MAAGIZO KWA MTAHINIWA:
- Karatasi hii ina maswali manne.
- Jibu maswali mawili pekee. Kila swali lina alama ishirini.
- Swali la kwanza ni la lazima.
- Chagua swali lingine lolote moja kutoka yale matatu yaliyosalia.
- Wewe ni katibu wa chama cha Kiswahili shuleni mwenu. Chama chenu kimefanya mkutano kuhusu changamoto zinazokabili Kiswahili shuleni mwenu. Andaa kumbukumbu za mkutano huo.[Alama 20]
- Jadili mikakati ambayo sharti itiliwe maanani ili kukabiliana na changamoto za utumizi na wenezi wa dawa za kulevya nchini Kenya. [Alama 20]
- Simulia kisa ili kuthibitisha maana ya methali ifuatayo: Mui huwa mwema. [Alama 20]
- Maliza insha yako kwa:[Alama 20]
…..na hapo ndipo nilipong’amua kuwa, mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.

MARKING SCHEME
Swali la kwanza.
- Kuibuka kwa lugha ya sheng
- Uhaba wa vitabu
- Vipindi vichache tukilinganisha na kingereza
- Ukosefu wa vielelezo mwema
- Mtazamo hasi kwa wana lugha
- Unenaji wa kingereza kutiwa shangwe zaidi kama lugha rasmi shuleni.
- Ukosefu wa sera madhubuti kwa Kiswahili shuleni.
- Maktaba zimeshughulikia vitabu vya kingereza
- Vyombo vya habari (kingereza)
- Mipango michache ya kutafitiki Kiswahili
Swali la pili.
- Wana kuelimisha vizuri kuhusu madhara yaletwayo na dawa za kulevya.
- Kubuni sheria kali kwa wanaotumia.
- Kufunza askari wa kupambana na walanguzi wa dawa za kulevya.
- Wazazi kufuata nidhamu ya watoto wao wakati wa likizo.
- Kuadhibu vikali wauzaji wa dawa za kulevya.
- Watumizi wa dawa za kulevya kupewa nasaha na wasHika dau husika.
Swali la tatu.
- Ni sharti mtahiniwa atoe maana ya ndani na nje ya methali. Kisha asimulie kisa kitakachooana na methali.
Swali la nne.
- Ni sharti mtahiniwa ahitimishe kwa kipengele alichopewa.
- Kisa atakachosimulia ni sharti kioane na kipengele alichopewa.
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 Term 1 Opener Exams 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates