Kiswahili Paper 2 Questions And Answers - Form 4 Term 2 Opener 2021

Share via Whatsapp

MAAGIZO

 • Jibu maswali yote
 • Majibu yako yaandikwe kwa kugha ya Kiswahili
 1. UFAHAMU: (alama 15)
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali

  Mageuzi yanayotarajiwa katika idara ya polisi nchini yameanza kubisha hodi baada ya kuzinduliwa kwa mtaala mpya wa kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi.

  Mtaala huo uliozinduliwa rasmi na Waziri wa Usalama wa ndani Prof. George Saitoti Jumatatu iliyopita, unalenga kuimarisha utendakazi katika kikosi ambacho kwa muda mrefu kimelaumiwa kwa kukolewa ufisadi na uvunjaji wa haki za kimsingi.

  Akihutubu katika hafla ya kuzindua mtaala huo iliyofanyika katika makao makuu ya shirika la ndege nchini mtaani Embakasi, Nairobi, Jumatatu iliyopita, Waziri Saitoti alisema, kuzinduliwa kwa mtaala huo kuliashiria mwanzo wa mageuzi makubwa yanayonuiwa kukipatia kikosi hicho sura mpya.

  “Nyakati zimebadilika na tutawapa maafisa wa polisi mafunzo mapya. Tunataka kuunda kikosi imara chenye nidhamu na kinachoheshimu haki za kibindamu. Tunataka kuwa na kikosi kinachoakisi sura ya karne hii na kinachoafikia hadhi ya kimataifa,” Waziri Saitoti alisema.

  Mtaala huo mpya wa kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi ni matunda ya jopo lililoteuliwa na Rais mwaka wa 2003 kutathmini mageuzi katika kikosi hicho. Uliandaliwa na taasisi ya elimu nchini ikishirikiana na wanafunzi kutoka chuo cha mafunzo ya polisi cha Kiganjo kwa usaidizi wa wataalamu wa masuala ya usalama kutoka Uswizi.

  Chini ya mtaala huo, maafisa wa polisi watapokea mafunzo kwa kipindi cha kati ya miezi 15 na 21 kinyume cha awali ilipowachukua miezi 9 tu kukamilisha mafunzo.

  Aidha, alama za kujiunga na kikosi hicho zimeongezwa. Katika mtaala huo, wanaonuia kujiunga na idara ya polisi wa kawaida, kitengo cha G.S.U au polisi wa utawala ni lazima wawe wamepata alama ya C katika mtihani wa K.C.S.E na itawachukua miezi 15 kukamilisha mafunzo ikiwa ni pamoja na miezi 3 ya kujifahamisha na huduma ya kikosi.

  Hii ni tofauti na awali ambapo alama ya kujiunga na kikosi cha polisi ilikuwa ni D katika mtihani wa KCSE. Mtaala mpya unasema ni sharti asilimia 10 ya makurutu wawe na digrii kutoka chuo kikuu na watapokea mafunzo kwa miezi na kuhitimu cheo cha Naibu wa Inspekta wa Polisi.

  Kuanzia sasa, ni sharti usawa wa kijinsia uzingatiwe kikamilifu katika uajiri wa maafisa wa polisi. Wachanganuzi wa masuala ya usalama wanasema ukizingatiwa ipasavyo, mtaala huo utasaidia kuunda msingi dhabiti wa kikosi imara ambacho Wakenya wamekuwa wakihitaji.

  Maswali
  1. Ni dalili ipi inayoonyesha mwanzo wa mageuzi? (al.1)
  2. Mtaala mpya unalenga nini? (al.4)
  3. Eleza lawama zinazoelekezewa kikosi cha polisi (al.2)
  4. Kwa mujibu wa taarifa eleza mageuzi matatu yaliyofanywa katika kikosi cha polisi (al.3)
  5. Taja makundi mawili yaliyohusika katika kuandaa mtalaa mpya (al.2)
  6. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu (al.3)
   1. Kubisha hodi
   2. Kukolewa
   3. Makurutu
 2. UFUPISHO (alama 15)
  Soma makala haya kisha ujibu maswali yanayofuata

  Mwezi jana serikali ya kitaifa na zile za kaunti ziliwasilisha makadirio yao ya bajeti, miezi miwili kabla ya mwaka wa kifedha kuisha kama zinavyohitajika na katiba. Serikali hizo zilieleza jinsi zinavyonuia kutumia mabilioni ya pesa kufadhili shughuli za mwaka ujao wa kifedha wa 2013/2014.

  Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta ilisema itatumia shilingi 1.6 trilioni kufadhili maendeleo na shughuli za sekta na idara zake tofauti. Makadirio haya yaliwasilishwa na kiongozi wa walio wengi bungeni, Bw. Aden Duale. Hata hivyo yalikosa kueleza jambo moja muhimu – jinsi kitita hicho kitakavyopatikana. Nasema hivi kwa sababu kuna habari ambazo zimenipa tumbojoto na wasiwasi mkubwa. Imebainika kuwa kufikia mwishoni mwa Machi mwaka huu, Kenya ilikuwa inadaiwa shilingi 1.8 trilioni na wafadhili wa humu nchini wa kigeni. Kama habari hizi hazijakushtua sitakulaumu kwa sababu huenda ukuwa hujui ukubwa wa kiasi cha fedha. Ili uweze kuelewa, nitazigawanya fedha hizi miongoni mwa Wakenya milioni 40 ili tujue kila mkenya anadaiwa kiasi gani. Kila Mkenya nchini, wakiwemo watoto na wazee wakongwe, anadaiwa shilingi 45,000! Hivyo basi ili deni hili liweze kulipwa, kila Mkenya atalazimika kutoa kiasi hicho cha fedha.

  Ni deni ambalo Rais Uhuru Kenyatta alirithi kitoka kwa mtangulizi wake, Rais Mwai Kibaki ambaye utawala wake ulivunja rekodi ya kukopa. Wahenga hawakukosea dawa ya deni ni kulipa. Deni hili linapaswa kimkosesha usingizi Rais Kenyatta ambaye anapaswa kutafuta njia za kulilipa bila kuathiri uchumi, maendeleo na utekelezaji wa ahadi nyingi alizowapatia Wakenya wakati wa kampeni.

  Hili halitafanyika kama Serikali itatenga fedha nyingi kuwalipa maafisa wake mishahara na marupurupu minono pamoja na kuwapa mabilioni ya pesa kununulia magari ya kifahari. Pengine Rais hajafahamiswa kuwa mwaka ujao wa kifedha serikali itajipata pabaya kwani Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru nchini (KRA), haitaweza kukusanya kiwango kilichowekwa na serikali baada ya shughuli ya ukusanyaji ushuru kutatizwa na hofu iliyotanda wakati wa uchaguzi mkuu.

  KRA ilikuwa imekusanya shilingi 560 bilioni kufikia mwishoni mwa Machi ilhali ilikuwa imeagizwa kukusanya. Baada yake zimeomba serikali kuu ujaze pengo hilo au zipewe idhini ya kukopa.

  Rais Kenyatta hana budi kuchukua hatua za dharura kuhakikisha kuwa wakenya hawataendelea kuandamwa na madeni maishani mwao.

  (imenukuliwa kutoka Taifa Leo – Mei 9, 2013)

  1. Kwa maneno yasiyozidi 70, fupishsa aya za kwanza nne. (al.9)
   Nakala ya matayarisho
   Nakala safi
  2. Kwa nini serikali haitaweza kulipa madeni yake. (maneno 40-50) (al.6)
   Nakala ya matayarisho
   Nakala safi
 3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
  1. Tambua sauti.
   Kipasuo ghuna cha kaakaa laini (al.1)
  2. Unda neno lenye muundo ufuatao wa sauti (al.1)
   KKKKI
  3. Eleza maana ya istilahi zifuatazo za sauti (al.4)
   1. Kiimbo
   2. Konsonanti mwambatano
  4. Tunga sentensi moja ukitumia neno –zuri kama kiwakilishi, kivumishi na kielezi (al.3)
  5. Eleza tofauti kati ya sentensi hizi (al.2)
   Ningesoma kwa bidii ningepita mtihani.
   Ningalisoma kwa bidii ningalipita mtihani
  6. Tunga sentensi moja sahihi itakayotumia vitenzi vifuatavyo (al.3)
   -wahi, -enda, -ona
  7. Huku ukitumia mifano mwafaka, tofautisha silabi wazi na silabi funge (al.2)
  8. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya yakinishi (al.2)
   Wanafunzi wasiposoma kwa bidii hawatapita mtihani
  9. Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo (al.2)
   Gaidi aliyelipua guruneti ile ametiwa mbaroni
  10. Andika katika msemo wa taarifa: (al.2)
   “Wakazi wa eneo hili ni wafugaji stadi wa sungura” Kakangu aliniambia.
  11. Bainisha aina za virai katika sentensi ifuatayo (al.3)
   Sheria hizo mpya zilitundikwa juu ya ukuta usiku wa manane.
  12. Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo (al.2)
   1. Sali
   2. La
  13. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya vielezo matawi (al.4)
   Jengo lijengwalo kwenye msingi thabiti hudumu sana.
  14. Andika katika kauli ya kutendesha (al.2)
   Amani alikunywa pombe mpaka akalewa sana
  15. Andika kwa udogo (al.2)
   Njia iendayo mbinguni ni nyembamba
  16. Neno changa lina maana ya kutoa kitu au fedha ili kukusanya kwa makusudi fulani. Eleza maana zingine mbili (al.2)
  17. Taja nahau zingine mbili sawa na “Enda ahera” (al.2)
  18. Andika kwa wingi (al.1)
   Zigo la kuliwa halilemei
 4. ISIMU JAMII (alama 10)
  Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali.
  “Naona “Horsepower” mwenyewe ndiye atakayepiga, atakayecheza foul hiyo. Wachezaji wa……”
  1. Tambua sajili inayorejelewa (al.2)
  2. Tambua sifa zinazobainisha sajili rejelewa (al.8)


MARKING SCHEME

 1. UFAHAMU
  1. Ni dalili ipi inayoonyesha mwanzo wa mageuzi? (al.1)
   • Kuzinduliwa kwa mtaala mpya wa kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi 1x1=1
  2. Mtaala mpya unalenga nini? (al.4)
   • Kuimarisha utendakazi katika kikosi ambacho kwa muda mrefu kimelaumiwa kwa kulowa ufisadi na uvunjaji wa haki za kimsingi
   • Unaashiria mwanzo wa mageuzi makubwa yanayonuiwa kukipatia kikosi hicho sura mpya
   • Kuwapa maafisa wa polisi mafunzo mapya
   • Kuunda kikosi imara chenye nidhamu na kinachoheshimu haki za kibinadamu 4x1 = 4
  3. Eleza lawama zinazoelekezewa kikosi cha polisi (al.2)
   • Ukosefu wa nidhamu
   • Kutoheshimu haki za binadamu/kimsingi
   • Kukolea kwa ufisadi
  4. Kwa mujibu wa taarifa eleza mageuzi matatu yaliyofanywa katika kikosi cha polisi (al.3)
   • Maafisa wa polisi kupokea mafunzo kwa kipindi cha kati ya miezi 15 na 21 kinyume na awali ilipochukua miezi 9
   • Alama za kujiunga na kikosi hicho zimeongezewa kutoka D hadi C
   • Asilimia 10 ya makurutu wawe na digrii kutoka chuo kikuu ili kuhitimu naibu wa inspekta wa polisi
   • Usawa wa jinsia kuzingatiwa katika uajiri wa maafisa wa polisi 3x1 = 3
  5. Taja makundi mawili yaliyohusika katika kuandaa mtalaa mpya (al.2)
   • Jopo iliyoteuliwa na Rais mwaka wa 2003
   • Taasisi ya elimu
   • Wakufunzi kutokea chuo cha mafunzo cha Kiganjo
   • Wataalam wa maswala ya usalama kutoka Uswizi 2x1 =2
  6. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu (al.3)
   1. Kubisha hodi
    • Kuingia/kutukia
   2. Kukolewa
    • Kuendeleza/kushamirisha
   3. Makurutu
    • Wanafunzi wanaojiunga na kikosi cha polisi
 2. UFUPISHO
  1. Kwa maneno yasiyozidi 70, fupishsa aya za kwanza nne. (al.9)
   • Serikali kuwasilisha bajeti
   • Kueleza jinsi mabilioni yalivyotumiwa
   • Serikali ya Kenyatta kusema itatumia shilingi 1.6 trilioni kwa maendeleo.
   • Makadirio kuwasilishwa na kiongozi wa walio wengi bungeni
   • Kukosa kueleza jinsi ya kupata kitifa hicho
   • Habari hizi kunipa wasiwasi
   • Kenya kudaiwa shilingi 1.8 trilioni na wafadhili
   • Kutolaumu wale wasiolewa ukubwa wa deni hili
   • Kugawanya deni hili kwa Wakenya wote
   • Kila Mkenya kadaiwa shilingi 45,000
   • Kenyatta kurithi deni kutoka kwa Kibaki
   • Deni kumkosesha usingizi Rais
   • Kutafuta njia ya kulipa bila kuathiri uchumi
    9x1 = 9
    Mtiririko alama 1
  2. Kwa nini serikali haitaweza kulipa madeni yake. (maneno 40-50) (al.6)
   • Serikali kutenga fedha nyingi kuwalipa wafanyikazi
   • KRA kutokusanya kiwango kinachohitajika
   • Ukusanyaji wa ushuru kutatizwa na hofu wakati wa uchaguzi
   • Serikali za kaunti kupendekeza kutumia mabilioni ambayo hawana
    4x1 = 4
    Mtiririko alama 1
 3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
  1. Tambua sauti.
   Kipasuo ghuna cha kaakaa laini (al.1)
   • /g/
  2. Unda neno lenye muundo ufuatao wa sauti (al.1)
   KKKKI
   • Mchwa
  3. Eleza maana ya istilahi zifuatazo za sauti (al.4)
   1. Kiimbo
    • Kupanda na kushuka kwa sauti mtu anapozungumza
   2. Konsonanti mwambatano
    • Mfuatano wa konsonanti mbili au zaidi katika silabi unapotamka
  4. Tunga sentensi moja ukitumia neno –zuri kama kiwakilishi, kivumishi na kielezi  (al.3)
   • Vizuri vile ni vya watu wazuri walioandikiwa vibaya
  5. Eleza tofauti kati ya sentensi hizi (al.2)
   1. Ningesoma kwa bidii ningepita mtihani.
    • Kuna uwezekano wa kitendo kutendeka/wakati uliopo
   2. Ningalisoma kwa bidii ningalipita mtihani
    • Hakuna uwezekano/wakati uliopita
  6. Tunga sentensi moja sahihi itakayotumia vitenzi vifuatavyo (al.3)
   -wahi, -enda, -ona
   • Aliwahi kwenda kumuona afisini mwake (1x3=3)
  7. Huku ukitumia mifano mwafaka, tofautisha silabi wazi na silabi funge (al.2)
   • Silabi wazi ni zile zinazoishia kwa irabu k.m. ru + ka ba + ba
   • Funge ni zile zinazoishia kwa konsonanti k.m. m + t u Da - k - ta - ri
  8. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya yakinishi (al.2)
   Wanafunzi wasiposoma kwa bidii hawatapita mtihani
   • Wanafunzi wakisoma kwa bidii watapita mtihani
  9. Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo (al.2)
   Gaidi aliyelipua guruneti ile ametiwa mbaroni
   • Gaidi aliyelipua guruneti – k – huru ametiwa baroni – Kishazi tegemezi
  10. Andika katika msemo wa taarifa: (al.2)
   “Wakazi wa eneo hili ni wafugaji stadi wa sungura” kakangu aliniambia.
   • Kakangu aliniambia kuwa wakazi wa eneo hilo ni wafugaji stadi wa sungura.
  11. Bainisha aina za virai katika sentensi ifuatayo (al.3)
   Sheria hizo mpya zilitundikwa juu ya ukuta usiku wa manane.
   • Sheria mpya – Kikundi nomino
   • Zilitundikwa juu ya – Kikundi tenzi
   • Juu ya ukuta – Kikundi kihusishi
   • Usiku wa manane – Kikundi kielezi
    1x4 = 4
  12. Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo (al.2)
   1. Sali
    • Sala, msala, msalihina,
   2. La
    • Chakula, mlo, mlaji, ulaji
  13. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi (al.4)
   f4 pp2 Kiswahili Q
  14. Andika katika kauli ya kutendesha (al.2)
   Amani alikunywa pombe mpaka akalewa sana
   • Pombe ilimlevya Amani
  15. Andika kwa udogo (al.2)
   Njia iendayo mbinguni ni nyembamba
   • Kijia kiendacho mbinguni ni chembamba 1x2 = 2
  16. Neno changa lina maana ya kutoa kitu au fedha ili kukusanya kwa makusudi Fulani.
   Eleza maana zingine mbili (al.2)
   • Umwa viungoni au mishiopani kama ugonjwa wa biridi ya bisi
   • Siyokomaa/siyopevuka
  17. Taja nahau zingine mbili sawa na “Enda ahera” (al.2)
   • Kata kamba
   • Aga dunia
   • Ipa dunia kisogo
   • Enda jongomeo
  18. Andika kwa wingi (al.1)
   Zigo la kuliwa halilemei
   • Mizigo ya kuliwa hayalemei
 4. ISIMU JAMII (alama 10)
  Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali.
  “Naona “Horsepower” mwenyewe ndiye atakayepiga, atakayecheza foul hiyo. Wachezaji wa……”
  1. Tambua sajili inayorejelewa (al.2)
   • Sajili ya michezo/kandanda/kambumbu
  2. Tambua sifa zinazobainisha sajili yenyewe (al.8)
   • Lugha changamfu/cheshi/porojo
   • Kupiga chuku/kutiwa chumvi
   • Lugha shawishi
   • Utohozi/mf. Foul, Horse power
   • Lugha mseto/kuchanganya ndimi/msimbo
   • Matumizi ya tamathali za usemi
   • Lugha nyepesi inayoeleweka
   • Kuhamisha ndimi
   • Huchanganywa na nyimbo
   • Matumizi ya msamiati teule wa kambukambu
   • Kauli/sentensi fupi fupi
   • Sentensi zisizokamilika
   • Uradidi/takriri/urudiaji
   • Matumizi ya lakabu
   • Sifa kemkem kwa wachezaji
    Zozote nane 1x8=8
    Adhabu
    Makosa ya sarufi ya kwanza manne yaondolewe alama 2 4x1/2 =2
    Makosa ya hijai hadi manne 4x1/2 =2
    Jumla alama 4
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions And Answers - Form 4 Term 2 Opener 2021.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest