Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Term 2 Opener Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

  1. UFAHAMU
    Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali. (alama 15)

    Mojawapo kati ya misingi na nguzo za maendeleao ulimwanguni ni viwanda. Viwanda ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyoigeuza malighafi inayopatikana na kuwa bidhaa zinazoweza kutumiwa na watu. Katika nchi zinazoendelea, ambazo hazina uwezo mkubwa wa mitaji viwanda vinavyoimarika ni vile vidogo. Hivi ni viwanda ambavyo huhusiana na amali za mikono. Kuimarika kwa viwanda hivi kunatokana na sababu mbalimbali.
    Nchi zinazoendelea huwa na masoko finyu sana kwa kuzingatia uwezo wa ununuzi wa wanaolengwa na bidhaa za viwanda. Katika msingi huu viwanda vitawiwa ugumu kufanya biashara katika mazingira ambako masoko yake ni finyu au utashi wa bidhaa zake sio mkubwa. Viwanda vidogo pia vinao uwezo wa kuwaajiri wafanyikazi wengi hasa kwa kuwa havina uwezo wa kugharamia mashine. Uajiri huu wa wafanyikazi wengi ni muhimu katika maeneo mengi ambako tatizo la ajira ni mojawapo wa hayana migumo imara ya kuwakimu watu wasiokuwa na kazi. Utegemezi wa jamaa wanaofanya kazi kwa hivyo unakuwa nyenzo ya pekee ya kuyamudu maisha.
    Kuanzisha viwanda vidogo vidogo hakuhitaji mataji mkubwa tofauti na viwanda vikubwa. Hali hii inasahilisha uwezekano wa watu wengi kujasurisha shughuli yoyote ile. Sambamba na suala hili ni kuwa ni rahisi kujarisha bidhaa mpya kwa kiwango kidogo cha kawaida. Ikiwa mzalishaji yeyote atazalisha bidhaa mpya kwa mapanu, kwa mfano kama ilivyo kwa viwanda vikubwa, pana uwezekano wa kupata hasara kubwa. Huenda utashi wa bidhaa uwe mdogo ukilinganisha na ugavi wa bidhaa yenyewe. Majaribio mazuri ni kwa kiwango kidogo.
    Kuwepo kwa viwanda vidogo huwa choche kubwa la usambazaji wa viwanda hadi maeneo ya mashambani. Hali hii inahakikisha kuwa nafasi za ajira zimezambazwa nchini hali ambayo inasaidia kuhakikisha kuwa pana mweneo wa kiununuzi wa umma. Huu ni msingi muhimu wa maendeleo. Aghalabu viwanda vikubwa huegemea kwenye mitaji ya mashirika ya kimataifa na huwa msingi wa kuendelezwa kwa utegemezi wa kiuchumi.

    Maswali
    1. Kwa nini viwanda ni muhimu? (ala 2)
    2. Ni nini kiini cha matatizo ya uuzaji wa bidhaa katika nchi zinazoendelea? (ala2)
    3. Eleza faida zinazotokana na kuwepo kwa viwanda vidogo (ala4)
    4. Usambazaji wa viwanda katika maeneo ya mashambani una faida gani? (ala 4)
    5. Fafanua maana ya msamiati huu kama ulivyotumika katika kifungu. (ala3)
      1. Kujasurisha
      2. amali
      3. Utashi
  2. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1. Taja na ueleze aina mbili kuu za ala za matashi (ala 2)
    2. Linganisha sauti zifuatazo (ala 2)
      1. /dh/ na /th/
      2. /o/ na /u/
    3. Onyesha silabi ambazo zitatiwa shadda katika maneno haya (ala 2)
      1. Msisimk
      2. Maswali
      3. Tafadhali
      4. Mchunga
    4. Tunga sentensi ukitumia mofimu huru ambayo ni kivumishi (ala2)
    5. Ainisha viambishi katika kitenzi kifuatacho kidhamira (ala 3)
      Aliyekufa
    6. Yakinisha katika wingi sentensi ifuatayo ( ala2)
      Wanafunzi walisoma vitabu hivyo
    7. Taja matumizi mawili ya paradesi (ala 2)
    8. Tunga sentensi ukitumia kiunganishi cha masharti (ala 1)
    9. Tunga sentensi moja na uonyeshe aina mbili za vishanzi (ala 2)
    10. Andika miundo mitatu ya ngeli ya U- ZI (ala 3)
    11. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao (ala 2)
      N+RH+t+E
    12. Andika upya ukifuata maagizo (ala3)
      1. Maji ambayo wanakunywa ni hatari ( Andika katika hali ya mazoea bila kutumia “amba”)
      2. Watu wengi walihasirika bomu lilipolipuka katika jingo hilo (tumia nomino badala ya vitenzi vilivyo pigwa mstari)
    13. Andika sentensi ifuatayo katika hali timilifu (ala 1)
      Waziri anasoma hotuba yake
    14. Tunga sentensi na uonyeshe kiima, kitondo na kipozi (ala3)
    15. Changanua utungo ufuatao kwa muundo wa mstari ( ala 3)
      Mimi nitaenda maktabani leo.
    16. Tunga sentensi kuonyesha majukumu matatu ya kiimbo.(al 3)
    17. andika sentensi ifuatayo katika kauli ya ketendewa (ala 2)
      Nzi hawa wamemsumbua Musa kwa muda mrefu
    18. Taja methali inayoafiki maelezo yafuatayo (ala 1)
      Mtu anayetegemea jamii akiondoka wanaomtegemea huwa mashakani
    19. Andika sentensi ifuatayo upya kwa kufuata maagizo kwenye mabano (ala 1)
      Mama alimkaripia mtoto mtoro (anza kwa mtoto)
  3. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
    1. Eleza dhana ya isimu jamii ( ala 2)
    2. Taja nadharia zozote tatu zinazoelezea chimbuko la Kiswahili (ala 3)
    3. Eleza sifa zozote tano za sajili ya hospitalini ( 5)
  4. FASIHI
    USHAIRI ANDISHI(alama 20)
    1. Taja vipengele vyovyote vitano vinavyozingatiwa wakati wa kuainisha shairi kiumbo/muundo.(al5)
  5. USHAIRI SIMULIZI
    1. Fafanua aina zifuatazo za nyimbo.(al 5)
      1. Mbolezi
      2. Sifa/tukuza
      3. Wawe/vave
      4. Nyiso
      5. Bembea/bembelezi
    2. Eleza dhima ya nyimbo.(al5)
  6. CHOZI LA HERI (alama 15)
    1. Fafanua sifa za wahusika wafuatao.
      1. Ridhaa
      2. Kaizari
      3. Mwangeka

Mwongozo wa Kusahihisha

  1. UFAHAMU
    Maswali
    1. Kwa nini viwanda ni muhimu? (ala 2)
      • Hugeuza malighafi inayopatikana kwa bidhaa za kutumiwa na watu.
    2. Ni nini kiini cha matatizo au uuzaji wa bidhaa katika nchi zinazoendelea? (ala2)
      • Masoko finyu kutokana na uwezo wa wanunuzi.
    3. Eleza faida zinazotokana na kuwepo kwa viwanda vidogo (ala4)
      • Vina uwezo wa kuwaajiri wafanyakazi wengi
      • Hakuhitaji mtaji mkubwa
      • Ni rahisi kujaribisha bidaa mpya kwa kiwango kidogo cha kiwanda kidogo.
      • Huwa chocheo kubwa la usambazaji wa viwanda hadi maeneo ya mashambani.
      • Watu wengi wanaweza kuanzisha viwanda hivyo.
    4. Usambazaji wa viwanda katika maeneo ya mashambani una faida gani? (ala 4)
      • Nafasi za ajira zimesambazwa.
      • Hutoa mweneo mzuri wa kimapatao
      • Huboresha uwezo wa kiununuzi wa umma
      • Ni msingi mkubwa wa kujitegemea kiuchumi.
    5. Fafanua maana y msamiati huu kama ulivyotumika katika kifungu. (ala3)
      • Kujasurisha - Kuanzisha
      • Amali - Kazi
      • Utashi Hamu
        • Adhibu kosa la kisarufi litokeapo mara ya kwanza hadi makosa sita (½ x 6 = 3)
        • Adhibu Kosa la hijai litokeapo mara ya kwanza hadi makosa sita (½ x 6 = 3)
        • Adhibu kosa la hijai hata pale amekosea jibu.
  2. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1. Taja na ueleze aina mbili kuu za ala za matashi (ala 2)
      • Ala tuli – ala ambazo hazisogei sauti inapotamkwa.
      • Ala sogezi - ala ambazo husogea sauti inaptamkwa.
    2. Linganisha sauti zifuatazo (ala 2)
      • /dh/ na /th/ Zote ni sauti za menoni
      • /o/ na /u/ - zote mdomo huwa umeviringwa
    3. Onyesha silabi ambazo zitatiwa shadda katika maneno haya (ala 2)
      • Msisimko - m
      • Maswali - wa
      • Tafadhali - dha
      • Mchunga – chu
    4. Tunga sentensi ukitumia mofimu huru ambayo ni kivumishi (ala2)
      • Mtoto safi ametuzwa
      • Mifano ya mofimu huru ambazo ni vivumishini hodari, jasiri, n.k.
    5. Ainisha viambishi katika kitenzi kifuatacho kidhamira (ala 3)
      • Aliyekufa
         A  li  ye  ku  f  a
         Nafsi/Ngeli  wakati   O rejeshi  mtendwa  mzizi  kiishio
    6. Yakinisha katika wingi sentensi ifuatayo ( ala2)
      Wanafunzi walisoma vitabu hivyo
      • Wanafunzi walisoma vitabu hivyo

    7. Taja matumizi mawili ya paradesi (ala 2)
      • Hutumiwa kutoa maelezo zaidi
      • Kutungia herufi au nambari
      • Hutumiwa katikamaandishi ya kitamthilia ili kufungia mambo zaidi.

    8. Tunga sentensi ukitumia kiunganishi cha masharti (ala 1)
      • Baadhi ya viunganishi vya masharti ni kama vile; kama, ikiwa, iwapo, mradi.

    9. Tunga sentensi moja na uonyeshe aina mbili za vishanzi (ala 2)
      • Mzee aliyefika leo alikuwa mwema.
      • Mzee alikuwa mwema – kishazi huru
      • Aliyefika leo – kishazi tegemezi.
    10. Andika miundo mitatu ya ngeli ya U- ZI (ala 3)
      •     U  – NY
        Uso  – Nyuso
        Uma – Nyuma
      •    U – ND
        Ujiti – Njiti
        Ujukuti – Njukuti
      •    W – NY
        Waya – Nyaya
        Wakaa – Nyakaa
    11. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao (ala 2)
      N+RH+t+E
      • Nguo ya mama ilishonwa vizuri
    12. Andika upya ukifuata maagizo (ala3)
      1. Maji ambayo wanakunywa ni hatari ( Andika katika hali ya mazoea bila kutumia “amba”)
        • Maji wanywayo ni hatari.
      2. Watu wengi walihasirika bomo lilipolipuka katika jengo hilo (tumia nomino badala ya vitenzi vilivyo pigwa mstari)
        • Watu wengi walipata hasara kulipotokea mlipuko katika jengo hilo.
    13. Andika sentensi ifuatayo katika hali timilifu (ala 1)
      Waziri anasoma hotuba yake
      • Waziri amekuwa akisoma hotuba yake.
    14. Tunga sentensi na uonyeshe kiima, kitondo na kipozi (ala3)
      • Mama alimpikia mgeni nyama tamu
      • Mama – kiima
      • Mgeni – kitondo
      • Nyama tamu - Kipozi
    15. Changanua utungo ufuatao kwa muundo wa mstari ( ala 3)
      Mimi nitaenda maktabani leo.
      • S(KN + N + KT) KN (W) KT CT + E + E)
    16. Tunga sentensi kuonyesha majukumu matatu ya kiimbo. (ala3)
      • Mtoto Analia.(sentensi ya taarifa)
      • Mtoto Analia!(sentensi ya kuonyesha mshangao)
      • Mtoto Analia?(sentensi ya kuonyesha swali)
    17. Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya ketendewa (ala 2)
      Nzi hawa wamemsumbua Musa kwa muda mrefu
      • Musa amesumbuliwa na nzi hawa kwa muda mrefu.
    18. Taja methali inayoafiki maelezo yafuatayo (ala 1)
      Mtu anayetegemea jamii akiondoka wanaomtegemea huwa mashakani
      • Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba.
    19. Andika sentesi ifuatayo upya kwa kufuata maagizo kwenye mabano (ala 1)
      Mama alimkaripia \]toto mtiro (anza kwa mtoto)
      • Mtoto mtoro alikaripiwa na mama.
  3. ISIMU JAMII (ALAMA 15)
    1. Eleza dhana ya isimu jamii ( ala 2)
      • Tawi la isimu linalochunguza matumizi ya lugha katika jamii.
    2. Taja nadharia zozote tatu zinazoelezea chimbuko la Kiswahili (ala 3)
      • Kiswahili ni lugha ya kibantu
      • Kiswahili ni lugha mseto
      • Kiswahili ni lugha ya kiarabu.
    3. Eleza sifa zozote tano za sajili ya hospitalini ( 5)
      • Huwa kuna kutohoa kwa maneno kama vila bendeji, operesheni, daktari n.k.
      • Kuna matumizi ya istilahi maalumu kama vile VCT, CD4, tembe, machela.
      • Lugha ya mafumbo/Usiri k ama vile tumempoteza kwa maana ya amekufa.
      • Kuna matumizi ya lugha ya tarakimu kama vile 1 x 3
      • Kuchanganya ndimi/msimbo, kwa mfano wawtoto w ote must be vaccinated.
      • Lugha ya kudadisi/Kuhoji kufahamu shida ya mgonjwa. k.g.
        Daktari: Umeanza kuendesha lini?
        Mgonjwa: Leo asubuhi
        Daktari: Je, umekunywa dawa yeyote?
        Mgonjwa: La
        (Sharti mwanafunzi atolee mifano; bila mifano ondoa nusu).
  4. USHAIRI ANDISHI: (ALAMA 5)
    1. Taja vipengele vyovyote vitano vinavyozingatiwa wakati wa kuainisha shairi kiumbo/muundo.
      • Mfangilio wa vina
      • Idadi ya mizani
      • Idadi ya vipande
      • Idadi ya beti
      • Idadi ya mistari/ishororo katika ubeti. n.k.)
  5. USHAIRI SIMULIZI
    1. Fafanua aina zifuatazo za nyimbo (ala 5)
      • Mbolezi - Nyimbo ambazo huimbwa wakati wa kuomboleza kama vile matanga, mazishi au janga.
      • Sifa/Tukuza – Huimbwa kumsifu mtu Fulani kwa mchango wakek katika jamii.
      • Wawe / Vave – Huimbwa wakati wa kulima.
      • Nyiso - Huimbwa wakati wa jando na unyago
      • Bembea / Bembelezi - Huimbwa watoto kuwafariji au kuwabembeleza walale au waache kulia .
    2. Eleza dhima ya nyimbo (ala 5)
      • Nyimbo hutumiwa kama burudani, kufurahisha, kustarehesha na kusisimua.
      • Hukuza ubunifu mlangoni mwa wanajamii kwani uimbaji ni kipawa na nyimbo hupalilia kipawa hiki.
      • Hupitisha amali na mambo ambayo jamii inayathamini.
      • Ni mbinu mojawapo ya kuhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii.
      • Nyimbo husaidia binadamu kutakasa hisia zake.
      • Nyimbo hutambulisha jamii kwa kusawiri shughuli na maisha ya jamii ilizibuni.
  6. CHOZI LA HERI
    1. Fafanua sifa za wahusika wafuatao.(ala 15)
      • Ridhaa
      • Ni mwenye bidii. Ni dakari ambaye alifanya kazi kwa uadilifu.
      • Ni msomi. Amesomea udaktari.
      • Mwenye uhusiano mwema. Anakula pamoja na majirani.
      • Ni mshirikina.anahusisha milio ya bundi na jambo mbaya kutokea.
      • Mwenye mapenzi. Anawapenda wanawe sana.
      • Ni mkarimu.anasaidia jamii kwa kujenga hospitali.
      • Amepevuka .anasema iwapo hakutakuwa na njia madhubuti ya kusuluhisha migogoro kunaweza shuka shida tena.
      • Ni mvumilivu.anavumilia kuona mabaki ya kuteketezwa kwa familia yake
        (mwanafunzi lazima afafanue sifa zingine zozote.)
    2. Kaizari
      • Alikuwa babake mwanaheri na lime.
      • Ni mwenye busara.aliyajenga maisha ya familia yake upya baada ya kurejea kutoka msitu wa mamba
      • Ni mvumilivu. Alivumilia kuiona familia yake ikifanyiwa ukatili na vijana .
      • Ni msomi.amesomea utabibu.
      • Ni mwenye uhusiano mwema.anajihusisha na wakimbizi wengine kwenye msitu wa mamba.
      • Ni mwenye mapenzi .anawapenda wanawe na mke wake subira
        (mwanafunzi afafanue sifa zingine zozote)
    3. Mwangeka
      • Ni mwanawe Ridhaa na Terry.
      • Ni msomi.ana shahada ya uhandisi.
      • Ni mlezi mwema. Analea familia yake vizuri.
      • Ana uhusiano mwema.anajihusisha vizuri na familia yake.
      • Ni mzalendo.anaenda mashariki ya kati kuleta Amani.
      • Ni mkarimu.anaonyesha ukarimu kwa umu na nduguye Dickson.
      • Ana mapenzi ya dhati. Anampenda mke wake lily nyamvula.
      • Ana msimamo dhabiti.anaamua kujiunga na wanamaji hata baada ya rai ya mkewe lily.
        (mwanafunzi afafanue sifa )
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Term 2 Opener Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest