Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA
MUHULA WA 1 2021
KIDATO CHA NNE
KARATASI YA 3
MUDA SAA 2

MAAGIZO

  • Jibu maswali manne pekee
  • Swali la kwanza ni la lazima
  • Maswali mengine yachaguloiwe kutoka sehemu zilzobaki
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
  • Kila swali lina alama ishirini
  1. SEHEMU A: RIWAYA: CHOZI LA HERI Na Assumpta Matei (ALAMA 20)
    “…Nimeonja shubiri ya kuwa mtegemezi kihali na mali.lakini katika yote hayo, nimejifunza mengi…”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
    2. Bainisha tamathali ya usemi inayojitokeza katika kauli hii. (alama 2)
    3. Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwa kumrejelea mzungumzaji. (ala 14)
  2. SEHEMU B:USHAIRI (ALAMA 20)
    Soma mashairi haya kisha ujibu maswali yanayofuata
    SHAIRI A                                                                                 SHAIRI B
    Wewe,
    Utazame mlolongo wa                                         Dunia kitendawili, hakuna ateguaye;
    Waja unaoshika njia likiwapo;                              Dunia kama tapeli, hadaa nyingi ujuye;
    Unaofuata pembe za barabara zisokuwapo,           Dunia mwenye akili, inampiku na yeye;
    Kwenda kuisaka auni,                                          Dunia ina mizungu, tena yapika majungu.

    Kuitafuta kazi inayowala chenga.                          Dunia na yake hali, hupumbaza hatimaye;
    Itazame migongo ya wachapa kazi,                      Dunia ina akili, binadamu sichezeye;
    Watokwao na jasho kapakapa na,                         Dunia uwe na mali, huiwezi dhorubaye;
    Wanaotafunwa uhai na jua liso                             Dunia ina mizungu,tena yapika majungu. huruma:
    Wakiinua vyuma na magunia,
    Wakiinua makontena,                                           Dunia wenye muali, ambao waichezeye;
    Wakichubuka mashambani,                                  Dunia kipigo kali, huwakumba hatimaye;
    Wakiumia viwandani,                                           Dunia wakaja kuli, “menipata nini miye?”
    Wakiteseka makazini,                                           Dunia ina mizungu, tena yapika majungu.
    Halafu
    Uangalie ule ujira wa kijungu meko,
    Mshahara usokifu haja,
    Nguo zisizositiri miili dhaifu,
    Kilo chao kisichokuwa na machozi,
    Na
    Ujiangalie Mwili wako unaomereta ujana wa ufanisi,
    Gari lako la kifahari lililozibwa vioo,
    Jumba lako la kujishasha kama uwanja mdogo,
    Malaki ya pesa unayomiliki,
    Ujiitapo mwajiri kwa raha, hunusi usaha wa hali yao?

    Maswali

    1. Je, mashairi haya mawili ni ya aina gani? Toa sababu. (alama 2)
    2. Taja dhamira kuu katika kila shairi. (alama 2)
    3. Kwa kutoa hoja zozote tatu linganua mashairi haya kiumbo. (alama 3)
    4. Taja na uelezee nafsi-nenewa katika mashairi haya mawili. (alama 2)
    5. Kwa kutolea mfano mmoja mmoja eleza matumizi ya mbinu hizi za kimtindo katika shairi la A. (alama 2)
      1. Kweli-kinzani
      2. Mishata
    6. Tambua idhini ya kishairi iliyotumika katika neno “Waichezeye” na uelezee dhima yake katika utoshelezi wa kiarudhi. (alama 1)
    7. Dondoa mfano mmoja mmoja wa mbinu ya tashhisi kutoka kwenye mashairi yote mawili. (alama 2)
    8. Andika ubeti wa tatu katika shairi la A kwa lugha nathari. (alama 4)
    9. Eleza maana ya msamiati huu kama ulivyotumika katika vifungu hivi. (alama 2)
      1. Inampiku.
      2. Makontena.
  3. SEHEMU C: FASIHI SIMULIZI (ALAMA 20)
    1. Umepewa jukumu la kutafiti kuhusu michezo ya watoto katika jamii yako.
      1. Taja eneo ambalo utafanyia utafiti wako. (alama 2)
      2. Fafanua mbinu ambazo utatumia kukusanyia data huku ukionyesha sababu za uteuzi wako. (alama 18)

        AU

    2.  
      1. Ni nini maana ya ulumbi (Alama 2)
      2. Eleza sifa nne za mtendaji katika ulumbi (Alama 8)
      3. Ngomezi zina majukumu yapi manne katika jamii yako? (Alama 8)
      4. Toa mifano miwili ya ngomezi katika jamii yako (Alama 2)
  4. SEHEMU D:TAMTHILIA: KIGOGO Na Pauline Kea (ALAMA 20)
    1. “…kulinda uhai, kulinda haki, kulinda uhuru…”
      1. Weka dondoo hili katika muktadha wake (alama 4)
      2.  Taja na ufafanue maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo hili (alama 4)
      3. Msemaji wa maneno haya alifanikiwa kulinda uhai, kulinda haki na kulinda uhuru.
      4. Dhibitisha kwa kurejelea tamthilia nzima (alama 12)
        AU 
    2. Fafanua aina zozote kumi za migogoro ijitokezayo katika tamthilia ya kigogo (alama 20)
  5. SEHEMU E: HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE Na Alifa Chokocho Na Dumu Kayanda (ALAMA 20)
    1. Shibe Inatumaliza- Salma Omar Hamad
      “…lakini kula kunatumaliza vipi?”
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
      2. Eleza jinsi kula kunavyotumaliza kwa mujibu wa hadithi. (alama 6)
    2. Mame Bakari-Mohammed Khelef Ghassany
      Eleza maudhui yafuatayo kama yalivyojitokeza katika hadithi ya Mame Bakari
      1. Uwajibikaji (alama 6)
      2. Ukatili (alama 4)

        AU
      3. Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki. (alama 20)


MARKING SCHEME

  1. SEHEMU A: RIWAYA: CHOZI LA HERI Na Assumpta Matei (ALAMA 20)
    “…Nimeonja shubiri ya kuwa mtegemezi kihali na mali.lakini katika yote hayo, nimejifunza mengi…”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
      • maneno ya Ridhaa
      • akimwambie mwanawe Mwangeka
      • wamo kwenye nyumba yao iliyochomwa
      • anamwelezea dhiki ambazo amepitia tangu ghasia za baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya kuzuka.
        4x1=4
    2. Bainisha tamathali ya usemi inayojitokeza katika kauli hii. (alama 2)
      • msemo/nahau-onja shubiri 1x2=2
    3. Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwa kumrejelea mzungumzaji. (ala 14)
      • Kubomolewa kwa nyumba mtaani Tononokeni bila kufidiwa
      • Kutapeliwa na raia wenzake fisadi wanaomuuzia ardhi katika eneo lililotengewa ujenzi wa barabara
      • Kuchomekewa na nyumba-jengo lake la kibiashara linachomeka kutokana na hitilafu ya moto
      • Kufiwa na familia yake katika moto, Mzee Kedi anafariki, hata nduguye Makaa anachomeka katika mkasa wa moto.
      • Kuitwa mfuata mvua akiwa shuleni kwa sababu ya kuwa mwanafunzi mlowezi katika eneo la msitu wa Heri
      • Kutengwa mchezoni akiwa shuleni
      • Kusimangwa na wanafunzi wenzake
      • Kusingiziwa wizi wa kalamu
      • Kubakwa kwa wapwake Lime na Mwanaheri wanapovamiwa na wahuni
      • Dadake Subira anavamiwa na wahuni na kukatwa kwa sime
      • Kula mizizi-mwitu kwa kukosa chakula katika kambi ya wakimbizi
      • Kuugua shinikizo la damu baada ya kupoteza aila yake. 7x2=14
        Tanbihi: kuonja shubiri ni kukumbwa na dhiki.Mtahiniwa ajadili dhiki alizopitia Ridhaa maishani mwake.
  2. SEHEMU B:USHAIRI (ALAMA 20)
    Soma mashairi haya kisha ujibu maswali yanayofuata

    SHAIRI A                                                                                 SHAIRI B
    Wewe,
    Utazame mlolongo wa                                         Dunia kitendawili, hakuna ateguaye;
    Waja unaoshika njia likiwapo;                              Dunia kama tapeli, hadaa nyingi ujuye;
    Unaofuata pembe za barabara zisokuwapo,           Dunia mwenye akili, inampiku na yeye;
    Kwenda kuisaka auni,                                          Dunia ina mizungu, tena yapika majungu.

    Kuitafuta kazi inayowala chenga.                          Dunia na yake hali, hupumbaza hatimaye;
    Itazame migongo ya wachapa kazi,                      Dunia ina akili, binadamu sichezeye;
    Watokwao na jasho kapakapa na,                         Dunia uwe na mali, huiwezi dhorubaye;
    Wanaotafunwa uhai na jua liso                             Dunia ina mizungu,tena yapika majungu. huruma:
    Wakiinua vyuma na magunia,
    Wakiinua makontena,                                           Dunia wenye muali, ambao waichezeye;
    Wakichubuka mashambani,                                  Dunia kipigo kali, huwakumba hatimaye;
    Wakiumia viwandani,                                           Dunia wakaja kuli, “menipata nini miye?”
    Wakiteseka makazini,                                           Dunia ina mizungu, tena yapika majungu.
    Halafu
    Uangalie ule ujira wa kijungu meko,
    Mshahara usokifu haja,
    Nguo zisizositiri miili dhaifu,
    Kilo chao kisichokuwa na machozi,
    Na
    Ujiangalie Mwili wako unaomereta ujana wa ufanisi,
    Gari lako la kifahari lililozibwa vioo,
    Jumba lako la kujishasha kama uwanja mdogo,
    Malaki ya pesa unayomiliki,
    Ujiitapo mwajiri kwa raha, hunusi usaha wa hali yao?

    Maswali

    1. Je, mashairi haya mawili ni ya aina gani? Toa sababu. (alama 2)
      • A – huru – halijazingatia arudhi za utunzi wa ushairi.
      • B – tarbia – lina mishororo 4 katika kila ubeti.
      • Kikwamba – neno ‘dunia’ laanzia kila mishororo.
      • Mtiririko – vina vya kati na mwisho vina keketo.
      • Mathnawi – kila mshororo una vipande viwili.
      • Shairi la arudhi kwa sababu limezingatia arudhi za utunzi wa ushairi.
        Kutaja na kueleza.(alama 2)

    2. Taja dhamira kuu katika kila shairi. (alama 2)
      • A - Kukashifu viongozi wanaouwatesa wafanyakazi.
        Kuangazia haki duni ya ufanyakazi mikononi mwa waajiri katili.
      • B - Kuangazia jinsi binadamu afaa kutahadhari na dunia inayo dhuru / angamiza. (Hoja 1x2 = 2) 

    3. Kwa kutoa hoja zozote tatu linganua mashairi haya kiumbo. (alama 3)
      A B
      Lina beti 4  Lina beti 4
       Idadi ya mishororo kwa kila ubeti ni tofauti  Lina mishororo nne kwa kial ubeti
      vina vyatofautiana kwa kila ubeti vina vina keketo
      halina kibwagizo lina kibwagizo maalum
      mishororo haija gawika vipande vipande limegawika kuwili ukwapi na utao 
      mizani yatofautiana kwa kila mshororo mizani ni sawa 8,8
    4. Taja na uelezee nafsi-nenewa katika mashairi haya mawili. (alama 2)
      • A – Mwajiri katili anayewadhulumu wafanyakaziakijitajirisha kwa jasho lao.
      • B – binadamu asiyetahadhari na dunia. Kila hoja alama 1 x 2
    5. Kwa kutolea mfano mmoja mmoja eleza matumizi ya mbinu hizi za kimtindo katika shairi la A. (alama 2)
      1. Kweli-kinzani - kilio kisichokuwa na machozi.
        - barabara zisizokuwapo.
      2. Mishata -  watokwao na jasho kapakapa na - wanaotafunwa uhai na jua liso.
        Ya kwanza al. 1 x 2
    6. Tabdila badala ya waichezee – kupata urari wa vina ‘ye’
      • Kutaja na kueleza umuhimu – alama 1

    7. Tambua idhini ya kishairi iliyotumika katika neno “Waichezeye” na uelezee dhima yake katika utoshelezi wa kiarudhi. (alama 1)
      A B

      -Kazi inawala chenga
      -Wanatafunwa uhai na jua
      -dunia yapika majungu

      -dunia kama tapeli inahadaa
      -dunia inampiku mwenye akili


    8. Dondoa mfano mmoja mmoja wa mbinu ya tashhisi kutoka kwenye mashairi yote mawili. (alama 2)

    9. Andika ubeti wa tatu katika shairi la A kwa lugha nathari. (alama 4)
      • Pia mchunguze maskini na mapato ya kazi yake duni, yasiyotosheleza mahitaji yake, na anayevalia nguo zilizochanika na zisizosetiri mwili usio na nguvu, na hulia bila kutokwa na machozi.(hoja zozte 4x1 = alama 4)

    10. Eleza maana ya msamiati huu kama ulivyotumika katika vifungu hivi. (alama 2)
      1. Inampiku. -  inamshinda / inamweza
      2. Makontena. -  shehena / mizigo mizito / makasha. (hoja 2x1 = alama 2)

  3. SEHEMU C: FASIHI SIMULIZI (ALAMA 20)
    1. Umepewa jukumu la kutafiti kuhusu michezo ya watoto katika jamii yako.
      1. Taja eneo ambalo utafanyia utafiti wako. (alama 2)
        • Mandhari ambapo pana watoto wachanga wanaocheza. 1x2=2
      2. Fafanua mbinu ambazo utatumia kukusanyia data huku ukionyesha sababu za uteuzi wako. (alama 18)
        • Kusikiliza-mtafiti anaweza kuwasikiliza Watoto wanapocheza na kusimulia visa vyao.
          Mtafiti atapata ujumbe asilia na halisi kwa sababu Watoto hawatatia chuku michezo yao
        • Kushiriki-mtafiti anaweza kujiunga na Watoto katika michezo yao na kujirekodia anachokibaini katika ushirika huo.
          mtafiti huja karibu na Watoto na kupata habari za kuaminika moja kwa moja.
        • Kurekodi-mtafiti anaweza kutumia vinasasauti, kanda za video, filamu au upigaji picha.
          mtafiti hupata habari za kutegemewa na anaweza kuzirejelea baadaye/kumbukumbu
        • Uchunzaji/kutazama-mtafiti anashuhudia kwa macho michezo ya Watoto inapoendelezwa.
          mbinu hii ni bora kwani utendaji hautaadhiriwa kwani wachezaji/washiriki hawatajua kuwa wanatazamwa.
        • Kutumia Hojaji-mtafiti anaweza kutayarisha hojaji ambayo ataipelekea mhojiwa ambaye anapaswa kuijaza.
          mbinu hii ni bora kwani mtafiti anaweza kuwafikia watoaji wengi wa habari kwa wakati mmoja.
        • Mahojiano-mtafiti anaweza kukabiliana ana kwa ana na waahusika anaonuia kupata maarifa kutoka kwao.
          mbinu hii inamwezesha mtafiti kupata ufafanuzi wa papo kwa hapo
          Zozote 6x3=18
          Tan :Mtahini atoe mbinu, aifafanue kisha atoe sababu ilia pate alama 3 katika kila hoja.

          AU
    2.  
      1. Ni nini maana ya ulumbi (Alama 2)
        • Ulumbi ni uhodari wa kutumia lugha kwa ufundi wa kipekee.      1x2=2
      2. Eleza sifa nne za mtendaji katika ulumbi (Alama 8)
        • Hutumia lugha kwa njia inayovutia na kushawishi hadhira
        • Mlumbi huwa jasiri- huwa mkakamavu.
        • Hutumia chuku kwa ufanisi mkubwa.
        • Anapaswa kutumia vipengele anuwai vya lugha kama vile ushairi, methali, nahau, taswira.
        • Hutumia lugha kutegemea muktadha na hadhira yake.
        • Huwa na kipawa cha kuwa viongozi katika jamii. (,Zozote 4 x 2= 8)

      3. Ngomezi zina majukumu yapi manne katika jamii yako? (Alama 8)
        • Ni njia ya kupitisha ujumbe wa dharura katika jamii ― vita.
        • Ni kitambulisho cha jamii.
        • Huhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii.
        • Hukuza uzalendo – wanajamii huionea fahari mbinu hii ya kuwasiilana.
        • Hukuza ubunifu – jinsi wanajamii wanavyokabiliwa na aina tofautitofauti za ujumbe ndivyo wanavyojifunza mitindo mipya.
        • Ni njia rahisi ya kuwasilisha ujumbe. 4x2=8

      4. Toa mifano miwili ya ngomezi katika jamii yako (Alama 2)
        • Toni katika rununu.
        • Kamsa /milio kwenye magari/ving‘ora ambulensi.
        • Kengele shuleni
        • Firimbi michezoni. (Zozote 2 x 1 = 2)

  4. SEHEMU D:TAMTHILIA: KIGOGO Na Pauline Kea (ALAMA 20)
    1. “…kulinda uhai, kulinda haki, kulinda uhuru…”
      1. Weka dondoo hili katika muktadha wake (alama 4)
        • maneno ya Tunu
        • akimwambia Sudi
        • wakiwa barazani mwa nyumba ya Sudi
        • wakizungumza kuhusu jinsi ya kuzitetea haki za wanasagamoyo
          4x1=4
      2.  Taja na ufafanue maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo hili (alama 4)
        • uwajibikaji-Tunu na Sudi wanawajibika kwa kujitolea katika kulinda haki za kimsingi za Wanasagamoyo na wanachukulia jambo hili kuwa jukumu lao uzalendo-Tunu na Sudi ni wazalendo kwani wanataka kuiona Sagamoyo iliyo na ufanisi kwa wananchi wote. 2x2=4
      3. Msemaji wa maneno haya alifanikiwa kulinda uhai, kulinda haki na kulinda uhuru.
        • Anaongoza maandamano Sagamoyo na kukiri kutolegeza msimamo wake hadi soko lifunguliwe
        • Anapanga kuleta wachunguzi kutoka nje kuchunguza mauaji ya Jabali
        • Anamkashifu Majoka kwa uongozi wake uliojaa mauaji
        • Anahutubia wanahabari kuhusu hali halisi Sagamoyo kwa ujasiri
        • Anapigania usalama wa kila mtu Sagamoyo bila ubaguzi
        • Anamsamehe Mamapima anapomwomba msamaha
        • Anakataa kuolewa na mhuni Ngao Junior jambo linalomwezesha kuendeleza utetezi wa haki za wanasagamoyo.
          Zozote 6x2=12
          Mwalimu akadirie majibu ya mwanafunzi yalingane na mafanikio ya Tunu.
      4. Dhibitisha kwa kurejelea tamthilia nzima (alama 12)

        • AU 
    2. Fafanua aina zozote kumi za migogoro ijitokezayo katika tamthilia ya kigogo (alama 20)
      • Kwanza kuna migogoro kati ya wananchi na polisi. Polisi wanawapiga na kuwajeruhi wananchi wasio na hatia.
      • Pili kuna migogoro kati ya polisi na viongozi wao. Viongozi wanawatisha polisi. Naye kingi mkuu wa wanapolisi anatishiwa kufutwa kazi.
      • Kuna migogoro kati ya wananchi na viongozi wao. Majoka anawatusi wancanchi waliojataa kuenda katika sherehe zilizoandaliwa katika uwanja wa wazalendo.
      • Kuna migogoro kati ya viongozi na vituo vya habari. Majoka anafunga vituo vyote vya habari baada ya kupeperusha mbashara mgomo uliongozwa na tunu.
      • Kuna migogoro kati ya viongozi na wapinzani wao. Tunaona jinsi majoka anapinga kuvamiwa kwa tunu wakiwa na kenga. Majoka pia anapanga mauaji ya jabali babake tunu.
      • Kuna mgogoro unaozuka kati ya kiongozi na mshauri wake. Kenga anapomgeuka majoka anaitwa kunguru.
      • Migogoro ya kitabaka ambapo tabaka la juu linadhulumu watu wa tabaka la chini. Watu wa tabaka la juu wana maisha mazuri kama vile Majoka huku wa tabaka la chini wakimia kama akina Hashima. Jambo hili linaleta kutoelewana baina ya matabaka haya.
      • Migogoro ya viongozi na wanachi. Viongozi wanaendeleza utawala wa kidhalimu, ni fisadi na hawajali raia jambo linalosababisha ktoelewana baina yao. Wanachi hata wanaanza harakati a kjikomboa mikononi mwao.
      • Migogoro ya wanachi na askari. Askari na raia hawaelewani. Kila raia wanapogoma, askari wanafurusha na kuwatesa
      • migogoro ya wafadhili na viongozi. Majoka hafurahishwi na wafadhili wanaosaidia akina Tunu na anawataka warudi kwao. Wafadhili hawa nao wanapinga utawala wa Majoka. 10x2=20
        Migogoro ya viongozi na vyombo vya habari. Majoka anapendelea vituo vinavyoeneza propaganda na kupinga vinavyoelea ukweli wa mambo
        migogoro baina ya watetezi wa haki na vibaraka. Akina Tunu na Sudi hawaelewani kabisa na vibaraka wa Majoka kama vile Ngurumo na Boza.
  5. SEHEMU E: HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE Na Alifa Chokocho Na Dumu Kayanda (ALAMA 20)
    1. Shibe Inatumaliza- Salma Omar Hamad
      “…lakini kula kunatumaliza vipi?”
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
        • Haya ni maneno ya Sasa
        • Akimwambia Mbura
        • Katika sherehe baada ya kula
        • Wanazungumzia ile hali ya matumbo yao kushiba ilhali wengine wanadhikika tu. 1x4=4
      2. Eleza jinsi kula kunavyotumaliza kwa mujibu wa hadithi. (alama 6)
        • Kula vibaya na vizuri-tunavyojua na tusivyovijua, hatujui vitokako na visikotoka
        • magonjwa-sukari, presha,saratani,obesity, madonda ya tumbo
        • vifo-kuuana kwa mabomu, risasi , kunyongana, kuuana kifikra, kimawazo, kunyang’anyana vinavyoonekana na visivyoonekana-haki, utu, heshima, uhuru
        • lawama       3x2=6

    2. Mame Bakari-Mohammed Khelef Ghassany
      Eleza maudhui yafuatayo kama yalivyojitokeza katika hadithi ya Mame Bakari
      1. Uwajibikaji (alama 6) -
        • Beluwa anawajibika katika kazi yake anapomwagiza Sara kwenda hospitalini kupimwa akiwa na ujauzito wa miezi sita. Sara anawajibika anapotunga mimba, ingawa alikuwa amebakwa, hakuavya mimba ila aliamua kuilea. Wazazi wa Sara wanapojua kuwa ana ujauzito, waliwajibika kwa mtunza vyema n ahata baada ya kujifungua wanamfanyia sherehe.    3x2=6
      2. Ukatili (alama 4)
        • Lile janadume bakaji lilikuwa na tabia ya kuwanajisi wasichana wadogo kama vile Sara. Sara alihofia kuwaeleza wazazi hali yake kwa kuhofia ukatili wa baba yake ambaye angemfurusha nyumbani iwapo angegundua ujauzito wa Sara. Umati unampiga yule mbakaji kwa hasira hadi kifo                                       2x2=4

          AU

      3. Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki. (alama 20)
        • Viongozi kuweka vitego na vikwazo vya sheria ili watu wadogo wasiweze kutetea mali zao.
        • Kutowahusisha maskini katika maamuzi muhimu yanayoathiri maisha yao.
        • Kunyakua ardhi ya madongoporomoka ambapo watu maskini waliishi.
        • Kupanga njama za kuwapatia wanyonge visenti vichache ili waondoke madongoporomoka.
        • Jitu la miraba mine kula chakula chote bila kubakishia wateja.
        • Wanamadongoporomoka kubomolewa vibanda vyao na mabuldoza.
        • Askari wa baraza kutimua watu waliokuwa wanabomolewa .
        • Jeshi la polisi kulinda askari wa baraza wakibomoa vibanda vya wanamadongoporomoka. 
        • Askari kuwapiga virungu watu.                                                               5x2=10

          SHIBE INATUMALIZA.
        • Mzee mambo kulipwa kwa vyeo viwili alivyovifanyia kazi.
        • Waajiriwa kwenda kazini na kukosa kufanya kazi.
        • Viongozi kuibia wananchi kwa kujipakulia mshahara
        • Waajiriwa wawili kufanya kazi moja – Sasa na Mbura ni mawaziri wa wizara moja.
        • Mzee mambo kuandaa sherehe ya kuingiza watoto nasari kwa kutumia pesa za umma.
        • Mzee mambo kuandaa sherehe kwa kutumia rasimali za nchi- magari, vyakula.
        • Sasa na mbura kula vyakula vyao na vya wenzao.                           5x2=10
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest