Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 Mid Term 1 Exams 2021

Share via Whatsapp
Download PDF for future reference Join our whatsapp group for latest updates

MAAGIZO

 • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
 • Kisha chagua insha moja nyingine kutoka hizo tatu zilizobakia
 • Kila insha isipungue maneno 400
 • Kila insha ina alama 20
 1. Wewe ni katibu wa chama cha waandishi habari chipukizi shuleni mwako. Andika kumbukumbu za mkutano uliofanyika mnamo MACHI 7, 2014.
 2. Fahali wawili wapiganapo ziumiazo ni nyasi.
 3. Anza kisa kwa maneno haya:
  Mtoto aliletwa mbele yangu akiwa anatiririkwa damu usoni. Singeweza kumtambua hadi pale………………………………………………………. 
 4. Mvua husababisha madhara mengi. Jadili

Marking Scheme

 1. Hii ni insha ya kumbukumbu.
  Ni muhimu mwanafunzi kufuata utaratibu wa uandishi wa insha ya kumbukumbu k.v
  1. Lazima kuwe na anwani ya kumbukumbu
  2. Majina ya waliohudhuria
  3. Walituma udhuru
  4. Ajenda
   1. wasilisho la mwenyekiti.
   2. Kusomwa na kuthibitishwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia.
   3. Yatokanayo na kumbukumbu hizo.
   4. Kusajiliwa kwa wanchama wapya.
   5. Ziara ya wanchama.
   6. Usafi wa mazingira.
   7. N.k
    (Watahini wahakiki ajenda za watahiniwa zikilenga mada na pia kufikia idadi inayohitajika)
   8. Mambo mengineyo.
   9. Kufungwa kwa mkutano/kufunga mkutano.
  5. Kumbukumbu zenyewe. Kv.
  6. Kuwe na sehemu ya sahihi ya mwenyekiti pamoja na katibu wake (aliyeandika kumbukumbu hizo)
   Mfano
                        Sahihi                          Tarehe
   Katibu…………………………………                 …………………………….
   Mwenyekiti ………………………….                …………………………….
 2. Insha ya methali.
  • Mtuhiniwa anaweza kuanza insha yake kwa kueleza maana ya methali au kuanza moja kwa moja kutoa kisa au visa.
  • Sharti mtahiniwa asimulie kisa au visa kuthibitisha ukweli wa methali “Fahali wawili wapiganapo ziumiazo ni nyasi”
  • Kisa au visa vilenge maana ya methali hii – wazozanapo viongozi/wakuu/wenye uwezo, wanyonge ndio huumia.
  • Sharti kisa kilenge pande mbili za methali, jinsi, wenye uwezo walivyozozana na jinsi wanyonge walivyoahudhiwa na mzozo huo.
  • Mtahinwa anayeshughulikia upande/sehemu moja ya swali au sehemu moja ya methali hajashughulikia swali kikamilifu na akadiriwe vilivyo. Asizoe alama zaidi ya C.
 3. Mtahiniwa aanze insha kwa maneno aliyopewa. Kisa chake kihusishe:
  • Chanzo cha kuvuja damu.
  • Uhusiano wa mwathiriwa na msimulizi.
  • Usaidizi aliopewa mwathiriwa.
  • Hatima ya tukio hilo.
   Tanabahi: Mtahiniwa aliyeanza kisa kwa maneno tofauti, atakuwa amejitungia swali lake.
   Kiwango chake ni D- ( 1 au 2 )
 4.  
  • Mwanafunzi anaweza kuzungumzia madhara na faida kisha atoe msimamo wake.
  • Anaweza kuzungumzia madhara pekee pia.

Hoja
Madhara

 • Mafuriko hutokea.
 • Vifo vya watu na mifugo.
 • Nyumba hubomoka.
 • Huathiri usafiri – barabarani.
 • Mimea huaharibiwa – huoza au hukosa kukua.
 • Magonjwa hutokea k.m malaria kwa sababu ya mbu (hakuna masika yasiyo na mbu )

Faida

 • Hukuza mimea / miti
 • Mandhari huwa ya kupendeza.
 • Chakula huwa kwa wingi.
 • Maji ya kunywa / kutumia kwa viwanda n.k.
 • Samaki na viumbe wa baharini

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 Mid Term 1 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-


Read 575 times Last modified on Monday, 02 August 2021 08:12

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.

Print PDF for future reference