Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 End Term 1 Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

Mjumbe huyu aliishauri Kusadikika kama iliweza kufikiri kutengeneza tayari bandari na viwanja vya kutua vyombo hivyo. Kwa shauri hili, alidhihakiwa kuwa alikuwa kama mama aliyekuwa akimwandalia mtoto aliyekuwa bado kuzaliwa. Ilisadikika kuwa watu wa Ardhi walikuwa hawawezi kuvumbua njia ya kuunda vyombo vya kusafiri hewani hata kama waliweza kusafiri baharini na barani. Kwa hivi, Kusadikika ilikuwa haina haja ya kutengeneza tayari bandari wala viwanja kwa ajili ya vyombo vya Ardhi. Andao lolote kwa ajili ya wakati ujao lilikuwa upuzi kwa washauri wa Kusadikika
Amini aliwaonya kuwa kama wakati ujao hauandaliwi mbele vema, hasara zake zitakuwa kubwa. Lakini walishikilia kusema kuwa maharibiko ya wakati huo yalikuwa si juu yao, ingawa walikuwa barabara kuwa watu watakaoishi katika wakati huo ni watoto wao wenyewe. Shairi hili lilikuwa si upuzi. Lilikuwa ni shauri la hekima sana.
Udhahiri wa mambo ni kuwa ulimwengu uliumbwa kabla ya wakaaji wake. Kama ulimwengu usingatangulia kuumbwa, wakaaji wake wasingalikuwa na mahali pa kukaa. Ukitaka biashara ya vitabu istawi watu hawana budi kufunzwa kusoma kwanza. Kusoma kusipotangulia, vitabu vizuri vitaonekana vibaya. Kabla ya kujenga msikiti, watu lazima wafunzwe utukufu wa dini mbele. Bila ya hivyo msikiti mtukufu utakuwa kama mkahawa mchafu tu. Kadhalika mfano, kama nchi haina bandari ya namna yoyote, haiwezi kutazamia kufikiwa na vyombo. Kila azimio katika maisha hutaka neno fulani kufanyizwa mbele ili kuyashawishi maendeleo yake. Watu watakao kustawi katika maisha huelekeza bidii zao juu ya mshawasha wa makusudi yao kwanza. Kama hili si shabaha ya kwanza katika maisha, basi, haiwi ya pili kwa nyingine yoyote. Mambo yaliyo makubwa na madogo yamefungamana na utaratibu huu.

 1. MASWALI
  1. Kwa kutoa sababu, Kusadikika ilikuwa katika hali gani kimandeleo. (alama 2)
  2. Je, ni vema mama kumwandalia mtoto ambaye hajazaliwa? Tetea jibu lako. (alama 2)
  3. Andika hoja alizozitoa mwandishi dhidi ya busara ya methali: Usikate kanzu kabla Mtoto hajazaliwa” (alama 3)
  4. Wakati ujao usipoandaliwa vema, hasara zake zitakuwa gani? (alama 2)
  5. Kutokana na habari hii, ni kwa nini nchi ya Kusadikika haikufikiwa na wajumbe kutoka nchi nyingine? (alama 2)
  6. “Watu watakao kustawi katika maisha huelekeza bidii zao juu ya mshawasha wa makusudi yao kwanza” Fafanua. (alama 2)
  7. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa kifunguni. (alama 2)
   1. Kutazamia
   2. Mshawasha
 2. UFUPISHO
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali
  Dawa za kulevya zinaweza kugawika katika makundi wawili makuu: dawa hasi na dawa sugu. Katika kundi la kwanza zinaingia dawa zozote ambazo hunywewa, hunuswa au hutumiwa kwa nia ya kulevya au kumwingiza mtumiaji katika hali ya kujihisi amepanda. Dawa za aina hii huwa na matokeo hasi kwenye mwili wa mtumiaji. Inawezekana jamii ikakubali kuwepo kwake, pamoja na kutumiwa kwake, lakini, matumizi ya kipindi kirefu huwa na matokeo mabaya sana kwa watumiaji. Baadhi ya dawa hizi ni bidhaa za tumbaku ambazo huwa na aina za kemikali inayoitea nikotini. Nyingine ni vileo kama wiski, bia, divai, miraa au mairungi, gundi ya viatu na bidhaa zinazotokana na petroli.
  Hebu sasa tuangalie zile zinazoitwa dawa sugu. Hizi ni dawa ambazo kimsingi humchangamsha mtumiaji na kumfanya apandwe na nishati za ajabu. Dawa hizi hufanya hivi kwa kuzitekenya seli za ubongo wa anayehusika. Katika kulifanya hili dawa zenywe huishia kuzuia seli za ubongo huo. Huu ndio msingi wa mtumiaji kuwa na ustahimilivu fulani wa dawa zenyewe. Ustahimilivu huu ndio unaomfanya awe kama aliyetawaliwa na dawa hizo. Yaani mtumiaji huwa hana njia nyingine ya kujizuia na huishia kuwa mtumwa wa dawa hizo. Baadhi ya dawa sugu ni bangi, afyuni, heroini, mihadarati na kokeini. Baadhi ya wataalamu wanajumlisha miraa katika kundi hii pia.
  Ni kawaida kusikia madai kuwa mtu anayetumia dawa za kulevya huonekana kuwa na furaha kuliko wenzake. Ili kuelewa chanzo cha msisimko na furaha hiyo ya ajabu, lazima tuzijue hatua anazopitia mtumiaji dawa za kulevya. Kimsingi kuna hatua tatu kuu. Mara tu mtu anapozitumia dawa za kulevya, dawa hizo huzichangamsha seli za ubongo kwa kiasi kikubwa. Kuchanginshwa huku kwa seli kunazuia mwili wa anayehusika kutopata hisia kutoka viungo vya mwili au misuli ya mwili. Matokeo ya hali hü ni kumfanya mtu anayehusika kutenda mambo kupita kawaida yake. Mathalan, ataonekana kuwa na furaha nyingi, atasoma kupita kawaida, anaweza kucheza kwa kipindi kirefu na kadhalika. Hali hii inaweza kuitwa hali ya ‘mpumbazo'. Mpumbazo huu unaweza kumdanganya anayehusika kuhisi kuwa ana uwezo usiokuwa wa kawaida. Lakini hii ni hali ya muda tu ambayo hutangulia kuuliwa na kuharibiwa kwa seli za ubongo. Mtumiaji anayeingia katika hatua ya pili huwa anatoka kwenye ile hali ya mpumbazo. Hatua ya pili hutambulishwa na dalili zifuatazo: Uchovu, kulala kupita kiasi, kutokuwa na hamu ya kazi au mambo mengine. Kupuuza maswala ya siha na afya, usahaulifu, kukosa malengo au shabaha katika kazi yake, kupungikwa na kumbukumbu, kujitenga na watu wengine na kuwa na hisia za chuki au uhasama na jamaa Mtumiaji anapofikia hatua hii hutambulikana waziwazi na watu walio karibu. Mtumiaji wa dawa za kulevya huweza tu kunusurika au kuokolewa katika hatua hii. Akipita hatua hii ya pili, huwa anaingia katika awamu mbaya sana.
  Hatua ya tatu ya mtumiaji wa dawa za kulevya huitwa hatua ‘isiyo ya kawaida'. Sifa za kutambulisha mtumiaji aliye kwenye ngazi hii ni fadhaa kubwa, unyonge wa mwili uiimbu wa kimawazo na uvunjifu mkubwa. Mtumiaji aliyefikia ngazi hii honyesha sifa kadha milele. Mathalani kujiten ga kabisa na jamaa au watu walio karibu naye, kupaliwa kabisa na usingizi, kuudhika haraka na kuwa na tabia ya kuonyesha uchukivu wa vitu kwa kupigana, kuchanganyikiwa kunakotokana na kuharibikiwa kwa seli za ubongo, wazimu au kuangukaanguka kama mgonjwa wa kifafa. Katika ngazi hii, seli za ubongo zinazomsaidia mtu kufanya uamuzi mzuri huwa zimeharibiwa na dawa zenyewe. Si ajabu basi kuwa mtumiaji anaonyesha tabia za kitoto na kuishi kama mtu aliye kwenye ndoto. Hatimaye ubongo unazongwa kabisa kutokana na madhara ya seli na mtumiaji huweza kushikwa na magonjwa ya kiakili kama wendawazimu.
  Mwisho wa mtumiaji wa dawa za kulevya aliyefikia ngazi hii ni kufariki baada ya mwili wake kushindwa kuhimili uzito wa dawa zenyewe. Wengine huishia kujinyonga au kufariki
  kutokana na madhara ya moyo.
  Maswali
  1. Fupisha aya ya kwanza na ya pili. (maneno 45 – 50) (alama 7, 1 ya utiririko)
   Matayarisho
   Jibu
  2. Eleza hatua anazopitia mtumiaji wa dawa za kulevya (maneno 90 - 100) (alama 8, 1 ya utiririko).
   Matayarisho
   Jibu
 3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1. Ainisha vielezi katika sentensi ifuatayo kisha ueleze ni vya aina gani. (alama 2)
   Mama alipoukaribia msitu huo alijikaza kiume huku akitembea harakaharaka. (alama 2)
  2. Yakinisha sentensi ifuatayo kwa nafsi ya tatu wingi.
   Sitaenda shuleni wala hospitalini kesho.
  3. Ainisha silabi katika neon (alama 2)
   Daktari
  4. Andika katika usemi halisi. (alama 2)
   Mwalimu alisema kuwa siku hiyo aliamini kuwa akili ni nywele na kila mtu ana zake. (alama 2)
  5. Akifisha. (alama 4)
   Usula alimwambia rafikiye njoo kesho nikufunze na wenzako angaa uelewe somo hilo rafikiye aliuliza mimi peke yangu nije. (1)
  6. Huku ukitoa mfano mmoja mmoja eleza matumizi matatu ya 'ni'. (alama 3)
  7. Andika katika hali timilifu (alama 2)
   Halima alimpikia mgeni wa Asha licha ya hayo alimpeleka hadi kituo cha basi.
  8. Andika katika umoja (alama 1).
   Wepi waliobahatika siku hiyo?
  9. Eleza matumizi ya kwetu katika sentensi zifuatazo (alama 2)
   1. Kwetu ni huku
   2. Mahali kwetu ni huku
  10. Eleza matumizi ya "hu' katika sentensi hizi. (alama 2)
   1. Hukuja karamuni jana
   2. Walimu huwapa wanafunzi ahadi za kweli
  11. Andika katika umoja. (alama 1)
   Maasi yaliyotekelezwa jana mabandani yamewatia watu wahka.
  12. Nyambua kitenzi “jua' katika kauli zifuatazo: (alama 2)
   1. Kutendeana
   2. Kutendana
  13. Eleza maana mbili za sentensi hii (alama 2)
   Watu wa pwani hawaogopi bahari kama watu wa bara.
  14. Tunga sentensi tatu ukitumia neno kifupi kama: (alama 3)
   1. Kielezi
   2. Kiwakilishi
   3. Kivumishi
  15. Changanua kwa kielelezo mishale (alama 4)
   Nguo yangu maridadi imeliwa na panya wa jirani.
  16. Nomino zifuatazo zimeundwa kutokana na vitenzi vipi? (alama 2)
   1. Kinywaji
   2. Hotuba
  17. Kanusha (alama 1)
   Siku hiyo ikifika tutaimba nyimbo nyingi za kumtukuza mungu.
  18. Andika katika udogo (alama 1)
   Mlango wake ulivunjwa na mwizi yuyu huyu.
 4. ISIMUJAMII (ALAMA 10)
  Eleza maana ya dhana zifuatazo
  1. Lahaja (alama 2)
  2. Lugha (alama 2)
  3. Usanifishaji (alama 2)
  4. Sajili (alama 2)
  5. Lugha rasmi (alama 2)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.    
  1. Ilikuwa nyuma kwa sababu haikuwa na bandari wala viwanja.(alama 2)
  2. Ni vema, la sivyo malezi yake yatakuwa magumu.(alama 2)
  3.      
   1. ikiwa ulimwengu haungeumbwa mapema, wakaaji wake hawangepata mahal pa kukaa.
   2. kw biashara ya vitabu kustawi watu ni lazima wafunzwe kusoma mbele la sivyo vitabu vizuri vitaonekana vibaya.
   3. watu wasipofunzwa utukufu wa dini kabla ya kujenga msikiti, utaonekana kama mkahawa mchafu.(alama 3)
  4. Wananchi hawatafikiwa na vyombo/hawatapata maendneleo(alama 2)
  5. ilikuwa na washauri wambaya na wenye mapuuza. haikuwa na vyombo, viwanja au njia/barabara(alama 2)
  6. kila azimio katika maisha hutaka neno Fulani kufanywa kwanza ili kuyashawishi maendeleo yake. (alama 2)
  7.      
   1. kutazamia-kutumaini/kutarajia/kutegemea(alama 2)
   2. mshawasha-hamu ya kujua/kufanya jambo.(alama 2)
    .adhabu
   3. Kila kosa ya sarufi litokeapo mara ya kwanza liadhibiwe hadi makosa 6-maki 3
   4. Kila kosa la tahaja litokeapo mara ya kwanza liadhibiwe hadi makosa 6-maki 3
 2. ufupisho
  1.          
   1. Dawa za kulevya zinaweza kugawika katika makundi mawili makuu
   2. Dawa basin a dawa sugu
   3. Dawa hasi huwa na matokeo hasi kwenye mwili wa mtumiaji.
   4. Dawa sugu humchangamsha mtumiaji na kumfanya apandwe na nishati za ajabu.
    1. Husitekenya selu y ubongo wa anayehusika.
    2. Mtumiaji huishia kuwa mtumwa wa dawa hizo.
    3. Mifano ya dawa za kulevya ni bangi, heroini, kokeini na miraa.
  2.      
   1. Dawa za kulevya huzichangamsha seli za ubongo kwa kiasi kikubwa.
   2. Mwili wa mhusika hukosa hisisa kutoka viungo vya mwili au misuli ya mwili
   3. Hutenda mambo kupita kawaida yake.
   4. Huwa mchovu, hulala kupita kiasi, hukosa hamu ya kazi na hupuuza maswala ya siha.
   5. Huwa msahaulifu, hupungukiwa na kumbukumbu na kuwa na hisia za uhasama na jamaa hivyo hujitenga.
   6. hatua ya tatu huwa isiyo ya kawaida
   7. mtumiaji hujitenga kabisa na jamaa yake.
   8. seli za ubongo huwa zimeharibiwa na hivyo kuonyesha uchukivu wa vitu kwa kupigana na kuchanganyikiwa.
   9. hushikwa na mgonjwa ya kiakili
   10. mwishowe mhusika hufariki
    hoja 6-alama 6
    Hoja 7-alama 7
    Utiririko-2
    Ujumla 15

Matumizi ya lugha (alama 40)

 1. Kiume-1/2maki
  Aina –kielezi chaa namna mfananuo-1/2 maki
  Harakabaraka-1/2 maki-kielezi cha namna kakariri ½ maki
 2. Wataenda shuleni na hospitalini kesho(alama 2)
 3. Da-k-ta-ri (alama 2)
 4. Mwalimu alisema, “leo nimeamini akili ni nywele na kila mtu ana zake’ 4x1/2=alama 2
 5. Usuala alimwambia rafikiye, “Njoo kesho nikufunze na wenzake angae uelewe somo hilo.
  Rafikiye aliuliza “mimi peke yange nije?(8 x ½ =alama 4
 6.      
  1. kitenzi kishirikishi kipungufu ltd.
   m.f-Huyu ni mwalimu.
  2. kielezi cha mahali
   m.f.Ameingia nyumbani
  3. katika baadhi ya viulizi
   m.f-Nani, gani, nini
  4. kuonyesha wingi wa watu hali ya kuamrisha
   m.f.-ondokeni!kaeni Lalenin.k.
   zozote 3x1=alama 3
 7. Halima anmempikia mgeni wa Asha licha ya hayo ampeeke hadi kituo cha basi.(alama 2)
 8. Yupi aliyebahatika siku hiyo? (alama 2)
  1. Kiwakilishi kimilikishi
  2. Kivumishi kimilikishi alama 2
 9. Masi yalitekelezwa mabondeni yamewatia watu walaka (alama 2)
 10.      
  1. Juliana
  2. juana
 11.      
  1. watu wa pwani kwa kuzoea kuona na kutumia bahari hawaiogopi lakini watu wa bara huingiwa woga wanapoona bahari.
  2. watu wa pwani huwaogopa watu wa bara lakini hawaogopi bahari.
 12.      
  1. kielezi
   k.m aliendika habari hizi kwa kifupi.
  2. kiwakilishi
   kifupi kimenunuliwa
  3. kivumishi
   kijitu kifupi kimevunjika
   hakiki sentensi 3x 1=alama 3
 13.  s-KN+KT
  KN-N+V+V
  N-Nguo
  v-yangu
  v-maridadi
  KT-T-H+N+V+N
  T-imeliwa
  H-na
  N-panya
  V-wa
  N-njirani 8x1/2=alama 4)
 14.        
  1. ku(nywa)
  2. Hutubu 2 x 1(alama 2)
 15. siku hiyo isipofika hatutaimba nyimbo nyingi za Mungu (alama 2)
 16. kilango chake kilivunjwa na kijizi hiki(alama 2)

isismu jamii

 1. Lahaja
  hii ni tofauti za kimatamshi na maumbo pamoja na matumizi katika lugha ambayo huhesabiwa kuwa lugha moja lakini hutofautiana katika mambo madogomadogo.(alama 2)
 2. Lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo zimebuniwa na jamii Fulani kwa madhumuni ya mawasiliano.9alama 20
 3. Usanifishaji ni uamuzi wa kuchagua lugha moja au mojawapo ya lahaja za lugha na kufanyia marekebisho ya kimatamshi, kisarafusi, kimana na kimaandishi ili iwezo kutumika katika shughuli rasmi.(alama 2)
 4. Sajili –mitindo au namna mbalimbali za matumizi ya lugha Fulani.(alama 2)
 5. Lugha ambayo hutumika ofisini au katika shughuli zote rasmi nchini kama vile shuleni, ofisini n.k.(alama 2
  Huu ndio ukurasa wa mwisho wa uliopigwa chapa.

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 End Term 1 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest