Kiswahili P3 Questions and Answers - Form 3 Term 3 Opener Exams 2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO:

  • Jibu maswali MATATU pekee
  • Swali la KWANZA ni la LAZIMA
  • Maswali mengine yachaguliwe kutoka sehemu zilizobaki
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
  • Kila swali lina alama ishirini


MASWALI

SWALI LA KWANZA NI LA LAZIMA

  1. SEHEMU YA D: USHAIRI
    Angawa mdogo, dagaa, amekomaa
    Kaanga kidogo, dagaa, atakufaa
    Kalia kinaya, dagaa, h’ondoa njaa

    Wa kwako udogo, kijana, sio balaa
    Na sio mzigo, kijana, bado wafaa
    Toka kwa mtego, kijana, sinyanyapaa

    Nasaha kidogo, kijana, ukubwa jaa
    Jikaze kimbogo, kijana, acha kukaa
    Chimbua mhogo, kijana, usibung’aa

    Na wake udogo, dagaa, ndani hukaa,
    Kuliko vigogo, dagaa, hajambaa
    Hapati kipigo, dagaa, hauna fazaa

    Maisha si mwigo, kijana ushike taa
    Sihofu magego, kijana, nawe wafaa
    Kazana kidogo, kijana, kugaaga

    Maswali
    1. Lipe shairi hili anwani mwafaka (alama 1)
    2. Eleza arudhi zilizofuatwa katika kutunga shairi hili (alama 4)
    3. Onyesha jinsi malenga alivyotumia uhuru wake (alama 3)
    4. Tambua bahari katika shairi hili (alama 3)
    5. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari (alama 4)
    6. Tambua mbinu za lugha zilizotumika katika shairi (alama 3)
    7. Eleza toni la shairi hili (alama 2)
  2. FASIHI SIMULIZI
    1. Eleza umuhimu wa Ngano za mtanziko katika jamii (al.5)
    2. Fafanua umuhimu wa maigizo ya watoto (al.5)
    3. Sifa tano za rara (al.5)
    4. Eleza dhima ya misimu kama kipera cha usemi (al.5)
  3.                      
    1. Maigizo ni nini? ( al.2)
    2. Fafanua sifa nne za maigizo. Al.4)
    3. Eleza vikwazo vya ukuwaji wa fasihi simulizi. Al.10)
    4. eleza tofauti kati ya misemo na misimu. Al.4)
  4. TAMTHILIA YA KIGOGO (PAULINE KEA)
    .`…………….wanadai kitu kikumbwa au kitu chote!`
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili al 4
    2. Tambua maudhui yanayodokezwa kwenye dondoo hili al 2
    3. Kwa kutumia hoja sita eleza namna maudhui uliotaja hapo juu yanavyojitokeza katika tamthilia ya kigogo al 6
    4. Fafanua sifa za msemewa al 4
    5. fafanua umuhimu wa msemaji al 4
  5. Jadili jinsi dhuluma inavyojitokeza katika Tamthilia ya Kigogo. (al 20)
    CHOZI LA HERI- A. MATEI
  6. “Mbona huna bashasha za kijana wa umri wako.”
    1. Eleza muktadha wa maneno haya. la 4)
    2. Ni yapi yalifuata baada ya maneno haya. ala 12)
    3. Eleza sifa nne za msemewa ala 4)
  7. “Riwaya ya Chozi la Heri inaakisi uozo uliomo katika Jamii nyingi barani Afrika”
    Thibitisha kauli hii kwa kurenjerea Riwaya al20


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1.    
    1. Dagaa au Kijana (1 x 2)
    2. Kuna urari wa vina
      • Lina beti tano
      • Mishororo mitatu katika kila ubeti
      • Lina pande tatu katika kila mshororo (4 x 1)
    3. Matumizi ya lahaja mf. Magego – Meno
      Inkisari – h’ondoa – huondoa
      Kuburoga sarufi – Na wake udogo – Na udogo wake (3 x 1)
    4. Ukara – Vina vya utao na mwandamizi havitiririki, vya ukwapi vinatiririka.
      Ukawafi – Pande tatu (2 x 1)
    5. Kijana nakupa mawaidha ya kwamba aliye cheoni kuhusishwa na makosa yote, kwa hivyo tia bidii afanyavyo mbogo uache kukaa. Chimbua mihogo utafute riziki (al. 4)
    6. Istiari / jazanda mf Jikaze kimbogo
      Methali – mf ukubwa jaa
      Msemo mf shika taa (kuwa mwangaza) taja na kutoa mfano (3 x 1)
    7. Toni ya matumaini
      Toni ya kuhimiza
      Toni ya kuonya (1 x 2)
  2.    
    1. Maigizo ni nini?
      Ni hali ya watendaji kutenda na kuiga matendo ya waty au viumbe katika jamii. [2M]
    2. Fafanua sifa nne za maigizo.
      1. Hujumuisha vitendo vinavyofanywa kiufundi.
      2. Huhususha sauti ainati
      3. Hutolewa mbele ya hadhira [ Fanani na hadhira]
        Huhitaji mahali maalum
        Hufungamana na shughuli za kijamii k.v. utambaji wa hadithi, sherehe za miviga k.m. jando, harusi, matanga…
      4. Waigizaji huvaa maleba yanayooana na hali waiigizayo.
      5. Maigizo huiga hali ya jamii kisiasa, kichumi na kitamaduni kwa nia ya kuonyesha mafanikio, udhaifu na migogoro katika nyanja za maisha.
      6. Huwa na miundo maalum ya mtiririko wa matukio k.m. utangulizi wa mchezo, ukuzaji wa mgogoro, kilele na mwisho.
      7. Huambatana na ngoma na uimbaji nyimbo.
        4 x 01 = 04
        1. Ukosefu wa utafiti wa kutosha – ingawa mengi yameandikwa kuhusu fasihi simulizi, kuna baadhi ya vipera ambavyo bado havijaandikwa sana.
        2. Uchache wa wataalam wa kuitafiti na kuiendeleza
        3. Maendeleo ya kiteknolojia na kisayansi – watu hupata burudani kupitia njia mbalimbali; rununu, runinga, tarakilishi
        4. Ukuaji wa kazi za kimaandishi k.m. ngano nyingi zimeandikwa hivyo basi hakuna haja ya utambaji.
        5. Kuhamia mjini kwa wanajamii wengi na kutangamana na watu wa jamii tofauti kumefanya uhifadhi wa fasihi simulizi kuathirika.
        6. Mtaala wa elimu kupuuza lugha za kiasili ambazo ndizo zinazohifadhi fasihi simulizi
        7. Wengine huihusisha na ukale
        8. Sababu hifadhi yake ni akilini, anayeihifadhi anaweza kuibadilisha au kufa basi fasihi simulizi kufifia
        9. Dini ya Kikiristo hupuuza baadhi ya vitendo vya miviga k.v. tohara ya wana wa kike, kurithi wake …
        10. Walimu wengi kukwepa mafunzo ya Fasihi Simulizi
          Zozote 5 x 02 = 10
          Huanza na kutumika kwa muda kisha kupotea * Hudumu
          Hujulikana na wachache *Hutumika na jamii nzima
          Hutumika kuficha siri *Haina siri
  3.    
    1.       
      1. Ngano za mtanziko
      2. Hukuza uwezo wa kupima mambo na kuamua kuteua lililo muhimu
      3. Hukuza uwezo wa kufadhiliana na kufikia uamuzi mwafaka
      4. Huonya dhidi ya kutenda bila kiwaza kwa kina
      5. Huadilisha
      6. Huburudisha
      7. Huonya dhidi ya tabia hasi kama vile usaliti
    2. Umuhimu wa maigizo ya watoto
      • Hukuza undugu na ushirikiano tofauti za kijamii
      • Hukuza ubunifu
      • Huimarisha uwezo wa kukumbuka
      • Ni kitambulisho cha jamii-watoto huigiza wayaonayo katika jamii zao
      • Hupitisha maarifa
      • Ni kiburudisho na njia nzuri ya watoto kupitisha muda
      • Huwafunza watoto majukumu yao ya utu uzima
      • Hupalilia vipaji vya uigizaji
      • Huwapa watoto ujasiri na kujiamini (6x1=6)
    3. Fafanua sifa za Rara
      • Ni hadithi fupi nyepesi za kishairi ambazo husisimua
      • Huweza kuandamana na ala za muziki
      • Nyingi zilihusu koo tukufu/zilizotajika
      • Hutolea kwa ...ya huzuni /kitanzia
      • Masuala hufumbua na kudokezwa tu
      • Lugha hujaa utendaji wa matukio
      • Hushughulikia maswala ya kawaida na ibuka kwa mtindo usio rasmi
      • Huwa na ucheshi wenye kinaya
      • Baadhi huwa za kiburi japo nyingine ni za kweli (zozote 5x1=5)
    4. Misimu
      • Huhufadhi siri
      • Hukuza uhusiano bora
      • Kuonea fahari kundi fulani kwa kuwaunganisha
      • Hutambulisha kundi
      • Huondoa makali kwenye lugha
      • Huongeza ladha katika lugha
      • Huondoa urasmi
      • Husawiri mpangilio wa jamii fulani kiuchumi (zozote 4x1=4)
        KIGOGO
  4.    
    1. Ashua anamwambia kombe maneno haya baada ya kombe kumuuliza hali ya biashara ilivyokuwa kwenye vioski vya kina Ashua.Ashua alikuwa amewaletea akina sudi,Boza, na Kombe chai na mahamri
    2. ufisadi
    3.    
      • wanasagamoyo wanatozwa kodi ya kiwango cha juu lakini hakuna maendeleo
      • Majoka analifunga soko la chapakazi kwa kisingizio kuwa linaharibia jimbo la saga moyo sifa kutokana na uchafu uliokithiri
      • Majoka na vikaragosi wake wananyakua ardhi ya umma , soko la chapakazi ilikujenga hoteli ya kifaharina kumgawia kenga kipande cha ardhihuko sokoni
      • majoka anawaambia wafuasi wa tunu kuwa ata wasipompigia kura moja ata shida kwahivyo basi huenda majoka akajihusisha katika wizi wa kura
      • Majoka anajitajirisha kupitia kwa majoka and majoka company,majoka and majoka resort na majoka and majoka academy.ukweli ni kuwa pesa alizotumia kuanzia na kuendeleza biashara hizi zimetokana na matumizi mzabaya ya umma
      • pesa anazokopa majoka kutoka nchi za mashariki na magharibi zinatumiwa kwa manufaa ya kibinafsi
        6x1
    4.    
      • mpenda amani
      • mwenye shukrani
      • Ni mkweli
      • ni mnafiki
      • ni mwenye bidii
      • Ni mwenye kushawishika haraka
      • Ni mtambuzi 2x2
    5.    
      • Ashua anatumiwa kama mwanamke Aliyeaminika kwenye ndoa kwa sababu anakataa kuhusiana kimapenzi na majoka
      • Anawakilisha wanawake wenye mapenzi ya dhati kwa waume wao licha ya changamoto ya kukumbwa na umaskini
      • Ametumiwa kuwakilisha wanawake wenye bidii na wasiobagua kazi
      • Ni kielelezo cha wazazi ambao ni walezi bora walio tayari kuyahatarisha maisha yao ili watoto wapate lishe ya ile siku 4x1
  5.       
    • Wafungwa katika gereza wanapigwa na wanadhulumiwa k.m Mkono wa Ashua unavuja damu pale kifungoni.
    • Majoka na Kenga walipanga kifo cha Jabali ili kuwaondoa wanaompinga kisiasa
    • Wafanyikazi wanahangaishwa na kuumizwa na askari wa Majoka wanapogoma.
    • Wanasagamoyo wanatozwa kodi zaidi ya inavyohitajika ilhali kodi hiyo haitumiki ipasavyo.
    • Majoka anawadhulumu wachuuzi wa soko la Chapakazi anapotoa amri ya kufungwa kwa soko hilo na kupanga kulinyakua ili kujenga hoteli ya kifahari.
    • Majoka anatumia njama ya kikatili kumnasa Ashua anapofika ofisini mwake. Anaamuru askari wamtie nguvuni kwa madai ya kuzua vurugu katika ofisi ya serikali.
    • Majoka anakosa kuwatenganisha Husda na Ashua, badala yake anawaeleza waende wapimane nguvu, wapatane wasipatane ni shauri yao na kusema hana time ya wanawake.
    • Majoka anamdhulumu Ashua kimapenzi.
      Anajaribu kumtongoza Ashua huku akifahamu vizuri kuwa Ashua ni mke wa Sudi.
    • Wenyeji wa jimbo la Sagamoyo wanapanga kuwafurusha wengine ambao si wazaliwa wa Sagamoyo ili wabaki peke yao.Wanaandika na kutupa vijikaratasi vinavyowaagiza wahame.
    • Vioski vya wachuuzi vinabomolewa kutokana na amrisho la Kenga. Badala ya kumkashifu, Majoka anapendezwa na kazi yake Kenga na kumwahidi kipande cha ardhi sokoni.
    • Majoka na vibaraka wake wanafuja pesa za umma na kushindwa, kusafisha soko la Chapakazi hata baada ya kutoza kodi zaidi. Soko halikaliki kutokana na uvundo.
    • Viongozi wanatumia chatu ambao ni Wanyama hatari kuwa walinzi wao. Chatu hawa wanaishi kusababisha vifo kwa watu kiholela. (10x2=20)
  6. Chozi la heri
    1. Haya ni maneno yake mwalimu Dhahabu kwa umulkheri. Ni katika shule ya Tangamano. Hii ni baada ya mwalimu Dhahabu kumpa umulkheri ripoti kuhusu maendeleo yake shuleni wanapoelekea likizoni na kuona hana furaha. (Ala 4)
    2.      
      • Umulkheri anamweleza mwalimu Dhahabu kuwa alikuwa na hamu ya kuishi nyumbani kuliko na wazazi.
      • Mwalimu Dhababu alimpigia simu rafiki yake wa utotoni,Apondi na kumweleza kadhia ya Umu.
      • Apondi alikubali kumchukua Umu kama mtoto wake wa kupanga.
      • Apondi anashauriana na mumewe Mwangeka ambaye hakuwa na pingamizi yoyote kuhusu kuwa mlezi wa Umulkheri.
      • Umu alipata wazazi wapwa na humo ndimo alimomalizia siku zake za likizo.
      • Umu aliwazoea na kuwapenda wazazi wake wapya kwa dhati. Alikuwa tayari kumsamehe mama yake na aliwazia pia kumsamehe Sauna.
        (ala 6 x 2 = 12)
    3. Msemewa ni Umulkheri.
      • Mwenye busara. Anapowakosa ndugu zake,anawatafuta kila mahali na hatimaye kupiga ripoti kwenye kituo cha polisi kuhusu kupotea kwa watoto wao.
      • Mwenye upendo. Anawapenda ndugu zake,na hivyo anatia bidii kuwatafuta.
      • Mwenye huruma na utu. Anawahurumia sana vijana wa mtaani na kutaka kuwasaidia.
        Anamwomba mamake pesa kidogo aweze kumsaidia kijana mmoja.
      • Mpenda haki. Alijitahidi kutafuta haki yake na ndugu zake na kuamua kuulinda utu wake kwa hali na mali. (Ala 4)
  7.      
    • Mauaji- K.m Tery na wanawe walikumbana na janga la kifo baada ya kuchomwa wakiwa ndani ya nyumba yao.
    • Dawa za kulevya- Dick alipotekwa nyara alilazimika kuuza dawa za kulevya kwa muda wa miaka kumi.
    • Ukabila – Ukabila unajitokeza wakati vita vinapozuka baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya.
      Majirani pia wanawageuka wenzao ambao walikuwawametoka katika kabila au ukoo tofauti na wao.
    • Ulevi – Kuna matumizi ya pombe haramu k.m vijana wa vyuovikuu wanabugia pombe yenye sumu inayowafanya wengine kuaga dunia.
    • Ukeketaji – Wasichana wa shule ya msingi wanapashwa tohara. Wengine wanayapoteza maisha yao huku wengine wakiponea chupuchupu.
    • Ndoa za mapema- Wasichana wachanga wanalazimishwa kuolewa na vizee na kuacha masomo yao
    • Usherati – Bi. Kimai alipoondoka kwenda shambani Bw. Tenge angeamua kumleta mwanamke mmoja baada ya mwingine.
    • Mahusiano ya kimapenzi kati ya walimu na wanafunzi k.m Fumba na mwanafunzi wake Rehema.
    • Ufisadi- Watoto kutoka familia zinazojiweza kiuchumi kupewa mikopo/ Ruzuku nao wana wa maskini kulazimika kufanya vibarua wakati wa likizo ili kujilipia karo.
    • Utekaji nyara- Dick anatekwa nyara na kulazimishwa kuuza dawa za kulevya.
    • Uavyaji mimba- Sauna anapopachikwa mimba na babake, mamake alimsaidia kuavya na kumwonya dhidi ya kumwambia yeyote kuhusu unyama wa babake.
    • Mahusiano ya kimapenzi bainai ya watoto na wazazi wao- Sauna anashirikiana na babake mlezi kimapenzi na kuishia kupachikwa mimba.
    • Ajira kwa watoto- Watoto wa darasa la tano kuhuzishwa katika kazi ya kuchuna majani chai kwa malipo kidogo m.f Chandachema
    • Wizi/uporaji wa mali- Wakati vita vinapozukabaadhi ya watu wanaonekana wakipora maduka ya Kihindi, Kiarabu na hata ya Waafrika wenzao
    • Ubakaji – Genge la mabarobaro watano linawabaka Lime na Mwanaheri hadharani.
    • Ulanguzi wa watoto- Bi. Kangara na Sauna walifanya biashara haramu ya kuwauza watoto wa vijana.
    • Kutupwa kwa watoto- Neema anakiokota kitoto kichanga kikiwa kwenye karatasi ya Sandarusi kwenye mchafukoge wa taka.
      (Zozote 10 x 2= 20)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili P3 Questions and Answers - Form 3 Term 3 Opener Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest