Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 Term 2 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO:

  • Jibu maswali yote katika karatasi hii

SEHEMU YA A: TAMTHILIA YA KIGOGO

  1. “Do! Do! Simameni! Simameni! Leo kutanyesha mawe!
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
    2. Fafanua mbinu za lugha z ilizotumika katika dondoo hili. (al.4)
    3. Fafanua sifa sita za msemaji. (al.6)
    4. Eleza umuhimu wa msemaji. (al.2)
    5. Fafanua maudhui yoyote mawili yanayojitokeza katika dondoo. (al. 4)
  2. Fafanua matatizo yoyote kumi yanayowakabili wanasagamoyo. (al.20)

SEHEMU YA B: FASIHI SIMULIZI.

  1.  
    1. Eleza umuhimu wa nyimbo katika usimulizi wa hadithi. (al.4)
    2.  
      1. Eleza maana ya misimu. (al.2)
      2. Taja mifano yoyote miwili ya misimu. (al.2)
    3. Taja sifa tatu za vitanza ndimi. (al.3)
    4. Taja sifa tatu za vitendawili. (al.3)
    5. Fafanua umuhimu wa vitendawili. (al.6)

SEHEMU YA C: USHAIRI.

  1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yote.

    Akosaye shukurani, zako juhudi hajali,
    Hata mfanyie nini, haoni huyo hajali,
    Hata mpe milioni, matusi ndio stahili,
    Aona huna akili, ni yeye ndiye mshindi.

    Patia kila la shani, bure unajisumbua,
    Takuona kama nyani, tena atakunyambua,
    Akuona punguani, chochote hutaambua,
    Usingoje shukurani, tenda wema wende zako.

    Utafute kwa juhudi, bila kukata tamaa,
    Mpe apate faidi, wala asipate njaa,
    Hatachoka kukaidi, atakuletea baa,
    Na mawazo yakujaa, maishayo hafikiri.

    Mpe vyote vya haluwa,wenzako wamtamani,
    Hatakupa ya muruwa, juhudi haioni,
    Ataka kuzidishiwa, asubuhi na jioni,
    Ufanyacho hathamini, aongeze ya karaha.

    Si ndugu wala si mwana, si rafiki si jirani,
    Shukrani kiwa hana, jua uko hatarini,
    Hadharani tatukana, aulize ndiwe nani,
    Ambe kama hajaona, kinyangarika kamawe.
    Hebu yeye msaili, amepata toa nini?
    Haweziye kukubali, kukupa hata thamani,
    Ni bure wake ukali, akutia mashakani,
    Yake wala hayaoni, mwovu hana shukurani.

    Mfadhili watengaje, jana alikuopoa,
    Mwaema wambwekeaje, mabaya wayachokoa,
    Mzazi wadharauje, mbali alishakutoa,
    Sasa jaribu kupoa, ujifunze shukurani.

    Maswali
    1. Lipe shairi hili anwani mwafaka. (al.1)
    2. Hili ni shairi la aina gani? Thibitisha. (al.2)
    3. Eleza dhamira ya mshairi katika shairi hili. (al. 2)
    4. Bainisha mifano mitatu ya uhuru wa mshairi katika shairi hili. (al.6)
    5. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (al. 4)
    6. Taja na utolee mfano tamathali zozote mbili za usemi katika shairi. (al.4)
    7. Eleza maana ya neno hili kama lilivyotumika katika shairi hili. (al1)
      1. Shani

MARKING SCHEME

SEHEMU YA A: TAMTHILIA YA KIGOGO

  1. “Do! Do! Simameni! Simameni! Leo kutanyesha mawe!
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
      • Ni maneno ya ngurumo
      • Anawaambia walevi wenzake
      • Wangweni kwa mamapima /asiya
      • Anawaambia maneno haya anapowaona tunu na sudi kwa mamapima, jambo ambalo halikuwa la kawaida
    2. Fafanua mbinu za lugha z ilizotumika katika dondoo hili. (al.4)
      1. Nidaa – D0! Do!
      2. Takriri – Simameni! Simameni!
      3. Jazanda – kutanyesha mawe
    3. Fafanua sifa sita za msemaji. (al.6)
      • Mwasherati – ngurumo anashiriki mapenzi na Asiya mke wa Boza
      • Mwenye taasubi ya kiume, anaapa kuwa hawezi kumpa kura mwanamke, heri ampe paka
      • Mwenye ushawishi – anawashawishi vijana walevi kwamba kura zao watampa majoka
      • Ni mlevi – anapenda kunywa pombe mf. Yuko mangweni kwa mamapima akinywa pombe.
      • Mzalendo wa kijinga – ni mfuasi wa Majoka, anasema asipompa kura afadhali ampe paka.
      • NI mfisadi/ mla rushwa – anapokea rushwa kutoka kwa vigogo – anadai rushwa kutoka kwa vigogo – anadai kuwa tangu soko lifungwe amefaidika sana, vigogo wanaopita hapo hawakosi kumwachia kitu kidogo.
      • Ni msaliti – anawasaliti wanasagamonyo kwa kumuunga mkono Majoka japo anafahamu wovu wake.
      • Ni katili – anakubali kushirikiana na Majoka katika kumwangamiza Tunu
      • Ni mbinafsi- ashirikiana na mamapima katika biashara yake haramu inayowaathiri vijina wengi.
    4. Eleza umuhimu wa msemaji. (al.2)
      • Ni kielezo cha vijan awalevi wanaotumiwa na viongozi kuendeleza uovu
      • Ni kielelezo cha vijana wanaosaliti jamii kwa kuendeleza tamaa ya pesa.
    5. Fafanua maudhui yoyote mawili yanayojitokeza katika dondoo. (al. 4)
      • Maudhui ya ulevi – walikuwa mangweni katika baa la mamapima wakilewa
      • Maudhui ya ufisadi – biashara ya Asiya ilikuwa haramu, aliiendeleza kwa kupewa kibali na vigogo.
      • Uozo wa jamii/ ukatili – Asiya alisababisha vifo, upofu kupitia kwa mauzo ya pombe hii haramu.
  2. Fafanua matatizo yoyote kuni yanayowakabili wanasagamoyo. (al.20)
    • Kufungwa kwa soko – soko la chapakazi linafungwa. Ni katika soko hili wanasagamoyo wanapata riziki ya kukithi/ kukimu familia zao, basi wamekosa riziki mf. Ashua na Sudi.
    • Ardhi ya umma kunyakuliwa – Majoka anaapa kujenga hoteli ya kifahali kwenye soko la chapakazi
    • Wapinzani wa Majoka kuuliwa – Jabali aliuliwa kwa njama za Majoka kwa nia ya kusambaratisha chama cha mwenge. Tunu anashamburiwa nusura afe.
    • Wati kushambuliwa na askari kwa kupigwa risasi mf. Anamwamrisha Kingi awapige risasi kwa kukataa kuhudhuria mkutano wake (Majoka) na kuhudhuria wa Tunu.
    • Elima Mbovu – Elimu inayotolewa katika Majoka and Majoka Academy inawageuza vijana kuwaMakabeji
    • Kufungwa gerezani/ seli hatia au hata kupelekwa kortini. Ashua anafungiwa kwenye seli bila kosa lolote.
    • Soko la chapakazi kuwekwa katika hali mbaya – kuna uchafu na maji machafu yanayotoa uvundo.
    • Majoka anaruhusu biashara haramu, mamapima anasema amepewa kibali cha kuuza pombe Mangweni – pombe hii imewapofusha na kusababisha vifo.
    • Majoka anaruhusu uharibifu wa mazingira kwa kukubali biashara ya ukataji wa miti
    • Wanasagamoyo kulipa kodi ya juu- Ashua anasema kuwa kwao wanadai kitu kikubwa au kiti chote!
    • Wafanyikazi wa serikali kulipwa mishahara duni- waalimu na madaktari wanagoma kwa sababu hii.
    • Wanaharakati wanaopinga utawala wa Majoka wanatishwa – Vijikaratasi vilirushwa kwenye makao ya kina Siti wakiangizwa wahame, kwamba huko sio
    • Njaa – watoto wa Ahus na Sudu wakosa chakula
    • Mauaji ya kiholela – Vijana watano wanauawa wakati wa maandamano na wengine kuumia.
    • Kukosa huduma zakimsingi- Tuna anasema kuwa wanataka huduma ziletwe karibu nao, kama vile, barabara, hospitali, umeme, maji safi, vyoo na elimu.
    • Ukosefu wa ajira kwa vijana – akina Tunu Ashua na Sudi wamesoma lakini hawana kazi.
      (zozote 10 x 2 = 20)

SEHEMU YA B: FASIHI SIMULIZI.

  1.  
    1. Eleza umuhimu wa nyimbo katika usimulizi wa hadithi. (al.4)
      • Kuburudisha hadhira
      • Huvuta hisia za hadhira
      • Huodoa ukinaifu
      • Husisitiza ujumbe katika hadithi
      • Huelimisha hadhira. (zozote 4 x 1 4)
    2.  
      1. Eleza maana ya misimu. (al.2)
        • Misimu ni misemo inayohusishwa na kundi ndogo la watu na huzuka katika kipindi cha wakati.
      2. Taja mifano yoyote miwili ya misimu. (al.2)
        • Beste – rafiki
        • Sare – kubebwa kwenye matatu bila kulipa
        • Ashuu – shilling kumi
        • Matatu/ Daladala – gari la uchukuzi wa umma
        • Boda – pikipiki/ baikeli inayobeba kwa malipo. (mwalimu ahakiki majibu ya mwanafunzi (yoyote 2 x 1=2)
    3. Taja sifa tatu za vitanza ndimi. (al.3)
      • Huwa kauli zinazokangabya kimatamshi
      • Huwa ni mchezo wa maneno
      • Huundwa kwa sauti zinazokaribiana kimatamshi
      • Hutumia maneni yenye maana zaidi ya majoa au zenye sauti sawa.
    4. Taja sifa tatu za vitendawili. (al.3)
      • Lugha huwa ya kimafumbo
      • Hutumia lugha ya istiara
      • Huwa na mianzo maalumu
      • Aghalabu huegemea mazingira
      • Huwa fupi     (3x1 =3)
    5. Fafanua umuhimu wa vitendawili. (al.6)
      • Huburudisha hadhira
      • Huelimisha jamii
      • Hukuza ewezo wa kufikiri
      • Huhifadhi historia ya jamii
      • Hukuza ubunifu
      • Hutambulisha mazingira
      • Hukejeli tabia zisizokubalika. (6x1=6)

SEHEMU YA C: USHAIRI.

  1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yote.
    Akosaye shukurani, zako juhudi hajali,
    Hata nfanyie nini, haoni huyo hajali,
    Hata mpe milioni, matusi ndio stahili,
    Aona huna akili, ni yeye ndiye mshindi.

    Patia kila la shani, bure unajisumbua,
    Takuona kama nyani, tena atakunyambua,
    Akuona punguani, chochote hutaambua,
    Usingoje shukurana, tenda wema wende zako.

    Utafute kwa juhudi, bila kukata tama,
    Mpe apate faidi, wala asipate njaa,
    Hatachoka kukaidi, atakuletea balaa,
    Na mawazo yakujaa, maishayo hafikiri.

    Mpe vyote vya haluwa,wenzako wamtamani,
    Hatakupa ya muruwa, juhudi haioni,
    Ataka kuzidishiwa, asubuhi na jioni,
    Ufanyacho hathamini, aongeze ya karaha.

    Si ndugu wa si mwana, si rafiki si jirani,
    Shukrani kiwa hana, jua uko hatarini,
    Hadharani tatukana, aulize ndiwe nani,
    Ambe kama hajaona, kinyangarika kamawe.
    Hebu yeye msaili, amepata toa nini?
    Haweziye kukubali, kukupa hata thamani,
    Ni bure wake ukali, akutia mashakani,
    Yake wala hayaoni, mwovu hana shukurani.

    Mfadhili watengaje, jana alikuopoa,
    Mwema wambwekeaje, mabaya wayachokoa,
    Mzazi wadharauje, mbali alishakutoa,
    Sasa jaribu kupoa, ujifunze shukurani.

    Maswali
    1. Lipe shairi hili anwani mwafaka. (al.1)
      • Mkosa shukurani hajali/ mkosa shukurani
    2. Hili ni shairi la aina gani? Thibitisha. (al. 4)
      • Tarbia – lina mishororo minne kila ubeti
      • Mathawi – lia vipande viwili kila mshororo
      • Ukaraguni – vin avinambadirika ubeti hadi mwingine
        Kutaja (1mk) Kuthibitisha(1mk) 1 x2 =2)
    3. Eleza dhamira ya mshairi katika shairi hili. (al. 2)
      • Tujifunze kutoa shukurani kwa wenzetu waliotutenda mema ili tuimarishe uhusiano mzuri nao.
    4. Bainisha mifano mitatu ya uhuru wa mshairi katika shairi hili. (al.6)
      • Inkisari – takuona badala ya atakuona/ maishayo baa badala ya balaa
      • Tabdila – haluwa badaa yah aula, Muruwa badala ya murua
      • Kubananga/ kuboronga sarufi – zako juhudi hajali – hajali juhudi zako - bure unajisumbua – unajisumbua bure
      • Utohozi – milioni - million
    5. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (al. 4)
      • Hata uki,pa vyovyote vitamu vinavyowafanya wenzako waonee wivu hawezi kuonyesha wema wala kutambua juhundi zako. Yeye hutaka kupewa zaidi kila wakati. Kila unachokifanya hakithamini bali huongeza usumbufu.
    6. Taja na utoelee mfano tamathali zozote mbili za usemi katika shairi. (al.4)
      • Tabaine – si rafiki si jirani/ si ndugu si mwana
      • Tashbihi – takuona kama nyani
      • Msemo – Tenda wema nenda zako
      • Balagha – hebu yeye msaili amepata toa nini?
    7. Eleza maana ya neno hili kama lilivyotumika katika shairi hili. (al1)
      1. Shani - ajabu
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 Term 2 Opener Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest