Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Term 1 Opener Exams 2021 Featured

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU

    Wahenga walisema “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”. Hii in maana ya kuwa ukiogopa kutumia ufito kumchapa mtoto wako, ukamdekeza, utadeka na hatimaye ataharibika. Methali hii ina pacha yake ambayo ni “ukicha mwana kulia, utalia wewe.

    Hizi ni methali zilizojaa busara kubwa. Mathalani, wewe ni mzazi au mtu yeyote mzima aliyetunukiwa madaraka juu ya watoto, lakini kila wanapokiuka uadilifu au mmoja wao anapokosea wewe unambembeleza tu, basi huwa unaizorotesha tabia yake. Mtoto huyo anaweza kuishia kuwa mtundu.

    Hata hivyo, ni sharti tujue ya kwamba tuko katika njia panda hapa. Kwa upande mmoja, zamani ilichukuliwa kwamba watoto na hata mtu mzima ana jambo la kuwaeleza, njia pekee ya kuliingiza katika ‘akili yao’ ni kuwatwanga ili kulikongomeza jambo hili. Ukweli ni kwamba akili ya mtoto si hafifu hata. Unaweza kusema ni kama mmea, ambao usiporutubishwa kimakusudi, ukapaliliwa vyema na kustawishwa stahiki yake, basi hudhoofu; na mwisho kufifia .

    Kwa upande mwingine, mtazamo wa kisasa ni tofauti kabisa. Imethibitishwa ya kwamba wanawake ni sawa kabisa katika maumbile yao wakilinganishwa na wanaume. Kwa jinsi hiyo, kweli wapo wanawake ambao hawana mwelekeo timamu kuhusu maisha, lakini ni kweli kuwa watoto wote, kwa sababu ya umri wao tu, basi hawana akili. Kadhalika, si kweli kuwa watoto wote, kwa sababu ya umri wao tu basi hawana akili. Ama kwa kusema kweli binadamu yeyote huzaliwa na akili pungufu. Hili litokeapo, basi tunalikubali tu. Hatuwezi kumlaumu mtu kama huyo au muumba wake. Kwa hakika huu ndio msingi wa methali, “akili ni nywele, kila mtu ana zake.” Vinginevyo, mtazamo wa kizamani ni taasubi kongwe tu za kiume zilizopitwa na wakati.

    Aidha, kwa sababu watu wote huzaliwa na akili timamu, tene hawawi watu wazima kabla ya kuwa watoto kwanza, mtu mzima yeyote ana hali gani ya kuwadhulumu watoto na kujipambaniza na lawama za uongo dhidi ya vijana hao kwa madai kuwa hawana akili? Na je, ikiwa hawana akili, basi ndipo waonewe? Wanyanyaswe? Hili si jambo la busara. Kurudi Mtoto kwa visa vya maonevu ni kumrudisha nyuma kiumbe huyo. Kurudi kufaako ni kwa kupeleka, sio kwa kurudisha nyuma. Kurudi kuelekezako mbele ni kwa uongozi ambao lengo lake ni kumulikia mtoto kurunzi ilimradi kumwangazia tariki njema.

    Mtoto asinyimwe vya tunu vyovyote ambavyo ni stahiki yake, kwa kisingizio kuwa vimetengewa mtu mzima, ndugu mkubwa, mwalimu, au mtu awaye yeyote Yule aliyekabidhiwa jukumu la kumlea au mtu mzima, ndugu mkubwa, mwalimu au mtu awaye yeyote. Yule aliyekabidhiwa jukumu la kumlea au kumwogoza mtoto.

    Mtoto ana haki ya kuhudumiwa kwa njia yeyote ifaayo ili akue na akili yake ikomae kikamilifu. Inafaa asomeshwe,apewe malezi bora ili naye alee wengine kistahiki.

    MASWALI
    1. Mapenzi yasiyo kipimo yanaweza kuwa hatari kwa mtoto. Eleza kikamilifu huku ukirejelea habari uliyosoma . (Alama 3)
    2. Fafanua njia panda inayorejelewa na mtunzi. (Alama 3)
    3. Mtoto analinganishwa na mmea katika taarifa hii, kwamba “usiporutubishwa kimakusudi, ukapaliliwa vyema na kustawishwa stahiki yake basi hudhoofu,” tathmini kulinganishwa huku, huku ukirejelea taarifa. (Alama 3)
    4. Akili ni nywele, ‘Kila mtu ana ;zake. Eleza maana ya ndani ya methali hii kulingana na taarifa. (Alama 2)
    5. Onyesha kwamba unaelewa maana ya: (Alama 2)
      Kurudi Mtoto kwa visa vya maonevu ni kumrudisha nyuma kiumbe huyo.”
    6. Eleza maana ya: (Alama 2)
      1. Kulikongomeza
      2. Kujipambaniza
  2. MATUMIZI YA LUGHA. (Alama 30)
    1. Eleza tofauti ya kimatamshi baina ya sauti zifuatazo.
      1. (K)
      2. (G)
    2. Eleza maana nne zinazojitokeza katika sentensi ifuatayo. (Alama 4)
      Tande alimpigia milimo mpira
    3. Sahihisha sentensi ifuatayo kwa njia tatu mwafaka. (Alama 3)
      Hapa Kwetu Mna Siafu Wengi.
    4. Eleza maana ya ngeli. (Alama 1)
    5. Andika sentensi mbili ili kuonyesha maana tofauti za alama ya kibainishi. (Alama 2)
    6. Eleza maana ya mofimu. (Alama 2)
    7. Eleza hali zinazodhihirika katika sentensi zifuatazo.
      1. Gari lake limebingirika mtaroni.
      2. Cha mlevi huliwa na mgema.
    8. Andika sentensi ifuatayo kwa usemi taarifa. (Alama 2)
      “Hamjambo wanafunzi”, mwalimu aliwasalimia
    9. Andika sentensi ifuatayo kwa ukubwa. (Alama 2)
      Watoto walinunuliwa viatu maridadi.
    10. Andika kinyume cha sentensi, (Alama 2)
      Shangazi alifurahishwa na wimbo huo.
    11. Tunga sentensi kuonyesha maana ya vitale vifuatavyo. (Alama 2)
      1. Pamba
      2. Bamba
    12. Toa maelezo ya msamiati ufuatao. (Alama 4)
      1. Nomino
      2. Kielezi
      3. Kiunganishi
      4. Kiwakilishi
  3. ISIMU JAMII
    1. Eleza maana ya. (Alama 5)
      1. Sajili
      2. Lahaja
      3. Isimu
      4. Lafudhi
    2. Eleza maana ya (Alama 5)
      Kuchanganya ndimi
  4. FASIHI SIMULIZI (Alama 10)
    1. Maigizo ni nini? (Alama 2)
    2. Toa mifano mine ya maigizo. (Alama 4)
    3. Taja dhima nne za maigizo. (Alama 4)


Marking scheme

  1. UFAHAMU 
    1. Mapenzi yasiyokipimo yana athari zifuatazo kwa mtoto;
      1. Mtoto huharibika 
      2. Huzorotesha tabia yake
      3. Atakosa heshima kwa wakubwa
    2. Niia panda 
      1. Kuwapa watoto uhuru wa kujielezea
      2. Kuwafundisha mambo kwa kuwatwanga 
      3. Kuamua kama mtoto ana akili au la 
    3. Mtoto na mmea
      1. Akili ya mtoto inahitaji kupaliliwa
      2. Akili ya mtoto ni hafifu
      3. Akili ya mtoto inaweza kudhoofika na kasha kufifia.
    4. Akili ni nywele kila mtu ana zake.
      • Kila mtu ana maumbile yake ambayo yanatofautiana na ya mwingine.
      • Akili za binadamu hazitoshani.
    5. Kumrudi mtoto kwa visa vya maonevu ni kumrudisha nyuma kiumbe huyo. 
      • Utamzuia mtoto kuendelea mbele (kuikula akili)
      • Mtoto atapoteza mwelekeo
    6. Msamiati
      1. Kulikongomeza – kulifungia jambo
      2. Kujipambaniza – kuliepusha /Kuliepuka jambo
  2. MATUMIZI YA LUGHA 
    1.  
      1. Sauti K – Kipasuo cha ka kaa laini – sauti sighuna 
      2. Sauti G – Kipasuo cha kaka laini – sauti ghuna
    2. Maana 
      1. Tande alipiga mpira kuelekea kwake milimo.
      2. Tande aliupiga mpira kwa niaba ya milimo
      3. Tande alimpiga milimo kwa sababu ya mpira.
      4. Tande alimpiga milimo kwa mpira kama adhabu. (Alama 4)
    3. Ngeli ya PA/KU/MU
      1. Hapa petu pana siafu wengi 
      2. Huku kwetu kuna siafu wengi
      3. Humu kwetu mna siafu wengi 
    4. Ngeli ni utaratibu wa kuweka nomino katika makundi maalum kulingana na mianzo yake.
    5. Matumizi ya kibainishi/ Ritifaa
      • Kuonyesha silabi iliyodondoshwa. 
        Ndu’ zangu tuheshimiane. (pia takwimu)
      • Wageni hawa wametoka ng’ambo .
      • Kuonyesha shadda 
      • Mahasimu hawa wamepatana bar’abara
    6.  
      • Mofimu ni kipashio kidogo kabisa katika muundo wa neno chenye kisarufi 
      • Mofimu ni vijisehemu vidogo katika neno vyenye maana kisarufi.
    7.  
      1. - Me – hali timilifu
      2. - Hu – hali mazoea
    8. Usemi taarifa 
      • Mwalimu aliwamkua / wasalimu wanafunzi wake. 
    9. Ukubwa 
      • Matoto yalinunuliwa majiatu maridadi.
    10. Kinyume.
      • Shangazi alikasirishwa na wimbo huo.
    11.  
      1. Pamba – zao la mpanda, posho ya safari, pendendekeza kitu 
      2. Bamba – kamata, kitu bapa tena chembamba.
        (Mtahini akadirie sentensi za watahiniwa)
    12.  
      1. Nomino – jina la mtu, kitu, mahali, hali
      2. Kielezi - neno linaloeleza zaidi kuhusu kitenzi.
      3. Kiunganishi – Neno linalounganisha mawazo katika sentensi
      4. Kiwakilishi – neno linalowakilisha au linalosimama badala ya nomino katika sentensi.
  3. ISIMU JAMII
    1.  
      1. Sajili ni matumizi ya lugha katika muktadha ya jamii.
      2. Lahaja ni namna mbalimbali za kuzungumza lugha moja kuu
      3. Isimu ni sayansi ya lugha.
      4. Lafudhi ni tofauti kimatamshi baina ya wazungumzaji wa lugha moja.
    2. Kuchanganya ndimi ni kutoa maelezo kupitia kwa lugha mbili tofauti.
  4. FASIHI SIMULIZI
    1. Maigizo ni utanzu wa fasihi simulizi unaohusu mtu kusema na kutenda kama mtu mwingine afanyavyo.
    2. Mifano ya maigizo
      1. Michezo ya watoto wa chekechea 
      2. Vichekesho
      3. Maigizo ya jukwaani (tamthilia)
      4. Mivigha 
      5. Uganga 
    3. Dhima ya maigizo /umuhimu /majukumu.
      1. Kukuza ujasiri
      2. Kupitishia hisia 
      3. Kukuza maadili
      4. Kukosa jamii
      5. Kuelimisha 
      6. Kuimarisha lugha na kipawa cha kuigiza
      7. Kuendeleza utamaduni
      8. Kuburudisha.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Term 1 Opener Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest