Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Term 1 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp
INSHA 
Andika ratiba kuhusu siku ya kutuza wanafunzi bora shuleni. 
  1. UFAHAMU (ALAMA 15)
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata

    Uwezo wa mtu kudanganya huonekana mapema zaidi na katika dunia yenye watu wakazi tofauti uwezo huu huonekana katika kila aina ya watu duniani kwa kipindi cha mapema zaidi.

    Saikolojia ya nadharia ya uwongo ambapo mtu anaweza au kuufinyanga anavyotaka nikidi ambapo mtu ana miaka minne, lakini si nchini ya hapo.

    Watoto hujifunza kutokana na uzoefu na kama wakigudua kwamba wanaposema uwongo wanaadhibiwa huacha kusema uwongo mpaka pale ambapo wanajua namna ya kuunga uwongo wao na kuacha maswali ambayo hayawezi kujibika.

    Watoto wanapokuwa wameshajua namna ya kuujenga uwongo mpaka ukakubalika wanakuwa hatari zaidi kwani wanakuwa wameshatoka katika maadili ya kawaida ya ubaya wa kudanganya.

    Watoto hawa huweza kujifunza kudanganya baada ya kuona kwa miaka mingi watu wanavyodanganya.  Wengine hudanganya kwa bahati mbaya na wengine huwa na tabia mbaya.

    Wanaodanganya kwa bahati mbaya mara nyingi hubadilika wanapokuwa watu wazima, lakini pia hata wale wanatengeneza tabia hubadilika baadaye lakini si sana.

    Wakati fulani wapo watu wanaofikiri kwamba watoto hudanganya zaidi kuliko watu wazima.

    Uwongo wa watu wazima huwa mbaya zaidi na wenye utata mkubwa kuutambua na hii hutegemea zaidi mbinu za udanganyifu, mazingira na tabia nyingine za watu wazima.  Na wapo watu wazima wenye tabia ya kudanganya au kwa lugha ya kitaalamu, pseudolojia fantastika.

    Wanafalsafa kama Mtakatifu Augustine, na pia Thomas Aquinas na Immanuel Kant, wanalaani aina zote za udanganyifu. Kwa mujibu wa watu hao watatu hakuna sababu ya aina yoyote ile ya kudanganya.

    Ni vyema mtu akauawa, kuteseka au kupata magumu kuliko kudanganya hata kama njia moja  pekee iliyobaki ya kujihami ikiwa ni hiyo.  Wanafalsafa hao wanasema kwamba kudanganya kunaharibu uwezo wa mtu kuaminika katika jamii au jamii yenyewe kuaminika. 
    1. Ipe taarifa anwani mwafaka. (alama 2)
    2. Ni katika hali gani uwezo wa mtu kudanganya huonekana mapema zaidi? (alama 2)
    3. Ni wakati gani uwongo waweza kuwa hatari zaidi. (alama 2)
    4. Ni nini sababu ya watoto kudanganya. (alama 3)
    5.  
      1. Eleza mtazamo wa mtakatifu Augustine na Thomas Aquinas kuhusu udanganyifu. (alama 2)
      2. Kulingana na watu waliotajwa hapo juu kudanganya kuna madhara gani. (alama 2)
    6. Eleza maana ya msamiati kama ulivyotumika katika taarifa. (alama 2)
      1. Kuufinyanga
      2. Kujihami
  2. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 25)
    1. Andika sauti yenye sifa zifuatazo.
      1. Sauti ya kaa kaa laini. (alama 1)
      2. Kikwamizo cha ufizi. (alama 1)
    2. Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo. (alama 2)
      1. Maziwa yote yamemwagika
      2. Maziwa yoyote yatamfaa mtoto
    3. Eleza maana ya mofimu. (alama 2)
    4. Andika ukubwa wingi wa. (alama 2)
      Mwizi aliiba kikapu na ng’ombe.
    5. Yakinisha kwa umoja. (alama 2)
      Kamba zisingekatika zisingepotea.
    6. Andika kwa usemi wa taarifa. (alama 3)
      “Viungo hivi havitatosha kuunga mchuzi wenu,” mpishi alilalamika.
    7. Tunga sentensi mbili kuonyesha maana tofauti za neno ‘jua’ (alama 2)
    8. Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo. (alama 2)
      1. Tuma
      2. Lima
    9. Eleza tofauti ya sentensi zifuatazo. (alama 2)
      1. Ningefurahi kama ungefanya kazi
      2. Ningalifurahi kama ungalifanya kazi.
    10. Kanusha sentensi ifuatayo (alama 2)
      Mkiondoka mapema mtafika kwa wakati.
    11. Jaza pengo. (alama 2)
      kitenda             kitendeshwa                  kitendeshea
      Lia                    ……………….                …………………..
      Cheza              ………………..               ………………….
    12. Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi ya kistari kifupi. (alama 2)
  3. ISIMU JAMII (ALAMA 5)
    A: Wee kuja hapa! Wewe ni nani? Sema haraka !
    B : Mimi ….. ni….. afande  Lona.
    A : Unatoka wapi saa ii?
    1. Tambua sajili hii. (alama 1)
    2. Fafanua sifa za sajili hii. (alama 4)
  4. FASIHI SIMULIZI (ALAMA 5)
    Fafanua umuhimu wa nyimbo katika jamii.

MARKING SCHEME

      • Udanganyifu na mwanadamu
      • Namna mtoto anovyojenga udanganyifu/ uwongo
    2. Ni katika hali gani uwezo wa mtu kudanganya huonekana mapema zaidi? (alama 2)
      • Katika dunia ya watu wa kzai tofauti na katika kila aina ya watu duniani
    3. Ni wakati gani uwongo waweza kuwa hatari zaidi. (alama 2)
      • Wakati mtoto atakuwa ameshatoka katika maadili ya kawaida ya ubaya wa kudanganya
    4. Ni nini sababu ya watoto kudanganya. (alama 3)
      1. Baada ya kuona kwa miaka mingi watu wanavyodanganya
      2. Wengine ni kwa bahati mbaya
      3. Wengine huwa na tabia mbaya
    5.  
      1. Eleza mtazamo wa mtakatifu Augustine na Thomas Aquinas kuhusu udanganyifu. (alama 2)
        • Kuwa hakuna sababu ya aina yoyote ile ya mtu kudanganya
      2. Kulingana na watu waliotajwa hapo juu kudanganya kuna madhara gani. (alama 2)
        • Kunaharibu uwezo wa mtu kuaminika katika jamii au jamii yenyewe kuaminika
    6. Eleza maana ya msamiati kama ulivyotumika katika taarifa. (alama 2)
      1. Kuufinyanga - kubuni/ kujenga uwongo
      2. Kujihami - kujichunga nafsi usidhurike/ kujitetea usijipate kwa matatizo/ kujitetea ili ujiondoe kwa matatizo
  2. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 25)
    1. Andika sauti yenye sifa zifuatazo.
      1. Sauti ya kaa kaa laini. (alama 1)
        • /k/, /g/, /ng'/, /gh/
      2. Kikwamizo cha ufizi. (alama 1)
        • /s/, /z/
    2. Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo. (alama 2)
      1. Maziwa yote yamemwagika
        • kwa ujumla/bila kubakisha
      2. Maziwa yoyote yatamfaa mtoto
        • bila kuchagua/ kutojali
    3. Eleza maana ya mofimu. (alama 2)
      • Sehemu ndogo ya neno inatyowasilisha maana
    4. Andika ukubwa wingi wa. (alama 2)
      Mwizi aliiba kikapu na ng’ombe.
      Majizi yaliiba majikapu na magombe.
    5. Yakinisha kwa umoja. (alama 2)
      Kamba zisingekatika zisingepotea.
      Kamba ingekatika ingepotea
    6. Andika kwa usemi wa taarifa. (alama 3)
      “Viungo hivi havitatosha kuunga mchuzi wenu,” mpishi alilalamika.
      • Mpishi alilalamika kuwa viungo hivyo havingetosha kuunga mchuzi wao.
    7. Tunga sentensi mbili kuonyesha maana tofauti za neno ‘jua’ (alama 2)
      1. Jua huchomoza asubuhi na hutua jioni
      2. Baba alipoitwa shuleni, alijua kulikuwa na jambo baya 
        (mwalimu akadirie majibu ya mwanafunzi)
    8. Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo. (alama 2)
      1. Tuma - mtumwa, utumwa, mtume
      2. Lima - kilimo, mkulima, ukulima
    9. Eleza tofauti ya sentensi zifuatazo. (alama 2)
      1. Ningefurahi kama ungefanya kazi
        • Kuna uwezekano
      2. Ningalifurahi kama ungalifanya kazi.
        • Hakuna uwezekano
    10. Kanusha sentensi ifuatayo (alama 2)
      Mkiondoka mapema mtafika kwa wakati.
      Msipoondoka mapema hamtafika kwa wakati.
    11. Jaza pengo. (alama 2)
      kitenda             kitendeshwa                  kitendeshea
      Lia                    …Lizwa…                 ……Lizia……………..
      Cheza              …chezeshwa......       ……chezeshea……... ( 4x½=2)
    12. Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi ya kistari kifupi. (alama 2)
      1. Tarehe - Wageni watawasili tarehe 2-01-2022
      2. Ufafanuzi wa maelezo - Mboni yua jicho - sehemu ya ndani ya jicho.
        ( mwalimu akadirie majibu ya mwanafunzi)
  3. ISIMU JAMII (ALAMA 5)
    A: Wee kuja hapa! Wewe ni nani? Sema haraka !
    B : Mimi ….. ni….. afande  Lona.
    A : Unatoka wapi saa ii?
    1. Tambua sajili hii. (alama 1)
      • Sajili ya polisi/ askari washika doria
    2. Fafanua sifa za sajili hii. (alama 4)
      • Lugha hutumia msamiati maalum mf. afande
      • Lugha huwa na utohozi  mf. Twende stesheni
      • Lugha ni ya kuamrisha - Kuja hapa!
      • Lugha si sanifu mf. unatoka wapi saa ii?
      • Lugha huchanganya ndimi
      • Lugha ya udadisi/ maswali - wewe ni nani? Unatoka wapi?
  4. FASIHI SIMULIZI (ALAMA 5)
    Fafanua umuhimu wa nyimbo katika jamii.
    1. Nyimbo huburudisha jamii
    2. Hutoa mafunzo kwa jamii/ kuelimisha
    3. Huhifadhi utamaduni wa jamii
    4. Hutumiwa kupitisha ujumbe maalum
    5. Hufunza maadili
    6. Hukashifu  tabia zisizokubalika
    7. Huliwaza k.m mbolezi
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Term 1 Opener Exams 2023.

Tap Here to Download for 50/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest