Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 End Term 3 2022 Exams

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
  Kiapo kwao majaji, wanosimamia haki
  Kwa sharia ni magwiji, wahalifu hawatoki,
  Wengi wao ni walaji, kwa rushwa ni mashabiki,
  Kwa rushwa mashabiki.

  Kiapo kwa daktari, wagonjwa hawadhiliki,
  Kazi zao ni dhariri, maradhi hayakwepeki,
  Na wengine ni hatari, bila pesa hutibiki,
  Bila pesa hutibiki.

  Kiapo cha mawaziri, kwa mbwembwe na itifaki,
  Na suti zao nzuri, shingo tai haitoki,
  Na wengi wana dosari, ni kwa mikataba feki,
  Ni kwa mikataba feki.

  Kiapo cha magavana, mikoa kuimiliki,
  Hujifanya ni mabwana, wala hawasogeleki,
  Nayo nchi huitafuna, na kuwa haikaliki
  Na kuwa haikaliki

  Kiapo cha maraisi, kwa mizinga na fataki,
  Na wageni mahususi, hualikwa kushiriki,
  Ikulu wakijilisi, kwa wizi hawashikiki
  Kwa wizi hawashikiki. 

  Viapo vya utiifu, kwa sasa havistahiki
  Wanoapa ni wachafu, tena hawaaminiki,
  Biblia misahafu, washikapo unafiki
  Washikapo unafiki

  Maswali

  1. ‘’Dhamira ya shairi hili ni kushtumu ukiukaji wa maadili ya kikazi.’’ Jadili. (alama 3)
  2. Eleza namna vipengele vifuatavyo vya kimtindo vilivyotumika katika shairi hili.
   1. Usambamba ( alama 2)
   2. Aina za taswira ( alama 3)
  3. Bainisha toni katika shairi hili. (alama 2)
  4. Fafanua mbinu mbili alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. (alama 4)
  5. Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo; ( alama 3)
   1. Mpangilio wa vina
   2. Mizani
   3. Mpangilio wa maneno
  6. Fafanua muundo wa shairi hili. (alama 3)

Sehmu ya B
Tamthilia ; Kigogo – P Kea
Jibu swali moja kutoka sehemu hii
2. “Na mwamba ngoma huvuta wapi?”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili (ala. 4)
 2. Tambua tamathali mbili za sauti zilizotumika katika muktadha huo (ala. 2)
 3. Fafanua sifa za msemewa wa maneno (ala. 3)
 4. Eleza umuhimu wa msemaji katika kuijenga Tamthilia hii. ( ala.3)
 5. Thibitisha ukweli kuwa kila mwamba ngoma huvuta kwake ukirejelea Tamthilia nzima ya Kigogo (ala. 8)
  au

3. Eleza jinsi maudhui yafuatayo yanavyojitokeza katika Tamthilia ya Kigogo

 1. Utabaka (alama 5)
 2. Usaliti (alama 5)
 3. Umaskini ( alama 5)
 4. Dhuluma ( alama 5)

Sehemu ya C
Hadithi Fupi
Jibu swali moja kutoka sehemu hii

4.

 1. Eleza jinsi maudhui ya umaskini yanavyojitokeza katika hadithi ya Mapenzi ya Kifaurongo. (alama 4)
 2. Onyesha jinsi unafiki unavyojitokeza katika hadithi, “ Shogake Dada ana Ndevu” ( alama 4)
 3. changanua mtindo katika dondooo lifuatalo. ( alama 6)
  “Bi. Hamida alitunga donge kifuani mwake. Na donge likaja juu. Likampanda na kumsakama kooni. Kweli? Uongo? Kweli au uongo yale maneno ya binti yake? Labda kweli anamfikiria mambo mabaya binti yake tu. Labda kweli, dhana yake ni mbovu. Bi. Haminda alichanganyikiwa na mambo. Alivutwa huku na huku na nafsi yake yenye chagizo. Upande mmoja sauti yake ya ndani ilikuwa inamtetea Safia, na upande wa pili wa nafsi yake ilikuwa ikimshuku Safia; na sauti zake zote mbili hizo zimo ndani ya kiwiliwili chake zinamvuta yeye mtu mmoja, Bi. Haminda. Hatimaye hakutambua afanye nini.
 4. sekta ya elimu imekumbwa na changamoto nyingi. Thibitisha ukirejelea hadithi zifuatazo; ( alama 6)
  1. Mtihani wa Maisha
  2. Mwalimu Mstaafu
   au

5. “ ukiukaji wa haki za watoto ni suala ambalo limeshughulikiwa katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine.’’ Jadili ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi zozote nne. (alama 20)

Sehemu ya D
Riwaya Chozi la Heri- Assumpta K
Jibu swali moja kutoka sehemu hii.
6. “…. Unatumia mantiki gani kusema sisi si watoto wa miaka hamsini?”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
 2. Taja mbinu ya lugha inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 1)
 3. Kwa kutumia hoja nane, onyesha jinsi ukoloni mamboleo umeendela kutawala waafrika (alama 8)
 4. Eleza wasifu wa msemaji wa maneno haya. ( alama 4)
 5. Eleza umuhimu wa msemewa wa maneno haya. (alama 3)
  au

7. Eleza athari za siasa za ukabila na ubabedume kwa mujibu wa riwaya ya Chozi la Heri. (alama 20)

Sehemu ya E
Fasihi simulizi
8.

 1. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
  “Mwanangu, dunia haitaki papara. Ikiwa unataka kufanikiwa katika mustakabali wako kuwa mtoto mtiifu na mwongofu. Kumbuka kuwa asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu…”
  1. Tambua na ueleze kipera hiki cha fasihi (alama 2)
  2. Eleza sifa tatu za kipera hiki. (alama 3)
  3.                      
   1. Fafanua dhima tano za kipera hiki katika jamii. (alama5)
   2. Fanani anawezaje kuihusisha hadhira katika usimulizi wake?(alama 4)
   3. Eleza utaratibu unaofuatwa wakati wa kutega na kutegua vitendawili. (alama 6)

MAJIBU YA KARATASI YA TATU

 1.                    
  1. ukiukaji wa maadili ya kikazi
   • majaji wanaostahili kutetea haki ni walaji rushwa
   • madaktari hawawajibiki kwa matibabu na kuwa magonjwa hayatibiki
   • madaktari wanakwenda kinyume na kiapo chao kwa kuweka pesa mbele.
   •  Licha ya mbwembwe nyingi za kiapo cha mawaziri, wana mikataba ghushi.
   • Magavana wanatafuna nchi na kuwa haikaliki.
   • Viongozi ni wanafiki hawaaminiki.
   • Maraisi wanashabikia wizi.
   • Waapaji ni wanafiki
    Zozote 3
  2. mbinu za kimtindo
   1. usambamba
    • Kila ubeti unaanza kwa neno kiapo
    • Sehemu ya utao ya mshororo wa tatu katika kila ubeti inarudiwa katika kimalizio
     Alama 2
   2. aina za Taswira
    • Taswira oni- kiapo cha mawaziri, shingo tai haitoki
    • Taswira sikivu- kwa mizinga na fataki
    • Taswira mwonjo- wengi wao ni walaji
     Alama 3
  3. toni katika shairi
   • Kulalamika- kuna ukosefu wa uwajibikaji kazini
   • Kushtumu/ kusuta- majaji wanaostahili kutetea haki ni walaji rushwa
    1*2= 2
  4. idhini/ uhuru wa mshairi
   • Utohozi- feki
   • Tabdila- dakitari
   • Kuboronga sarufi- shingo tai haitoki
   • Inkisari- wanosimama- wanaosimama
    Alama 4
  5. Aina ya shairi
   1. Mpangilio wa vina- ukara- vina vya nje vinatiririka ilhali vya ndani vinabadilika badilika
   2. Mizani- msuko- kimalizio kimefupishwa
   3. Mpangilio wa maneno- kikwamba- neno kiapo limetumika kuanzia mwanzo wa kila ubeti.
    Pindu- sehemu ya utao ya mshororo wa tatu katika kila ubeti inarudiwa katika kimalizio
    Alama 3
  6.                
   1. shairi hili lina beti tano
   2. kila ubeti una mishororo mine
   3. lina pande mbili; ukwapi na utao
   4. kituo kimefupishwa
   5. vina vya nje vinatiririka ilhali vya ndani havitiririki
   6. mizani 8, 8 kwa kila mshororo ila kwa kituo n inane.
    Zozote 3
    Tamthilia kigogo
 2. “Na mwamba ngoma huvuta wapi?
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
   1. Msemaji ni Kenga
   2. Msemewa ni Majoka
   3. Wako katika ofisi ya Majoka
   4. Ni baada ya Majoka kumwelezea kuhusu habari gazetini kuhusu maarufu wa Tunu
    (4 x 1 = 4)
  2. Tambua tamathali mbili za semi zilizotumika katika muktadha huu (alama 2)
   1. Methali – mwamba ngoma huvuta……
   2. Swala la balagha - huvuta wapi?
    (1 x 2 = 2)
  3. Fafanua sifa sita za msemewa wa maneno haya
   Msemewa ni Majoka
   • Ni katili – alishiriki katika mauaji ya Jabali
   • Ni mkware - Alikuwa amemuoa Husda lakini alitaka kujihusisha kimapenzi na Ashua
   • Ni mpyaro – aliwatukana wanasagamoyo wajinga
   • Ni fisadi – alinyakua mali ya uma kam vile soko la chapakazi
   • Ni msaliti – Aliwasliti wanasagamoyo kwa kuwa walimchagua ilhali anajinufaisha yeye, pia anamsaliti Husda kimapenzi.
   • Ni mwenye dharau
   • Ni laghai
   • Ni dikteta
   • Ni mwoga zozote 3
  4.                        
   • Ni kielelezo cha washauri wabaya
   • Anasaidia kuibua maudhui ya ubinafsi, ukatili
   • Ametumiwa kujenga tabia za wahusika wengine kama vile ukatili wa Majoka
   • Ametumia kuibua migogoro na dhamira ya mwandishi
    Zozote 3
  5. Thibitisha ukweli kuwa kila mwamba ngoma huvuta kwake ukirejelea Tamthilia nzima ya Kigogo (alama 8)
   • Kenga anamfuata Majoka na uongozi dhalimu kwani ananufaika nao. Mfano ardhi
   • Ngurumo anaunga mkono uongozi dhalimu wa Majoka ili aendelee kunufaika. Mfano pombe.
   • Mama pima anautetea uongozi wa Majoka kwa kuwa ananufaika nao, mfano. Kandarasi ya kuoka keki, kibali cha kuuza pombe haramu
   • Majoka ana ari ya kuwafurusha wafanyabiashara kutoka sokoni ili alinyakue kwa matumizi yake kibinafsi ya kujenga hoteli ya kifahari.
   • Wafadhili wa kina Tunu wanatia habari chumvi kuhusu umaarufu wa Tunu.
   • Wanapolisi wanayafuata maagizo ya Majoka ya kuwashambulia wanasagamoyo ili walinde kazi yao.
   • Chopi anatekeleza uhuni wa Majoka ndiposa asije akamwaga unga wake. (Kufutwa kazi)
   • Husda anaolewa na Majoka kwa sababu ya utajiri wa Majoka.
   • Boza anajipendekeza kwa kenga ili apewe mradi wa kuchonga kinyago. Pia anasema mke wake ndiye aliyeioka keki
    (8 x 1 = 8)
 3. Maudhui
  1. Utabaka
   • Majoka na Kenga ni wa tabaka la juu ilhali wafanyakazi wa sokoni ni wa tabaka la chini
   • Majoka anamiliki mali nyingi huko sagamoyo, kwa mfano- Majoka and Majoka Academy, Majoka and Majoka modern Resort
   • Matajiri kama majoka wanapata huduma bora za kiafya , anaye hata daktari wake huku huduma za afya Sagamoyo zikidorora
   • Tabaka la juu lina fedha za kuendeleza miradi yao kwa haraka kama vile ujenzi wa hoteli ya kifahari ilhali ni vigumu kwa maskini kupata lishe au kumudu bei ya vyakula
   • Tabaka la juu linatumia tabaka la chini kutimiza malengo yake. Vijana wahuni kwa mfano wanalipwa na wanasiasa ili wamuumize Tunu
   • Tabaka la chini halina vitu vya kimsingi kama mavazi kwa mfano Ashua ilhali Husda ana mavazi mazuri ya kisasa. Sudi ni maskini kiasi kwamba anashindwa kumpa mkewe pesa za matumizi.
    Zozote 5
    Kadiria majibu ya mwanafunzi
  2. Usaliti
   • Majoka anawasaliti wafanyabiashara kwa kuwafungia soko la chapakazi
   • Majoka anawasaliti wafanyakazi kwa kupandisha kodi licha ya hali ngumu ya maisha
   • Majoka anamsaliti Ashua kwa kumpangia njama ya kumkutanisha na mkewe Husda na kufungwa korokoroni
   • Majoka aliwasaliti wanahabari kwa kupanga kuwafungia vituo vya habari kwa kupeperusha habari za maandamano
   • Boza aliwasaliti wafanyakazi wenzakekwa kumuunga mkono Majoka licha ya kuwa aliwafungia soko walikofanyia biashara
   • Boza anawasaliti wenzake kwa kukosa kuwapasha habari kuhusiana na mradi wa kuchonga kinyago
   • Kenga alimsaliti Majoka kwa kuungana na wananchi mambo yanapomharibikia Majoka
   • Uongozi wa Sagamoyo unawasaliti wananchi kwa kuwatupia vijikaratasi wahame Sagamoyo si kwao
   • Serikali ya Majoka inawasaliti walimu na madaktari kwa kuwaongezea mshahara na kisha kupandisha kodi
   • Asiya aliwasaliti wananchi kwa kuwauzia pombe haramu iliyodhuru afya yao na hata kupelekea maafa
    Zozote 5
    Kadiria majibu ya mwanafunzi
  3. Umaskini
   • Wachongaji vinyago walitoka tabaka la chini. Wanakunywa chai ya mkandaa
   • Watoto wa Sudi wanalala njaa. Hii inamlazimu Ashua kwenda kuomba msaada kwa Majoka
   • Mamapima anauza pombe haramu kama njia ya kujipatia riziki
   • Mzee Majoka ana mpango wa kutoa chakula kwa wale wasiojiweza. Hii ni ithibati tosha kuna umaskini katika jimbo la Sagamoyo
   • Soko la Chapakazi linapofungwa wafanyakazi wanahangaika. Soko hili ni la walalahoi ambao walitarajia kuchuma riziki ya kila siku kutoka soko hili.
    Zozote 5
    Kadiria majibu ya mwanafunzi
  4. Dhuluma
   • Majoka napanga njama na Kenga na kumfungia Ashua kwa kisingizio kuwa alizua rabsha ofisini mwake
   • Korokoroni Ashua alipigwa na kujeruhiwa
   • Tunu alivamiwa na wahuni na kuvunjwa muundi wa mguu
   • Majoka na Kenga walipanga njama ambapo jabali aliaga dunia katika ajali ya barabarani.
   • Watu wanaoandamana wanapigwa na polisi na wengine kuuawa.
   • Serikali ya Majoka inafunga soko la Chapakazi ambalo lilikuwa tegemeo la kila siku
   • Hashima anatujulisha kuwa kumekuwa na umwagikaji mwingi wa damu pale Sagamoyo kiasi cha damu kuitia ardhi najisi.
    Zozote 5
    Kadirira majibu
    HADITHI FUPI
 4.                                  
  1. Umaskini katika mapenzi ya kifaurongo
   • wazazi wa Dennis wanafanya vibarua ili kukidhi mahitaji ya familia
   • Dennis akiwa shuleni hakuwa na mavazi ya kuvutia kama wanafunzi wenzake, hana simu na kipatakilishi
   • Chuoni dennis anapika uji mweupe kama chamcha kwa kukosa pesa za kununua chakula
   • Umaskini unamfanya Dennis kuchelea uhusiano wa mapenzi na wasichana chuoni
   • Umaskini unakuwa chanzo cha utengano wa watu. Peninah anamfukuza Dennis kwa ajili ya ukata
   • Dennis anakosa kuajiriwa katika shirika la uchapishaji kwa sababu ni maskini hajulikani. Alama 4
  2. unafiki katika Shogake Dada ana Ndevu
   • Safia anajifanya alivyo mzuri kwa wazazi wake kwa jinsi anavyovalia mavazi yenye staha ndani na nje ya nyumba. Kumbe alikuwa anawapumbaza wazazi wake.
   • Safia anatumia unafiki kwa kutajia wazazi wake masomo ili apate nafasi ya kumleta kimwana nyumbani
   • Kitendo cha Safia kujitia hasira anapoulizwa na mamake kuhusiano na mabadiliko yake ni cha unafiki
   • Swala la Safia kuavya mimba ni la kinafiki. Hakutaka wazazi wake wajue kuwa ulikuwa mjamzito
   • Kimwana ni mnafiki. Anajifanya mwanamke kwa kuvaa buibui ili aweze kukutana na mpenzi nyumbani kwao.
   • Wenye kliniki ambako safia alienda kuavya mimba ni wanafiki.wnatekeleza uovu huu huku wakijua madhara ya kitendo kile
    Zozote 4
    Kadiria majibu
  3. mtindo
   • Uhuishi- donge likaja juu,
   • Balagha- kweli? Uongo?
   • Takriri- labda kweli
   • Msemo- tunga donge kifuani
   • Taswira- alitunga donge kifuani mwake
   • Taharuki- hakutambua afanye nini
  4.                
   1. Mtihani wa maisha
    • Kuthaminiwa sana kwa elimu ya mtoto wa kiume huku elimu ya mtoto wa kike ikipuuzwa
    • Kuthaminiwa sana kwa elimu ya vitabu na kuipuuza elimu ya maisha
    • Kupuuzwa kwa wanafunzi wasioelewa masomo ya vitabu
    • Wanafunzi kusafiri masafa marefu kuelekea shuleni.
    • Kujiamini sana miongoni mwa wanafunzi
     Zozote 3
   2. Mwalimu Mstaafu.
    • Kutamauka:Wanafunzi kujiona zuzu wasiposhika masomo,mfano,Jairo.
    • Ubaguzi: Kufeli katika elimu kunachukuliwa kama ni kufeli maishani. Hata hawapewi nafasi ya kuzungumza mbele ya watu.Mwalimu Mosi anawashinikiza wasimamizi katika sherehe ya kustaafu kwake kumpa Jairo nafasi ili naye aihutubie hadhira.
    • Umaskini: Watoto kufukuzwa shule kwa kukosa vitabu vya kaida – Sabina bintiye Jairo.
    • Mfumo wa elimu: Haushughulikii wasioshika masomo darasani- Jairo.
    • Mapenzi ya kiholela:Wanakijiji walishuku kuwa huenda Mwalimu Mosi alikuwa amemtorosha shule Sabina bintiye Jairo.
     zozote 3
 5. Ukiukaji wa haki za watoto kwa kurejelea diwani
  Tulipokutana tena
  • Haki ya malezi- babake Bogoa alimlazimisha kwenda kulelewa na Bi. Sinai bila hiari yake
  • Haki ya kutobaguliwa- Bi. Sinai alimbagua Bogoa kwa kuhakikisha alikula mwisho na kulia kutoka kwa sufuria
  • Haki ya kupata elimu- Baadhi ya wanafunzi kutokana na tabia ya Bogoa ya kukosa shule walisema kuwa watoto wa kimaskini walihitaji jutumikishwa na hawastahiki kusoma shuleni
  • Haki ya kupata mapenzi ya wazazi- Bogoa anaterngwa na wazazi wake wakati walipofika kwa bi. Sinai.
  • Haki ya kutodhulumiwa- Bogoa alidhuluimiwa na Bi. Sinai kwa kuchomwa na kijinga moto vigajani
  • Haki ya kutotumikishwa- Bogoa aliytumikishe=wa alipokuwa kwa Bi. Sinai
  • Haki ya kutangamana- Bogoa ananyimwa haki ya kutangamana na kucheza na watoto wa rika lake
  • Bogoa ananyimewa haki ya kujieleza na kutoa maoni yake anapojaribu kumweleza babakehakutaka kwenda alikokuwa anapelekwa .
  • Haki ya kutohusishwa katika ajira- Bogoa alilazimishwa na Bi. Sinai kuwauzia wanafunzi wenzake mandazi
  • Haki ya kupata elimu- janadume bakaji linaathiri masomo ya Sara kwa kumbaka bado angali anasoma
  • Haki ya Sara ya kulindwa inakiukwa. Wazazi wake wanamwachilia arudi masomo usiku peke yake.
  • Samueli anadharauliwa na kupuuzwa anapoenda kuchukua matokeo yake.
  • Kitoto kilichotunguliwa na Sara kilinyimwa haki ya kuishi.
   10*2= 20
   Kadiria majibu
   RIWAYA CHOZI LA HERI
 6.                              
  1. muktadha
   Ni mawazo yanayompitia Ridhaa anapokumbuka maneno ya marehemu mwanawe Tila
   Mjadala wenyewe wahusu mafanikio ya baada ya uhuru
   Ridhaa yumo nyumbani kwake akitazama masazo ya aila yake ambayo ni majivu
   Hii ni baada ya kuuawa kwa familia yake kinyama na mzee Kendi alipoliteketeza jumba lake
   alama 4
  2. mbinu
   balagha-
   jazada- watoto wa miaka hamsini kumaanisha kuwa waafrika bado hawajaweza kujitegemea
   alama 1
  3. ukoloni mambo-leo
   • kuwepo kwa walowezi waafrika wanaowafanya waafrika wenzao maskwota kv Kiriri
   • waafrika kuendelea kuwa watumwa wa wakoloni kiuchumi
   • wakoloni kuendelea kuamua waafrika watakuza nini katika nchi yao
   • waafrika kuendelea kuwategemea wakoloni kwa lishe na kwa ajira duni
   • waafrika wanakuza mazao yanayomfaidi mkoloni kama vile kahawa
   • mwafrika alirithi umilikaji wa ardhi kwa kutumia hatimiliki kutoka kwa mzungu
   • uchimbaji wa madini ulifadhiliwa na nchi za kigeni kv |Shirika la Chai la Tengenea, Kisiwa Bora
   • mifumo kandamizi ya utawala- uongozi unatumia vyombo vya dola kudhibiti raia na upinzani
    alama 8
  4. wasifu wa msemaji
   Ni maneno ya Tila yanayompitia babake Ridhaa mawazoni
   • mwenye busara- Ridhaa hakuacha kushangazwa na upevu wa mawazo wa mwanawe Tila
   • mwenye matumaini- alikuwa na matumaini kuwa siku moja atakuwa jaji katika mahakama kuu
   • mpenda haki- alikuwa na mazoea ya kumwambia babake kuwa angekuwa jaji katika mahakama angehakikisha kuwa kila mtu angepata haki
   • mwenye kumbukumbuku- anakumbuka kuwa Ridhaa aliwahi kumwambia kuwa mifumo ya uzalishaji ilibadilika
    alama 4
  5. umuhimu wa msemewa
   msemewa ni Ridhaa
   • anawakilisha wanaume wenye bidi katika jamii
   • ametumiwa kuendeleza maudhui ya ushirikina
   • ni kielelezo cha wanaume wanaowapa wanao ushauri mwema maishani
   • ametumiwa na mwandishi kuonyesha athari za kutokuwa na udhabiti wa kisiasa
   • ni mmojapo wa wasimulizi wa matukio ya hadithini. Anasimulia kisa cha kupoteza majumba yake mawili, kuchomeka kwa ndugu yake makaa, nk
   • anachipuza migogoro inayosababishwa na tofauti za kiusuli. Wanafunzi shuleni wanamtenga kwa sababu yeye ni mgeni
   • kupitia kwake, mwandishi amekuza maudhui mbalimbali kama vile uwajibikaji,utu, uongozi, ndoa, malezi nk
    zozote 3
 7. Athari za siasa za ukabila na ubabedume
  • Vitisho- majirani waliwatupia kina Ridhaa vijikaratasi vya kuwafahamisha wahame
  • Kukatika kwa urafiki wa wanajamii- jirani wa Ridhaa Mzee Kedi alikata guu kwake mara moja licha ya kuishi pamoja kwa miaka hamsini
  • Wivu- mkewe mzee Kedi alikuwa akilalamika kuhusu kuuzwa kwa mashamba ya wenyeji
  • Mauaji- mzee Kendi anaiangamiza familia ya Ridhaa
  • Uharibifu wa mali- jumba la Ridhaa liliteketezwa na mali za thamani ya juu kuharibiwa
  • Uhaba wa chakula- kambini watu waling”anng”ania chakula. Hata waliokuwa wenye hadhi hapoawali akina Waziri Mstaafu
  • Mazingira duni- wakimbizi kambini hawakuwa na makazi. Kaizari anaeleza alivyowahurumia wanawe waliponyeshewa na mvua
  • Watu kujeruhiwa/ kuvamiwa- Kaizari anaeleza jinsi mkewe Subira alivyojeruhiwa vibaya na wavamizi
  • Ukosefu wa Amani- mzee Kaizari anaeleza kuwa ilibidi vyombo vya dola kutumwa ili kudumisha usalama katika vijiji
  • Wizi/ uporaji- wakati wa fujo kuna wale walijijasirisha na kuingia kwenye maduka ya wafanyabiashara wa Kihindi,Kiarabu na hata Waafrika wenzao na kupora bidhaa.
  • Ubakaji- Kaizari anaeleza jinsi vijana barobaro walivyoingia walipokuwa mabinti wake na kuwabaka
  • Utengano- Kaizari anatengana na jirani yake Tulia.
  • Kusambaratika kwa ndoa- tunaelezwa kuwa ndoa ya Selume ilisambaratika baada ya vita kutokea
  • Magonjwa- kambini wakimbizi walimenyana na ndwele ainati kama vile homa ya matumbo
  • Ukosefu wa huduma za kijamii- huduma za kijamii kambini zilikosekana
  • Dhiki za kisaikolojia- dhiki za kisaikolojia zinawakumba wahasiriwa wa vita vya baada ya uchaguzi na hata kupelekea wengine kupata shinikizo la damu
  • Ugavi usio sawa wa raslimali- Shamshi analalamika kutwaliwa kwa nafasi za kazi na ndugu za walio nacho huku wanyonye wakihitajika kutoa hongo

   Alama 20
   Kadiria majibu

   SEHEMU YA E
   FASIHI SIMULIZI

 8.                  
  1.                         
   1. kipera- mawaidha alama 2
   2. sifa za mawaidha-
    • matumizi mapana ya mbinu za lugha kama vile vile methali
    • hutolewa na mzee, mzazi au mtu anayechukuliwa kuwa na hekima
    • lugha inayotumiwa huwa ya kipekee inayolengwa kuathiri wanaousiwa
    • huweza kufungamanishwa na visa au matukio maalum yanayotokea katika jamii
    • huweza kuambatanishwa na mbazi na istiara
     alama 3
   3. umuhimu wa mawaidha
    • hutoa ushauri kwa walengwa
    • Hutoa maelekezo kwa anayepewa mawaidha
    • Humtolea mlengwa maonyo asije akapotoka na kutumbukia mashakani
    • Humkosoa muathiriwa ambaye huenda alikuwa ameuchukua mkondo usiofaa wa maisha
    • Hutambulisha jamii- kila jamii huwa na aina yake ya mawaidha kulingana na thamani zake
     Alama 5
  2. jinsi ya kuihusisha jamii katika masimulizi
   • Kuwauliza maswali
   • Kuimba wimbo pamoja na hadhira
   • Kuwauliza kukariri jambo alilolisema
   • Kuwashirikisha katika vitendo mathalani kupiga makofi au kuigiza wahusika
  3. utaratibu wa vitendawili
   1. Mtegaji hutanguliza kwa kuiambia/ kutangaza vitendawili
   2. Hadhira hujibu tega
   3. Mtegaji hutoa kitendawili chenyewe
   4. Hadhira hupewa muda wa kufikiri na kujaribu kukitegua
   5. Hadhira ikitoa jibu lisilo sahihi, mtegaji huomba apewe mji ili aweze kutoa jibu
   6. Mtegaji akipewa mji anaotaka hukubali na kutoa jibu
    Alama 6
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 End Term 3 2022 Exams.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest