Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 End Term 1 Exams

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Jibu maswali manne pekee
  • Swali la kwanza ni la lazima
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani Tamthilia, Ushairi, Hadithi Fupi na Riwaya
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili

SEHEMU YA A: LAZIMA.

FASIHI SIMULIZI

  1.  
    1. Eleza vitambulisho vya mtambaji bora wa hadithi. (alama 4)
    2. Fanani huihusisha hadhira kwa njia gani? (alama 4)
    3. Eleza mbinu mlumbi anazoweza kutumia ili afanikishe uwasilishaji wa ulumbi (alama 12)

SEHEMU YA B: TAMTHILIA 

KIGOGO - Pauline  Kea

Jibu swali la 2 au la 3

  1. “Wamenimaliza… wamenigeuka.”
    1. Weka dondoo hili katika muktadha wake.
    2. Eleza namna msemaji alivyomalizwa na kugeukwa. (alama4)
    3. Eleza jinsi wahusika wengine walivyomalizwa katika tamthilia. (alama 8)
  2. Utawala wa jimbo la Sagamoyo umejaa sumu ya nyoka.”Jadili usemi huu.(alama 20)

SEHEMU YA C: USHAIRI

Jibu swali la 4 au la 5

  1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.

    Nyoosha mkono, uviringe ngumi, unyanyuwe kwa hasira.
    Nyoosha mkono, sema hunitumi, ila haki ujira.
    Nyoosha mkono, alama ya kukataa.
    Alama ya nguvu

    Nyoosha mkono, na macho makali, uwaonyeshe kukerwa
    Nyoosha mkono , wataka halali , kwamba hutaki kuporwa
    Nyoosha mkono, alama ya kukataa
    Alama ya nguvu.

    Nyoosha mkono, umekula njama, uyakatae madhila
    Nyoosha mkono, nyanyua kwa hima, watambue hukulala
    Nyoosha mkono, alama ya kukataa
    Alama ya nguvu.

    Nyoosha mkono, jiunge umoja, na wateswaji wenzako
    Nyoosha mkono, mwonyeshe miuja, yaondoke masumbuko
    Nyoosha mkono, alama ya kukataa
    Alama ya nguvu.

    Nyoosha mkono, ivume sauti, inayojaa kitisho
    Nyoosha mkono, mumejizatiti kwa mengi maamrisho
    Nyoosha mkono,alama ya kukataa
    Alama ya nguvu.

    Nyoosha mkono, mumeshikamana, huo ukuta wa chuma
    Nyoosha mkono, kitisho hakuna , wao watarudi nyuma
    Nyoosha mkono, alama ya kukataa
    Alama ya nguvu.

    Maswali

    1. Bainisha bahari tatu zinazojitokeza katika shairi.(alama 3)
    2. Andika ujumbe mkuu unaojitokeza katika shairi hili.(alama 4)
    3. Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 4)
    4. Onyesha tamathali mbili za lugha zilizotumiwa. (alama 2)
    5. Bainisha kwa njia tatu ni vipi mtunzi amefanikiwa kutumia uhuru wa kishairi .(alama 3)
    6. Tambua toni ya shairi hili (alama 1)
    7. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hili. (alama 2)
      1. Madhila
      2. Jizatiti

        AU

  1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

    MWANA
    Kwani mamangu, u ng’ombe, au punda wadobi?
    Nakuuliza usambe, nayavunja madhehebi
    Nalia chozi kikombe, uchungu wanisibabi
    Hebu nambie
    Kweli jaza ya kiumbe, ni madhila na mapigo?

    MAMA
    Nong’ona mwana, nong’ona, nikaumiza umiyo
    Sinipe kuja sonona, kwa uchungu na kiliyo
    Babayo mkali sana, kubwa pigo la babayo
    Kwani kelele kunena, huyataki maishiyo?
    Hilo nakwambia

    MWANA
    Sitasakamwa kauli, nikaumiza umiyo
    Nikabeba idhilali, ikautweza na moyo
    Siuvuwati ukweli, hazidisha gugumiyo
    Baba hafanyi halali, nawe hwachi vumiliyo
    Hebu niambie

    Kweli jaza ya kiumbe, ni madhila na mapigo?
    Nambie ipi sababu, ya pweke, kwenda kondeni
    Nini ya, matulubu, kulima hadi jioni?
    Na jembe ukidhurubu, ukilitua guguni
    Yu wapi wako, muhibu, Baba kwani simuoni?
    Hebu niambie

    Kweli jaza ya kiumbe, ni madhila na mapigo?
    Baba kwani simuoni, kuelekea shambani?
    Kutwa akaa nyumbani, na gumzo mtaaani
    Hajali hakuthamini, wala haoni huzuni
    Mwisho haya ni nini , ewe mama wa imani?
    Hebu niambie

    Kweli jaza ya kiumbe, ni madhila na mapigo?
    Na kule kondeni kwako, ukatekuni kwa shoka
    Ufunge mzio wako, utosini kujitwikaKwa 
    haraka uje zako, chakula upate pika
    Ukichelewa vituko, baba anakutandika Hebu niambie
    Kweli jaza ya kiumbe, ni madhila na mapigo?
    Chakula kilicho ndani,ni jasho lako hakika
    Kisha mbioni, wapita kupokapoka
    Urudi nje mekoni, uanze kushughulika
    Ukikosa kisirani, moto nyumbani wawaka Hebu niambie
    Kweli jaza ya kiumbe, ni madhila na mapigo?

    MAMA
    Wanitonesha kidonda, cha miaka na miaka
    Usidhani nayapenda, madhila pia mashaka
    Nakerwa na yake inda, na sasa nimeshachoka
    Ninaanza kujipinda, kwa mapambano hakika
    Hilo nakwambia.

    Maswali

    1. Mtunzi wa shairi hili alikuwa na dhamira gani katika kutunga shairi hili. (alama 2)
    2. Shairi hili ni la aina gani? Toa ithibati. (alama 2)
    3. Yataje mambo yoyote matano anayoyalalamikia mwana. (alama 5)
    4. Eleza kanuni zilizotumika kusarifu ubeti watatu. (alama 5)
    5. Andika ubeti wa nane kwa lugha tutumbi (alama 4)
    6. Eleza maana ya maneno haya yalivyotumika katika shairi hili
      1. Jaza(alama 1)
      2. Muhibu (alama1)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI:

TUMBO LISILO SHIBA NA HADITHI NYINGINE - A. Chokochona, D. Kayanda 

Jibu swali la 6 au 7.

  1.  
    1. Jadili matatizo yanayowakumba wakazi wa madongoporomoka katika Tumbo Lisiloshiba. (alama 10)
    2. Ubadhirifu wa mali ya umma umetamalaki katika hadithi ya Shibe Itatumaliza. Jadili kwa kutoa mifanomwafaka. (alama 10)

      AU

  1. “Aliyeumwa na nyoka akiona ung’ong’o hushtuka .”
    1. Weka dondoo hil katika muktadha wake. (alama 4)
    2. Eleza namna mzungumziwa alivyoumwa na nyoka. (alama 6)
    3. Eleza vile mzungumziwa anaendeleza maudhui ya ushauri na ukosefu wa utu. (alama 10)

SEHEMU YA E: RIWAYA

CHOZI LA HERI - Asumpta Matei

  1. “Dada Umu, Di, ni mimi, Ni ndugu yenu. Ni hai . Auntie Sauna alishikwa na polisi.”
    1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
    2. Fafanua sifa tatu za msemaji (alama 6)
    3. Taja tamathali moja iliyotumika katika dondoo. (alama 2)
    4. Kwa nini Auntie Sauna alishikwa na polisi? Eleza kikamilifu. (alama 8)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI (LAZIMA)

  1.  
    1. Vitambulisho vya mtambaji bora.
      • sauti nzuri inayosikika
      • Kumbukumbu nzuri
      • Matumizi ya toni
      • Matumizi ya viziada Lugha/ishara
      • Matumizi ya miondoko/kunengua viungo vya mwili
      • Ushirikishi wa hadhira
      • Utambuzi na weledi wa hadhira
      • Uwezo wa ufaraguzi- kufanyia hadithi mabadiliko
      • Awe mcheshi/aibue kicheko kwa hadhira
      • Uwezo wa kukadiria kasi wakati wa utambaji
      • Avae maleba
      • Makamavu
      • Kuibua hisia zahadhira
      • Aelewe lugha ya hadhira zozote (4x1 = 4)
    2. Njia za kuihushisha hadhira.
      • Maswali
      • Kushiriki unyimbo wanazoelewa
      • Kuwapigisha makofi (2x2 =4
    3. Mbinu anazotumia mlumbi ili kufanikisha uwasilishaji wa ulumbi
      • matumizi ya miondoko
      • Matumizi ya mada zinazoafikiana na utamaduni wa hadhira
      • Kuipaza sauti yake asike vyema
      • Kuihushisha hadhira katika ulumbi
      • Matumizi ya alama ka fimbo .
      • Uvaaji wa malema
      • Ufahamu wa visa vya kihistoria vya jamii husika
      • Ujuzi wa kutumia masolugha/ishara
      • Matumizi ya lugha fasaha katika ulumbi
      • Kuwa na ukakamavu.
      • Matumizi ya vichekesho
      • Kuigiza ili kuibua hisia
      • Matumizi ya vipera vingine vya fasihi simulizi kama vile methali, ngano, nyimbo n.k
        zozote 12 x 1 =12

SEHEMU YA B: TAMTHILIA YA KIGOGO

  1. “Wamenimaliza… wamenigeuka.”
    1. Weka dondoo hilI katika muktadha wake. (alama 4x1)
      1. Maneno ya mama pima yaani Asiya
      2. Anamwambia Tunu
      3. Wako katika soko chapakazi
      4. Hii ni baada ya kupinduliwa kwa seirkali ya majoka ambaye mamapima alikuwa mfuasi wake.
    2. Eleza namna msemaji amemalizwa na kugeukwa?(alama 4)
      1. Mambo yameanza kumuendeda segemnege (Kinyume)
      2. Serikari iliyopinduliwa ilikuwa inamwinda ili imuue.
      3. Anasema wamegeuka hata kufika kuimwaga pombe yake.
      4. Anaomba ulinzi kutoka kwa akina wanasogamoyo na tunu anamhakikishia usalamu.
    3. Eleza jinsi wahusika wengine walivyo maliziwa katika tamthilia. (alama 8)
      Tunu

      Mwanaharakati huyu na kuvunjwa mguu, Mpango wa awali ulikuwa ni kumuua. Hata hivyo alipona kwa bahati tu.
      Ngurumo
      Ngurumo ananyongwa na chatu hata baada ya kuwa na manufaa makubwa katika utekelezaji maasi katika uongozi wa majoka.
      Kijana huyu anajitolea kufanya kila analoambiwa na utawala lakini anaangamizwa kwa sababu alijua siri nyingi za uongozi .
      Chopi
      Ni mlinzi wa majoka ambaye anatekeleza maovu ya utawala kama vile mateso kwa kenga ipasavyo. Hivyo katika mwendelezo uo huo majoka na kenga wakubaliana kumuua Chopi ili asitoe siri zao.
      Jabali
      Alikuwa mpinzani wa karibu sana wa majoka. Alifanyiwa njama akauwawa kwa vile kilichoonekana kama ajali ya barabarani.
  1. Utawala wa majoka katika jimbo la sagamoyo umejaa sumu ya nyoka. ‘Jadili usemi huu kwa hoja kumi.
    • Unyakuzi wa ardhi. Majoka na mshauri wake wajitwalia eneo la soko la chapakazi ili wajenge hoteli ya kitalii jambo hili linasababisha madhara makubwa kwa wananchi waliokuwa wakitegemea soko hii kukimu familia zao.
    • Mauaji ya watu : vijana watano wanauwawa wakati wa maandamano na wengine wanaumia.
    • Kuna vitisho. Wanaharakati wanaopinga utawala wa majoka wanatishwa, kuna vikaratasi vinavyo rushwa katika makazi yao ili wahame.
    • Kuangamiza wapinzani wake; Jabali aliuwawa kwa njama za Majoka na chama chake kikasambaratika . Tunu kiongozi wa wanaharakati wa kudai haki nusura auawe. Yule aliyetumwa kutekeleza mauaji yake hakutimiza lengo lake.
    • Ukosefu wa utu. Majoka hadhamini utu/uhai wa mtu. Majoka anaamlisha watu wapigwe risasi bila kujali kuwa wana haki ya kuchagua viongozi wanaotaka.
    • Tengatawala: katika jimbo la Sagamoyo kuna sumu ya nyoka: yaani uhasama unapendwa na viongozi ili kuwagawa wananchi kwa mfano Sudi ana uhasama na Boza ambaye ni mchonga vinyango mwenzake . Sababu ya uhasama wao ni kwa kuwako katika milengo tofauti ya kisiasa. Aidha , Ngurumo na kundi lake la walevi tayari wameshatiwa sumu na utawala wa majoka, hivyo wanahasimu wanaharakati, Tunu na sudi.
    • Kuzorota kwa maendeleo. Jimbo la sagamoyo limetimiza miaka sitini ya uhuru lakini bado liko nyuma kimaendeleo.
    • Rushwa: Mamapima anatoa hongo ya uronda kwa Ngurumo ili apate mladi wa kukata keki ya Uhuru. Vilevile Boza na kombe wanapokea kipande cha keki kutoka kwa Kenga ili wawe wafuasi wa utawala wa majoka vivyo hivyo kwa ngurumo , ukataji wa miti.
      • utakaji wa miti
      • kufunga soko
      • Kubomoa viosiki
      • Kuongeza kodi
      • Kutoa kibali cha kuuza pombe haramu
    • Mapendeleo Mama pima anapewa mradi wa kuoka keki.
    • Uzalishaji wa dawa za kulevya
    • Ukwame wa majoka kwa kunyemelea Ashwa.
    • Anasa ya Husda kwa kujipodoa
    • Kutozingatia usafi wa soko/mazingira
    • Ukabila: Siti na kombe wanapata vijikaratasi wahame Sagamoyo.
    • Kudorora kwa kiwango cha ellimu ; Wanafunzi wa majoka academy wamekuwa makabeji.
    • Matumizi ya vyombo vya usalama /askari/polisi kuzima maandamano
    • Kudhibiti vyombo dola na kuweka watu kwa seli bila hatia.
    • Matumizi mabaya ya rasilimali/mikopo. (20x1=20)

SEHEMU YA C: USHAIRI.

  1.  
    1. Ukawafi – Mishororo ya kwanza mitatu ina vipande vitatu
      Msuko- Kibwagigo ni kifupi
      Tarbia – Mishororo minne kila ubeti
      Ukaraguni – Vina vinavyoftofautiana
      Kikwamba kianzio nyoosha mkono
    2. Msimamo dhabiti katika utetezi wa haki, kataa kudhulimiwa na uungane na wenzako, lazima uwe na usajiri. 2x2 =4
    3. Inuka kwa ujasiri kama ishara ya kutoridhika kwa sababu unadai haki yako kwa njia halali.
      - Simama imara na ukatae kudhulumiwa na utashinda. 4x1 alama 4
    4. Taswira – nyooosha mkono
      -Misemo - Kula njama-
      - Uhuishi/ tashihisi – Sauti inayojaa kitisho. Inksari jiunge – ujiunge
    5. Lahaja – Mangi,- Kuboronga- yaondoke masumbuko, masumboko yaondoke
    6. Toni ya – kutoridhika/kulalamika kuhamasisha/kuzindua. (alama 2)
    7.  
      1. Mateso, taabu
      2. JIkaze/ Jikakamue/Jitolee/Kujibiidisha. 2x1= alama 2

        AU

  1.  
    1. Kuonyesha madhila anayopitia mwanamke/mama mikononi mwa mwanaume.
    2. Ngonjera – ni mazungumzo kati ya Mama na Mwana. (1x2 = alama 2)
    3. Kufanywa kufua nguo (aina 1, idhibati 1; jumula alama 2)
      Mama huenda shambani peke yake.
      Baba hubaki nyumbani tu na kupiga ngumzo mitaani
      Baba hamthamini mama
      Mama hukata kuni kondeni na kuzibeba kichwani.
      Mama akichelewa kufika nyumbani akitoka kondeni huadhibiwa.
      Mama ndiye hutafuta chakula( yoyote 5x1 =5)
    4. Ubeti una mishororo sita.
      Mishororo imegawika katika vipande viwili isipokuwa mshororo wa tano ambao umegawika katika kipande kimoja.
      Kila mshororo una mizani kumi nasita isipokuwa mshororo wa sita ambao una mizani tano.
      Kibwagizo kimefupishwa/ mshororo wa mwisho umesukwa.
      Mjpangilio wa vina
      bu , ni
      bu, ni
      bu,ni
      bu,ni
      mbe,go (alama 1 kwa kila jibu sahihi, jumla alama 5)
    5. Umenifanya nihisi uchungu ambao nimekuwa nao kwa miaka mingi , usidhni kuwa nayapenda madhira na mashaka, nakerwa na hali yake ya kunidhibiti kufanya jambo na sasa nimechoka, ninaanza kwa hakika kujitayarisha kwa mapambano, hilo nakwambia. (alama 4)
    6. Jaza – Malipo kwa kutenda wema/shukrani/asante (alama 1)
      Muhibu – Mpenzi (alama 1)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE

  1.  
    1. Jadili matatizo yanayowakumba wakazi wa mandogoporomoka katika Tumbo Lisiloshiba. (alama 10)
      • Wanamadongoporomoka wanadharauliwa na kutwaliwa ardhi yao.
      • Kuporwa aridhi yao imenyanyaswa na tabaka la mabwanyenye.
      • Wanawatoa katika ardhi yao na kuvunja vibanda vyao pasipo hata kuwalipa fidia.
      • Unyanyasaji huu unafanywa kwa wakazi hawa kwa kuwa hawana mtetezi.Haki imenunuliwa na wenye nacho.
      • Wanabomolewa vibanda vyao ilhali hawajaonyeshwa mahali mbadala pa kwenda kuishi.
      • Ukosefu wa haki: Watu wa mandogoporomoka hawana haki wenye fedha wanawaona wakazi hawa kama takataka tu.
      • Ardhi ya madongoporomoka inaponyakuliwa na wenye nacho wanashindwa kupata mtetezi . wanasheria wamenunuliwa na matajiri ni vigumu kupata mwanasheria mwaminifu. Mzee Mago anashauriana na wenzake namna ya kurukaviunzi hivi vya kisheira.
      • Makazi duni : Wakazi wamadongoporomoka wanaishi katika makazi yenye mandhari chafu. Kulikuwa na mashonde ya vinyesi.Wanaishi katika vibandachwara vinavyozungukwa na uozona bubujiko la maji machafu. Hakuna mamlaka yoyote ya maji taka inayojishughulisha nao.
      • Wakazi madogoporomoka wananyimwa fidia inayolingana na thamani ya makazi yao yaliyopokonywa na mabwanyenye.
      • Watu wa madongoporomoka wanaachwa njaa baada ya jitu kubwa kula chakula chote . Jitu linaingia katika mkahawa mshenzi na kuagiza kila chakula kilichopo kiletwe . jibu linabugia chote huku watu waliokuwa wamesubiri chakula hicho wakibakia njaa.
      • Wakazi wa madongoporomoka wanabaguliwa sehemu wanaoishi hakuna maendeleo yoyote kuna uchafu mwingi sana sehemu hii ilipaswa kusafishwa ili walau ifafanane na sehemu nyingine za mji ho.
      • Wanamadongoporomoka wamekosa usalama. Wanaishi kwa wasiwasi sana. Wanaamshwa kwa vishindo vya mabuldoza .
      • Askari wa baraza la mji wanaangusha vibanda vyao na kuwatimua waliokuwa bado wamelala. Jeshi la polisi linawapa ulizi askari kwa mirau na bunduki Mali zao duni zinaharibiwa.
      • Wanadongoporomoka wanalia na kulalamika kwa kukandamizwa na vyombo vya ulinzi. Wanakandamizwa kwa sababu ya umaskini wao . Matajiri wanawakandamiza. (10x1)
    2. Ubadhirifu wa mali ya umma umetamalaki katika hadithi ya Shibe Itatumaliza. Jadili kwa kutoa mifano mwafaka. (alama 10)
      • Mzee Mambo analipwa msharahra mnono kama mkuu wa wizara zote ilhali kila wizara ina waziri wake.
      • Sherehe kubwa za viongozi wa serikali ziantumia mali ya umma. Hivyo basi kuchangia ubadhilifu wa mali katika jamii.
      • Viongozi huendeleza ubadhirifu kwa kutumia mali ya umma kwa manufaa yao wenyewe. Magari ya serikari ykanatumika katika sherehe na kazi za nyumani kama vile kuleta maji katika sherehe.
      • Vyakula katika sherehe vinanunuliwa kwa pesa za umma. Pesa hizi zingetumika kuendeleza asasi za kijamii.
      • Ubadhirifu unadhihirishwa na DJ pale anapokea mabilioni ya pesa kwa kuwatumbuiza wageni katika sherehe.
      • Ubadhirifu unadhihirishwa na viongozi wa serikali wanaowachukua watu wao wa karibu na kuonelea wamefaidika kutokana na rasilmali za wanajamii bila kuzitolea jasho.
      • Viongozi wa serikali kama vile Sasa na Mbura wanaamua kujipakulia chakula kupita kiasi katika sherehe za mzee mambo na jamii yake ubadhirifu wa mali ya umma unaonekaran ambapo mali ya umma inatumika kuwaajiri mawaziri wawili wenye majukumu sawa katika wizara moja kazini . Kazi hii ingefanywe ana waziri mmoja na mshahara wa waziri wa pili ungechangia katika kuinua sekta nyingine.
      • Upeperushaji wa matangazo ya sherehe ya kiongozi binafsi katika vyombo vya habari kitaifa kwa siku nzima ni ubadhirifu wa mali ya umma. Pesa zilizotumika zingechangia pakubwa katika kuinua uchumi wa taifa.
      • Uuzaji wa dawa zilizotolewa katika bohari la kitaifa katika duka la DJ ambayo ni biashara ya mtu binafsi ni ubadhirifu wa mali ya umma.
      • DJ kulipwa kutumbuiza watu katika sherehe ya Mzee Mambo na kulipwa mabilioni ya fedha ni ubadhirifu wa mali ya umma.
      • DJ kupewa kazi ya mipango na mipangilio katika sherehe ilhali kuna mawaziri wawili wanaolipwa mshahara kwa kazi hiyo ni ubadhirifu wa mali ya umma. (zozote 10x1 =10)
  1.  
    1. Majibu
      Maelezo ya mwandishi /Msimulizi kuhusu Otii pale nyumbani Kitandani Otii alirejelea maisha yake ya awali, aliumia mguu na kupoteza umaarufu wake.
      Otii alikuwa amerejeshwa pale nyumbani mwake kwa amri ya daktari angojee kifo.
      Otii alipovunjika mguu na kutumia mikongojo miezi sita, alikataa kurejelea kandanda uwanjani.(4x1=4)
    2. Otii alikuwa uwanjani akichezea timu ya bandari FC.
      • Kutokana na uhodari wake alikuwa mwiba kwenye timu kinzani ya Yanga kwene kinyang’anyirocha kuwania kombe la klabu bingwa Afrika mashariki na kati.
      • Alikuwa amewala chenga mabeki wote wa Yanga na kuelekea kufumua kiki kali kwenye eneo hatari , ndipo jibabajoja la miraba minne lilipomkwaa akaanguka
      • Alianguka vibaya kama gunia la chumvi. Picha ya eksirei ilionyesha kuwa amevunjika mfupa wa muundi na nguyoni.
      • Baada ya kuumia alitelekezwa kabisa na maafisa wa Bandari FC
      • Hata maafisa wa serikalini hawakumjali hata kidogo
      • Alitupwa kama masimbi na hakuna aliyemkumbuka
      • Maumizu na mateso hayo ndiyo kuumwa na nyoka.
    3.  
      1. Ukosefu wa utu
        • Mwandishi anonyesha kuwa utu umepotea na haupo tena katika jamii.
        • Otii anatoa mchango mkubwa kwa kuichezea timu ya Bandari FC na hatatimu ya taifa ya Harambee lakini anapovunjika mguu hakuna anaejali kipaji chake.
        • Hakuan fidia anayopewa hata baada ya kuacha mchezo huo kwa kuumizwa.
        • Chama cha watu wa nyumbani wananza kujadili mazishi ya mtu akiwa bado hai.
        • Wanachama wa chama cha nyumbani wanakosa utu na kuanza kujadili kusafirisha maiti ya Otii wakati Otii bado yu hai an anawasikiliza.
        • Rehema anakosa utu kwa kumwambukiza Otii Maradhi.
      2. Umuhimu wa kuzingatia ushauri
        • Otii anaitwa na rafiki yake na kushauriwa dhidi ya kujihushisha na msichana mrembo Rehema Wanjiru.
        • Otii anapuuza ushauri huo na kusema kuwa yuko radhi kuwa nzi na kufia kidondani.
        • Matokeo ni kuwa rehema anamuambukiza ugojwa wenye dalili za Ukimwi.Wote wawili wanafariki mtawalia.
        • Otii anamshauri mwenyekitiwa chama nyumbani azikwe Mombasa.Wao walikataa ushauri huo.
        • Baadaye wanapata ajali mbaya.

SEHEMU YA E: RIWAYA YA CHOZI LA HERI 

  1. “Dada Umu, Di, ni mimi, Ni mimi ndugu yenu . Ni hai Auntie Sauna aishikwa na polisi”.
    1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama4)

      Jibu
      Maneno haya yalisemwa na Mwaliko.Alikuwa akiwaambia Umulkheri naDick . Tendio hili lilitukia katika mkahawa na Mjaliwa walipokutana kisadfa. Hii ni baada ya mwaliko kumepeleka babake mlezi maeneo yale kusheherekea siku ya kuzaliwa kwake.

    2. Fafanua sifa tatu za msemaji (alama 6)

      Jibu
      Msemaji ni mwaliko. Ana sifa zifuatazo.
      Mwenye maadili mema, Mwaliko alipolelewa mwangemi na Neema aliinuka kuwa ghulamu ya hali ya juu akiwaheshimu wazazi na majirani na kuwatii wazazi.
      Mwenye shukrani- Mwaliko aliamua kumnunulia babake chakula cha mchana siku yake ya kuzaliwa kwenye hoteli ya Majaliwa .
      Mwenye bidii- Alifanya bidii masomoni hadi kufikia chuo kikuu . Alisajili kwa shahada ya uzamili katika taaluma ya mawasiliano na kuhitimu . Mwaliko anafanya kazi yake kwa bidii ya mchwa.
      Zozote =3 (3x2 =6)

    3. Taja tamathali moja ya lugha iliyotumika katika dondoo (alama2)
      Jibu Kuchangaya ndimi –Auntie
    4. Ni kwa nini Aunitie Sauna alishikwa na polisi? Eleza kikamilifu (alama 8)
      Jibu.
      Baada ya Umu kupiga ripoti kwenye kituo cha polisi kuwa nduguze wanuna wamepotea, polisi walifanya uchunguzia wao na kujua kuwa walitekwa nyara. Aliyetekelea kitendo hiki ni kijakazi Sauna . Sauna alikuwa akimfanyia biashara Bi Kangara. Polisi walipojua mahali alikokuwa akijificha Bi Kangara, walishika njia hadi nyumbani kwake ambako waliwatia mbaroni. Bi Kangara na Sauna Walifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la ukiukaji wa haki za watoto hivyo basi wakafungwa miaka saba gerezani na kazi ngumu.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 End Term 1 Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest