Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 Term 1 Opener Exams 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARATASI YA PILI
KIDATO CHA NNE
MUHULA WA KWANZA
SAA 2½

MAAGIZO

  1. Jibu maswali MANNE Pekee.
  2. Swali la kwanza ni la lazima.
  3. Maswali mengine yachaguliwe kutoka sehemu zilizobaki.
  4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  5. Kila swali lina alama ishirini

SEHEMU A: USHAIRI (LAZIMA)

  1. Soma shairi hili na ujibu maswali

    Eti
    Mimi niondoke hapa
    Niondoke hapa kwangu
    Nimesaki, licha ya risasi
    Vitisho na mauaji, siondok

    Mimi
    Siondoki
    Siondoki siondoki
    Niondoke hapa kwangu!
    Kwa mateke hata na mikuki
    Marungu na bunduki, siondoki

    Hapa
    Siondoki
    Mimi ni Pahame!
    Niondoke hapa kwangu!
    Fujo na ghasia zikizuka
    Na kani ya waporaji, siondoki

    Haki
    Siondoki
    Kwangu siondoki
    Niondoke hapa kwangu!
    Nawaje; waje wanaokuja
    Mabepari wadhalimu, siondoki

    Kamwe
    Siondoki
    Ng’oo hapa kwangu!
    Katizame chini mti ule!
    Walizikwa babu zangu, siondoki

    Sendi
    Nende wapi?
    Si hapa kitovu changu
    Niondoke hapa kwangu
    Wangawa na vijikaratasi
    Si kwamba hapa si kwangu, siondoki

    Katu
    Siondoki
    Sihitaji karatasi
    Niondoke hapa kwangu
    Yangu mimi ni ardhi hii
    Wala si makaratasi, siondoki

    Maswali

    1. Shairi hili ni la aina gani? Kwa nini (alama 2)
    2. Taja masaibu anayopitia mzungumzaji (alama 4)
    3. Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
    4. Eleza muundo wa shairi hili (alama 3)
    5. Tambua matumizi ya mbinu ya usambamba (alama 2)
    6. Andika ubeti wa tano kwa lugha nathari (alama 4)
    7. Tambua idhini moja ya mtunzi (alama 1)
    8. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi (alama 3)
      1. Karatasi
      2. Nimesaki
      3. kitovu

SEHEMU B: TAMTHILIA YA KIGOGO

  1. Uliona nini kwa huyo zebe wako ? Eti mapenzi!

    1. Eleza muktadha wa dondoo. (al. 4)
    2. Andika mbinu za lugha zinazojitokeza kwenye dondoo hili (al. 4
    3. Taja hulka za mnenaji unajitokeza katika dondoo. (al. 2)
    4. Mwanamke ni kiumbe wa kukandamizwa. Thibitisha kauli hii ukirekjelea tamthilia. (al. 10)

  2. wa kurejelea tamthlia ya 'Kigogo ya Pauline Kea, onyesha jinsi ambavyo viongozi wengi katika nchi za kiafrika wamejawa na tamaa. (alama 20)

SEHEMU C: RIWAYA YA CHOZI LA HERI(ASSUMPTA MATEI)

  1. “ Kwa kweli ni hali ngumu hii”
    1. Weka dondoo katika muktadha wake. (alama4)
    2. Ni hali gani yamsemewa inayorejelewa kwenye dondoo. (alama16)

  2. Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za Kiafrika. Tetea kauli hii ukilejelea Chozi la Heri ( al. 20)

SEHEMU D:TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE(ALIFA CHOKOCHO NA DUMU KAYANDA)
jibu swali la 6 au la 7

  1. Ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza jinsi maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanavyojitokeza. (alama20)
    1. Mapenzi ya kifaurongo
    2. Masharti ya kisasa
    3. Ndoto ya Mashaka
    4. Mtihani wa maisha

      Au

  2. Shibe inatumaliza : Salma Omar Hamad
    “Hiyo ni dharau ndugu yangu. Kwa nini kila siku tunakula sisi kwa niaba ya wengine ?”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Eleza sifa za msemaji. (alama 6)
    3. Eleza jinsi viongozi wanavyokuwa wabadhirifu. (alama 10)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

  1.    
    1. Fafanua mchakato/fomula ya uwasilishaji wa vitendawili. (alama4)
    2. Linganisha naulinganue vitendawili na methali. (alama10)
    3. Toa sababu sita za kudidimia kwa fasihi simulizi. (alama6)

MAAKIZI

SEHEMU A: USHAIRI (LAZIMA)

  1. Soma shairi hili na ujibu maswali

    Eti
    Mimi niondoke hapa
    Niondoke hapa kwangu
    Nimesaki, licha ya risasi
    Vitisho na mauaji, siondok

    Mimi
    Siondoki
    Siondoki siondoki
    Niondoke hapa kwangu!
    Kwa mateke hata na mikuki
    Marungu na bunduki, siondoki

    Hapa
    Siondoki
    Mimi ni Pahame!
    Niondoke hapa kwangu!
    Fujo na ghasia zikizuka
    Na kani ya waporaji, siondoki

    Haki
    Siondoki
    Kwangu siondoki
    Niondoke hapa kwangu!
    Nawaje; waje wanaokuja
    Mabepari wadhalimu, siondoki

    Kamwe
    Siondoki
    Ng’oo hapa kwangu!
    Katizame chini mti ule!
    Walizikwa babu zangu, siondoki

    Sendi
    Nende wapi?
    Si hapa kitovu changu
    Niondoke hapa kwangu
    Wangawa na vijikaratasi
    Si kwamba hapa si kwangu, siondoki

    Katu
    Siondoki
    Sihitaji karatasi
    Niondoke hapa kwangu
    Yangu mimi ni ardhi hii
    Wala si makaratasi, siondoki

    Maswali

    1. Shairi hili ni la aina gani? Kwa nini (alama 2)
      • Ni shairi huru kwa sababu mshairi ametumia (i) mishata mf. katu, eti, niondoke
      • Shairi lina umbo la paa la nyumba
      • Matumizi ya alama za uakifishaji kwa wingi

    2. Taja masaibu anayopitia mzungumzaji (alama 4)
      • Anatishwa kwa risasi
      • Kupigwa mateke na mikuki
      • Kuponda mali yake
      • Kuletewa hatimiliki bandia (mwalimu akubali hoja nyingine yoyote) Al. 4

    3. Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
      • Huzuni
      • Ujasiri (2 x 1)

    4. Eleza muundo wa shairi hili (alama 3)
      • Shairi lina beti saba
      • Kila ubeti una mishororo sita
      • Lina umbo la paa la nyumba 

    5. Tambua matumizi ya mbinu ya usambamba (alama 2)
      • Usambamba – Ni urudiaji wa kiwango cha sentensi, kirai (n.k)
      • mf. (i) Niondoke, mimi niondoke hapa, niondoke hapa kwangu
      • Siondoki, siondoki, siondoki niondoke hapa kwangu 

    6. Andika ubeti wa tano kwa lugha nathari (alama 4)
      • Mshairi anasema kamwe hatoki kwake.  Anaashiria chini ya mti  waliozikwa babu zake na kusisitiza kwamba hawezi akaondoka 

    7. Tambua idhini moja ya mtunzi (alama 1)
      1. Inkisari
        • Sendi – Siendi
        • Nende wapi – Niende wapi

      2. Kuboroga sarufi mf yangu mimi ni ardhi hii – Ardhi hii ni yangu mimi

    8. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi (alama 3)
      1. Karatasi - Hati miliki
      2. Nimesaki - Nimebaki
      3. kitovu - Asili

SEHEMU B: TAMTHILIA YA KIGOGO

  1. Uliona nini kwa huyo zebe wako ? Eti mapenzi!
    1. Eleza muktadha wa dondoo. (al. 4)
      • Maneno ya Majoka
      • Anamwambia Ashua
      • Ofisini mwa Majoka
      • Ni baada ya Ashua kumkataa Majoka Kimapenzi alipokwenda kutaka msaada kwake

    2. Andika mbinu za lugha zinazojitokeza kwenye dondoo hili (al. 4)
      • Mbinu – Swali la balagha – uliona nini kwa huyo zebe wako? (al 2 )
      • Nidaa – Eti mapenzi! (al 2 )
      • Kutaja alama 1
      • Mfano alama 1

    3. Taja hulka za mnenaji unajitokeza katika dondoo. (al. 2)
      • Hulka za Majoka
      • Dharau/ bezo – Eti mapenzi!
      • Mpyaro – zebe ( mjinga / mpumbavu) 1 x 2 = 2
        1x 2 = 2 Mwalimu akadirie

    4. Mwanamke ni kiumbe wa kukandamizwa. Thibitisha kauli hii ukirekjelea tamthilia. (al. 10)
      • kupigwa: Ashua akiwa gerezani anapigwa na askari
      • kubezwa / kukejeliwa: Tunu anakejeliwa na Ngurumo na walevi wengine
      • Chombo cha mapenzi. Majoka anamtaka Ashuakimapenzi anapokwenda kumwomba msaada.
      • Kijakazi nyumbani. Majoka anamtuma chopi kumuagiza mkewe kumpikia kuku na nyama na kumuokea chapatti
      • Kutusiwa. Boza anamwambia Sudi kuwa asifikiri kuwa yeye anauza nyong’a kama Tunu wake.
      • Kufungwa. Ashua anafungwa na Majoka
      • Kunyimwa kura/uongozi. Nurumo anamwambia Tunu kuwa kama hampi kura Majoka ni heri ampe paka wake. Majoka lakini si mwanamke Tunu.
      • Kunyimwa ajira. Licha ya Ashua kufuzu taaluma ya ualimu, hakuajiriwa na serikali. Anaishia kuchuuza maembe sokoni la chapakazi.
      • Kuozwa bila hiari. Majoka nataka kumwoza Tunu kwa mwanawe Ngao Junior bila hiari yake.
      • Kunyimwa fidia. Majoka alitaka kumnyima Hashima fidia baada ya kifo cha mumewe

  2. wa kurejelea tamthlia ya 'Kigogo ya Pauline Kea, onyesha jinsi ambavyo viongozi wengi katika nchi za kiafrika wamejawa na tamaa. (alama 20)
    • Tamaa ya kupata sanamu/ Majoka anataka Sudi amtengenezee sana
    • Tamaa ya kupata kodi. Majoka anawatoza kodi wafanyibiashara wa soko la Chapakazi kwa manufaa yao.
    • Tamaa ya shule zao kufunzwa na walimu waliofuzu vyuoni. Majoka anamrai Ashua afunze katika shule zake.
    • Tamaa ya kuungwa. Majoka anapata uungwaji mkono kupitia watu kama Ngurumo, Asiya na Boza -
    • Anawapa hongo ili wamuunge mkono.
    • Tamaa ya kupewa sifa lufufu. Kwa mfano Majoka lazima atangazwe katika vyombo vya habari.
    • Tamaa ya kutafutia wanao wachumba. Majoka anamtaka Tunu aolewe na mwanawe Ngao Jur.
    • Tamaa ya mapenzi - Majoka ana tamaa ya kupendwa na Ashua.
    • Tamaa ya kujenga nyumba za kifahari. Majoka anatamani kujenga hoteli ya kifahari katika soko la Chapakazi.
    • Tamaa ya usalama - Majoka ana walinzi wengi.
    • Starehe na anasa. Majoka ana tamaa ya burudani. Anaenda kuogelea katika hoteli ya‘ Majoka and Majoka resort’
    • Tamaa ya viongozi kurithisha jamaa zao uongozi.

SEHEMU C: RIWAYA YA CHOZI LA HERI(ASSUMPTA MATEI)

  1. “ Kwa kweli ni hali ngumu hii”
    1. Weka dondoo katika muktadha wake. (alama4)
      • Mzungumzaji ni Ridhaa
      • Anayezungumziwa ni Kaizari
      • Ni katika kambi/mabanda- Kwenye Msitu wa Mamba
      • Ni baada ya Kaizari kumsimulia Ridhaa magumu aliyoyapitia kutoka kwake nyumbani hadi kujipata kweye hali nyingine ngumu katika kambi.

    2. Ni hali gani yamsemewa inayorejelewa kwenye dondoo. (alama16)
      • Mke wa Kaizari, Subira ananyakwa kofi kubwa
      • Anarejelewa kama kidume kijoga-kudharauliwa
      • Mke wake anakatwa kwa sime na kuzirai kwa uchungu
      • Bintize –Lime na Mwanaheri- wanafanyiwa unyama na mabarobaro
      • Jirani yake Tulia anamfukuza anapojaribu kuwapa mke wake na watoto huduma za kwanza
      • Wanawe wanazirai ubavuni mwake
      • Anaabiri gari bila kujua waendako na jamaa zake
      • Walitazama mabasi yakichomwa kwenye safari iliyokuwa ndefu
      • Gari linaisha petroli- wanajitoma msituni
      • Wanakula mate usiku wa kwanza kutokana na ugeni/ukosefu wa chakula
      • Kuna hali mbaya ya baridi na umande wa asubuhi
      • Wanakosa maji safi ya kunywa kwenye msitu
      • Kunywa maji ya Mto wa Mamba kunawasababishia homa ya tumbo.
      • Vijumba vichache havikutosha kuhimili idadi ya wakimbizi
      • Huduma za kijamii zinaadimika –ukosefu wa misala na misala ya kupeperushwa
      • Sandarusi za kutumiwa kama misala zilitafutwa mbali kwenye milima ya taka.
      • Roho za watoto zilibwakurwa na magarimoshi kwenye reli walipoenda haja kule
      • Kuna hali ya njaa na vilio vya watoto wenye njaa

  2. Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za Kiafrika. Tetea kauli hii ukilejelea Chozi la Heri ( al. 20)
    • Subira alitengwa na familia ya mume wake kwa kuwa wa kabila tofauti na lao
    • Mwanaheri anatueleza kuwa mama yake alikuwa ametoka kwenye jamii ya mamwezi lakini babake alikuwa wa jamii tofauti. Kila mara subira aliitwa ‘muki’ au huyo wa kuja
    • Kijana mmoja alimwita Ridhaa mfuata mvua jambo lilimuumiza sana Ridhaa.
    • Mzee kendi alimtendea udhalimu Ridhaa na kuiteketeza aila yake licha ya wao kuwa majirani kwa miaka hamsini. Ridhaa alifanyiwa hivi kwa kuwa alikuwa ametoka kwenye kabila tofauti na mzee kendi.
    • Ndoa ya Selume ilisambaratika baada ya vita vya kutawazwa kwa kiongozi mpya.kuoa msichana wa kikwao.
    • Tulia alimsaidia kaizari kufunganya na kumsidikiza hadi njia panda. Alimkumbatia na kumwambia kuwa mwenyezi Mungu ndiye hupanga na nguvu na mamlaka pia hutoka kwake
    • Uongozi mpya umezua uhasama kati ya koo ambazo zimeishi kwa amani kwa karibu karne moja.
    • Subira aliweza kuvumilia kubaguliwa, kufitiniwa na kulaumiwa kwa asiyoyatenda, Mwishowe alihiari kujiondokea na kwenda mjini alikojinywea kinywaji kikali. (zozote 10 x 2)

SEHEMU D:TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE(ALIFA CHOKOCHO NA DUMU KAYANDA)
jibu swali la 6 au la 7

  1. Ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza jinsi maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanavyojitokeza. (alama20)
    1. Mapenzi ya kifaurongo
      • Ndoa iliyotarajiwa ya Dennis na Penina ilitawaliwa na unafiki. Penina anamjia Dennis na wazo la kuwa wapenzi bila kuzingatia hali duni ya familia yake. Dennis anapokosa ajira anamfukuza
      • Inatawaliwa na kuhimiliana
      • Imetawaliwa na kukata tamaa - Penina anakata tamaa baada ya Dennis kukosa kazi
      • Imezingirwa na utabaka wa kiasili
      • Mapenzi hukua, huugua na hufa 5 x 1 = 5

    2. Masharti ya kisasa
      • Ndoa ya Dadi na Kidawa
      • Ndoa inayodhibitiwa na masharti
      • Ndoa ya kupanga uzazi
      • Ndoa inayoruhusu mwanamke kufanya kazi. Kidawa anafanya kazi ya umetroni usiku na kuuza bidhaa mtaani
      • Baadhi ya watu huingilia ndoa za wenzao kama njia ya kuona mapenzi yamevunjika baina ya wanandoa husika

    3. Ndoto ya Mashaka
      • Kuna ndoa ya Mashaka na Waridi
      • Kuna ndoa ya mtumwa na mumewe mzee Rubeya
      • Tatizo la kwanza ni ndoa ya kulazimishwa. Mashaka na Waridi walitoka kwenye matabaka mawili tofauti
      • Waridi - tabaka la kitajiri
      • Mashaka - tabaka la maskini
      • Kuna kutohusisha wanawake katika ndoa. Mamake Waridi hakuhusishwa katika harusi
      • Ndoa inakumbwa na tatizo la malazi bora - upendo, kujikubali, ukosefu wa taasubi ya kiume
      • Kuna changamoto zinazojitokeza baada ya kifo cha mmoja. Mashaka anawachwa yatima
      • Kuna utengano katika ndoa. Waridi anatengana na mumewe kutokana na hali ngumu ya kiuchumi

    4. Mtihani wa maisha
      • wazazi wa Samueli ni wenye mapenzi wanaonyesha mapenzi kwa mtoto huyu wao kwa kumpeleka shuleni akajipatie elimu
      • Samuel anaonyesha mapenzi kwa Nina. Kwa muda amekuwa mpenziwe
      • Nina anaamini kuwa mwanaume huyu ni bingwa kutokana na kudanganywa alikodanganywa na mwanaume huyu
      • mamake Samueli ana mapenzi ya dhati kwake, baada ya Samuel kujaribu kujitoa uhai mamake anamsihi waende nyumbani “Twende zetu nyumbani mwanangu.” zozote 4 x 1 = 4

        Au

  2. Shibe inatumaliza : Salma Omar Hamad
    “Hiyo ni dharau ndugu yangu. Kwa nini kila siku tunakula sisi kwa niaba ya wengine ?”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
      • Maneno haya yanasemwa na Mbura
      • alikuwa anazungumza na Sasa
      • walikuwa kwenye sherehe iliyoandaliwa na mzee Mambo
      • walikuwa wanazungumza kuhusu ‘kula kwao’ 4 x 1 = 4

    2. Eleza sifa za msemaji. (alama 6)
      • ni mzalendo - anafanya kazi kwa bidii katika wizara yake kama njia ya kuonyesha uzalendo
      • mwenye tamaa - anajaza sahani kwa chakula na kukila chote
      • mwenye utu - anataka wananchi wale kwa niaba ya viongozi kama vile wao wamekuwa wakila kwa niaba yao
      • ni fisadi - amepokea kazi kwa afisi ya serikali kwa njia isiyo halali
      • mzembe - baada ya kula sahani tatu za vyakula kwenye sherehe analala usingizi mzito badala ya kwenda kazini
      • mtetezi wa haki - mvumilivu-

    3. Eleza jinsi viongozi wanavyokuwa wabadhirifu. (alama 10)
      • hulipwa mishahara mikubwa sana na serikali jambo linalochangia ubadhirifu wa mali ya umma
      • sherehe kubwa za viongozi wa kiserikali huchangia pakubwa ubadhirifu
      • viongozi hutumia raslimali za nchi kwa manufaa yao ya kibinafsi - magari ya serikali
      • raslimali zilizotumiwa katika kuvinunua vyakula na vinywaji vingetumika katika kuendeleza asasi tofauti za kijamii
      • DJ na wenzake wanapata mabilioni ya fedha kutokana na kuwatumbuiza wageni katikasherehe kama hizi
      • viongozi wanawachukua baadhi ya watu wao wa karibu na kufanya juu chini kuona kwamba wanajifaidi na mali na raslimali za wananchi pasipo kuzitolea jasho kamwe
      • upeperushaji wa matangazo katika vyombo vya habari ya sherehe za kiongozi binafsi ni njia ya kuendeleza ubadhirifu wa raslimali za umma
      • Mbura na Sasa wanaendeleza ubadhirifu pale wanapoamua kuchukua vyakula kupita kiasi katika sherehe za mzee Mambo
      • kuwaajiri viongozi wawili wenye nyadhifa sawa katika sekta tofauti za umma
      • vibaraka na vikaragosi kupewa mali ambayo ingewafaidi wananchi zozote 10 x 1 = 10

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

  1.    
    1. Fafanua mchakato/fomula ya uwasilishaji wa vitendawili. (alama4)
      • Kitangulizi- Mtegaji: kitendawili
      • Mteguaji: tega
      • Swali lenyewe- kitendawili kutegwa
      • Majibu kutolewa
      • Mtegaji asipooridhika huomba kupewa zawadi kisha hutoa jibu.

    2. Linganisha naulinganue vitendawili na methali. (alama10)
       

      MFANANO

       
      • Zote ni tungo fupi za semi
      • Zote huwa na maana fiche
      • Zote hutumia lugha inayojenga taswira
      • Zote huwa na miundo maalum ya lugha
      • Zote hupata maana kulingana na jamii
       

      TOFAUTI

       
      • Vitendawili vina fomyula ilhali methali hazina fomyula
      • Fumbo la kitendawili hufumbuliwa papo hapo fumbo si lazima kufumbuliwa papo katika methali.
      • Vitendawili hutumiwa na watoto sana, methali hutumiwa kuonyesha hekima miongoni mwa watu wazima na wazee
      • Vitendawili hutolewa katika vikao maalum, methali si lazima kutengewa vikao maalum.
      • Vitendawili hutumia lugha ya majibizano , methali aghalabu huwa kauli moja ya msemaji.
    3. Toa sababu sita za kudidimia kwa fasihi simulizi. (alama6)
      • watu kuwa na mtazamo hasi kuhusu fasihi simulizi
      • ubidhaaishaji wa fasihi simulizi- kuandika kitabu kama vile cha methali na kubadilisha umiliki
      • watu kupendelea kusoma
      • mwingiliano wa watu huwafanya kusahau fasihi yao
      • teknolojia yasasa ambayo fasihi simulizi huhifadhiwa badala yaakilini.
      • Utamaduni wa fasihi simulizi umebadilika – babu na bibi hawawatambii watoto hadithi. Mwalimu akadirie

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 Term 1 Opener Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest