Hali ya usalama iendelee kustawishwa ili kuzidi kuwavutia wawekezaji, na hivyo kubuni nafasi zaidi za kazi.

Maswali

  1. Kulingana na kifungu ‘umasikini ni hali inayoletwa na udhaifu wa mtu binafsi’. Jadili (maneno 30-40) AL.7
    MATAYARISHO

    NAKALA SAFI

  2. Jamii ina uwezo wa kukabiliana na hali ya umaskini inayowakumba raia wake. Thibitisha kwa mujibu wa kifungu (maneno 40-50) AL.8
    MATAYARISHO

    NAKALA SAFI

SEHEMU C.MATUMIZI YA LUGHA: (ALAMA 40)

  1. Eleza sifa za sauti /ch/ (alama 2)
  2. Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia kirejeshi “O”. (alama 2)
    • Mtoto anayelia huchapwa
  3. Pambanua viungo vya kisarufi katika neno lifuatalo. (alama 3)
    • Tuliwalimia
  4. Tunga sentensi ukitumia neno mzee kama: (alama 2)
    1. Kivumishi
    2. Kielezi
  5. Jaza mapengo. (alama 3)
    Kutenda  Kutendewa 
     Pa  
     Cha  
     Nya  
  6. Eleza maana ya misemo ifuatayo. (alama 2)
    1. Giza la ukata 
    2. Meza mate machungu 
  7. Bainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
    • Maksundi alimjengea Tamari nyumba kwa matofali mazuri.
  8. Nomino zifuatazo zinapatikana katika ngeli gani? (alama 2)
    1. Topasi
    2. Kambare 
  9. Andika sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo. (alama 2)
    • Mizizi ya mibaruti hii iliwaponya watu ambao walikuwa na shida kama hii yenu 
      (kanusha kwa umoja).
  10. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia kielelezo matawi. (alama 4)
    • Mwizi aliyetuibia jana amekamatwa hatimaye.
  11. Tunga sentensi yenye masharti yafuatayo. (alama 3)
    1. Kiima
    2. kiarifu
    3. chagizo
  12. Andika sentensi ifuatayo kwa ukubwa huku ukikanusha. (alama 3)
    • Kijibwa chake ni kikali
  13. Jaza neno ambalo ni kinyume cha lile lililopigwa mstari katika sentensi. (alama 2)
    1. Vile vitu ulivyovichanganya itakubidi 
    2. Bomba hili limeziba mwite fundi aweze 
  14. Andika katika usemi halisi. (alama 3)
    1. Mama aliwahimiza warudi siku hiyo la sivyo wangekosa tuzo.
  15. Tambulisha kishazi tegemezi na kishazi huru. (alama 2)
    1. Wanafunzi waliofanya vyema walituzwa jana
  16. Kamilisha methali ifuatayo. (alama 2)
    • Jitihada za mja

SEHEMU D.ISIMU JAMII (ALAMA 10)

A : Ingia 46! Adams mbao Kenyatta, railways beba! 46 Adams mbao kenyatta, railways!
B : Namba nane ngapi?
A : Mbao ingia, blue.
B : Nina hashuu.
A : Blue Auntie.
B : Sina.
A : Ingia. 46 Adams mbao, kenyatta railways gari bebabeba.
C : Mimi sinako shirini. Chukuako tu kumi.
A : Dinga inakunywanga petrol mzee.
C : Kumi mingi.
A : Haaya ingia twende. Driver imeshona twende.

Maswali

  1. Eleza muktadha wa mazungumzo haya AL.2
  2. Taja sifa nane za lugha inayotumika katika sajili hii AL.8


MAAKIZO

SEHEMU C: MATUMIZI YA LUGHA

  1. Eleza sifa za sauti /ch/
    • ni konsonanti
    • Hutamkiwa kwenye kaakaa gumu
    • Ni sauti hafifu
    • Ni kizuio – kwamizo 4 x ½ = 2
  2. Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia kirejeshi “O”.
    • Mtoto anayelia huchapwa
      • Mtoto aliaye huchapwa 2 x 1
  3. Pambanua viungo vya kisarufi katika neno lifuatalo.
    • Tuliwalimia
      • Tu – nafsi ya kwanza wingi
      • Li – wakati uliopita
      • wa – watendwa
      • lim – mzizi
      • i - kauli ya kutendea
      • a - kiishio 6 x ½ = 3
  4. Tunga sentensi ukitumia neno mzee kama:
    1. Kivumishi
      • Mkulima mzee alipata mavuno mengi
    2. Kielezi
      • Juma aliifanya kazi ile kizee 2 x 1
  5. Jaza mapengo.
    Kutenda  Kutendewa 
     Pa  Pewa
     Cha  chiwa
     Nya  nyika/nyeka
  6. Eleza maana ya misemo ifuatayo.
    1. Giza la ukata – Hali ya umaskini
    2. Meza mate machungu – Vumilia shida/taabu
  7. Bainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo.
    • Maksundi alimjengea Tamari nyumba kwa matofali mazuri.
      • Kitondo kipozi Ala 3 x 1
  8. Nomino zifuatazo zinapatikana katika ngeli gani?
    • Topasi – A - WA
    • Kambare – A -WA
  9. Andika sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo.
    • Mizili ya mibaruti hii iliwaponya watu ambao walikuwa na shida kama hii yenu
      (kanusha kwa umoja).
      • Mzizi wa mbaruti huu haukumponya mtu ambaye alikuwa na shida kama hii yako
  10. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia kielelezo matawi.
    • Mwizi aliyetuibia jana amekamatwa hatimaye.
      kisspp2
  11. Tunga sentensi yenye masharti yafuatayo.
    1. Kiima
    2. kiarifu
    3. chagizo
      • Kijana amekatwa vibaya 3 x 1
      • Kiima kiarifu chagizo
  12. Andika sentensi ifuatayo kwa ukubwa huku ukikanusha.
    • Kijibwa chake ni kikali
      • Jibwa langu si kali sana 3 x 1
  13. Jaza neno ambalo ni kinyume cha lile lililopigwa mstari katika sentensi.
    1. Vile vitu ulivyovichanganya itakubidi - Vichanganue
    2. Bomba hili limeziba mwite fundi aweze - Zibua
  14. Andika katika usemi halisi.
    • Mama aliwahimiza warudi siku hiyo la sivyo wangekosa tuzo.
      • “Harakisheni mrudi leo, la sivyo mtakosa tuzo,” mama alisema. 6 x ½
  15. Tambulisha kishazi tegemezi na kishazi huru.
    • Huru – wanafunzi walifunzwa jana
    • Tegemezi – Waliofanya vyema
    • Wanafunzi waliofanya vyema, kishazi tegemezi
    • Walituzwa jana kishazi huru (2 x 1
  16. Kamilisha methali ifuatayo.
    • Jitihada za mja- haziondoi kudura ya Mungu

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 End Term 3 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest