Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 Term 2 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp
MAAGIZO
  • Jibu maswali yote
  • Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa  katika kijitabu hiki cha maswali
  1. UFAHAMU 
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

    Ufisadi ni uhalifu unaohusu kuzitumia njia za ulaghai kujipatia pesa, mali au vitu hasa vya umma.  Nchini Kenya ufisadi hujitokeza kwa njia mbalimbali na kila mojawapo ina athari zake.  Kwa mfano, kama maafisa wa serikali wajipatiao pesa kwa kuuza stakabdhi za serikali kama vile pasi, vyeti vya kuzaliwa, vyeti  ya kumiliki mashamba, vitambulisho na nyinginezo kwa raia. Kuna hatari kubwa kwa sababu watu wasio raia wa Kenya wameweza kusajiliwa kama wakenya na kuendeleza uhalifu kama ugaidi, wizi na ulanguzi wa dawa za kulevya.

    Wengine hujipatia vibali vya kufanya kazi na kuajiriwa kazi ambazo zingefanywa na wakenya.  Hii imechangia ongezeko la uhaba wa kazi nchini.  Watumishi wengine wa umma huuza mali ya serikali kama vile magari, nyumba na ardh na kufutika pesa za mauzo mifukoni mwao.  Wengine wao hujinyakulia na kufanya vitu hivyo kuwa mali yao.  Ufisadi wa aina hii umegharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha.  Serikali imelazimika kununulia maafisa wake magari baada ya muda mfupi,  kulipia wafanyi kazi  wake kodi za nyumba na kukosa viwanja vya upanuzi na ujenzi wa shule hospitali, vituo vya polisi na taasisi zingine maalumu.

    Baadhi ya wataalamu kama madaktari huiba dawa kutoka hosptiali za umma na  kupeleka vituo vyao vya afya.  Pia hutumia wakati wao mwingi katika kazi zao za kibinafsi na kuwaacha wagonjwa katika hospitali za umma wakihangaika.  Sio madaktari tu, kuna masoroveya, wahandisi, mawakili, walimu na mahasibu ambao hukwepa majukumu yao serikalini na kufanya kazi za kibinafsi.

    Wengine wasio wataalam huendesha biashara za aina tofauti, na huku wanaendelea kopokea mishahara.

    Wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo na shule bora za umma na hawakuhitimu wakati mwingine halazimika kusalimu amri na kutoa hongo ili wapate nafasi za kusoma.  Kiasi cha pesa kinachohitajika huwa  kikubwa  hivi kwamba ni wachache humudu hizo rushwa.

    Wale wasiojimudu kifedha hubaki wakilia ngoa.  Kuna wazazi ambao hutumia vyeo vyao na ‘udugu’ kupata elimu.  Matokeo huwa ni kuelimisha watu wasiostahili na ambao mwishowe hawaziwezi kazi wanazosomea wakihitimu na kuanza hudumia jamii.

    Ufisadi umekita mizizi na kushamiri katika sekta za  umma na za kibinafsi kwa upande wa kuajiri wafanyakazi.  Ni vigumu kupata kazi ikiwa humjui mtu mkubwa katika shirika linalohusika au uzunguke mbuyu.  Matokeo ni kuajiri wafanyikazi wasiohitimu na wasiowajibika kazini.
    Hata hivyo, mbio za sakafuni huishia ukingoni.  Serikali imetangaza vita dhidi ya ufisadi.

    Tayari tume kadhaa zimebuniwa kuchunguza visa vya ufisadi uliotekelezwa hapo mbeleni.  Mojawapo ya tume hizo ni tume ya kuchuguza kashfa ya “Goldenberg” ambapo pesa za umma (mabilioni)  ziliporwa na mashirika na watu binafsi kwa njia zisiso halali.  Watakaopatikana na hatia ya kushiriki ufisadi huo watahitajika kurudisha pesa hizo.

    Serikali pia imeunda kamati ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi waliohasiriwa na mawakili walaghai ambao hupokea ridhaa kwa niaba ya wateja wao na kukosa kuwalipa au kuwatetea mahakamani ilhali wamekwishalipwa.  Ni matumaini yetu kuwa ulaghai huu  utaangamizwa kabisa kwani hakuna refu lisilokuwa na ncha.

    Maswali
    1. Eleza aina nne za ufisadi zilizotajwa katika kifungu ulichosoma (al. 4)
    2. Kulingana na kifungu ulichosoma, ufisadi umeathiri nchi yetu kwa njia gani?   (al. 2)
    3. Serikali inafanya jitihada gani ili kukomesha ufisadi? (al.3)
    4. Kwa maoni yako, unafikiri ufisadi husababishwa na nini? (al.2)
    5. Toa msamiati mwingine wenye  maana sawa na rushwa (al. 1)
    6. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa kifunguni. (al.3)
      1. shamiri ______________________________________
      2. Kashfa ______________________________________
      3. kita mizizi ___________________________________
  2. UFUPISHO
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali uliyolizwa


    Uzalishaji wa vyakula popote pale ulimwenguni unahusiana, na labda hata kudhibitiwa, na mazingira ambamo wanaohusika wanaishi.  Hata  hivyo, jambo la kusikitisha ni kuwa uharibifu wa kimazingira umefikia hatua ya kusikitisha.  Uharibifu huo unatokana na amali nyingi za kibinadamu ambazo zinaishia kuwa msingi wa mazingira yake kuathirika.  Ikiwa mazingira yameharibiwa kwa jinsi yoyote, kuna athari hasi ambazo hutokea.  Kwanza, rutuba iliyoko mchangani inafifia.  Kiwango cha mvua kinafifizwa pia na matendo hayo sawa na kuzuka kwa ongezeko la joto.  Wataalamu wanaeleza kuwa jangwa la Sahara linapanuka kwa zaidi ya kilometa kumi kwa mwaka.  Ikiwa hali hii itaendelea, itachukua miaka michache kwa sehemu kubwa ya bara la Afrika kugubikwa na mchanga wa jangwa hilo.  Mgubiko huo utakuwa na matokeo ambayo ni ya kusikitisha.

    Yapo maeneo  ambako miaka michache iliyopita yalisheheni rutuba namboji lakini sasa hivi hayana uwezo wa kuikuza hii mimea yoyote ile.  Zipo njia nyingi ambazo huchangia kwenye tanzo hili la mazingira.  Mojawapo katika matatizo hayo ni ukataji wa miti kiholela.  Ukataji huu ona athari mbaya hasa pale ambapo kiwango cha miti iliyokatwa au miche inayoatikwa.

    Tatizo jingine ni ufugaji unaokiuka uwezo wa  kipande cha ardhi cha kuhimili mifugo.  Ufugaji wa aina hii unatokana na kupungua kwa malisho yenyewe na labda kwa kiasi Fulani kuendelezwa kwa tamaduni zinazohimiza ufugaji pasi na kuwepo juhudi za kuipunguza mifugo yenyewe.  Lipo tatizo linalohusiana na kilimo, yaani ulimaji uliozidi.  Ulimaji huu unahusisha upandaji wa-zao lile lile katika ardhi ile ile msimu hadi insimu.  Huhusisha pia kilimo kisichotegemea mbolea au samadi.  Hali kama hii inaweza kutokana na wakulima kutumia mabua ya  mabaki ya chakula kwa ajili ya moto badala ya kuwa nyenzo ya kuundia mbolea.

    Kuwepo kwa mazingira kuna mchango mkubwa kwenye  lishe ya jamii inayohusika. Kwa mfano, miti na mimea inaweza kuwa chanzo cha rutuba ya udongo.  Aidha husaidia kukuzuia udongo usimomonyolewe na maji.  Husaidia pia kuhifadhi maji.

    Hali kama hii inawezesha kuwepo kwa miti ya matunda kama miembe, michungwa, mitufaa, mipera na kadhalika.  Hali hii pia inasaidia kuwepo kwa miti inayozalisha mafuta kama minazi.  Mazingira mazuri ni msingi muhimu wa kuwepo kwa majani.  Majani haya ni chakula muhimu cha wanyama ambao  pia ni chanzo  cha chakula kwa wanadamu.  Misitu, inayokua katika mazingira ya mvua huwa maskani ya nyuki  (wanaoleta asali) na mimea kama uyoga (unaoliwa),  Mikoko inayoota karibu na bahari na mazingira mazuri ya kamba na samaki wengine.  Isitoshe, miti huwa kuwa chanzo cha kuni za kupikia.

    Maswali
    1. Kwa kutumia maneno  60 – 65,eleza vile uharibifu wa mazingira kuendelezwa  (al.8)
      Matayarisho
      Nakala Safi
    2. Eleza uhusiano uliopo kati ya mazingira na lishe bora (al.7)
      Matayarisho
      Nakala safi
  3. MATUMIZI YA LUGHA    (ALAMA 40)
    1. Ni nini tofauti kuu kati ya irabu na konsonanti (al.2)
    2.  
      1. Taja sifa bainifu za  /e/
      2. Tofautisha sauti /f/ na (v) ukizingatia namna ya kutamka. (al.2)
    3. Tumia viunganishi vifuatavyo katika sentensi (al. 2)
      1. Mighairi
      2. madhali
    4. Tumia visawe vya maneno yafuatayo katika sentensi (al.2)
      1. mwandani
      2. Nyoka
    5. Tunga sentensi kuonyesha matumizi matatu ya ‘ku’ (al.3)
    6. Tunga sentensi moja ukitumia nomino katika  ngeli ya  Li-Ya (al.2)
    7. Ainisha vitenzi katika sentensi zifuatazo (al.3)
      1. Lenaiyara alikuwa nyumbani
      2. Lenaiyara alikuwa akilala  nyumbani
    8. Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa (wingi) (al.2)
      Nyumba hiyo ni ya mwanamke wa mzee huyo
    9. Andika katika usemi wa taarifa (al.3)
      “Kumbuka kuwa lazima ufike mapema kama wataka tuandamane leo”.  Baba akaniambia.
    10. Tambua virai vilivyopigiwa mstari chini (al.2
      Mwanafunzi mchafu  amefukuzwa  shuleni leo
    11. Andika sentensi kwa kutumia viambishi vya nyakati na hali zifuatazo (al.4)
      1. a
      2. ja
    12. Taja aina tatu za sentensi na kwa kila mojawapo toa mfano (al.3)
    13. Tambua shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi (al.2)
      Mtoto alisomea mama kitabu
    14. Nyambua kitenzi   ‘fa’ katika kauli zifuatazo (al.2)
      1. Tendea   ________________________________
      2. Tendewa  _______________________________
    15. Eleza matumizi ya  ‘kwetu’ katika sentensi zifuatazo (al.2)
      1. kwetu ni huku
      2. Mahali kwetu ni huku
    16. Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo (al.2)
      Khalif alisema kwamba lazima afaulu mtihani mwaka huu
    17. Unda vitenzi kutokana na nomino zifuatazo (al.2)
      1. Kinywaji
      2. hotuba
  4. ISIMU JAMII      (AL. 10)
    “Mabibi na Mabwana …………. Kaunti yetu imebaki nyuma kwa sababu ua uongozi duni.  Raudi hii wababa na wamama pamoja  na vijanaa lazima mabuda maanalogue  tuwasend home.  Mkinidunga votes zenu nitamake sure ………………..
    1. Tambua sajili iliyotumika (al.2)
    2. Eleza sifa za sajili hii (al.8)

MARKING SCHEME

  1. UFAHAMU (al.15)
    1.  
      • Wizi wa mali ya umma
      • Uuzaji wa stakabadhi za serikali
      • Kuiba dawa
      • Kuhonga au kutumia udugu kupata kazi
      • Kutowajibika kazini
        Zozote  4 x 1  Al.  4
    2.  
      • Kufilisi serikali
      • Kunyima wagonjwa matibabu
      • Kuzorotesha maendeleo na huduma muhimu
      • Kupandisha vyeo wasiostahili
      • Kutowajibika kazini
        Zozote  4 x ½   Al.  2
    3.  
      • Kuwashtaki  wahalifu
      • Kurudisha mali iliyoibwa
      • Kuunda kamati za kuchunguza visa vya ufisadi     3 x 1  Al.  3
    4.  
      • Tamaa ya mali
      • Umaskini
      • Uongozi mbaya
      • Uozo wa jamii
        Zozote  2 x 1  Al.  2
    5.  
      • Hakiki majibu ya mwanafunzi
      • Hongo/kadhonya/mlungula/chai/kitu kidogo/zunguka mbuyu.    1 x 1 Al. 1
    6.  
      1. Shamiri - kwenea kwa jambo au habari
      2. Kashifa - jambo la aibu kufichuliwa
      3. Kita mizizi  - kushikilia/kukolea     3 x 1  Al.  3
  2. UFUPISHO    (Al. 15)
    1.  
      • Mazingira yameharibiwa kupita kiasi
      • Mali za binadamu zimekuwa nyingi
      • Rutuba iliyoko mchangani imepungua
      • Ukataji wa miti kiholela
      • Ufugaji wa wanyama usiozingatia uwezo wa ardhi
      • Ulimaji uliozidi
      • Ulimaji ambao hautilii maanani suala la mbolea
      • Upandaji wa zao mara nyingi
        Zozote  7 x 1 
         1 uriririko
        Jumla  8
    2.  
      • Mimea ni chanzo cha rutuba ya udongo
      • Miti husaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo
      • Kuna miti ya matunda
      • Miti/misitu ni maskani ya nyuki wanaotoa asali
      • Mikoko ni mazingira ya samaki
      • Miti ni chanzo cha kuni zinazotumika kupika
      • Mazingira mazuri ni msingi muhimu wa kuwepo kwa maji
        Zozote  7 x 1 
         1 uriririko
        Jumla  7
  3. MATUMIZI YA LUGHA   (AL. 40)
    1. Hewa huzuiliwa wakati wa kutamka konsonanti lakini haizuiliwe wakati wa kutamka irabu  (al.2)
    2.  
      1.  
        • irabu ya mbele,
        • Kati
        • Mtandazo wa mdomo.
      2.  
        • /f/ – sighuna  (hafifu
        • /v/  -  ghuna
    3.  
      1. Mighairi  -  pasipo na, bila ya.
      2. Madhali  - kwa kuwa, kwa sababu (al.2)
    4.  
      1. Mwandani  - rafiki
      2. Nyoka  - kuwa bila mkunjo, mchango (al.2)
    5. Ngeli ya ku
      1. Kukanusha wakati uliopita
      2. Kiambishi cha mahali
      3. Kuwakilisha nafsi ya pili
      4. Mianzo ya vitenzi jina. (al.3)
    6.  
      • Tunda
      • Jitu (al.2)
    7.  
      1. alikuwa  - kitenzi  kishirikishi  (t)
      2. alikuwa – kitenzi kisaidizi  (Ts)
        Akilala    - kitenzi kikuu  (T)
        Vitenzi sambamba.
    8. Majumba hayo ni ya majanakike ya mazee hayo (al.2)  (½ x 4)
    9. Baba alinikumbusha kuwa ni lazima ningefika mapema kama ningetaka tuandamane naye siku hiyo. (al.3)
      Mwalimu akadirie
    10.  
      • Mwanafunzi mchafu   - Kirai nomino
      • Shuleni  leo -  kirai kielezi (al.2)
    11.  
      1. a – hali isiyodhihirika ya wakati uliopo
      2. Ja – ukanusho wa hali timilifu (al.4)
    12.  
      1. Sentensi sahili
      2. Sentensi ambatano
      3. Sentensi changamano (al.3)
        Kutaja ½  kutunga ½ nusus                                       =1 x3
      • Mama  - kitondo
      • Kitabu  - kipozi (al.2)
    13.  
      1. Tenda   - fia
      2. Tendewa  - fiwa (al.2)
    14.  
      1. Kwetu   - Kiwakilishi
      2. Kwetu  -  kivumishi
    15.  
      1. Khalif alisema kwamba  - kishazi tegemezi
      2. Lazima afaulu mtihani mwaka huu  -  kishazi huru (al.2)
    16.  
      1. Kinyuaji   - nywa/kunywa
      2. Hotuba   - hutubu (al.2)
  4. ISIMU  JAMII     (AL.10)
    1.  
      1. Lugha ya kisiasa
      2. Mkutano wa kisiasa
      3. Lugha ya  kuomba kura       2 x 1 = 2
    2.  
      • Lugha isiyo  sanifu
      • Kuchanganya ndimi
      • Ahadi nyingi
      • Lugha ya kushawishi
      • Msamiati mteule
      • Kukashifu  wengine
      • Kujisifu
        Kutaja   4 x 1  = 4
        Maelezo  4 x 1 = 4
        Jumla  -  8 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 Term 2 Opener Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest