Maswali
INSHA (AL.20)
Mwandikie chifu wa sehemu unayotoka barua ukimjulisha juu ya mzazi katika kijiji chako anayewatesa na kuwanyima haki watoto wake.
MATUMIZI YA LUGHA (AL.30)
- Taja irabu mbili za kati. (AL.2)
- Taja konsonanti moja ya koromeo. ( AL.1)
- Eleza sifa tatu za kamusi .(al.3)
- Taja aina mbili za viambishi( Al.2)
- Eleza maana ya mofimu.(al.2)
- Taja matumizi mawili ya alama za italiki.(al.1)
- Eleza maana ya kielezi. (al.2)
- Tofoutisha maneno yafuatayo.(al.2)
- Dhamini
- Thamini
- Tumia kiulizi kifaacho kukamilisha maswali yafuatayo.(al.3)
- ………………wanitaniaa hivyo?
- ………………..ulienda kumwona?
- …………….Koko amewasilli?
- Tunga sentensi zinazokuwa na miundo ifuatayo. (al.3)
- N+T+N+E
- N+T
- N+V+T
- Andika ukubwa wa .(al.2)
- Mtoto
- Kikapu
- Eleza maana ya viwakilishi. (al.2)
- Kamilisha sentensi zifuatazo Kwa kutumia kirejeshi amba- (al.3)
Tarishi…………………………..anayekuja ni mchezaji hodari
Viazi…………………………… vimeliwa vilikuwa vimeiva.
Nyufa …………………………. Zilizibwa jana zimebomoka. - Tunga sentensi ukitumia vitenzi hivi katika hali ya kutendwa.(al.2)
- Vunja
- Funga
TAMTHILIA YA KIGOGO AL 20
- Fafanua ufaafu wa anwani kigogo. (al.10)
- …..Ni hilo embe lako,linanuka fee!
- Weka dondoo hili katika mktadha wake. (al.4)
- Taja tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. (al.1)
- Taja sifa za msemewa. (al.5)
Mwongozo wa Kusahihisha
INSHA (AL.20)
Hii ni insha ya barua rasmi.
Lazima iwe na anwani mbili.
- Anwani ya mwandishi
- Tarehe
- Anwani ya mwanikiwa
- Mtajo
- Mada
- Maudhui
- Sahihi
VIPENGELE VYA KUZINGATIA
- Kuwanyima elimu.
- Kuwanyima chakula.
- Kutowapa mavazi.
- Afya bora.
- Kuwafanyiza kazi nyingi.
- Uhuru wa kujiamlia.
- Kutowapa malazi.
MATUMIZI YA LUGHA (AL.30)
- Taja irabu mbili za kati. (AL.2)
/a/ na /e / - Taja konsonanti moja ya koromeo. ( AL.1)
/ h/ - Eleza sifa tatu za kamusi .(al.3)
- Maneno yamepangwa kialfabeti
- Huonyesha homonemia
- Huonyesha mifano ya maneno mbalimbali
- Taja aina mbili ya viambishi( Al.2)
- Viambishi awali
- Viambishi tamati
- Eleza maana ya mofimu.(al.2)
- Mofimu ni sehemu ndogo ya neno inayobeba maana kamili
- Mofimu ni sehemu ndogo ya neno inayobeba maana kamili
- Taja matumizi mawili ya alama za italiki.(al.1)
- Kuonyesha kiambishi cha kurejesha
- Kuonyesha jina la kitabu
- Kuonyesha maneno ya kigeni
- Eleza maana ya kielezi. (al.2)
- Ni Kipashio katika sentensi kinachotumika kuelezea jinsi tendo linalotajwa na kitenzi lilivyofanyika.
- Ni Kipashio katika sentensi kinachotumika kuelezea jinsi tendo linalotajwa na kitenzi lilivyofanyika.
- Tofoutisha maneno yafuatayo.(al.2)
- Dhamini-kuchukulia mtu dhamana ili mshtakiwa asiwekwe rumande
- Thamini-tia maanani ,heshimu
- Tumia kiulizi kifaacho kukamilisha maswali yafuatayo.(al.3)
- Mbona wanitaniaa hivyo?
- Je, ulienda kumwona?
- Je,koko amewasilli?
- Tunga sentensi zinazokuwa na miundo ifuatayo. (al.3)
- N+T+N+E
- Mwanafunzi anasoma kitabu haraka
- N+T
- Mwanafunzi anasoma
- N+V+T
- Mtoto mtundu ameondoka
- Mtoto mtundu ameondoka
- N+T+N+E
- Andika ukubwa wa .(al.2)
- Mtoto
- toto
- Kikapu
- kapu
- kapu
- Mtoto
- Eleza maana ya viwakilishi. (al.2)
- Ni maneno yanayoleta dhana ya kuwa na kitu
- Ni maneno yanayoleta dhana ya kuwa na kitu
- Kamilisha sentensi zifuatazo Kwa kutumia kirejeshi amba- (al.3)
- Tarishi ambaye anayekuja ni mchezaji hodari
- Viazi ambavyo vimeliwa vilikuwa vimeiva.
- Nyufa ambazo Zilizibwa jana zimebomoka.
- Tunga sentensi ukitumia vitenzi hivi katika hali ya kutendwa.(al.2)
- Vunja
- Musa alivunjwa mguu mpirani
- Funga
- Mlango ulifungwa na mtoto
- Vunja
TAMTHILIA YA KIGOGO-MAJIBU AL.20
- Kigogo ni mtu mwenye madaraka makubwa kiutawala.
- Majoka anatumia madaraka yake kulaghai wananchi.
- Majoka anatangaza kipindi cha mwezi mzima cha kusherehekea uhuru.
- Majoka anafunga soko la chapakazi ili ajenge hoteli ya kifahari.
- Majoka anatumia mamlaka yake kumteka na kumtia ndani Ashua.
- Majoka anapanga kutumia mamlaka yake kuzima uchunguzi wa Tunu kuhusu kifo cha Jabali.
- Majoka anafuja pesa za kusafisha soko huku akijua hakuna wa kumhukumu kwa kuwa ndiye kiongozi.
- Majoka anampa mamapima kibali cha kuuza pombe haramu kwa kutumia mamlaka yake.
- Majoka anatumia mamlaka yake kudhibiti vyombo vya habari.
- Majoka kwa mamlaka yake anaamuru polisi kutawanya waandamanaji.
- Kwa mamlaka yake,Majoka anafadhili miradi isiyo muhimu.
-
- Anayezungumza-Boza
- Anayezungumziwa- Sudi
- Mahali- katika karakana kwenye soko la Chapakazi
- Tukio- walikuwa wakizungumza kuhusu uvundo ulioko kwenye mazingira
- Tanakali ya sauti-kunuka fee!
- Sudi
- Ni mchonga kinyago
- Ni mwenye bidii
- Ni jasiri
- Ni mwenye utu
- Ni mkweli
- Anayezungumza-Boza
Download Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Opener Term 1 Exams 2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates