Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

MAAGIZO.

  • Majibu yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili
  1. UFAHAMU
    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

    Ilikuwa jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya habari.

    Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe pesa za kiinua mgongo. Mwezi mmoja mzima nilikuwa katika shughuli za kulipa deni hapa na kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na kununua hili. Sasa shilingi lake mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki. Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika. Katika taarifa ya habari jioni hiyo, Waziri wa Kilimo alitangaza bei mpya. Shilingi 1,500 kwa kila gunia. name nilikuwa naanza kuumakimikia mradi huu.

    Baada ya tarifa, nilikoga, nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi ulinichulua mara moha. Usingizi niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa kilimo nilitenga ekari kumu za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima ni wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi 1,200 kila ekari. Katikati ya mwezi wa Machi, nilitafuta trekta la kutifua shamba tena kwa gharama ya shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nilipa shilling elfu kumi na tatu kupiga shamba lote haro.

    Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejeo. Kwanza, nililipa shilling 20,500 kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunu amagunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa kilo 25 kwa shilling 3,300 kila gunia. Mwzi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda. Ili nipate mazao bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilling 1,000 kila ekari. Mvua ilinesha vizuri na baada ya siku saba mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mebgu mchangani.

    Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua wa kupalilia. Malipo yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilal kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa yananifikia magotini. Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo ‘amonia’. Gharama yake ikawa shilling 1,300 kila gunia. Hivyo, nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia kumi na matano.

    Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa maisha. Yalibadilika rangi yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapita njia waliajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa kila siwanawaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanzi wanfu. Hapo nikaanza kuhesabu mavuno nitakayopata kukadiria faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa ‘Usikate majani, mnyama hajauawa.’

    Bila taarifa wala tahadhari mvua ikatoweka. Hayakupita majuma mawili mahinda yakaanza kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahind, shamba ilkageuka la vitunguu vilivyochomwa na jua. Makasio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi yfanyavyo moshi.

    Lakini ‘Muumba ndiye Muumbua’. Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha.Muda si muda mahind yalianaza kunawiri. Kumbe tukio lililonivunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwaa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa limetapakaa barafu huku majani ya mahindi yamechanika kama nyuzi. Niliugua. Baada ya wiki moja, nilipata nafuu. Nilipotazama upande wa shamba nikaona dalili za majani mapya ya mahindi yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli. Muda sio mferu mahindi yalirudi hali yake tena, kisha yakakomaa. Haraka za kutafuta watu wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli kii ikawa shilingi 5,000. Kuvuna, kusafirisha kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500. Kufikia hapo nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi yalipokuwa tayari kwenye magunia nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko. Niliposhuka tu niliona gazeti. habari motomoto siku hiyo ilikuwa: “MAHIND GUNIA 900/-” Niligutuka usingizini.

    Maswali
    1. Andika kichwa mwafaka kwa kifungu hiki cha habari. (al 1)
    2. Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha pesa katika benki baada ya mradi kukamilika? (al 1)
    3. Taja matatizo matatu yaliyotisha mradi wa msimulizi wa kukuza mahindi. (al 3)
    4. Eleza maana ya methali zifuatazo: (al 4)
      1. Usikate majani, mnyama hajauawa
      2. Muumba ndiye muumbua
    5. Eleza mambo mawili yaliyosababisha msimulizi asipate faida alivyotarajia. (al 2)
    6. Kwa nini msimulizi alisem maumbile ni kitu cha ajabu? (al 2)
    7. Eleza maana ya: (al 2)
      1. kiinua mgongo
      2. manyakanga wa kilimo
  2. UFUPISHO (alama 15)

    Jamii ya leo inatawaliwa na kuendeshwa na kanuni ya maarifa. Inawezekana kusema kuwauchumi wa jamii za leo na zijazo utategemea maarifa zaidi kuliko utakavyotegemea uwezo wowote mwingine. Utambuzi wa uwezo mkubwa wa maarifa katika maisha ya binadamu ndio msingi wa watu kusema ‘maarifa ni nguvu.’

    Maarifa huelezwa kwa tamathali hii kutokana na uwezo wa: kuyadhibiti,kuyaendesha, kuyatawalana kuyaongoza maisha ya binadamu popote pale walipo. Mtu ameyakosa maarifa fulani huwa ameikosa nguvu hiyo muhimu na maisha yake huathirika pakubwa. Kwa msingi huu, maarifa yanawezakuangaliwa kama utajiri mkubwa ambao binadamu anaweza kuutumia kwa faida yake au kwa faida ya wanajamii wenzake. Ukweli huu ndio unaoelezwa na methali ya Kiswahili: ‘Elimu ni mali.’ Elimu ni chimbuko la maarifa muhimu maishani.

    Msingi wa utajiri na maendeleo ya binadamu popote alipo basi ni maarifa. Je, maarifa kwa upande wake yana sifa gani? Maarifa yenyewe hayana upinzani. Maarifa uliyo nayo huweza kuwa na watu wengine pasiwe na upinzani baina yenu kwa kuwa kila mmoja ana maarifa sawa. Kila mmoja ana uhuru wa kuyatumia maarifa hayo kama chanzo cha kuyazalisha mengine. Utumiaji wa maarifa yenyewe hauyamalizi maarifa hayo. Maarifa hayawezi kugusika ingawa mtu anaweza kuyanyumbua maarifa yenyewe kwa kuyatumia kwa namna tofauti.

    Maarifa huingiliana na maarifa mengine. Maarifa aliyo nayo mtu huweza kuhusishwa na maarifa aliyo nayo mtu mwingine ili kuvyaza au kuzuka na maarifa tofauti. Maarifa yanaweza kuchukuliwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa namna ambavyo mtu huweza kufanya bidhaa nyingine ile. Kwa mfano, ni muhali mtu kulalamika kuwa hawezi kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa sababu ana mzigo wa maarifa kichwani.

    Sifa nyingine muhimu ya maarifa ni kuwa yanaweza kuwasilishwa kwa njia au mitindo mingine ya kidhahania. Ikiwa unataka kukihamisha chombo fulani kutoka sehemu moja hadi nyingine, lazima uwazie ukubwa wake, uzito wake na labda hata umbali wa panapohusika. Maarifa huweza kubadilishwa au kugeuzwa na kuwa ishara ambazo huyafanya kuwasilishswa kwa njia nyepesi kuliko kwa mfano ikiwa mtu atayawasilisha katika muundo wa, kwa mfano,kitabu.

    Maarifa yana sifa ya uhusianaji. Kipengele fulani cha maarifa huwa na maana kinapowekwa sambabmba au kugotanishwa na kipengele kingine cha maarifa. Huo huwa muktadha mzuri wa kueleweka au kuwa na maana kwa mfano, neno ‘mwerevu’ huweza kuwa na maana kwa kuwekwa katika muktadha wa ‘mjinga’, ‘ mjanja’, ‘hodari’ na kadhalika.

    Maarifa huweza kunifadhiwa katika nafasi ndogo sana. Suala hili linaeleweka kwa njia nyepesi tunapoangalia maarifa katika muktadha wa teknolojia. Data zinazowahusu mamilioni ya watu,ambazo zingehitaji maelfu ya maktaba na lukuki ya vitabu, huweza kuhifadhiwa kwenye kifaa kidogo kinachoweza kutiwa mfukoni.

    Maarifa hayawezi kuthibitiwa au kuzuiliwa mahali fulani yasisambae. Maarifa huenea haraka sana. Maarifa ni kitu kinachoepuka pingu za watu wanaopenda kuwadhibiti binadamu wenzao. Hata pale ambapomfumo wa kijamii au wa kisiasa unafanya juu chini kuwadhibiti raia au watu wenyewe,ni muhali kuyadhibiti maarifa yenyewe. Inawezekana kuzidhibiti njia fulani za uenezaji wa maarifa lakini maarifa hayo yatapata upenyu wa kusambaa. Ni kweli kuwa maarifa ni nguvu inayozishinda nguvu zote.
    1. Fupisha aya ya pili na tatu (maneno 55-60)(alama 5, 1 ya utiririko)
      Matayarisho
      Nakala safi
    2. Eleza sifa kuu za maarifa kama zinavyojitokeza kuanzia aya ya nne hadi aya ya nane.
      (maneno 100-110) (alama 10, 2 za utiririko)
      Matayarisho
      Nakala safi
  3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1. Taja na utofautishe irabu za mbele. (alama 2)
    2. Tunga sentensi Moja kubainisha maana mbili za neno kikosi. (alama 2)
    3. Andika katika wingi. (alama 1)
      Jino langu bovu linaloniuma linanitatiza.
    4. Tumia kielezi cha wakati badala ya kielezi kilichotumika katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Watalii walitutembelea mjini Nakuru.
    5. Geuza sentensi zifuatazo kulingana na maagizo. (alama 2)
      1. Maimuna anapika wali. (wakati uliopo hali isiyodhihirika)
      2. Wao walisoma riwaya hiyo. (wakati ujao hali timilifu)
    6. Unda neno lenye muundo ufuatao. (alama 2)
      1. Nafsi ya kwanza umoja.
      2. Hali timilifu
      3. Mtendewa
      4. Mzizi
      5. Kauli ya kutendea
      6. Kauli ya kutenda/ kiishio
    7. Tumia nomino zifuatazo za kawaida kuunda nomino za jamii. (alama 2)
      1. Nzige
      2. Zabibu
    8. Tunga sentensi kuonyesha matumizi yafuatayo ya neno KAMA. (alama 2)
      1. Kihusishi
      2. Kitenzi
    9. Eleza matumizi ya neno wale katika sentensi hii. (alama 3)
      Wale walioiba ni mabanati wale ambao waliambiwa wale kabla ya kitendo hicho.
    10. Changanua kwa mstari. (alama 4)
      Yohana na Otieno hucheza kandanda.
    11. Andika sifa tatu zinazobainisha sentensi changamano. (alama 3)
    12. Onyesha matumizi ya viwakifishi vifuatavyo katika sentensi. (alama 2)
      1. Kibainshi
      2. Parandesi
    13. Tumia neno –baya kama: (alama 3)
      1. Kiwakilishi
      2. Kivumishi
      3. Kielezi katika sentensi
    14. Onyesha miundo miwili ya nomino za ngeli ya A- WA. (alama 2)
    15. Bainisha maana mbili ya sentensi hii. (alama 2)
      Umu alimwandisha mkewe.
    16. Unda nomino nne kutokana na kitenzi. (alama 4)
      Fa
    17. Geuza katika usemi halisi. (alama 2)
      Askari jela alimuuliza Kendi kama alidhnani hapo ni kwao. Alimwamuru aende kwake mara moja.
  4. ISIMU JAMII (alama 10)
    (Mdundo wa muziki) kina mama mpo…..! Kina siste nanyi… are you there? Kampuni ya platinium imewaletea mafuta mpya ya silk. Mafuta hayo yana vitamin C, Sunscreen na yana marashi ya kupendeza. Ukiyatumia kwa wiki moja tu, ngozi yako itakua laini na nyororo kama ya kitoto kichanga. Nayo macho ya wote, Waaa! Yatakuwa kwako 24/7. Jinunulie! Jinunulie! Mafuta ya silk. Mafuta ya wanawake wa kisasa.
    1. Taja sajili iliyotumiwa hapa. (alama 1)
    2. Taja sifa nne za sajili hii. (alama 4)
    3. Kwa nini Wakenya wengi hupenda kuchanganya na kubadili msimbo? (alama 5)

Mwongozo wa Kusahihisha

  1. UFAHAMU

    Maswali
    1. Andika kichwa mwafaka kwa kifungu hiki cha habari. (al 1)
      • Mashaka ya kilimo cha mahindi
    2. Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha pesa katika benki baada ya mradi kukamilika? (al 1)
      • Shilingi elfu saba na mia tatu
    3. Taja matatizo matatu yaliyotisha mradi wa msimulizi wa kukuza mahindi. (al 3)
      • Kiangazi
      • Mvua ya barafu
      • Gharama kubwa
      • Tisho la korongo na vidiri kufukua mbegu
    4. Eleza maana ya methali zifuatazo:
      1. Usikate majani, mnyama hajauawa
        • Haikuwa vizuri kufurahia faida kabla ya kuuza mahindi.
      2. Muumba ndiye muumbua
        • Mungu ana uwezo wa kuleta mafanikio palipo na changamoto.
    5. Eleza mambo mawili yaliyosababisha msimulizi asipate faida alivyotarajia. (al 2)
      • Kiwango cah chini cha mvua
      • Kushuka kwa bei
    6. Kwa nini msimulizi alisem maumbile ni kitu cha ajabu? (al 2)
      • Mahindi aliyodhani yameangamizwa na kiangazi au barafu yalinawiri tena.
    7. Eleza maana ya:
      1. kiinua mgongo
        • Malipo ya kustaafu
      2. manyakanga wa kilimo
        • Wataalamu wa kilimo

  2. UFUPISHO (alama 15)
    1. Fupisha aya ya pilina tatu (maneno 55-60)(alama 5, 1 ya utiririko)
      • Maarifa huyadhibiti, huyatawala, huyaendesha na kuyaongoza maisha ya binadamu.
      • Anayekosa maarifa huthirika pakubwa
      • Maarifa ni utajiri mkubwa ambao binadamu huutumia kwa faida yake na wanajamii wenzake/ elimu ni mali/ msingi wa utajiri na maendeleo ya binadamu ni maarifa.
      • Elimu ni chimbuko la maarifa muhimu maishani.
      • Maarifa hayanna upinzani.
      • Utumiaji wa maarifa hauyamalizi.
      • Utumiaji wa maarifa hauyamalizi.
      • Kila mtu ana uhuru wa kutumia maarifa kuzalisha maarifa mengine/anaweza kunyumbua maarifa na kuyatunza kwa namna tofauti.
      • Maarifa hayagusiki.

    2. Eleza sifa kuu za maarifa kama zinavyojitokeza kuanzia aya ya nne hadi aya ya nane.
      (maneno 100-110) (alama 10, 2 za utiririko)
      • Maarifa huingiliana na maarifa mengine.
      • Hayawezi kuchukuliwa kwa njia ya ishara au mitindo ya kidhahania.
      • Huweza kubadilishwa/kugeuza na kuwa ishara
      • Yana sifa ya uhusianaji.
      • Huweza kuhifadhiwa katika nafasi ndogo.
      • Hayawezi kudhibitiwa/kuzuiliwa mahali Fulani yasisambae/ huenda haraka sana.
      • Huepuka pingu za wat kudhibiti wenzao.
      • Ni nguvu inayoshinda nguvu zote.

  3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1. Taja na utofautishe irabu za mbele. (alama 2)
      • /e/ na /i/
      • /i/ ni irabu ya juu
      • /e/ ni irabu ya wastani

    2. Tunga sentensi Moja kubainisha maana mbili za neno kikosi. (alama 2)
      • Mkusanyiko wa askari zaidi ya mia moja.
      • Sehemu ya nyuma ya shingo
      • Mkosi mdogo
      • Sentensi zionyeshe maana , mwalimu akadirie majibu ya wanafunzi.

    3. Andika katika wingi. (alama 1)
      Jino langu bovu linaloniuma linanitatiza.
      • Meno yetu mabovu yanavyotuuma yanatutatiza.

    4. Tumia kielezi cha wakati badala ya kielezi kilichotumika katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Watalii walitutembelea mjini Nakuru.
      • Watalii walitutembelea jana/juzi/ mwezi uliopita nakuru.
      • Mwalimu akadhirie majibu ya wanafunzi.

    5. Geuza sentensi zifuatazo kulingana na maagizo. (alama 2)
      1. Maimuna anapika wali. (wakati uliopo hali isiyodhihirika)
        • Maimuna apika wali.

      2. Wao walisoma riwaya hiyo. (wakati ujao hali timilifu)
        • Wao watakuwa wamesoma riwaya hiyo.

    6. Unda neno lenye muundo ufuatao. (alama 2)
      1. Nafsi ya kwanza umoja.
        • /ni/
      2. Hali timilifu
        • /me/
      3. Mtendewa
        • /m/
      4. Mzizi
        • /lim/
      5. Kauli ya kutendea
        • /i/
      6. Kauli ya kutenda/ kiishio
        • /a/ mfano wa neno ; nimemlimia

    7. Tumia nomino zifuatazo za kawaida kuunda nomino za jamii. (alama 2)
      1. Nzige
        • Wingu la uzige
      2. Zabibu
        • Kikonyo za zabibu

    8. Tunga sentensi kuonyesha matumizi yafuatayo ya neno KAMA.(alama 2)
      1. Kihusishi
        • Otieno ni mrefu kama twiga.
      2. Kitenzi
        • Baba aliwakama ng’ombe wote

    9. Eleza matumizi ya neno wale katika sentensi hii. (alama 3)
      Wale walioiba ni mabanati wale ambao waliambiwa wale kabla ya kitendo hicho.
      • Wale walioiba ni mabanati wale ambao waliambiwa wale kabla ya kitendo hicho.
      • 1 – kiwakilishi
      • 2 – kivumishi
      • 3 - kitenzi

    10. Changanua kwa mstari. (alama 4)
      •             KN                         KT
        Yohana na Otieno / hucheza kandanda.
              N      U      N           T                N
        S – KN + KT
        KN – N + U + N
        N – Yohana
        U – Kiunganishi
        N – Otieno
        KT – T + N
        T – huchuza
        N – Kandanda
        Toa alama moja kwa kila kosa

    11. Andika sifa tatu zinazobainisha sentensi changamano. (alama 3)
      • Huwa na vishazi viwili (huru na tegemezi)
      • Huwa na kirejeshi
      • Vitenzi viwili au zaidi

    12. Onyesha matumizi ya viwakifishi vifuatavyo katika sentensi. (alama 2)
      1. Kibainshi
        • Kuweka king’ong’o mf ng’ombe.
        • Kudodosha nambari au sauti mf ‘4 au n’taenda
      2. Parandesi / mabano.
        • Mf maelezo ya ziada. Mwalimu (wa historia) amekuja/ Kuzingira nambari 1

    13. Tumia neno –baya kama: (alama 3)
      1. Kiwakilishi
        • Kibaya chajitembeza.
            w
      2. Kivumishi
        • Kiatu kibaya kitatupwa pipani.
                       v
        • Kielezi katika sentensi
        • Timu yetu ilicheza vibaya jana
                                             E
          (Kadiria majibu ya wanafunzi)

    14. Onyesha miundo miwili ya nomino za ngeli ya A- WA. (alama 2)
      • M – wa mf mtoto – watoto
      • Ki – vi mf kiziwi – viziwi
      • Ѳ –Ѳ mf mbuzi – mbuzi
      • Ѳ – ma mf daktari – madaktari
      • M – mi mf mtume – mitume
      • Ch – vya mf chura - vyura

    15. Bainisha maana mbili ya sentensi hii. (alama 2)
      Umu alimwandikisha mkewe.
      • Umu alimfanya aajiriwe kazi
      • Umu alimfanya aandike
      • Umu alisabaisha kitendo cha jina lake kuandikwa.
      • Aliyeandikwa ni mke wa umu.
      • Aliyeandikwa ni mke wa mtu mwingine

    16. Unda nomino nne kutokana na kitenzi. (alama 4)
      Fa
      • Mfu
      • Kufa
      • Kifo
      • Wafu

    17. Geuza katika usemi halisi. (alama 2)
      Askari jela alimuuliza Kendi kama alidhani hapo ni kwao. Alimwamuru aende kwake mara moja.
      • Askari jela alimuuliza Kendi, “Unadhani hapa ni kwenu? Kuja kwangu mara moja.”
  4. ISIMU JAMII (alama 10)

    (Mdundo wa muziki) kina mama mpo…..! Kina siste nanyi… are you there? Kampuni ya platinium imewaletea mafuta mpya ya silk. Mafuta hayo yana vitamin C, Sunscreen na yana marashi ya kupendeza. Ukiyatumia kwa wiki moja tu, ngozi yako itakua laini na nyororo kama ya kitoto kichanga. Nayo macho ya wote, Waaa! Yatakuwa kwako 24/7. Jinunulie! Jinunulie! Mafuta ya silk. Mafuta ya wanawake wa kisasa.

    1. Taja sajili iliyotumiwa hapa. (alama 1)
      • Sajili ya matangazo ya biashara.

    2. Taja sifa nne za sajili hii. (alama 4)
      • Hajaa porojo nyingi
      • Lucha huwa nyepesi na rahisi
      • Lugha haizingatii kanuni za lugha
      • Lugha ya kupiga chuku ili kushawishi wasikilizaji.
      • Mbinu ya kuchanganya na kubadili msimbo hutumika.
      • Mbinu ya picha na muziki hutumiwa nikuzidisha mvuto kwa wasikilizaji.
      • Lugha ya mshawasha mno hutumika
      • Lugha ya mkato hutumika.

    3. Kwa nini Wakenya wengi hupenda kuchanganya na kubadili msimbo? (alama 5)
      • Kuonyesha umahiri wa lugha zote mbili.
      • Kuonyesha hisia k.m chuki, huzuni, furaha n.k
      • Kufidia upungufu wa msamiati au lugha anayotumia kukosa msamiati.
      • Ili kujitambulisha na kundi linalotumia lugha Fulani.
      • Kujinasibisha na hadhi ya lugha iwapo katika jamii lugha moja ina hadhi kuliko nyingine.
      • Kutokana na ari ya kutaka kueleweka zaidi.
        Zozote tano
        Kusahihisha
        Makosa ya sarufi hadi nne. ½ x 4 = 2
        Makosa ya hijai hadi nne ½ x 4 = 2 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest