Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 Mid Term 2 Exams 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARATASI YA 1
KIADTO CHA NNE
MTIHANI WA KATI YA MUHULA

MAAGIZO

  1. Andika insha mbili.
  2. Insha ya kwanza ni ya lazima kisha uchague insha nyingine moja kati ya hizi tatu zilizosalia.
  3. Kila insha isipungue maneno 400.
  4. Kila insha ina alama 20.

Maswali

  1. Kumekuwepo na ongezeko la visa vya ufisadi, wewe kama mkazi wa jimbo la Kirinyaga mwandikie mhariri wa gazeti la Taifa Leo barua ukilalamikia suala hili.
  2. Eleza sababu tano zinazochangia matumizi ya mihadarati miongoni mwa wanafunzi huku ukipendekeza njia mwafaka za kukabiliana na tatizo hilo.
  3. Andika insha itakayomalizia kwa maneno haya. “ ............ alianza kubabaika, kijasho kikamtiririka kwapani.
    Nikatambua moja kwa moja kuwa yeye ndiye mkosi.
  4. Mgala muue na haki umpe.

MAAKIZO

Swali la 1

  • Insha ichukue muundo wa barua rasmi. (alama 5)
  • Anwani ya mwandishi na tarehe
  • Anwani ya mwandikiwa (mhariri wa Taifa Leo)
  • Mtajo
  • Kiini / Lengo (kukashifu / kulalamikia ufisadi
  • Hitimisho

    MAUDHUI (Alama 5)
  • Mtahiniwa aweze kujadili maudhui ya ufisadi na athari zake.
  • Matumizi mabaya ya ofisi.
  • Dhuluma / ukosefu wa haki.
  • Unyakuzi wa ardhi na rasili mali.
  • Umasikini na utabaka n.k.
    Mtahini akandilie hoja zingine ambazo mtahiniwa atatoa.
    Mtahiniwa aonyeshe msimamo imara wa kukashifu, kusuta na kukemea ufisadi. (Alama 2)
    Mtahiniwa azingatie sarufi ipasavyo. (Alama 6)
  • Mpangilio wa maneno.
  • Upatanisho wa kisarufi
  • Uakifishaji na tahajia
    Kosa la sarufi liadhibiwe kwa nusu alama (1/2)

Swali la 2

  • Mtahiniwa aipe insha yake anwani mwafaka. (al 1)
  • Mtahiniwa anaweza kuanza kwa kueleza dhana ya mihadarati na kutoa mifano mwafaka. (alama 2)
  • Mtahiniwa ajifunge kwa mambo matano yanayochangia matumizi ya mihadarati na ayafafanue ipasavyo
    Mfano
  • Kuiga mitindo kutoka kwa watu mashuhuri mf. Wasanii.
  • Ukosefu wa maadili na malezi mema.
  • Imani na itikadi potovu.
  • Utepetevu wa sheria.
  • Ukosefu wa sera mwafaka nk.
    (Hoja na ufafanuzi 5 x 2)

    Mtahiniwa aweze kutoa baadhi ya mapendekezo mwafaka.
  • Utekelezaji wa sheria ipasavyo.
  • Kutoa nasaha / mawaidha / ushauri.
  • Ushirikiano miongoni mwa wazazi na walimu.
  • Kuunda sera mwafaka shuleni nk.
    (Alama moja kwa hoja (5 x 1)
  • Mtahiniwa azingatie sarufi ipasavyo.
  • Mtahiniwa azingatie mtiririko mzuri wa hoja na kuhitimisha insha yake. (alama 2)
  • Mtahiniwa atumie msamiati kwa njia mwafaka.

Swali la 3

  • Hii ni insha ya mdokezo.
  • Mtahiniwa aandika kisa cha kubuni ambacho kitamalizikia kwa kusema na kauli iliyotolewa.
  • Mtahiniwa aipe insha yake kichwa mwafaka.
  • Mtahiniwa aonyeshe ubunifu wa hali ya juu na kuzingatia msamiati ipasavyo.
  • Mtahini akadirie kila kosa
  • Mtahiniwa ameandika kwa mjibu wa mdokezo uliotolewa.

Swali la 4

  • Ni insha ya methali na mtahiniwa atoe kichwa mwafaka.
  • Methali yenyewe inaweza ikatumika kama kichwa.

    Utangulizi
  • Mtahiniwa anaweza akaanza kwa kueleza maana ya methali (maana ya juu na yandani) (alama 2)
    Mtahiniwa anaweza kuingia moja kwa moja kwa kusimulia kisa kitakachoonyesha maana ya methali.

    Mwili
    Mtahiniwa afafanue na kudhihirisha pande zote mbili za insha. (alama 10)
  • Mgala muue - Dhuluma / unyanyasaji kwa masikini / mnyonge.
  • Na haki umpe - Mpumuko wa hadithi kwa kuonyesha utekelezaji wa haki.
  • Kisa kionyeshe ubunifu na kiweze kuaminika.
  • Mtahiniwa azingatie mtiririko mzuri wa mawazo.
  • Msamiati utumike ipasavyo na insha isipungue maneno 400 (alama 5)
  • Mtahiniwa azingatie sarufi ipasavyo na kosa lolote liadhibiwe kwa nusu alama (1/2)
  • Mtahainiwa ahitimishe insha yake ipasavyo. (alama 1)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 Mid Term 2 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest