Kiswahili Questions and Answers - Form 4 Mid Term 2 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. SEHEMU A. UFAHAMU
  Soma taarifa hii kisha ujibu maswali
  Aisifuye mvua imemnyea. Huu ni msemo wenye hakika isiopingika, na kutilia shaka ni sawa na kudai jua linaweza kubadilika na kuchomozea upande wa magharibi badala ya mashariki. Huu ndio ukweli uliodhihirika juzi katika vyombo vyetu vya magazeti.
  Lisemwalo lipo, na kama halipo li njiani. Waama, pafukapo moshi pana moto. Mwanafunzi mmoja wa kike kwa jina P.N. katika chuo kikuu kimojawapo nchini alishangaza umma wa Kenya na ulimwengu kwa jumla alipodai kuwaambukiza wanafunzi wenzake wa kiume mia moja na ishirini na wanne virusi vya Ukimwi.
  Kisa na maana? Aliambukizwa Ukimwi na mwanafunzi mwenzake aliyekuwa akifanya majaribio ya ualimu katika shule yao ya upili. Baada ya kushawishika sana alijuana naye kimwili, na matokeo yakawa kifo ambacho sasa alikuwa anawagawia wenzake.
  Kisa kama hiki kinachangia kueleza kina kirefu cha kutamauka na upweke ambao maisha ya waja wengi yameingia kiasi cha kuwaacha wanyama ijapo wanaenda kwa miguu miwili bado. Katika mojawapo ya mafunzo ya kidini ambayo Padre alinifunza mimi na wanafunzi wenzangu, tuliambiwa kisasi ni chake Mola, sisi waja wetu ni kushukuru tu. Mbona basi mwanafunzi kama huyu kutaka kulipiza?
  Ima fa ima, na waswahili husema, “mlaumu nunda na kuku pia”. Huyu mwanafunzi hawezi kuachiwa atende alivyotenda. Aliyekula naye raha alikuwa mtu aliyefahamika vizuri sana kwake. Isitoshe, huenda wakati huo alikosana na mama na baba kwa kulala nje. Huenda alikosana na ndugu zake kwa kuhepa nyumbani usiku wa manane kwenda kumwona huyu kalameni. Huenda alikosana na mwalimu wake kwa sababu kiburi kilianza kuingia. Kwa vyovyote vile, alikula raha na hastahili kuwaadhibu watu wasio na hatia kufidia makosa yake. Je, kama yeye na huyo jamaa wasingekuwa na Ukimwi, raha kiasi gani wangezila hadi leo?
  Jamii na watu wote kwa jumla hawana budi basi kulaani vitendo vya P.N. vya kuambukiza wanafunzi wenzake virusi huku akijua. Hili ni kosa ambalo linastahili adhabu ya kifo. Dawa ya moto ni moto ni adhabu inastahili kuchukuliwa haraka ili P.N. ambaye tayari amekiri hatia, atiwe nguvuni na adhabu itolewe.
  Barua ya P.N. inafafanua jambo jingine sugu. Kwamba kiwango cha maadili katika vyuo vyetu kimezorota kiasi cha kufanyiana unyama usiosemeka. Vijana wengi siku hizi wanashiriki tendo la ndoa bila haya. Huu upotofu wa maadili katika jamii wapaswa kushutumiwa na wote. P.N. hana sababu yoyote ya kibinadamu, kidini au kitu chochote kile kudai haki kwa uovu huo wake.
  Maswali
  1. Taja kichwa kwa makala haya ( al.2
  2. Katika aya mbili za kwanza, mwandishi anamlaumu mwanafunzi kwa kosa gani? (al.2)
  3. Eleza chanzo cha tabia za P.N ( al.2)
  4. Mwandishi wa taarifa hii anataka P.N achukuliwe hatua gani? Kwa nini? (al.4)
  5. Barua ya P.N. bila shaka imeonyesha uvumbuzi mpya. Utaje (al.2)
  6. Eleza maana ya vifungu hivi kama vilivyotumiwa katika taarifa: (al.3)
   Kina kirefu cha kutamauka...............................................................................................
   Ima fa ima.......................................................................................................................
   Kufidia makosa yake.......................................................................................................
 2. SEHEMU B:UFUPISHO ( ALAMA.15)
  Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

  Nchi nyingi za ulimwengu wa tatu huathirika na biashara ya kimataifa.Biashara hiyo inaweza kuwa inafanya kwa uagizaji ama uuzaji wa bidhaa za nchi nyingine.
  Biashara ya kimataifa ina umuhimu mkubwa. Kwanza, inawezesha nchi kupata bidhaa ambazo haitengenezi mbali na kusaidia kuwepo na uhusiano kati ya nchi mbalimbali. Uhusiano huu huiwezesha nchi kupata bidhaa kwa bei rahisi kuliko ambavyo ingekuwa kama zingetengenezwa kwao, hasa ikiwa nchi inayohusika haina malighafi yanayohusika katika utengenezaji wa bidhaa hizo. Pia husaidia wakati nchi imekumbwa na dharura au majanga kwani itaauniwa na nchi nyingine ingawa hali kama hii haihakikishwi, ushirikiano huu vile vile huchochea upatikanaji wa nafasi za kazi kwa wengi.
  Kwa sababu za kushughulikia utengenezaji wa bidhaa na utoaji huduma nyingine kutokana na uzoefu wa muda na kuwepo raslimali, nchi huwa na uzoefu fulani. Ni kwa sababu hii nchi inawezeshwa kupata pesa za kigeni na kuuza bidhaa za ziada.
  Hata hivyo kuna matatizo yanayozikumba nchi za kiafrika katika biashara hii. Kwanza, biashara ya aina hii hutatiza viwanda vichanga katika nchi zinazoendelea kwa ushindani usio sawa. Ajabu ni kwamba nchi zilizoendelea zimetumia bishara hii ‘kutupa’ bidhaa za hali ya chini ama zenye athari kwa hali za kijamii.Urafiki haukosi. Ikiwa nchi inategemea uagizaji wa bidhaa, haitaweza kuikosea ama kuhitilifiana na nchi ambayo inategemea, hivyo kuathiri uhuru wa nchi kama hiyo.
  Hata hivyo, nchi mbalimbali zimeweka mikakati ya kulinda viwanda kutokana na athari ya biashara kama hii. Baadhi zimeweka ushuru wa juu kwa bidhaa zinazoagizwa utoka nje kwa wasio washirika wa kibiashara. Licha ya hayo, baadhi ya bidhaa zinazonuiwa kwa nje kwa matumizi ya kielimu, utafiti wa kisayansi nabidhaa za maonyesho huagizwa bila ushuru huo. Wakati mwingine ni benki kuu ndiyo hutoa leseni kwa niaba ya serikali kama njia ya kudhibiti bidhaa kutoka nje. Njia nyingine ya kuvisaidia viwanda nchini ni kuuza bidhaa kwa njia ya kuvipunguzia ushuru, usafirishaji nafuu na kuvipa ushuru.
  Serikali nyingine huhakikisha kuwa ni bidhaa kiasi fulani tu ambazo zinaweza kuagizwa kwa kipindi fulani. Kwa mfano, kuna idadi fulani ya magari kutoka nje yanayoweza kuagizwa kuja Kenya kwa mwaka mmoja. Hata hivyo, wakati mwingine, serikali husitisha uagizaji wa bidhaa kama vile dawa, sinema, maandishi ya kisiasa na vitabu kutoka nje; bidhaa ambazo zinachukuliwa kuwa hatari kwa nchi. Licha ya matatizo haya, biashara imekuwepo na inaendelea kujiimarisha.
  Maswali
  1. Kwa mujibu wa mwandihsi wa makal haya, bishara ya kimataifa itaendelea kujiimarisha.
   Eleza (al. 7) (maneno 40-50)
  2. Dondoa hoja muhimu zinazojitokeza katika aya mbili za mwisho. (maneno 40-50) Al.8

SEHEMU: MATUMIZI YA LUGHA

 1. Andika sifa bainifu za sauti (al.4)
  1. /e/ 
  2. /n/
 2. Eleza maana mbili ya sentensi:- (al.2)
  Tumetengeneza barabara
 3. Akifisha sentensi ifuatayo:- (al.3)
  Sijaona kitabu kizuri kama mayai waziri wa maradhi, utaniazima siku ngapi bashiri alimwuliza rita
 4. Changnanua kwa njia ya mishale (al.4)
  Mama anapika na baba akisoma gazeti
 5. Tunga sentensi moja na uonyeshe kwa mstari; (al.3)
  1. Shamirisho kipozi
  2. Shamirisho kitondo
  3. Shamirisho ala/kitumizi
 6. Tungia vitenzi vifuatavyo sentensi katika hali zilizobanwa:- (al.3
  1. Fa(mazoea)
  2. La(kutendeka)
  3. Pa (kutendea)
 7. Tambulisha kishazi tegemezi na kishazi huru (al.2 Wanafunzi walifoanya vyema walituzwa jana
 8. Pambanua viambishi mbalimbali katika sentensi ifuatayo (al.3
  Waliwapendezea
 9. Huku ukitumia mifano ya sentensi eleza matumizi mawili ya kiambishi, ‘ji’ (al.2
 10. Andika udogo wa: (al.2
  Magari yote yaliyobakia yatauzwa na mzee yule mwembamba
 11. Tumia – ‘ako’ katika sentensi kama: (al.3
  1. Kivumishi
  2. Kiwakilishi
  3. Kitenzi
 12. Bainisha matumizi ya “po” katika sentensi ifuatayo:- (al.2
  Alipowasili alionyeshwa walipo.
 13. Andika kwa usemi wa taarifa:- (al.3
  “Wasichana wakielimishwa wataweza kuwa bora kuliko wavulana,” Naibu wa Chansela wa chuo Kikuu aliwaambia mahafala.
 14. Tunga sentensi ambayo ina aina za maneno uliyopewa:-(al.4
  N + V + V + T

SEHEMU YA D.ISIMU JAMII (AL.10)
Lugha ya kiswahili inakabiliwa na matatizo mengi sana. Yataje na kuyaeleza. (AL.10)

SEHEMU E.FASIHI ANDISHI (KIDAGAA KIMEMWOZEA ) ALAMA 20
Maudhui ya kazi yamejadiliwa kwa mapana na marefu. Kwa kurejelea riwaya ya kidagaa jadili kauli hii.MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.    
  • Mwanafunzi aliyeambukizwa Ukimwi
  • Ukimwi vyoni
  • Hofu ya kuambukizwa Ukimwi (yeyote moja =al. 2)
 2. Kuwaambukiza wanafunzi wenzake mia moja na ishirini na wanne virusi vya Ukimwi
 3. Aliambukizwa Ukimwi na mwanfunzi wa chuo hicho ambaye alikuwa akifanya majaribio ya ualimu shuleni mwao
 4.      
  • Apewe adhabu ya kifo
  • Atiwe nguvuni maramoja
  • Tayari amekiri kosa lake na hivyo kumfanya awe na hatia (zozote mbili al. 4)
 5. Maadili hayapo tena katika vyuo vikuu nchini
 6.      
  • Kupoteza tumaini kabisa/kuwa katika taharuki kuu
  • Daima dawamu/ kwa vyovyote vile
  • Kutumia watu wengine kuwatia adhabu kwa kosa lake mwenyewe (1x3=al.3)

Ufupisho

 1. Inawezesha nchi kupata bidhaa ambazo haitengenezi
  • Husaidia kuwepo na uhusiano kati ya nchi mbalimbali
  • Nchi hupata bidhaa kwa bei rahisi kuliko ambavyo ingekuwa kama zingetengenezwa kwao
  • Husaidia wakati nchi imekumbwa na dharura au majanga kwani itasaidiwa na nchi nyingine
  • Huchochea upatikanaji wa nafasi za kazi kwa wengi
  • Nchi inawezesha kupata pesa za kigeni na kuuza bigdhaa za ziada ()
 2. Kuna matatizo yanayozikumbuka nchi za kiafrika katika biashara hii
  • Hutatiza viwanda vichanga katika nchi zinazoedelea kwa ushindani usio sawa huku nchi zilizoendelea zikitumia biashara hii ‘kutupa’ bidhaa za hali ya chini
  • Nchi zinaweka mikakati ya kulinda viwanda vichanga
  • Kuwekwa kwa ushuru wa juu kwa bidhaa zinazoagizwa
  • Kupunguzia viwango vyao ushuru
  • Kuvipa viwanda vyao mikopo
  • Kuhakikisha usafirishaji nafuu wa bidhaa kwa viwanda vyao
  • Kuweka viwango vya bidhaaa zinazoweza kuagizwa kutoka nje kwa kipindi Fulani (6x1=ala.6)
 3. Matumizi ya lugha
  1. andika sifa bainifu za sauti 8x1/2
   1. / e/ – ni Irabu
    hutamkwa midomo ikiwa imetandazwa
    ni irabu ya kati mbele
   2. /n/ – ni konsonanti
    hutamkiwa kwenye ufizi
    nazali
    si ghuna
  2. Eleza maana mbili ya sentensi 1x2
   tumetengeneza barabara
   • Njia
   • Vizuri/ mwafaka/ sawasawa
  3. akifisha sentensi ifuatayo
   Sijaona kitabu kizuri kama mayai waziri wa maradhi ,utaniazima siku ngapi bashiri alimwuliza rita al.3
   “Sijaona kitabu kizuri kama “Mayai waziri wa Maradhi,” Utaniazima siku ngapi?” Bashiri alimwuliza Rita.
  4. changanua kwa njia ya mishale
   Mama anapika na baba akisoma gazeti. (al. 4)
   S → S1 + U + S2
   S1 → KN + KT
   KN → N
   N → Mama
   KT → T
   T → anapika
   U → na
   S2 → KN + KT
   KN → N
   N → baba
   KT → T+N
   T → akisoma
   N → gazeti
  5. Tunga sentensi moja na uonyeshe kwa mstari al.3
   1. shamirisho kipozi
   2. shamirisho kipozi
   3. shamirisho ala/kitumizi
    Hakiki jibu la mwanafunzi.
    k.m. Ziada alimfagilia mama nyumba kwa ufagio
    Nyumba – kipozi, mama-kitondo- ufagio – ala/kitumizi
  6. tungia vitenzi vifuatavyo sentensi katika hali zilizobanwa al.3
   1. Fa (mazoea) k.m. watu hufa kwa maradhi mbalimbali
   2. La(kutendeka) k.m. Chakula hiki hulika upesi.
   3. Pa(kutendea ) k.m Alinipea mtoto maziwa nilipochelewa kazini (kwa niaba yangu )
  7. tambulisha kishazi tegemezi na kishazi huru ..al.2
   • wanafunzi waliofanya vyema walituzwa jana
   • Wanafunzi waliofanya vyema – kishazi tegemezi
   • Walituzwa jana- kishazi huru
  8. pambanua viambishi mbalimbali katika sentensi ifuatayo al.3
   waliwapendezea
   wa – nafsi
   li – wakati
   wa – nafsi (mtendewa)
   pend – mzizi .shina
   eze- kauli/kinyambuzi
   a – kiishio 6x ½ = 3)
  9. huku ukitumia mifano ya sentensi ,eleza matumizi mawili ya kiambishi ‘ji’ al.2
   • kuonyesha ukubwa
    Jia la kuingia ikulu limefungwa
   • Kiambishi cha kurejelea mtenda
    Rehema anajitahidi sana.
  10. andika udogo wa:
   magari yote yaliyobakia yatauzwa na mzee yule mwembamba al.2
   Vigaari vyote vilivyobakia vitauzwa na kizee kile chembamba
  11. tumia –‘ako’katika sentensi kama: al.3
   1. kivumishi
   2. kiwakilishi
   3. kitenzi
    1. Darasa lako ni safi.
    2. Chako kinapendeza sana.
    3. Watoto wako uwanjani
  12. bainisha matumizi ya ‘po’katika sentensi ifuatayo .al.2
   alipowasili alionyeshwa walipo
   po- ya kwanza wakati
   po -ya pili-mahali
  13. andika kwa usemi wa taarifa
   ‘‘Wasichana wakielimishwa wataweza kuwa bora kuliko wavulana,’’Naibu wa chansela wa chuo kikuu aliwaambia mahafala.
   Naibu wa Chansel wa chuo kikuu aliwaambia mahafala kuwa wasichana wakielimishwa
   wangeweza kuwa bora kuliko wavulana.
  14. tunga sentensi ambayo ina aina za maneno uliyopewa .al.4
   N+V+V+t+N+V
   Mtoto wetu mdogo ni mwanafunzi bora . (Mwalimu akadirie)

ISIMU JAMII       

 • Ushindani kutoka lugha nyingine kama kiingereza
 • Hadhi – Kiswahili kimedunishwa
 • Athari za lugha ya mama
 • Mitazamo hasi kuhusu Kiswahili
 • Kutokuwepo kwa sera mwafaka kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa muda mrefu
 • Kuhusishwa kwa lugha ya Kiswahili na dini ya kiislamu/ eneo la pwani
 • Wamishenari walieneza dini zao kwa lugha ya kiingereza
 • Kutokouwa na vitabu vya kutosha vilivyoandikwa kwa Kiswahili
 • Uchache wa wataalamu wa lugha ya Kiswahili
 • Mkazo wa ufundishaji wa lugha za kikabila katika shule za msingi
 • Kuwepo kwa sheria katika shule kuwa Kiswahili kizungumzwe siku moja kwa juma
 • Lugha imetengwa katika matumizi ofisini za kiserikali

FASIHI kidagaa kimemwozea
Maudhui ya kazi yamejadiliwa kwa mapana na marefu katika riwaya ya kidagaa kimemwozea.Jadili ukweli wa kauli hii 10x2

 • Nasaba Bora alifanya kazi kama karani wa mzungu katika enzi za kikoloni
 • DJ anafuga ng’ombe kwa Bw.Maozi
 • Amani ni mfanyakazi katika boma la Nasaba Bora ;hukama ng’ombe na kuwapeleka malishoni
 • Imani ni mfanyakazi katika boma la Majisifu nduguye Nasaba Bora
 • Baada ya Madhubuti kutoka Urusi ,alipata kazi za uhasibu katika kampuni ya mawakili mjini Songoa
 • Wanajeshi katika hadithi hii wana jukumu la kulinda nchi yao kwani baadhi yao wanafia vitani
 • Majisifu ni mwalimu katika shule ya Nasaba Bora,aliwahi kuwa mhariri wa gazeti la Tomoko leo ,mhadhiri wa chuo kikuu..
 • Askari wanafanya kazi ya kulinda usala ;jelani,kufunga na kufungia Mtemi lango anapopita kwa gari lake
 • Babake Fao alikuwa meneja wa benki mjini Ulitima
 • Mamake Fao ni mwalimu wa historia katika shule ya upili
 • Watangazaji katika kituo chao redio ambao wanasaidia askari na wasikilizaji wengine kujua kuhusu kandanda kati ya timu ya Songoa FC na Meza Wembe.

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 4 Mid Term 2 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest