Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 4 Mid Term 2 Exams 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARATASI YA 2
KIADTO CHA NNE
MTIHANI WA KATI YA MUHULA

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote

UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo:-

Pengine mwandishi George Orwell alikuwa na maono ya jinsi mataifa mengi ya Kiafrika yangekuwa pindi baada ya kujinyakulia uhuru, alipoandika riwaya ya ‘Shamba la wanyama.’

Riwaya hiyo inaakisi hali halisi ya mataifa haya, Kenya ikiwemo, ambapo imejikita katika dhihirisho la jinsi ujenzi wa matabaka ya kitawala, ubinafsi na ukandamizaji wa wananchi, unavyoweza kuzua maasi na hatimaye mapinduzi ya uongozi ulio mamlakani.

Baada ya kuwaambia wanyama kuhusu maono aliyokuwa nayo ya ulimwengu ambao kila mmoja angeishi huru, nguruwe mmoja anayeitwa Old Major, alijenga ari ya wenzake ili kushinikiza ndoto yake, kwa kuandika amri saba ambazo zilihakikisha kuwa rasilimali zote katika shamba hilo zingegawanywa kwa kila mmoja.

Lakini haya yote hayakuzingatiwa muda mfupi baadaye kwani ubinafsi uliokithiri ulichakachua amri hizo na kusambaratisha mfumo wa uongozi katika shamba hilo. Hali hiyo ndiyo tunayoshuhudia kwa sasa, wananchi wanapoandamana katika majimbo mbalimbali kulalamikia ‘kodi mpya za maendeleo’ zinazoanzishwa na serikali hizo. Huu ndio mkasa wa ubepari, uliojificha katika mfumo kandamizi wa ugatuzi, ambao kwa wazo langu,hatukuwa tumejitayarisha kabisa kuuanzisha.

Tumegatua kila aina ya uovu, umero na wizi. Tulilolisahau ni kuwa ‘magavana’ hawa tulioamka mapema kuwachagua walikuwa viongozi wale wale waliokuwa wakihudumu katika serikali za hapo awali, na hawakuwa ‘,miungu wa ukombozi kama walivyotupulizia baragumu zao walipokuwa wakitunadia kila aina ya ‘ahadi’ wakati wa kampeni.

Kwani ufisadi ndio umekithiri uovu mwingine tulioagatua ni ukabila. Kwa sasa, tofauti zilizopo si za kumchukia Mkikuyu au Mturkana akihiana na Mluo. Kila jamii kwa sasa zinaona wenzao kwa misingi ya kiukoo.

Mathalani, mzozo wa uongozi jimboni Embu unaelezwa ‘kuchochewa’ na tofauti za uwakilishi kati ya jamii za Waembu na Wambeere. Hapo awali, hatungesikia ‘mikataba’ kama hii! Huu ni moto uwakapo, kama si safari ya kuzimu tunayoelekea!

Kwani vita vya kikabila havitasikika tena, bali mafarakano yatakayochukua nafasi yake ni ‘mizozo ya kiukoo, ambayo katika majimbo yote 47 ni mkasa kama si saratani tuliyojiambukiza.

Ikiwa hatutatahadhari, huenda tukashuhudia maasi ya kiukoo katika nchi ndogo 47’ – na kizungumkuti kitakuwa jinsi ya kuyazima, kwani kila koo ‘likipigania nafasi yalo.’

MASWALI

  1. Kwa mujibu wa mwandishi wa makala haya ni mambo yapi yanayoweza kuzua maasi katika nchi ?(alama 3)
  2. Eleza mifano miwili ya maovu ambayo yamezungumziwa katika kifungu .(alama 2)
  3. “Huu ni moto uwakapo, kama si safari ya kuzimu…..” maneno haya yana maana gani kwa mujibu wa taarifa hii. (alama 3)
  4. Kwa nini mwandishi amefananisha mataifa mengi ya kiafrika baada ya uhuru na shamba la wanyama?(alama 3)
  5. Dhihirisha kauli ya mwandishi kuwa ‘tumegatua kila aina ya uovu, umero na wizi.(alama 2)
  6. Eleza maana za msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika taarifa (alama2)
    1. Inaakisi…………………………………………………………………………………………
    2. Mizozo ya kiukoo……………………………………………………………………………

MUHTASARI (alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima sawa. Utaifa hujengwa kwenye misingi ya mapenzi kwa nchi, Utambuzi wa cheo, eneo, hadhi, rangi na hata makabila wanakotoka raia wa taifa moja si chanzo cha kuwatenganisha. Nchi moja huweza kuundwa na watu walio na tofauti chungu nzima zikiwemo tofauti za kikabila, kitabaka na kimawazo. Hata hivyo, watu hao huwa na falsafa na imani sawa kama taifa linaloashiriwa hasa na wimbo wa taifa. Hata hivyo haya yote hayawezi kuwafikia katika kiwango cha kuunda taifa. Uzalendo ndio mhimili mkuu wa utaifa. Uzalendo ni mapenzi aliyo nayo mtu kwa nchi yake. Mapenzi haya humwongoza mtu katika mawazo yake, itikadi yake, matendo yake, matamanio yake na mkabala wake kuhusu nchi na hatima ya nchi yake. Mzalendo hawezi kushiriki katika matendo yanayoweza kuiletea nchi yake maangamizo kwa vyovyote vile. Mzalendo huongozwa na mwenge wa wema.

Mzalendo hawezi kushiriki kwenye shughuli zozote zinazohujumu mshikamano wa kitaifa. Yeye hatawaliwi na ubinafsi wa kutaka kufaidi nafsi yake na ya jamii yake finyu. Matendo yake yote huongozwa na ari ya kuiboresha nchi yake. Anayeipenda nchi yake hujiepusha na ulafi wa kujilimbikizia mali. Yuko radhi kuhasirika mradi taifa lake linufaike. Utaifa ni mche aali unaopaliliwa kwa uzalendo, kuepuka uchu wa nafsi na taasubi hasi zikuwepo za kikabila na ubinafsi. Hali hii inapofikiwa, hatima ya taifa na mustakabali wa raia wake huwa wenye matumaini makubwa.

  1. Kwa maneno 40 – 50 dondoa sifa kuu za utaifa.(alama 6, 1 ya mtiririko)
    Matayarisho
    Jibu
  2. Ni nini misingi ya kutathmini mzalendo? (maneno 60 - 70) (alama 9, 1 ya mtiririko)
    Matayarisho
    Jibu

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

  1.    
    1. Eleza maana ya sauti za likwidi.(alama 1)
    2. Tolea mifano miwili ya sauti za likwidi.(alama 1)
  2. Tunga neno lenye muundo ufuatao:
    Konsonanti , Kiyeyusho, Irabu Konsonanti Irabu Konsonanti Irabu
  3. Ainisha viambishi katika sentensi hii , kimuundo na kidhamira. (alama 4)
    Watamsomesha
  4. Bainisha kiima, kiarifa, kipozi na kitondo katika sentensi ifuatayo. (alama 4)
    Jacob alimjengea Halima nyumba nzuri.
  5. Huku ukitolea mifano, eleza matumizi mawili ya kistari kifupi katika uakifishaji.(alama 2)
  6. Tunga sentensi ukitumia vivumishi vinavyoleta maana zifuatazo
    1. kutobagua ( alama 1)
    2. kumiliki ( alama 1)
  7. Andika sentensi ifuatayo katika usemi taarifa. ( alama 2)
    “ Nitawapa zawadi mwaka ujao.” Mkurugenzi alitwambia.
  8. Nomino hizi ziko katika ngeli gani?
    1. kipepeo ( alama 1)
    2. maiti (alama 1)
  9.  Changanua sentensi hii kwa kutumia kielelezo cha mstari. (alama 2)
    Mzee aliyefika hapa atamleta mtoto mdogo leo
  10. Andika neno lenye muundo ufuatao. (alama 2)
    1. Nafsi ya tatu wingi, wakati uliopo, mzizi, kauli tendwa, kiishio
    2. kiambishi cha wingi, mzizi
  11. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao. ( alama 2)
    Nomino, kishazi tegemezi, kitenzi nomino
  12. Ainisha virai katika sentensi ifuatayo. ( alama 2)
    Watu wale wote walikuwa wasomi sana.
  13. Tunga sentensi moja ili kuleta maana mbili za neno paka.
  14. Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maigizo. ( alama 2)
    1. Peter, Kelvin na Musa ndio watapewa vitabu. (Tumia Kiwakilishi nafsi badala ya nomino zilizopigiwa mstari)
    2. Yusufu alimsomea Rahman hadithi. ( Geuza sentensi hii iwe kwenye kauli ya kutendewa)
  15. Tolea maana nne za sentensi hii. ( alama 4)
    Bakari alimpigia Otieno mpira.
  16. Anza sentensi ifuatayo kwa yambiwa. ( alama 1)
    Juma alimlimia Wafula shamba kwa trekta
  17. Fafanua maana za istilahi hizi. ( alama 3)
    1. kishazi tegemezi
    2. kibadala
    3. mofimu

ISIMU JAMII (ALAMA 10)

  1. Fafanua changamoto zozote kumi zinazokumba lugha ya Kiswahili nchini Kenya.

MAAKIZO

UFAHAMU

  1.    
    • Matabaka ya kitawala
    • Ubinafsi
    • Ukandamizaji wa wananchi
  2.      
    • Hali ya magavana kupigania njia za kujilimbikizia mali.
    • Dhana ya ukabila-watu wanajitambua kulingana na jamii/ukoo wao.
  3. Watu kujitambua kulingana na koo zao ni sawa na moto kama uadui utachipuka kati ya watu wa jamii moja. Kwa mfano Waembu na Wambere.
    • Hali hii inaweza kusababisha maafa kama vile vita vya kiukoo.
  4. Katika shamba la wanyama, nguruwe anayeitwa Old Major aliandika amri saba ambazo zilihakikisha kuwa rasilimali zote katika shamba zingegawanywa kwa wanyama wote. Baada ya mapinduzi wanyama waliochukua hatama ya uongozi waliendeleza ubinafsi uliosambaratisha mfumo wa uongozi.
  5. Kwa sasa hali hii inaendelea Kenya ambapo viongozi waliochaguliwa kuwakilisha kaunti/majimbo wanakandamiza raia kwa kuwatoza kodi, wanaendeleza ubepari n.k.
  6. Kila uovu kama vile ulafi, wizi n.k unaoendelezwa na viongozi magavana unasingiziwa ugatuzi.
  7.     
    • Inaakisi-inaashiria
    • Mizozo ya kiukoo-ugomvi/vita/ghasia za kikabila, watu wanaotokana na nasaba moja.

      Adhabu:
    • Kila kosa la sarufi litokeapo mara ya kwanza liadhibiwe kwa kutozwa (½ maki hadi makosa 6.
    • Kila kosa la hijai litakeapo mara ya kwanza liadhibiwe kutozwa (½ maki Hadi makosa 6.

MUHTASARI (alama 15)

  1. Kwa maneno 40 - 50 dondoa sifa kuu za utaifa.(alama 6, 1 ya mtiririko)
    • Kuwepo kwa hatima sawa
    • Kuwepo kwa maono sawa
    • Kuwepo kwa falsafa/imani/itikadi sawa.
    • Kuwepo kwa mwelekeo mmoja.Umejengwa kwa hisia za mapenzi kwa nchi.
  2. Ni nini misingi ya kutathmini mzalendo? (maneno 60 - 70) (alama 9, 1 ya mtiririko)
    • Hawezi kushiriki kwenye shughuii zozote zinazohujumu mshikamano wa kitaifa.
    • Hawezi kutawaliwa na ubinafsi
    • Hujiepusha na ulafi wa kujilimbikizia mali.
    • hawezi kutenda mambo ya kuiletea nchi yakemaangamizo.
    • Yuko radhi kuhasirika kwa manufaa ya taifa lake.
    • Matendo yake huongozwa na mwenge wa wema.
    • Matendo yake huongozwa na ari kuiboresha nchi yake.

MATUMIZI YA LUGHA

  1.    
    1. Sauti ambazo huwa na mkwaruzo fulani wakati wa matamshi
    2. /l/ na /r/
  2. Mwalimu, mwavuli
  3.    
    1. Kidhamira
      • wa- Kiima Nafsi ya tatu wingi
      • ta- wakati ujao
      • m- yambwa nafsi ya tatu umoja
      • som- mzizi wa kitenzi
      • esh- kauli ya kutendesha
      • a- kiishio
    2. Kimuundo
      • watam- viambishi awali
      • som-
      • esha- viambishi tamati
  4.      
    • Jacob- Kiima
    • Alimjengea- Kiarifa
    • Halima- Kitondo
    • Nyumba nzuri- Kipozi
  5.        
    • Kuandika tarehe k.m 02-10-2019
    • Kutenganisha neno na ufafanuzi wake. K.m Kaa- kipande cha kuni kilichoungua.
  6.      
    • kutobagua ( alama 1)
      Nitampa kitabu chochote.
    • kumiliki ( alama 1)
      Mzee mwenye gari amewasili.
  7. Mkurugezi alitwambia kwamba angetupa zawadi mwaka uliofuata.
  8.         
    • A-WA
    • I-ZI
  9. S- KN(N+S)+KT(T+N+V+E) au S- KN(N+S)+KT(T+KN2(N+V)+KE(E) )
  10.      
    • Wa+na+pig+w+a = wanapigwa
    • wa+toto= watoto
  11. Mama aliyekasirika amemwadhibu mtoto.
  12.      
    • RN- watu wale wote
    • RV- wale wote, wasomi
    • RT- kuwa wasomi sana
    • RE- sana
  13. Paka wetu alipotea tulipoanza kupaka rangi.
  14.         
    • Wao ndio watapewa vitabu.
    • Rahman alisomewa hadithi na Yusufu.
  15.     
    • Bakari aliutumia mpira kama kifaa.
    • Bakari alimpiga Otieno kwa sababu ya mpira.
    • Bakari aliupasi mpira kwa Otieno.
    • Bakari aliupiga mpira kwa niaba ya Otieno.
  16. Wafula alilimiwa shamba kwa treka na Juma.
  17.       
    • kishazi tegemezi- Hiki ni kishazi ambacho hakijitoshelezi kimaaana na huvitegemea Vishazi vingine ili kikamilike kimaana.
    • kibadala- hili ni neno ambalo husimama mahala pa nomino katika sentensi.
    • mofimu- hiki ni kipashio kidogo cha lugha ambacho huwa na maana na hakiwezi kugawika zaidi.

ISIMUJAMII (ALAMA 10)

  1.    
    • Uhaba mkubwa wa wataalamu wa Kiswahili
    • Athari kutoka kwa lugha ya kwanza.
    • Watu kuchangamka lugha nyinginezo kama vile kiingereza, kijerumani.
    • Imani potovu – lugha ya Kiswahili ni duni
    • Uhaba wa walimu wa Kiswahili.
    • Uhaba wa vitabu vya Kiswahili.
    • Kutokuwepo kwa sera ya lugha kutoka kwa baadhi ya serikali za mataifa ya Afrika mashariki.
    • Uhaba wa pesa za kutafiti.
    • Nchi za Afrika za kukuza na kuendeleza Kiswahili.Kuchipuka kwa lugha ya Sheng
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 4 Mid Term 2 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest