Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 Term 2 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO KWA MTAHINIWA:

  • Karatasi hii ina maswali manne.
  • Jibu maswali mawili pekee. Kila swali lina alama ishirini.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Chagua swali jingine lolote kutoka kwa matatu yaliyosalia.
  • Majibu yote yaandikwe katika lugha ya Kiswahili.
  1. SWALI LA LAZIMA.
    Gari unalosafiria limehusika katika ajali mbaya barabarani. Japo kuna walioaga dunia, wewe hujadhurika kwa njia yoyote.
    Andika mahojiano kati yako na mwandishi wa gazeti la Mwangaza ambaye amekuja kukuhoji kuhusu ajali hiyo.
  2. Pendekeza njia mbalimbali zinazoweza kutumiwa ili kuleta utangamano wa kitaifa.
  3. Sitapiki nyongo harudi haramba.
  4. Malizia kwa maneno haya… hapo ndipo nilipogundua umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.

MARKING SCHEME

  1. Mahojiano
    1. Mwanafunzi aandike kichwa kikamilifu, kwa kutaja mahojiano ni baina ya nani na nani.
    2. Ahusishe maelezo kwenye mabano.
    3. Asiwache mhusika mmoja kutawala mahojiano.
    4. Maswali yasiwe ya kumwelekeza mhojiwa.
    5. Mane ya wazungumzaji yaandikwe upande wa kushoto.
  2. Utangamano wa kitaifa.
    Mwanafunzi ashughulikie kila hoja katika aya yake.
    • Elimu
    • Michezo/spoti
    • Michezo ya kuigiza(drama)
    • Dini
    • Ugatuzi wa rasilimali katika kila jimbo/kaunti
    • Kuhimiza ndoa baina ya makabila tofauti.
    • Kupitia kwa vyombo vya habari (magazeti, redio, televisheni)
    • Mikutano ya kuhubiri amani n.k.
    • Kutafuta mbinu ya kupunguza jumbe za chuki kupitia mtandao.
    • Ikiwezekana kutolewe nafasi sawa za kazi kwa jamii zote.
  3. Methali: mwanafunzi athibitishe methali katika masimulizi
    Sitabiki nyongo harudi haramba.
    Nyongo – utomvu au maji machungu yaliyomo katika kibofu kidogo juu ya ini.
    Maana yake – siwezi kutapika nyongo kisha nikarudi nikairamba. Jambo ambalo mtu alilisema hawezi tena akalikana au mtu hawezi kuwa ameiasi tabia fulani kisha airudie.
  4. Insha ya kumalizia. (Mdokezo)
    . . . Hapo ndipo nilipogundua umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.
    • Yaliyomo kwenye mwili yaoane na maneno yaliyomalizia insha.
    • Mada ikuzwe kikamilifu ili kuibua taharuki.
    • Mbinu za uandishi kama vile methali, tashbihi n.k. zitumiwe kwa njia ifaayo.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 Term 2 Opener Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest