- UFAHAMU
- Ni dalili ipi inayoonyesha mwanzo wa mageuzi? (al.1)
- Mtaala mpya unalenga nini? (al.4)
- Eleza lawama zinazoelekezewa kikosi cha polisi (al.2)
- Kwa mujibu wa taarifa eleza mageuzi matatu yaliyofanywa katika kikosi cha polisi (al.3)
- Taja makundi mawili yaliyohusika katika kuandaa mtalaa mpya (al.2)
- Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu (al.3)
- Kubisha hodi
- Kukolewa
- Makurutu
- UFUPISHO
- Kwa maneno yasiyozidi 70, fupishsa aya za kwanza nne. (al.9) Mtiririko alama 1
- Kwa nini serikali haitaweza kulipa madeni yake. (maneno 40-50) (al.6) Mtiririko alama 1

- SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
- Tambua sauti.
Kipasuo ghuna cha kaakaa laini (al.1) - Unda neno lenye muundo ufuatao wa sauti (al.1)
KKKKI - Eleza maana ya istilahi zifuatazo za sauti (al.4)
- Kiimbo
- Konsonanti mwambatano
- Tunga sentensi moja ukitumia neno –zuri kama kiwakilishi, kivumishi na kielezi (al.3)
- Eleza tofauti kati ya sentensi hizi (al.2)
Ningesoma kwa bidii ningepita mtihani.
Ningalisoma kwa bidii ningalipita mtihani - Tunga sentensi moja sahihi itakayotumia vitenzi vifuatavyo (al.3)
-wahi, -enda, -ona - Huku ukitumia mifano mwafaka, tofautisha silabi wazi na silabi funge (al.2)
- Andika sentensi ifuatayo katika hali ya yakinishi (al.2)
Wanafunzi wasiposoma kwa bidii hawatapita mtihani - Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo (al.2)
Gaidi aliyelipua guruneti ile ametiwa mbaroni - Andika katika msemo wa taarifa: (al.2)
“Wakazi wa eneo hili ni wafugaji stadi wa sungura” kakangu aliniambia. - Bainisha aina za virai katika sentensi ifuatayo (al.3)
Sheria hizo mpya zilitundikwa juu ya ukuta usiku wa manane. - Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo (al.2)
- Sali
- La
- Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi (al.4)
Jengo lijengwalo kwenye msingi thabiti hudumu sana. - Andika katika kauli ya kutendesha (al.2)
Amani alikunywa pombe mpaka akalewa sana - Andika kwa udogo (al.2)
Njia iendayo mbinguni ni nyembamba - Neno changa lina maana ya kutoa kitu au fedha ili kukusanya kwa makusudi Fulani. Eleza maana zingine mbili (al.2)
- Taja nahau zingine mbili sawa na “Enda ahera” (al.2)
- Andika kwa wingi (al.1)
Zigo la kuliwa halilemei
- Tambua sauti.
- ISIMU JAMII (alama 10)
Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali.
“Naona “Horsepower” mwenyewe ndiye atakayepiga, atakayecheza foul hiyo. Wachezaji wa……”
- Tambua sajili inayorejelewa (al.2)
- Tambua sifa zinazobainisha sajili yenyewe (al.8)
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
- UFAHAMU
- Ni dalili ipi inayoonyesha mwanzo wa mageuzi? (al.1)
- Kuzinduliwa kwa mtaala mpya wa kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi 1x1=1
- Mtaala mpya unalenga nini? (al.4)
- Kuimarisha utendakazi katika kikosi ambacho kwa muda mrefu kimelaumiwa kwa kulowa ufisadi na uvunjaji wa haki za kimsingi
- Unaashiria mwanzo wa mageuzi makubwa yanayonuiwa kukipatia kikosi hicho sura mpya
- Kuwapa maafisa wa polisi mafunzo mapya
- Kuunda kikosi imara chenye nidhamu na kinachoheshimu haki za kibinadamu 4x1 = 4
- Eleza lawama zinazoelekezewa kikosi cha polisi (al.2)
- Ukosefu wa nidhamu
- Kutoheshimu haki za binadamu/kimsingi
- Kukolea kwa ufisadi
- Kwa mujibu wa taarifa eleza mageuzi matatu yaliyofanywa katika kikosi cha polisi (al.3)
- Maafisa wa polisi kupokea mafunzo kwa kipindi cha kati ya miezi 15 na 21 kinyume na awali ilipochukua miezi 9
- Alama za kujiunga na kikosi hicho zimeongezewa kutoka D hadi C
- Asilimia 10 ya makurutu wawe na digrii kutoka chuo kikuu ili kuhitimu naibu wa inspekta wa polisi
- Usawa wa jinsia kuzingatiwa katika uajiri wa maafisa wa polisi 3x1 = 3
- Taja makundi mawili yaliyohusika katika kuandaa mtalaa mpya (al.2)
- Jopo iliyoteuliwa na Rais mwaka wa 2003
- Taasisi ya elimu
- Wakufunzi kutokea chuo cha mafunzo cha Kiganjo
- Wataalam wa maswala ya usalama kutoka Uswizi 2x1 =2
- Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu (al.3)
- Kubisha hodi
- Kuingia/kutukia
- Kukolewa
- Kuendeleza/kushamirisha
- Makurutu
- Wanafunzi wanaojiunga na kikosi cha polisi
- Kubisha hodi
- Ni dalili ipi inayoonyesha mwanzo wa mageuzi? (al.1)
