Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - End Term 3 Exams 2021

Share via Whatsapp


KISWAHILI FASIHI 102/3

KARATASI YA 3
KIDATO CHA TATU

MAAGIZO:
Jibu maswali yote kwenye nakala ulizopewa.

  1. Ushairi
    • SHAIRI ‘A’.
      Umekata mti mtima
      Umeangukia nyumba yako
      Umeziba mto hasira
      Nyumba yako sasa mafurikoni
      Na utahama
      Watoto Wakukimbia

      Mbuzi kumkaribia chui
      Alijigeuza Panya
      Akalia kulikuwa na paka
      Kichwani
      Mchawi kutaka sana kutisha
      Alijigeuza Simba
      Akalia na risasi kichwani

      Jongoo kutaka sana kukimbia
      Aliomba miguu elfu
      Akaachwa na nyoka

      Hadija wapi sasa yatakwenda
      Bwanako kumpa sumu ?
      Hadija umeshika nyoka kwa mkia
      Hadija umepitia nyuma ya punda

    • SHAIRI ‘B’
      Piteni jamani, Piteni haraka
      Nendeni, nendeni huko mwendako
      Mimi haraka, haraka sina
      Mzigo wangu, mzigo mzito mno
      Na chini sitaki kuweka

      Vijana kwa nini hampiti ?
      Kwa nini mwanicheka kisogo ?
      Mzigo niliobeba haupo.

      Lakini umenipinda ngongo na
      Nendako
      Haya piteni ! Piteni haraka ! Heei !

      Mwafikiri mwaniacha nyuma !
      Njia ya maisha ni moja tu.
      Huko mwendako ndiko nilikotoka

      Na nilipofikia wengi wenu
      Hawatafika.

      Kula nimekula na sasa mwasema
      Niko nyuma ya wakati
      Lakini kama mungepita mbele
      Na uso wangu kutazama
      Ningewambia siti miaka
      Mingi.

      Maswali
      1. Haya ni mashairi ya aina gani ? Toa sababu
      2. Washairi hawa wawili wanalalamika. Yafafanue malalamishi yao
      3. Onyesha jinsi kinaya kinavyojitokeza katika tungo hizi mbili
      4. Ni vipi Hadija :-
        1. Amekata mti mtima ?
        2. Amepita nyuma ya Punda (al.2)
      5. Toa mifano 2 ya uhuru wa mashairi kwa kurejelea mashairi haya
      6. Kwa kurejelea shairi ‘B’ eleza maana ya:-
        1. Mzigo
        2. Siri
        3. Kula nimekula
        4. Niko nyuma ya wakati

  2. Soma hadithi hii halafu ujibu maswali .
    Hapo zamani za kale, Mungu alituma wajumbe wawili waende duniani. Wajumbe hawa ni Kinyonga na Mjusi. Kwanza alimtuma Kinyonga na kumwagiza akaseme “wanadamu hamtakufa.” Kinyonga alienda kwa mwendo wa kuduwaa, akasimama hapa na pale akila matunda ya miti. Kwa sababu ya hali hii alichelewa sana kufikisha ujumbe kwa binadamu.
    Baada ya muda kupita, Mungu alimtuma Mjusi na ujumbe akaseme, “Mwanadamu sharti kufa.” Mjusi aliunyanyua mkia akafyatuka pu! Mbio akawahi duniani kabla ya kinyonga kuwasili. Kwa haraka alitangaza agizo kuu, “Wanadamu sharti kufa!” Akarejelea haraka kwa Mungu. Baada ya muda kinyonga naye akafika duniana na kutangaza, “Wanadamu hamtakufa!” Wanadamu wakapinga mara na kusema, “La! Tumeshapata ujumbe wa Mjusi, wanadamu sharti kufa! Hatuwezi kupokea tena neno lako! Basi kulingana na neno la mjusi, wanadamu hufa.

    Maswali
    1. .
      1. Hadithi hii huitwaje?
      2. Toa sababu zako
    2. Eleza sifa tatu zinazohusishwa na ngano za fasihi simulizi katika hadithi hii
    3. Kinyonga ni mhusika wa aina gani?
    4. Hadithi hii ina umuhimu gani?
    5. Taja njia zozote nne za kukusanya kazi za fasihi simulizi
    6. Tambulisha vipera hivi:-
      1. Kula hepi
      2. Sema yako ni ya kuazima
      3. Baba wa Taifa

  3.  “Nilijua ni utoto tu”
    1. Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
    2. Eleza sifa na umuhimu wa mnenaji (alama 20)

  4. Onyesha jinsi uongozi mbaya unavyojitokeza katika tamthilia ya Kigogo. (alama 20)


MAAKIZO:

  1. Ushairi
    1.  .
      1. Mashairi huru (2X1)ala. 2
      2. Hayazingatii arudhi za betu,vina, mishororo, mizani na kibwagizo (2x1)ala. 2
    2. .
      1. SHAIRI A – Anamlalamikia Hadija kwa kumuuwa mumewe kwa kumpa sumu.
      2. SHAIRI B – Anawalalamikia vijana ambao wanamcheka eti amezeeka na kupitwa na wakati Wanamramba Kisogo (2x2)ala 4
      1. Katika SHAIRI ‘A’ - Hadija alidhani kumuua mewe angepata suluhisho lakini badala yake amejiletea matatizo zaidi. Watu sasa wamemsuta kwa kitendo chake na watoto wanamsumbua.
      2. Katika SHAIRI ‘B’ – Mshairi anawakejeli vijana ambao wnamramba mzee kisogo bila kujua kwamba hawataki kupita. (2x2) ala.4
      1. Amemuua mumewe – Mti mkuu au kichwa cha nyumba.
      2. Anapata shida za Kujitakia – matatizo yamefurika ngyumbani kama mto (ukupita nyuma ya punda atakutega au kukupiga teke) (2x2)ala.2
    3. .
      1. Inkisari
        • Nendako – Niendako
        • Mwendako – Mnakoenda
        • Bwanako – Bwna yako (1x2)ala.2
    4.   
      1. Mzigo – uzee/umri.
      2. Jiri – Tajriba /Waarifa / Elimu ya maisha.
      3. Kula nimekula - Ameishi miaka mingi
      4. Niko nyuma ya wakati - Amebaki nyuma ne usasa (4x1)ala.4




  2. Soma hadithi hii halafu ujibu maswali
    1.  
      1. Kisasili
      2. Inaeleza jinsi kifo kilivyoingia duniani
        Asili ya kifo (alama 2)
    2. Sifa za ngano
      • Mwanzo maalum (fomula) hapo zamani za……..
      • Wahusika wanyama mfano mjusi na kinyonga
      • Wanyama kuwasilisha tabia na hisia za binadamu mfano kuongea, kujibizana n.k.
      • Tanakali za sauti m.f pu! Zozote 3x1=3
    3. Kinyonga ni
      • Mvivu/ mzembe/mlegevu
      • Si mzingativu- anachelewesha ujumbe
      • Mtiifu- mwishowe alifikisha ujumbe zozote 3x1=3
    4. Umuhimu wa hadithi
      • Kuelezea asili ya binadamu
      • Asili ya kifo
      • Huipa jamii melekeo
      • Hukumbusha jamii
      • Huburudisha/ huliwaza
      • Ni historian a utamaduni wa jamii
      • Huonya/ huadhibu zozote 4x1=4
    5. Njia za kusanya fasihi simulizi
      • Mahojiano yaliyopangwa na mtafuti na wahojiwa wake
      • Kutumia vinasa sauti
      • Kutumia video
      • Kwa kuandika data au kazi husika zozote 4x1=4
    6. Tambulisha vipera
      1. Kula hepi- msimu(kuwa na haraka)
      2. Sema yako ni ya kuazima- msemo (mtu asiringe)
      3. Baba wa taifa – lajabu (kiongozi wan chi)

  3.  “Nilijua ni utoto tu”
    1. Msemaji ni Boza. Yuko pamoja na wachongaji wenzake barazani mwa nyumba ya Sudi. Alisema
      haya baada ya kumsikiliza Siti akimjibu Sudi kuwa mojawapo ya malalamishi kiwandani ilikuwa bei
      ghali ya chakula.
    2. Sifa za Boza
      1. Mwenye bidii
        • Anafanya kazi ya uchongaji vinyago kwa bidii katika soko la \chapakazi ili aweze kujikimu pamoja na familia yake.
        • Soko inapofungwa anashirikiana na wenzake kuchongea vinyago barazani mwa nyumba ya Sudi.
      2. Mwenye dharau
        • Anamwambia Sudi kuwa embe alilokuwa kila lilikuwa likinuka fee! (uk 1)
        • Anamwambia Kombe anapenda kubaki nyuma kama mkia wa kondoo.
        • Anawadharau na kuwapuuza Sudi na Tunu kwa kuwa huwa wanafuatana wakitetea haki za watu. (uk 6) 
        • Anadharau vitu vya wenzake. Kwa mfano anaita redio kwenye rununu ya Sudi kijiredio kwa kujirununu. Anasema haina dhamana yoyote hata iliitwa redio tu kwa kukosa jina (uk 7)
        • Anaidharau kazi ya Sudi kwa kuchonga watu wasioljulikana asili au usuli wao, anamuuliza,“Kazi ya kuchonga watu wasiojulikana nayo ni kazi?” (uk 8)
        • Anaipuuza azama ya Sudi ya kuleta mabadiliko katika jamii. Sudi anaposema angeiandika historia yao upya, Boza namjibu kuwa kufanya hivyo hakungempeleka popote na kwa dharau anamwambia “kila la kheri” (uk 8)
      3. Mnafiki
        • Anapoulizwa na Kombe alikuwa kichonga nini anamjibu kuwa ni mhenga fulani tu.
        • Hamwambii ukweli kuwa alikuwa akichonga sanamu ya shujaa Marara Bin Ngao, hakutaki ajue.
        • Hakuwaletea wachongaji wenzake taarifa kuwa walihitajika kuchonga sanamu na wangelipwa
        • vizuri.
        • Kenga anapofika Boza alitaka Kombe akubali kuwa aliwapa taarifa ili asionekana mbaya mbele ya mshauri mkuu.
      4. Mpumbavu
        • Anafurahia kipindi cha mwezi mzima cha sherehe za uhuru asijue kuwa watu wasipofanya kazi uchumi wa nchi unadidimia. \aidha watu wasipofanya kazi wengine hawawezi kupata chakula cha kila siku.
        • Anafurahia kuwa kilele cha sherehe kingesadifiana na siku ya kuzaliwa kwa mzee, analifanya lionekane kama jambo la muhimu mno kwa jimbo ilhali hafla hii haina umuhimu wowote kwa raia.
        • Anakasirika na kumtusi Sudi kwa kufunga redio. Anakasirikia vitu vya wenyewe ilhali ni mtu mkubwa.
        • Anauliza kijinga mambo ya Kenya kuwa pamoja na wahuni kupanga mabaya yaliwahusu kwa njia ipi.
        • Analiwa kivuli (kuendewa kinyume) na Ngurumo katika ndoa yake na ananyamaza tu.
        • Alishasikia kuwa mkewe kampa uroda Ngurumo lakini hakuuliza jambo hilo mapaka lilipotajwa na kina Sudi na Tunu. Mkewe alituhumiwa kuwa na uhusiano na Ngurumo na ndipo akapata mradi wa keki; zikaitwa keki za uroda (uk 64)
        • Awali Sudi alikuwa amemwonya Boza kuwa achunguze uhusiano wa mkewe na Ngurumo lakini hakutilia jambo hilo maanani. La muhimu kwake ilikuwa kwamba mkewe kapata mradi wa keki kwa kuwa karibu na Husda na Ngurumu.
        • Anapokea keki iliyoletwa na Kenya na kuchekacheka kipumbavu. Anafurahishwa na vizawadi visivyo na maana.
      5. Mwenye ubinafsi
        • Hakuwafahamisha wachongaji wenzake kuhusu mradi wa kuchonga mashujaa. Alitaka anufaike peke yake.
        • Hakujali kuwa sherehe za uhuru zingechukuwa muda wa mwezi mmoja maana mkewe angekuwa anapata pesa za kukimu familia yao kwa mwezi mmoja kupitia kandarasi ya kuoka keki. 
        • Anasema kuwa kijikeki kilicholetwa na Kenya si cha kumfanya mtu afikirie kuhusu jamaa yake.
        • Anayaita malalamishi ya wafanyakazi wa kiwanda utoto. Walikuwa wakidai haki lakini yeye kwa vile hayakumhusu anasema, “Nilijua ni utoto tu” (uk 17)
        • Anakataa kuandamana na wenzake Sudi, Kombe na Tunu kwenda kusaidia majeruhi wa maadamano. Sudi anapowahimiza kwenda, Boza anasema, “Sisi hatuendi” (uk 17). Alisema haya akifikiria Kombe hangeenda. Mwishowe alibaki peke yake baada ya wengine kuondoka.
      6. Umuhimu wa Boza
        • Ni kielelezo cha watu wenye dharau. Huwadharau, kuwapuuza na kuwakosea wengine dhamana. Kwa mfano anamdharau Sudi na kukidharau kijiredio chake katika kujirununu.
        • Anakiita kijiredio kwenye kijirununu cha pesa nane. Analidharau embe la Sudi na kumwambia lilikuwa likinuka fee. Anamwambia anawachwa nyuma mambo yanapotendeka. Alimdharau Sudi na kuonyesha kana kwamba hakuwa na uwezo wa kulea mabadiliko katika jamii.
        • Ni kielelezo cha watu wenye unafiki katika jamii. Hakuwaambia wenzake kuwa kulikuwa na mradi wa kuchonga vinyago kisha walipwe, lakini Kenga alipofika alijifanya alikuwa amewajulisha taarifa hio. Alitaka Kombe aseme walifahamu hilo. Hakutaka kuonekana mbaya machoni mwa Kenga. Hakutaka wenzake wajue alikuwa akichonga kinyago cha shujaa Morara Bin Ngao. 
        • Ni kielelezo cha vikaragosi katika mfumo wa utawala. Boza, ni mfuasis wa Majoka mwenye ‘upofu’. Anafurahia utawala wa Majoka kufunga soko la Chapakazi, hakuona kuwa watu wangekosa riziki. Na kama alifahamu hili alilipuuza kwa vile mkewe alikuwa na kazi ya kuikimu familia.
        • Ni kielelezo cha watu wenye ubinafsi katika jamii, watu ambao hawajali maslahi ya watu wengine. Soko lilipofungwa alifurahia maradufu. Yeye hangekosa chakula kwa muda wa mwezi mmoja. Kwanza mkewe alikuwa ampata kandarasi kubwa kuuza pombe maana watu walikosa kwa kwenda baada ya soko kufungwa wakatorokea ulevini. Anamwambia Tunu “….Usiniharibie biashara” (uk 63). Hakutaka kujua watu hawa wangejikimu vipi maishani.
        • Ubinafsi wake pia unajidhihirisha kwa kukosa kuandamana na wenzake kwenda kushughulika na masaibu yaliyowapata vijana wachuuzi wa soko na pia maafa ya wafanya kazi wa kampuni ya Majoka and Majoka. Hata aliposikia malalamishi ya wafanyakazi, aliyaita ya kitoto.
        • Mwandishi amemtumia pia kuonyesha kuwa kuna waume wasiokuwa makini katika ndoa zao. Alipata fununu mapema kuwa mkewe alimpa Ngurumo uroda ili apate kandarasi ya kuoka keki. Hakujishughulisha kupata ukweli wa mambo. Alitaka kutatua hilo lilipogusiwa na Tunu na Sudi; ndipo alitaka kumpiga Ngurumo.
        • Aidha mkewe anachezewachezewa na Ngurumo kule ulevini kwa maneno na vitendo. Kwa mfano Ngurumo anamtania “…… Asiya umeliachia nani?” (uk 56). Kisha wawili hawa wanagoteana konzi. Haya yote yanafanyika na Boza yu mle mle ulevini. Yeye si mfano wa waume wa kuigwa.

  4. Onyesha jinsi uongozi mbaya unavyojitokeza katika tamthilia ya Kigogo. (alama 20)
    1. Mwandishi ameangazia uongozi mbaya kupitia wahusika wa tamthilia.Viongozi wanachaguliwa na wananchi lakini wanakosa kuwahudumia . Kwa mfano, sokoni,maji machafu yanapita mitaroni na kusababisha uvundo mkuu. Ashua anasema huko sokoni hakukaliki .
    2. Viongozi hawajali na hatunzi mazingira.Kombe analalamika,……angalia hiko povu jeupe ….huoni wameligeuza soko letu uwanja wa kumwagia kemikali na taka?’’ viongozi hawajali athari ya takataka na kemikali kwa wananchi wao.
    3. Mfumo wa uongozi pia unamnyanyasa mwananchi.Kwanza kumdai kodi ilhali hamna huduma bora .Bali na kodi wananchi wanadaiwa pesa zaidi.Kombe anasema ni lazIma wapate chakula chao cha pili. Tuwape wenye nchi kitu kidogo’’ashua asema wao hawaitishwi kitu kidogobali kikubwa au chote .Isitoshe wasipotoa wanatishwa tishwa.
    4. Uongozi wa Sagamoyo ni mbaya.Viongozi wanakiuka haki za raia ,wanakosa kuwajibikia kazi zao,hawajali maslahi ya wananchi na huwatusi watu waliowachagua.Majoka anawaita watu wajinga .Watu wa Sagamoyo mu wajinga sana’’.Tunu anashauri watu wasichague tena viongozi wa aina hii,viongozi wanaoongozwa na tama na ubinafsi,viongozi ambao hukutana na wananchi tu wakati wanahitaji kitu kutoka kwao.Kwa mfano Kenga alilitembelea soko la Chapakazi ili kuangalia mradi wa uchongaji.Sudi anashangaa kumwona Kenga sokoni,kumaanisha viongozi walifika huko tu iwapo lilikuwa ni jambo la kujinufaisha si kuwapa wananchi huduma.
    5. Bali na haya viongozi wa Sagamoyo hawajali hali ya uchumi wa sagamoyo na mzigo wanaobebesha wananchi.kwanza majoka na watu wake wanaamrisha soko lifungwe hivyo kuwanyima wananchi mapato.anawageuza wananchi wake omba omba kwa kukosa namna ya kujikimu.Kufungwa kwa soko kunafifisha maendeleo maana hakuna kodi inayotozwa ya kutumika katika maendeleo ya jimbo.
    6. Pia mikopo inayokopwa ni mzigo kwa mwananchi wa kawaida .Mikopo hiyo inapaswa kulipwa kwa muda wa miaka mia moja kumaanisha utalipwa na kizazi cha sasa na cha baadaye .Kinaya ni kuwa mkopo ni wa kunufaisha wachache.Kwa mfano Kenga anadokeza kuwa mradi wa kuchonga vinyango vya mashujaa umefadhiliwa kwa mkopo kutoka nchi za magharibi na mashariki.Vinyago hivyo ni vya kudumisha sifa ya babake Majoka si cha muhimu kwa jimbo.
    7. Viongozi wanavunja sheria za katiba .Asiya anapata kibali kuuza pombe haramu kutoka kwa serikali ya Majoka .Kama asemavyo Ngurumo, serikali na katiba ni mambo mawili tofauti”.Viongozi wanavunja sheria kupendelea watu wa jamii(Asiya ni mkoi wa Husda ) na ni rafiki.
    8. Majoka anatumia nafasi yake kama kiongozi wa Sagamoyo kujinufaisha na kujitayarisha .Kwa mfano ndiye ndiye mwenye Majoka na Majoka Academy,Majoka and Majoka Resort,Majoka and Majoka Company na alikuwa mbioni kunyakua ardhi ya soko la Chapakazi ajenge hoteli ya kifahari.
    9. Licha ya hayo uongozi wake unawanufaisha watu wa karibu naye na wa mkewe .Kwa mfano,Kenga alikuwa amegewee kipande cha ardhi katika soko la la Chapakazi .Ngurumo na Asiya wanapata kandarasi ya keki kwa kuwa washirika wa karibu na kiongozi.Ngurumo alikuwa mfuasi sugu wa Majoka aliyemtekelezea hata mauaji(k.m kesi ya Tunu).Asiya naye alikuwa mkoi wa Husda. Hivyo anaruhusiwa kuuza pombe haramu.Pia alipata mradi wa keki kupitia ufisadi.
    10. Majoka anadhihirisha uongozi mbaya kwa vile hana stahamala hata kwa washirika wake wa karibu.Anamkaripia Kenga anapokuja kumwona pale Majoka and Majoka Modern Resort.Hakutaka kusumbuliwa maana alikuwa katika starehe zake.Kiongozi kama huyu atakosa kujua mambo muhimu maana watu wataogopa kumwambia lolote .
    11. Ithibati nyingine ya uongozi mbaya ni mauaji yanayotokea.Wapinzani wa Majoka wanauawa.Jabali aliuawa kwa kuwa mpinzani wa Majoka na chama chake cha Mwenge kikafifishwa.Mauaji hayta yalikuwa kumsumbua Majoka baadaye.
    12. Tunu aliponea chupuchupu, Majoka na Kenga walikuwa wamepanga mauaji yake .Tunu alikuwa mpinzani wa Majoka pia.
    13. Wafanyakazi waliodai haki waliuawa .Kwa mfano wale vijana watano wa kiwanda cha Majoka and Majoka company,wachuuzi wa soko wakajeruhiwa.
    14. Baada ya kumtumikia Majoka na kujua siri zake nyingi mtu aliuawa ili asitoboe siri hizo.Kwa mfano Majoka na Kenga wanakubaliana kuwa , chopi lazima aende safari” na auawe one touch ili asije kujulikana ni nani alitenda uovu huo.
    15. Ngurumo aliuawa na chatu akitoka ulevini.Mpango ulikuwa amezwe na chatu si kuuawa tu.Kwa hivyo Majoka anaghadhabika kuwa chatu hawakummeza.Kifo cha Ngurumo hakikumsikitisha Majoka ,ushauri wake ni kwamba azikwe mara moja siku iyo hiyo na hata kama maziara yamejaa afukiwe juu ya miili mingine kimba si ni kimba tu”
    16. Ni uongozi mbaya pia lutumia vyombo vya habari kueneza propaganda .Redio inatabngaza jinsi mambo yalivyo shwari katika jimbo la Sagamoyo,kuwa kuna maendeleo mengi na watu wasijihusishe na siasa duni za kuwagawanya na kurudisha nyuma maendeleo.Wimbo wa kizalendo unaochezwa unaeneza propaganda tu.Kwamba watu wanampenda na kumtukuza kiongozi wao daima .Huu ni uongo ikikumbukwa kuwa kuna vuguvugu la mabadiliko linalotaka kumwondoa Majoka.
    17. Ni uongozi mbaya pia kwa kiongozi kuwanyima raia uhuru wa kupata habari na habari za kweli.Majoka aliapa kuwa runinga ya mzalendo iliokuwa ikitangaza na kupeperusha harakati za Tunu za kuleta mabadiliko ingefungwa.Kungebaki kituo kimoja tu,Sauti ya Mashujaa.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - End Term 3 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest