Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 End Term 1 Exams

Share via Whatsapp

Maagizo.
Jibu maswali yote .

  1. UFAHAMU (alama 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
    Haki za watoto na wanawake

    Makamishina wa Tume za Haki za Binadamu, waandalizi, waalikwa, watoto, mabibi na mabwana. Kwa muda mrefu kumekuwa na tofauti katika uhusiano baina ya wanajamii. Tofauti hizi zimewapelekea wanawake na watoto kudunishwa. Udunishaji unachukua mwelekeo mbaya zaidi kama watoto ni wa kike.

    Kupuuzwa kwa wanawake na watoto kuna historia ndefu. Jambo hili limepata usugu kutokana na imani hasi zilizoota akilini mwa wanaume na hata wanawake. Rasilimali na majukumu yamegawanywa kwa misingi inayowatabakisha wanajamii kuanzia wanaume, wanawake halafu chini kabisa watoto. Katika jamii nyingi, wanawake na watoto wa kike hawarithi chochote ingawa ndio wenye mchango mkubwa katika uzalishaji mali. Aidha mchango wao kuhusu masuala muhimu nyumbani na katika jamii hupuzwa hata kama wamesoma kuliko waume na akina baba zao.

    Inasikitisha kuwa wanawake na watoto hawana sauti kuhusu uamuzi nyumbani. Wao hulazimishwa kutenda wanavyoamriwa na wanaume.Kwa mfano, si ajabu mwanamke kulazimishwe kupika pombe na watoto kusukumizwa kwenda kununua sigara. Yote haya ni kinyume cha matarajio ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu.

    Ili kuzuia tabia ya ‘ujuaji’, wanaume wengi hupiga marufuku redio, simu, magazeti na televisheni kwa wanawake na watoto. Amri hii hutekelezwa vikali ili wahusika wasijifunze tabia ya kukaidi amri za wazee. Pengine hii ndiyo sababu katika jamii fulani, neno mzee lina maana moja tu; ya wanaume waliokomaa kiumri wala si wanawake. Hii si kweli.

    Haki za binadamu ni msingi wa utu. Bila haki hizo mwanadamu hawezi kutumia vipawa na uwezo wake wa kiakili na kihisia kikamilifu.Udunishaji wa wanawake na watoto unapingana na ukweli huu. Imani potofu zinazoendeleza uovu huu zimejikita akilini na katika utamaduni. Zinahitaji kuondolewa. Nafurahi kuwa mmeibua mikakati thabiti ya kulipiga vita tatizo hili. Kwa kweli, sherehe kama hizi ni muhimu sana katika kuwafumbua macho wadau kuhusu haki za wanawake na watoto. Naamini hotuba zilizotolewa hapa zitakuwa mbegu zitakazochipua mabadiliko katika fikra na matendo ya watu. Yafaa watu wakubali kuwa mke na watoto ni wenza na wadau katika safari ndefu ya maisha.

    Nimeona mabango, maigizo, ngoma na michoro ya waume kwa wake, wazee kwa watoto na wavulana kwa wasichana kuhusu mada hii. Ujumbe umewasilishwa wazi. Ni moyo uliofumwa kwa chuma tu ambao hauwezi kuathiriwa na ujumbe kuhusu nafasi ya wanawake kurithi na kusikilizwa. Lakini vita vya panga haviamuliwi kwa fimbo. Kilichobaki sasa ni kufanya utafiti wa kukusanya data kuhusu mielekeo na itikadi zinazopingana na lengo letu. Kutokana na matokeo, mikakati iwekwe ili kuvunja nguvu, desturi zinazochochea taasubi za kiume.

    Mabibi na mabwana, yapasa juhudi zifanywe za kusambaza habari kuhusu umuhimu wa kuheshimu na kujali binadamu wote na mchango wao. Aidha hatuna budi kuhakikisha nafasi sawa kwa kila mtu kutoa maoni na kusikizwa. Litakuwa jambo la kusikitisha kama jamii itasahau mchango wa wanawake na watoto katika kuzalisha na kulinda mali. Twahitaji kuondoa uoga kutoka kwa mama zetu wasiotaka mabadiliko. Sekta zote za umma lazima zijitahidi kutekeleza haya.

    Ningependa kuwakumbusha kuwa kanuni za ubalozi haziniruhusu kuingilia masuala ya ndani ya nchi hii. Hata hivyo, nalazimika kushauri jambo moja. Nashauri ibuniwe Wizara ya Maendeleo ya Wanawake, Vijana na Watoto. Wizara hii itakuwa na jukumu Ia kuondoa vikwazo dhidi ya wanyonge.

    Kubuni wizara tu hakutasaidia. Wakereketwa washawishi mabadiliko katika sheria kuhusu wanawake na watoto hasa wajane na mayatima. Wanaharakati nao yapasa wahakikishe kuwa sheria hizo zinaheshimiwa. Shirika langu liko tayari kutoa msaada wa kifedha na kitaaluma kwa sababu hii.

    Mambo haya yasikomee hapa. Mrudi mlikotoka na mbuni vikundi vya kufuatilia mapendekezo yaliyotolewa. Ni muhimu kusambaza mliyojifunza hapa ili mambo hayo yapenye kila nyumba.Asanteni.
    1. Tambua na kuthibitisha anayehutubia washika dau. (al.2)
    2. Eleza mielekeo hasi inayopeleka wanawake na wanaume hudunishwa. (al.4)
    3. Kwa kuzingatia swala ibuka la haki,orodhesha haki zozote tatu ambazo wanawake na watoto wananyimwa (al.3)
    4. “Vita vya panzi haviamuliwi kwa fimbo” (al.2)
      Fafanua
    5. Taja mchango wa mwandishi wa hotuba hii katika kuirekebisha hali hii ya kudumisha wanawake na watoto. (al.2)
    6. Eleza maana ya
      1. Kukaidi amri
      2. Moyo uliofumwa kwa chuma
  2. UFUPISHO

    Ujambazi wa kimataifa ni tatizo lililowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana. Serikali nyingi zimetumia mapesa mengi kwa miaka mingi sana zikijitahidi kupambana na janga hili. Hata hivyo, fanaka haijapatikana, wala haielekei kamwe kuwa itapatikana leo au karne nyingi baadaye.

    Yamkini tatizo kubwa lililopo ni kuhusu jelezi la dhana ya “ujambazi” tena “Wa kimataifa”. Hili ni tatizo mojawapo na yapo mengi sana. Tatizo la pili ni kiburi. Kuna wale watu binafsi na hasa viongozi wa nchi kubwakubwa na serikali zao zilizojiaminisha kuwa ujambazi ni balaa kweli, tena belua, lakini huo ni wa huko, wala hauwezi kuwagusa licha ya kuwashtua wao.

    Kulingana na maoni ya watakaburi hao, ujambazi ni wa watu ‘washenzi’ wasiostaarabika, wapatikanao katika nchi zisizoendelea bado. Ujambazi pekee wanaouona unafaa kukabiliwa ni dhidi ya mbubujiko wa madawa ya kulevya uliosabäbishwa na vinyangarika kutoka nchi hizo maalum za “ulimwengu wa tatu”. Kulingana na wastaarabu wa nchi zilizoendelea, vinyangarika hivi ndivyo hasa adui mkubwa wa ustaarabu ulimwenguni na ni sharti vifagiliwe mbali bila huruma. Baada ya kusagwasagwa, ulimwengu mstaarabu utazidi kutononoka na ahadi ya mbingu hapa ardhini itakamilika.

    Imani ya watu hawa ya kuwa ujambazi wa kimataifa, hata iwapo upo, hauwezi kuwashtua wala kuwatingisha wao ilikuwa kamili na timamu. Ilikuwa kamili na timamu hadi hapo mwezi Septemba tarehe 11 mwaka va 2001, ndege tatu za abiria zilipoelekezwa katika majumba mawili ya fahari, yenye urefu wa zaidi ya ghorofa mia moja na kuyatwangilia mbali. Mshtuko na kimako! Kimako kwa kuwa, kabla ya siku hiyo, Wamarekani hawangeweza kudhani kwamba ingewezekana taifa lolote au mtu yeyote kuthubutu kuishambulia nchi yao, taifa wasifa lililojihami barabara dhidi ya aina yoyote ile ya uchokozi kutoka pembe lolote la dunia.

    Hakuna ulimwenguni mzima, aliyeamini kuwa Marekani ingeweza kushambuliwa. Kwa ajili hiyo, mshtuko uliitingisha ardhi yote na huzuni ilitanda kote, kama kwamba sayari nzima imeshambuliwa, wala sio Marekani pekee.

    Mintarafu hiyo, Marekani ilipolipiza kisasi kwa kuwaunguza waliokuwemo na wasiokuwemo kwa mabomu hatari huko Afghanistan, idadi kubwa ya watu duniani ilishangilia na kusherehekea. Kwa bahati mbaya, tafsiri ya shambulizi la minara-pacha ya Newyork na lile la Pentagon, uti wa uwezo wa kivita wa Marekani, ilizorota. Kuna wengi waliodhani huo ni mwanzo wa vita vya Waislamu dhidi ya Wakristo na kwa muda, Waislamu wote wakashukiwa kimakosa kuwa ni majambazi wa kimataifa.

    MASWALI
    1. Bila kubadilisha maana,fupisha aya tatu za kwanza maneno (65-75) (alama 8; 2 za utiririko)
      Matayarisho
      Nakala safi
    2. Ukizingatia aya tatu za mwisho fafanua fikra za watu na mambo yote yaliyotokea baada ya Septemba 11 2001(Maneno 65-75) Alama 7:alama 1 ya utiririko)
      Matayarisho
      Nakala safi
  3. Matumizi ya lugha (alama 40)
    1. Ainisha vielezi katika sentensi ifuatayo:
      Mwanamke huyo alibebwa juu juu hadi kanisani. (al.2)
    2. Bainisha jinsi maneno yaliyopigiwa mstari yalivyotumika. (al.2)
      1. Kula kwake ni chanzo cha afya yake nzuri.
      2. Kula vizuri kama unataka kuwa na afya bora”.Daktari alisema.
    3. Sauti /e/ na /u/ hutamkwa vipi? (al.2)
    4. Eleza matumizi matatu ya italiki kisha tolea mifano kwa kila aina. (al 3)
    5. Tunga sentensi ukitumia kitenzi kifuatacho katika kauli ya kutendeka - la (al-2)
    6. Andika katika usemi wa taarifa (alama 3)
      “Hicho kijicho cha paka cheupe leo marufuku kwangu” alisema Mzee Kambumbu
    7. Tunga sentensi moja ukitumia kitenzi kimoja kilichoundwa kutokana na nomino zawadi (alama 2)
    8. Tambua matumizi ya kiambishi ji katika sentensi ifuatayo (alama 2)
      Jino la jitu hilo lililiwezesha kujilia chakula kingi kuliko mkimbiaji yule
    9. Tunga sentensi moja kuonyesha maana ya neno: Ililmradi. (alama 2)
    10. Andika sentensi moja ukitumia kihisishi cha bezo (alama 1)
    11. Ainisha viambishi katika neno waliibiana (alama 2)
    12. Nini maana ya kiimbo? (alama 1)
    13.  
      1. Vokali ni nini? (alama 1)
      2. Eleza sifa mbili za sauti ifuatayo /i/ (alama 2)
    14. Panda ni kuatika mbegu ardhini au kuparaga mti. Andika maana nyingine mbili (alama 2)
    15. Andika katika wingi. (al 2)
      Huzuni aliyokuwa nayo yatima huyu ilinitia kite na imani.
    16. Andika kinyume cha neno lililopigwa mstari. (al 1)
      Mhalifu huyu alitunga mimba
    17. Bainisha matumizi ya KI katika sentensi ifautayo. (al 1)
      Jua limekuwa likiwaka tangu Januari
    18. Bainisha maana mbalimbali za sentensi ifuatayo: (al 3)
      Mwalimu amempigia mwanafunzi simu
    19. Silabi mwambatano ni nini? (al 1)
    20. Tunga sentensi moja udhihirishe maana mbili za neno hili: Rudi (al 1)
    21. Pigia mstari vivumishi katika sentensi ifuatayo kisha uandike aina yake. (al 2)
      Bibi huyu ni mpole uso wake wenye haya huuinamisha kila mara.
  4. ISIMU JAMII (Alama 10)
    1. Eleza nadharia tatu kuhusu chimbuko la Kiswahili. (alama10) 


Marking Scheme

  1. UFAHAMU
    1. Balozi✔ wa nchi Fulani.Yuasema kanuni za ubalozi hazimruhisu✔
    2. Ugonjwa mbaya wa mali ambapo wanawake na watoto hubaguliwa
      • Michango ya wanawake na wanaume haitiliwi maanani katika jamii.
      • Hawana uamuzi kuhusu yatokeayo nyumbani
      • Hutenda wanayoamriwa na wazee
      • Wanawake na watoto hunyimwa haki ya kuwasiliana ili kuzuia ujuaji wao (4x1=4)
    3.  
      • Haki ya kutengamana na wenzako
      • Haki ya kutobaguliwa
      • Haki ya kurithi
      • Haki ya usawa
      • Haki dhidi ya kukandamizwa n.k (3x1=3)
    4. Methali inataka wadau watafute suluhu za kisayansi udunishaji wa wanawake na watoto (1x2=2)
    5. Shirika lake litatoa msaada wa kifedha na kitaaluma (1x2=2)
    6.  
      1. Kukaidi amri – kupuuza maagizo
      2. Moyo uliofumwa kwa chuma – moyo mgumu (2x1=2)
  2. UFUPISHO
    1.  
      1. Ujambazi wa kimataifa umewasumbua walimwengu kwa muda✔mrefu sana
      2. Serikali nyingi zimetumia mapesa mengi kupambana na janga hili
      3. Fanaka haijapatikana wala haielekei kupatikana
      4. Tatizo kubwa ni kuhusu jelezi la dhana ya ujambazi wa kimataifa
      5. Tatizo lingine ni kiburi cha mataifa makibwa kuona kuwa hayawezi kuarithiwa na ujambazi.
      6. Watakaburi wanaamini kuwa ujambazi ni wa watu washenzi.
      7. Ujambazi wa kukabiriwa ni mbubujiko wa dawa za kulevya unaosababishwa na vinyangarika kutoka ulimwengu wa tatu.
      8. Vinyangarika hivi sharti viangamizwe ili ulimwengu mstaarabu uzidi kutononoka. (hoja 8)
    2.  
      1. Mshtuko na kimako kwa Wakerekani.
      2. Hakuna ulimwenguni mzima aliyeamini Marekani ingeshambuliwa.
      3. Mshtuko ulitingisha ardhi na huzuni ilitandakote duniani.
      4. Marekani ililipiza kisasi mkwa kuwaunguza waliokuwemo na wasiokuwemo kwa mabomu huko Afghanstan.
      5. Idadi nzima yawatu duniani ilishangilia na kusharehekea.
      6. Tafsiri ya shambulizi la minara pacha ya New York na Pentagon ilizorota
      7. Wengi walidhani kuwa huo ulikuwa ni mwanzo wa vita dhidi ya wakristo.
      8. Waislamu wakashulawa kimakosa kuwa ni majambazi (zozote 7)
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1.  
      • juu juu – kielezi cha namna
      • Kanisani – kielezi cha mahali
    2.  
      1. Kula – kitenzi nomino
      2. Kula – kitenzi (2x1=2)
    3.  
      • /e/ - Hutamikiwa mbele ya ulimi midomoikiwa imetandazwa.
      • /u/ - Hutamkiwa nyuma ya ulimi mdomo ukiwa umeviringwa. (2x1=2)
    4. Matumizi ya kiitaliki / Herufi mlazo
      • Hutoa maelekezo na maagizo katika mazungumzo au mchezo wa kuigiza.
      • Kutenga neno, fungu la maneno au sentensi iliyo na maana maalum katika makali.
        Mfano: Uvumbizi wa utendawazi katika sekta ya sayansi.
      • Kuandika maneno ya lugha nwingine .
        Mfano: Kula Obusuma hotelini.
      • Kusisitiza neno kifungu cha neno au jambo Fulani. Zozote 3 x 1 = Alama 3
    5. Lika 1 x 2 = Alama 2
    6. Mzee kambumbu alisema kuwa hicho kijicho cheupe cha paka kilikuwa marufuku kwake siku hiyo.
    7. Zawadi(N)- zawidi(T)
      k.m Alizawidiwa kwa kupasi mtihani (1x2=02)
    8. Jino Ngeli ya LI-YA (4x ½ )
      1. Jitu-ukubwa/uduni wa kitu
      2. Kujilia-kirejeshi/kujirejelea
      3. Mkimbiaji-mazoea/uzoefu
    9. Ilimradi-ili,iwapo,kwa masharti kwamba,mradi. (Alama 1x2=02)
      Mf. Nitaruka maji ilimradi nipewe zawadi
    10. Kihisishi cha bezo k.m mmm! Po! Nyoo! Mnh! Ngoo! Mawe! Ebo! Wapi! Zii! Aka! 1x1=01
    11. Wa- nafsi (alama 4x ½ =02)
      li-wakati uliopita
      an-kauli ya kutendana
      a-tamati
    12. Kiimbo-ni kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti wakati wa utamkaji (alama 1x1=01)
      Ni kiwango cha utoaji wa sauti kutegemea ujuu na uchini wake unaowezesha kupata tofauti za hisia za msemaji
    13.  
      1. Vokali- ni sauti zinazotamkwa hewa inapotolewa bila kikwazo/kuzuiliwa (alama 1x1=01)
      2. /i/ ni sauti ya mbele ya kinywa (alama 2x 1 =02)
        • Ni sauti ya juu ya kinywa
        • Midomo hutandazika inapotamkwa
    14.  
      • Kugawika kwa njia (Alama 2x1=02)
      • Ingia katika chombo cha kusafiria
      • Paji la uso
      • Pembe kubwa inayopigwa nchani
      • Manati/chombo cha kurushia mawe
    15. Huzuni waliyokuwa nayo yatima hao ilitutia kite na imani
    16. Alitungua
    17. Ki- mfululizo wa vitendo/utokeaji wa vitendo vingi kwa wakati mmoja.
    18.  
      1. Ametumia simu kama chombo kumpiga mwanafunzi.
      2. Amepiga simu kwa niaba ya mwanafunzi.
      3. Amempiga kwa sababu ya simu
    19. Silabi mwambatano ni nini? (al 1)
      • Ni silabi ambayo ina muundo wa zaidi ya konsonanti moja
    20. Tunga sentensi moja udhihirishe maana mbili za neno hili: Rudi (al 1)
      • Rudi – adhibu mwana
      • Rudi – Rejea
    21. Pigia mstari vivumishi katika sentensi ifuatayo kisha uandike aina yake. (al 2)
      Bibi huyu ni mpole uso wake wenye haya huuinamisha kila mara.
      Huyu – Kivumishi kiashiria.
      Wake – kivumishi kimilikishi.
      Wenye – Kivumishi cha pekee.
  4. ISIMU JAMII
    • Kiswahili ni lugha ya Kibantu - Lugha ya Kiswahili ina maneno mengi ya Kibantu hivyo basi chimbuko lake ni Kibantu.
    • Kiswahili imetokana na lugha ya Kiarabu - Lugha hii ina maneno kadha ya Kiarabu. Hii yaonyesha kuwa ni lugha ya Kiarabu.
    • Kiswahili ilitokana na mchanganyiko wa lugha ya Kibantu na Kiarabu - Maneno mengi ya Kiswahili yana asili ya aidha Kibantu ama Kiarabu. Hii yaonyesha kuwa lugha hii ni uzawa wa lugha hizi mbili
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 End Term 1 Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest