Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 End Term 3 2022 Exams

Share via Whatsapp

MASWALI

  1. UFAHAMU
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali:
    Kwa nafsi ya pekee napenda kupongeza hatua ya wananchi wa kanda mbalimbali kupata nafasi ya kushiriki katika jukwaa la wazi ili kuzungumzia mambo yanayoathiri afya za wasichana na wanawake nchini.
    Masuala matatu yanayoathiri afya za wasichana na wanawake yamekuwa yakijadiliwa ambayo ni vifovya uzazi, vipigo kwa wanawake na ukatili dhidi ya wasichana walioajiriwa kufanya kazi majumbani.
    Lengo kubwa la majadiliano hayo ni kuuwezesha umma kujadili jinsi gani matatizo hayo yanaweza kupungua nchini na ndio maana watu wa mamlaka mbalimbali, wanasheria, madaktari, wanaharakati wa haki za kibinadamu wa wananchi kwa jumla.
    Nashukuru kuwapo kwa jukwaa hili kwani washika dau wameamua kujadili suala la vifo vya wanawake kwa sababu tatizo hilo ni kubwa na wanawake wanaendelea kupoteza maisha kila siku wakati jamii inaweza kuokoa maisha yao.
    Ripoti ya taifa kuhusu watu na afya ya mwaka 2004/2005 inakadiriwa kuwa idadi ya wanawake wanaofariki kutokana na matatizo ya uja uzito ni 24 kwa siku, wakati kila mwaka wanawake 578.
    Pamoja na kwamba sera na sheria zipo lakini kumekuwa na mzunguko mrefu wa kushughulikia matatizo yanayowakabili wanawake.
    Umefika wakati jamii inapaswa kutambua kazi ya wafanyakazi wa majumbani ni taaluma na iheshimiwe na vile vile umefika wakati wa kuokoa maisha ya akina mama wajawazito lakini yatawezekana iwapo kila mmoja katika jamii atawajaibika na kuchukua nafasi yake kuzuia manyanyaso zaidi dhidi ya wanawake wa Kiafrika.
    1. Eleza azma ya mwandishi wa makala haya. (alama 2)
    2. Pendekeza anwani ya makala haya. (alama 1)
    3. Taja masaibu yanayowakumba wanawake ukirejerea kifungu hiki. (alama 3)
    4. Eleza kizingiti kikuu cha kukambili matatizo ya wanawake kulingana na taarifa hii (alama 2)
    5. Taja hatua tatu ambazo washika dau wafaa kuchukua ili kutatua tatizo hili linalokumba wanawake. (alama 3)
    6. Eleza maana ya msamiati na mafungu yafuatayo kama yalivyotumika kwenye makala. (alama 4)
      1. Kushiriki katika jukwaa ...........................................................................................................................
      2. Kumekuwa na mzunguko ........................................................................................................................
      3. Wadau ......................................................................................................................................................
      4. Sera ..........................................................................................................................................................
  2. UFUPISHO
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
    SUBIRA HUVUTA HERI
    Alipofika umri wa kuvunja ungo, Sarabi alikuwa kibamba aliyevutia yeyote aliyemtia jicho. Ama kweli,kidosho huyu alikuwa mtanashati aidha mlimbwende mithili ya mbega. Naam, alikuwa dhairi shairi kwamba Manani alichukua siku ayami katika kuliwazisha umbo lake tebwere.Chambilecho wahenga na wahenguzi, chema chajiuza kibaya chajitembeza.
    Hata hivyo,shakawa si dawa ya kosa.Sarabi alijipata katika aila fukara hohe hahe.Wavyele wa kipusa huyu hawakuwa na mbele wala nyuma.Bukrata wa ashiya ilikuwa ni kukuru kakara katika harakati za kupata riziki.Cha mno ni kwamba iliwabidi kupanga mbavu huku matumbo yakililia haki zao. Naam, ulitima uliendelea kuwaandama falau kupe kwenye mkia wa ng’ombe.
    Maadam ya uchefuchefu wa dirhamu, mwana mwali huyu hakudiriki kuitia ozi milango ya shule.
    Wasemao husema kuku wa mkata hatagi,na akitaga hatotoi, na akitotoa hutwaliwa na mwewe. Sarabi alijawa na simazi kuona mahirimu wake wakijishasha kuwa wameelimika na kudai kuwa yeye alikuwa chizi bin bozi,yaani ,mbumbumbu mzungu wa reli. Hata hivyo hakukata tamaa.Alijipa moyo kuwa mja hajikuna ajipatapo.

    Muda aliota mbawa na kupaa upesiupesi.Aushi ya Sarabi iliingia masika.Naam, mambo yakawa magumu kama kifuu cha nazi. Hapo ndipo aliamua kuwa maji yamezidi unga. Akawaaga wavyele wake na kukimbilia mjini kutafuta gange.Aisee! Mwenda bure si mkaa bure mathalani huenda akafumaniwa na nyota ya jaha!
    Mji ulimpokea kwa mikogo na vitushi.Alipatwa na vikwazo hapa na pale. Ni yale yale ya mahenga kuwa jogoo wa shamba hawiki mjini aidha limbukeni hana siri.Kwa siku nenda siku rudi, alikanyaga lami huku akitumai kuwa atabahatika lakini wapi! kokote alikoenda vibao vya "HAKUNA KAZI" vilimkaribisha. Kukuli kuntu, alijipiga moyo konde na kujipa uhakikisho atafutaye hachoki na hakichoka keshapata.
    Maulana si Athumani.Baada ya kutaataa hapa na pale kikuti kilimwangazia.Akabahatika mithili ya tasa aliyejaliwa mwana wa kipekee. Waima , mtegemea Rabuka katu si mtovu. Sarabi alijawa na bashasha mpwito mpwito sitataja kipovu aliyetanabahi yuaona.Gange aliyoipata ilikuwa ni ya tarishi katika shirika la uchukuzi na mawasiliano.Gange bambam na sheshe !
    Sarabi alimaizi fika kuwa mchumia juani hulia kivulini. Wakuu zake hawakutoma kumnyeshea sifa fokofoko maadam ya jitihada alizobainisha pale kazini. Haikuchukua muda kwake kupandishwa cheo mfululizo huku akipata donge nono la mshahara.Chambilecho magalacha wa lugha, chanda chema huvikwa pete aidha mcheza kwao hutuzwa.
    Banati huyu aliwajengea wavyele wake kasri akhiyari kule mjini. Akawafuta machozi ya ufasiki na kuwavika taji la ukwasi mkuu. Wanajamii walipokea pumbao wasiweze kuamini.Iweje wakati hohe hahe wapinduke kuwa mabwenyenye wa kupigiwa mifano? Wengi waliwaonea gere lakini hilo halikuwanyima ile ari ya kupiga hatua.
    Sarabi alikuwa mfano maridadi kabisa wa jinsi jitihada zinavyoleta ufanisi mkuu aushini.Nilitazama haya yote kwa mshangao.Ama kweli ulimwengu ni uga wa mafunzo tele .Kila uchao mja hana budi kujijuza mapya na kupata upenye zaidi.Shabashi!
    1. Huku ukirejelea uthibitisho wa methali hii, onyesha sehemu ya kwanza namna subira imebainika katika maelezo haya(Tumia maneno 70-80 (alama 7) (Mtiririko alama 1)
      Matayarisho
      Jibu
    2. Fupisha ujumbe uliomo katika makala haya na uonyeshe sehemu ya pili ya methali "Subira huvuta heri "( maneno 70) (alama 5 ) (Mtiririko 2)
      Matayarisho
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Huku ukionyesha mifano, fafanua dhana ya kiimbo. (alama 2)
    2. Weka nomino ‘chai’ katika ngeli mwafaka.Onyesha upatanisho wa kisarufi kwa kutunga sentensi. (alama1)
    3. Andika katika wakati ujao ‘me’ timilifu
      Kisu kilimkata mwizi akafa (alama 2)
    4. Yakinisha sentensi ifuatayo.
      Tafadhali usimwazime kalamu, hatakurudishia. alama 1
    5. Toa sifa bainifu za sauti ‘k’ na ‘j’ (alama 2)
    6. Tumia maneno haya katika sentensi kulingana na maagizo
      1. Kasi(nomino) (alama1)
      2. Kiziwi (kivumishi) (alama1)
    7. Ainisha sentensi hii kiuamilifu
      Mzazi amemwandikia mwalimu chakula mezani (alama 3)
    8. Changanua sentensi kimuundo kwa kutumia matawi .
      Mchezaji atakayeshinda atatuzwa zawadi murua. (alama 4)
    9. Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya kivumishi cha pekee cha kusisitiza (alama1)
    10. Nyambua katika kauli ya kutendata
      1. okoa (alama 1)
      2. suka (alama1)
    11. Andika katika usemi halisi;Rukia alimwambia Juma kuwa shughuli yao ingemalizika siku iliyofuata.ala.2
    12. Eleza matumizi mawili ya alama ya dukuduku.
      Toa mfano (alama 2)
    13. Sahihisha sentensi :Bahari ambayo iliyochafuliwa imetulia. (alama 1)
    14. Tambua dhana inayojitokeza katika sentensi
      Sawa ! Nitakurudishia kitabu chako. (alama 1)
    15. Onyesha shina la kitenzi katika neno ‘walipigana’. (alama 1)
    16. Ainisha viambishi- Tuliyemkaribisha (alama 3)
    17. Tambua hali tatu tofauti katika sentensi .
      Alipokuwa akicheza alianguka akavunjika mguu. (alama 3)
    18. Tambua aina za nomino katika sentensi
      Kuongoza kwa mtawala huyo kumewaletea wasomali dhiki kuu. (alama 2)
    19. Nyoka huyu amemuuma msichana Yule. Andika katika ukubwa. (alama2)
    20. Onyesha matumizi ya aina mbili kuu za viwakilishi vya nafsi. (alama 2)
    21. Tambua kirai na kishazi :Baba na mama waliofika jana wameondoka. (alama 1)
  4. ISIMU JAMII
    1. Eleza dhana ya uwingi lugha kama kipengele cha isimu jamii (alama 2)
    2. Fafanua mambo manne yanayochangia uwingi lugha katika jamii (alama 8)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA LUGHA

  1. Ufahamu
    1.                
      • Kuonyesha masaibu yanayowakumba watoto wasichana.
      • Kuhamasisha watu wafuate suluhu ya masaibu ya watoto wasichana. zozote2x1=2
    2.                    
      • Afya za watoto wasichana.
      • Masaibu ya mtoto msichana. 1x1=1
    3.                      
      • Vifo vya wazazi.
      • Kuchapwa kwa wanawake.
      • Ukatili dhidi ya watoto –yaya.
      • Sera hazitekelezwi kumsaidia msichana. zozote 3x1=3
    4. Sera zipo lakini serikali huchukua muda mrefu kuzitekeleza. 1x2=2
    5.                    
      • Sera zote zitekelezwe kwa wakati kuhusu watoto wasichana.
      • Jamii itambue umuhimu wa wafanyikazi wote.
      • Kila mtu azuie kunyanyaswa kwa mtoto msichana. (sahihisha hoja za kwanza tatu zozote 3x1=3)
    6.                            
      1. Kutetea hadharani.
      2. Kuchukua muda mrefu kutekeleza jambo.
      3. Washiriki wote/wahusika wote.
      4. Mbinu/njia/mikakati ya kutafuta. 4x1=4
        KUTUZA: Ondoa ½ alama alizotuzwa kwa kila kosa la sarufi.
        Ondoa ½ alama kwa kila kosa la hijai hadi makosa 6
  2. UFUPISHO                   
    1.                      
      • Sarabi alikuwa mrembo ajabu.
      • Alikuwa maskini ajabu –familia yake.
      • Wazazi wake walitaabika kupata riziki.
      • Kila aina ya ulitima ilimwandama.
      • Yeye hakupata elimu.
      • Wenzake walimkejeli kwa njia nyingi kitongojini.
      • Alivumila masimango hayo yote.
      • Daima alikuwa mwenye simanzi
      • Aliamua kwenda mjini kutafuta riziki.
      • Alitafuta kazi mjini lakini mambo yalitumbukia nyongo.
      • Yeye hakufa moyo, alijikaza zaidi. zozote 7x1=7
    2. Namna subira ilifuta heri.
      • Alipata kazi hatimaye kama tarishi.
      • Alifanya kazi kwa bidii kwa matumaini.
      • Uzembe aliuwekwa kando.
      • Wakuu wa kampuni walitambua bidii yake na kupandishwa cheo.
      • Mshahara wake uliongezwa pia.
      • Aliwajengea wavyele wake kasri kule mjini.
      • Waliishi kwa furaha tele.
      • Wengi walistaajabu maskini kuwa tajiri. zozote 6x1=6
        2B sfsfsfs
        UTUZAJI
      • Makosa ya sarufi – ondoa ½ alama hadi makosa 6x½=3
      • Makosa ya hijai/tahajia – ondoa hadi makosa 6x½=3
      • Ziada – maneno 10 ya kwanza ondoa alama 1, kila maneno 5 ya ziada ½ alama.
  3.                                        
    1. Hali ya mpando na mshuko wa sauti wakati wa utamkaji wa maneno katika sentensi.
      mfano;
      • Mwalimu anadundisha. (kauli/taarifa)
      • Mwalimu anafundisha!(mshangao ) Mwalimu anafundisha?(swali)
        maelezo -1x1=1
        Mfano mmoja-1x1=1
    2. Ngeli ya I-I –chai imemwangika. Ngeli-½
      sentensi ½
    3. Kisu kitakuwa kimemkata mwizi hadi afe. al.2
    4. Tafadhali mwazime kalamu atakurudishia. al.1
    5. k - si ghuna, ni ya kukaa laini.
      J - ni ghuna, ni ya kukaa ngumu. zozote 4x½=2
    6. Kasi aliyokuwa nayo hangeepuka ajali hiyo. al.1
      Mwanafunzi kiziwi ametunzwa. al.1
    7. Mzazi – kiima.
      Mwalimu – shamirisho yambwa /kitondo.
      Chakula – shamirisho yambwa /kipozi.
      Mezani – chagizo. zozote 3x1 =3
    8.                                   
      h ygvabyghdba
    9. Mwanafunzi mwenyewe amejaribu mchezo huo.
      - kutilia mkazo 1x1=1
    10. Okota. al. 1
      Sokota. al. 1
    11. "Shughuli yetu itamalizika kesho".Rukia alimwambia Juma. zozote 4x½=2
    12. - Huonyesha kuwa kuna usemi uliokatawa kabla ya kumalizika. mfano:
      A: Asiye na wake.............
      B: Aeleke jiwe!
      - Kuonyesha neno lililoachwa ambalo labda huenda likawa la kimatusi au lisilokuwa la adabu.
      - Kuonyesha takwimu zilizoachwa.Mfano 2013-’14. 2x2=4
    13. - Bahari ambayo imechafuliwa imetulia.
      au Bahari iliyochafuliwa imetulia. 1x1=1
    14. Hisia za kukubali/kuridhia. 1x1=1
    15. -pig– shina la kitenzi /mzizi wa kitenzi.
    16. Tu- li-ye-m-karibi-sh-a.
      Tu- kiambishi awali nafsi ya kwanza wingi.
      -li- " " wakati uliopita .
      -ye- " " ‘o’ rejeshi.
      -karibi –mzizi wa kitenzi.
      -sh- kiambishi tamati kauli
      -a- " " kiishio. ½x6=3
    17. -Hali ya –‘po’ ya wakati maalum.
      -Hali ya ‘ki’ ya kuonyesha kitendo kimoja kikitendeka kingine kilikua kikiendelea.
      -Hali ya ‘ka’- Mfuatano wa matukio. ½x6=3
    18. -Kuongoza- nomino ya kitenzi /jina.
      -Mtawala- nomino ya kawaida.
      -Wasomali- nomono ya pekee.
      -Dhiki- nomino ya dhahania. zozote 4x½=2
    19. Joka hili limeliuma jisichana lile. ½x4=2
    20. Viwakilishi nafsi huru –mimi ninafunza.
      -wewe unasoma.
      -yeye anasoma.
      W-nafsi viambata -ninasoma.
      -unasoma.
      -anasoma.
      Taz - Aina -2x½=1
      Mifano 2x½=1
    21. Baba na mama –Kirai nomino.
      waliofika jana - kishazi tegemezi.
      Wameondoka -kishazi huru. zozote 2x½=1
  4.                          
    1. Ni hali ya mtu au jamii ya watu kuweza kuzitumia lugha zaidi ya mbili. alama 2
    2. Ndoa baina ya watu wasio wa kabila /taifa moja.
      • Ujirani wa makabila /mataifa tofauti.
      • Sera za lugha za wakoloni zilizowalazimu waafrika wa Afrika mashariki kujifunza lugha wawasiliane.
      • Sera za lugha za nchi husika zinazoteua lugha fulani zifuzwe shuleni ziwe rasmi au za taifa.
      • Mavamizi /vita/uhamaji.
      • Dini.
      • Elimu.
      • Uchumi na biashara .
      • Hali ya mwingiliano wa watu mijini. zozote 2x4=8
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 End Term 3 2022 Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest