Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 End Term 2 Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. Wewe ni katibu wa chama cha viongozi wa wanafunzi katika shule za sekondari katika kaunti. Hivi majuzi mmekuwa na mkutano wa kujadili matatizo yanayowakumba viongozi hao.
  Andika kumbukumbu za mkutano wenu.
 2. Njaa ni tatizo sugu katika nchi yetu.
  Fafanua mbinu mwafaka zinazofaa .
 3. Andika insha juu ya Methali mcheza na tope humrukia.
 4. Andika insha itakayoishia kwa maneno haya.
  …………………………. Nilisimama na kuangalia nyuma. Nilipokumbuka wosia wa walimu, wazazi na wenzangu nilidondokwa na machozi.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. KUMBUKUMBU

Anwani ishughulikie

 • Kutambulisha mkutano ni wa nini?
 • Mahali
 • Tarehe
 • Saa

Mahudhurio kuwe na: -

 • Waliohudhuria na nyadhifa zao
 • Waliotoa udhuru
 • Waliokosa kuhuduria

Ajenda
Yafuatayo ni lazima yawemo:

 1. Wasilisho la mwenyekiti
 2. Kusoma na kuthibitsha kumbukumbu za mkutano uliotangulia
 3. Yaliyotokana na kumbukumbu hizo
 4. Ajenda
 5. Shughuli nyinginezo
 6. Kufunga mkutano
 7. Thibitisho

Tanbihi lazima mtahiniwa atilie maanani hoja
Baadhi yazo ni:

 • Kukosa mamlaka ya kuwaadhibu wanafunzi wasio na nidhamu.
 • Kulemewa na masomo ingawa ni viongozi.
 • Kushindwa kujieleza mbele ya wanafunzi.
 • Kushindwa kusawazisha wakati wa masomo na wa uongozi.
 • Kutoungwa mkono na wanafunzi wenzao.
 • Sheria kali katika shule ambazo huwawia vigumu kutekeleza.
 • Kuchukiwa na wanafunzi wenzao na kuchukuliwa kama adui
  Mwalimu asahihishe hoja nyinginezo.
 1. Mbinu mwafaka zinazofaa kufuatwa ili kukabiliana na tatizo la njaa.
  1. wakulima wasaidiwe na mbegu, mbolea.
  2. Bei ya mbolea, mbegu, jembe kushushwa.
  3. kuwasaidia wakulima kuuza mazao yao.
  4. kuhimiza upanzi wa vyakula vya kiasili: kwa mfano: mtama, viazi, vitamu, mihogo
  5. kuhimiza vyakula vinavyohimili kiangazi.
  6. Wakulima kufunzwa mbinu za kisasa za kilimo.
  7. Kuleta taasisi za kilimo mashinani kama vile K.F.A.
  8. Maonyesho ya kilimo yapewe kipaumbele.
  9. Wakulima wahamasishwe kuhusu kilimo biashara.
 2. Mtahiniwa atambue hii ni methali wala si fungu la maneno tu.
  • Mchezo – anayecheza
  • Tope – undongo uli maji
  • Humrukia, humshika, hupatwa na matope.
  • Mtu anayehusika na jambo, Fulani au anayefanya jambo mahali Fulani huathirika baadaye kutokana na hali hiyo.
  • Si lazima atoe maana
  • Atoe kisa au visa vinavyoafikiana na methali.
 3. Mtahiniwa aandike insha inayoaana na dondoo hili.
  Lazima mtahiniwa amalizie kwa maneno haya.

MAMBO YA JUMLA YA KUZINGATIA KATIKA KUSAHIHISHA INSHA

 1. UREFU WA INSHA:
  sharti kila insha iwe na maneno yasiyopungua 400
  • Maneno 350 hadi 400 alama 20.
  • Maneno 300 hadi 350 alama 15.
  • Maneno 300 hadi 350 alama 10.
  • Maneno 150 hadi 200 alama 5.
 2. MSAMIATI
  • Mtahiniwa atumie maneno au msamiati anaoelewa barabara
  • Mtahiniwa apambe insha yake kwa methali, misemo, milio, tashbihi n.k.
  • Mtahiniwa atumie msamiati unaooana na mada aliyopewa.
 3. SARUFI
  • Matumizi mazuri ya uambatanisho wa ngeli
  • Matumizi yafaayo ya nyakati
  • Kuakifisha insha yake ipasavyo.
  • Kuunganisha na kutenganisha maneno ifaavyo n.k.
 4. MTINDO
  • Mpangilio mzuri wa aya
  • Insha iwe na utangulizi, mwili na tamati
  • Kazi iwe nadhifu – asifute ovyo.
  • Mtiririko mzuri wa mawazo/vitushi kutoka mwanzo au mwisho.
 5. MAUDHUI
  • Ikiwezekana,insha iwe na hoja SITA kuu.
  • Kila moja itajwe, ielezwe kwa undani na itolewe mifano mwafaka
  • Kila moja iwe na aya yake.
 6. UBUNIFU
  Mtahiniwa adhihirishe kiwango cha juu cha ubunifu kuhusu hoja kuu na majina ya wahusika na pahali – husika.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 End Term 2 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest