Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 4 Term 1 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp
MAAGIZO
 • JIBU MASWALI YOTE KATIKA NAFASI ZILIZOACHWA
 1. UFAHAMU (ALAMA 15)
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali

  Ni bayana kuwa mtoto wa kike humu nchini anabaguliwa tangu akiwa malaika.  Tamaduni za jamii nyingi nchini humbagua mtoto wa kike katika masuala ya elimu na umiliki wa mali. Ndoa za  mapema pamoja na ajira ya watoto wa kike pia huchangia katika kumdhalalisha na kumdunisha mtoto wa msichana. Kadhalika, tamaduni zilizopitwa na wakati hasa tohara kwa wasichana huiathiri mno jinsia ya kike.

  Kutokana na dharura, wanasiasa, wasomi, viongozi wa kidini miongoni mwa wengine, wameanza kutambua haja ya kumpa mtoto wa kike fursa sawa na mwenzake wa kiume.  Wengi wa walio katika mstari wa mbele kupigania haki hizi ni wasomi wanawake.  Msomi mmoja ambaye ametekeleza wajibu mkuu ni Daktari Momanyi wa chuo kikuu cha Kenyatta.  Daktari huyu anaamini kwamba kumwelimisha msichana ni kumpa uwezo zaidi wa kukabiliana na matatizo ya kila siku yanayomkumba.

  Daktari huyu hutumia mbinu gani kufanikisha malengo yake? “Mimi hutumia fasihi ya Kiswahili katika kumtetea mtoto wa kike,” anasema. Anaamini kwamba fasihi ni chombo muhimu na chenye uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko katika jamii.  Mojawapo ya hadithi zake fupi “Ngome ya nafsi” kwenye mkusanyiko wa hadithi fupi, “Mayai waziri wa maradhi na hadithi nyingine” uliohaririwa na K.W Wamitila, Daktari anaangazia madhila yanayomkumba mtoto wa kike hasa ndoa za lazima.

  “Wakati wa kumfungia mtoto wa kike katika duara dogo la jikoni umepitwa na wakati” anakariri Daktari Momanyi.  Juhudi za msomi huyu katika kumtetea mtoto wa kike zimetambuliwa katika ulingo wa kimataifa. Mbali na kushikilia nyadhifa mbalimbali katika mashirika ya mataifa yanayotetea haki na nafasi ya mwanamke katika jamii, Daktari alifadhiliwa na shirika la Fullbright mwaka 2006.  Ufadhili huo ulimwezesha kufanya utafiti kuhusu ufundishaji wa Kiswahili katika  chuo kikuu cha Pennsylvania, Philadelphia nchini Marekani.

  Aliendelea kufanya utafiti kuhusu jinsia alipofadhiliwa na shirika la OSSREA kumwezesha kufanya utafiti kuhusu maswala ya jinsia. Katika utafiti huo alichunguza imani za kijamii na kitamaduni zinazochangia tofauti za kiidadi masomoni baina ya mtoto wa kike na wa kiume miongoni mwa jamii ya waislamu mkoani pwani.  Daktari anatoa wito kwa serikali kubuni sera mahususi inayotambua usawa baina ya mtoto wa kike na wa kiume.  Msomi huyu amechapisha vitabu kadha wa kadha na makala mengi ya kitaalamu kuhusu uana katika majarida barani Afrika, Ulaya, Marekani na Asia. Alisomea katika chuo kikuu cha Nairobi ambapo alijipatia shahada ya ualimu kisha alituzwa shahada ya uzamili na huko chuo kikuu cha Kenyatta akapata shahada ya uzamifu.
  MASWALI 
  1. Yape makala haya anwani mwafaka. (alama 1)
  2. Mbali na elimu, umiliki wa mali, ndoa za lazima na mapema, ni vipi vingine anavyodhulumiwa mtoto wa kike? (alama 2)
  3. Taja washikadau wengine wanaopigania haki za watoto wa kike. (alama 2)
  4. . Ni vipi fasihi ya Kiswahili ilivyopata nafasi katika utetezi huu? (alama 2)
  5. Je, ni silaha ipi itamwezesha mtoto wa kike kujihami dhidi ya ubaguzi huu. (alama 1)
  6. Taja wafadhili wawili wa Daktari Momanyi. (alama 2)
  7. Idadi kubwa ya wavulana ikilinganishwa na wasichana shuleni inasababishwa na nini? (alama 2)
  8. Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika makala haya. (alama 3)
   1. Utafiti
   2. Uana
   3. Sera
 2. UFUPISHO (ALAMA 15)
  Soma makala haya  kisha ujibu maswali yanayofuatia

  Mwelekeo wa utoaji mafunzo kwa mwalimu wa shule za sekondari nchini unazua mjadala.  Hatua katika Nyanja hizi zinaonekana kuchukuliwa bila kutilia maanani utabiri wa idadi katika siku za usoni.

  Hapo miaka ya tisini, walimu wengi waliohitimu katika shahada za digrii na diploma hawakuegemea upande wa hesabati, sayansi na lugha (kingereza na Kiswahili). Hivyo kukazuka kampeni za chini kwa chini katika vyuo vya nchi ambapo walimu – wanafunzi walihimizwa kusomea Hesabati, Sayansi na lugha.  Hili lilionekana kuwa suluhu kwa wakati ule kwani punde idadi ya walimu hawa iliyokuwa imepungua ilionekana kuongezeka.  Ni wakati huu ambapo walimu wa masomo haya walipewa marupurupu maalum maarufu kwa jina “special allowance” kwenye mishahara yao.

  Idara za Dini, Historia na masomo mengine husika zilipuuzwa na idadi ya wanafunzi waliojisajili hapa kupunguka kabisa.  Wanafunzi katika idara hizi walionekana kutokuwa na matumaini ya kuajiriwa kwani wenzao waliokwisha hitimu walikuwa wengi kupindukia.

  Hali hii ilidumishwa na miaka ya karibuni imeshuhudia tatizo lingine tofauti;  uhaba wa walimu wa Dini na Historia na ongezeko kubwa la walimu wa Hesabati, Sayansi na lugha. Dalili zake ni ukweli kwamba shule nyingi hazina walimu wa kutosha katika Dini na Historia na zinapotangaza nafasi hizi kuwa wazi, hakuna wanaojitokeza kuzichukua. Miongoni mwa walimu waliohitimu na wanaosaka nafasi za kazi, asilimia kubwa zaidi ni wa Hesabati, Sayansi na lugha. Swali ni ‘je, kwa nini mambo yabadilike haraka jinsi hii?’

  Lawama zote zafaa kurudikiwa wizara ya Elimu hasa idara zinazohusika na tarakimu na utoaji wa mafunzo kwa elimu hasa idara zinazohusika na tarakimu na utoaji wa mafunzo kwa walimu.  Kwa kufuata njia za kitaalamu, inawezekana kukadiria idadi ya walimu watakaohitajika katika masomo mbalimbali kwa kipindi cha miaka hamsini au hata zaidi. Maafisa katika idara hizi wafaa kuwajibika na kutoa mwelekeo dhabiti ili kuiepushia nchi matatizo kama haya.
  1. Fupisha aya ya kwanza na ya pili kwa maneno 50. (alama 6, mtiriko 1)
   Nakala chafu
   Nakala safi
  2. Ni hoja zipi muhimu zinazojitokeza katika aya tatu hadi ya mwisho. (alama 7, mtiririko 1)
   Nakala chafu
   Nakala safi
 3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1. Taja mifano miwili ya sauti za mdomo – meno. (alama 3)
  2. Taja irabu mbili za juu. (alama 2)
  3. Tambua aina za nomino katika sentensi hizi. (alama 2)
   1.   Abdi alijiunga na halaiki ya watu.
   2. Kupigwa kwake kulisababishwa na ujeuri wake.
  4. Andika ukubwa na wingi wa sentensi hii. (alama 2)
   Sahani hii imevunjwa na mtoto huyu.
  5. Andika kinyume cha sentensi hii. (alama 2)
   Mama hushona nguo ikapendeza.
  6. Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mawili ya neno. (alama 2)
   Mchanga
  7. Tenganisha silabi katika neno. (alama 2)
   Ghadhabishwa
  8. Andika sentensi hizi upya ukitumia visawe vya maneno yaliyopigwa msitari. (alama 2)
   1. Ole Matope alishtuka alipomwona nyati kichakani.
   2. Wanafunzi wako karibu kurudi shuleni baada ya gonjwa la korona kudhibitishwa.
  9. Je, ni nini maana ya mofimu ? (alama 1)
  10. Onyesha na uainishe mofimu katika neno hili. (alama 3)
   Tuliwapikisha
  11. Changanua sentensi hii kwa njia ya matawi. (alama 3)
   Mkoba mkubwa mweusi ulipotea jana.
  12. Tambua shamrisho katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
   Mhunzi alimjengea mkulima jembe kwa chuma.
  13. Anika sentensi ifuatayo katika usemi halisi. (alama 2)
   Mama aliambia Juma asitoke nje ya nyumba baada ya yeye kwenda sokoni.
  14. Andika sentensi hizi katika minyambuliko iliyo mabanoni. (alama 2)
   1. Mama alimfanya mtoto ale. (kutendesha)
   2. Maria alifagia chumba vizuri. (kitendewa)
  15. Kanusha sentensi ifuatayo. (alama 2)
   Angeenda sokoni angenunua nyanya nyingi.
  16. Andika wingi wa sentensi hizi. (alama 2)
   1. Ubawa wa ndege huyo ulivunjika akitua.
   2. Sonara yule alitengeneza pambo zuri.
  17. Namino hizi ni za ngeli gani ? (alama 2)
   1. Asali
   2. Mkeka
  18. Ina maana gani kusema kuwa mtu alikubali jambo ‘shingo upande’. (alama 1)
  19. Kamilisha methali hizi. (alama 2)
   1. Mwenye shibe
   2. Usikate kanzu
  20. Sahihisha sentensi hii. (alama 1)
   Chakula  tulizokula zilitushibisha.
 4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
  Halooo! Wapi hapo …………….
  Una …….Unasikia …………. (Anasikiliza kwa makini)
  Aaaaa! Kamishna Herderson.
  Ok! Ok! Ha! Hatoboi.
  Ningekwambia but….. Atoe chai. 

  1. Tambua rejesta hii ya lugha. (alama 1)
  2. Andika sifa zozote tano za sajili hii. (alama 5)
  3. Ni nani dhima ya lugha ? (alama 4)

MARKING SCHEME

   • Mtoto wa kike/ Usawa wa Kijinsia/ Haki za watoto wa kike.
  2. Mbali na elimu, umiliki wa mali, ndoa za lazima na mapema, ni vipi vingine anavyodhulumiwa mtoto wa kike? (alama 2)
   • Tohara za utamaduni
   • Kufungiwa katika duara dogo la jikoni
  3. Taja washikadau wengine wanaopigania haki za watoto wa kike. (alama 2)
   1. Wanasiasa
   2. Viongozi wa dini
   3. Mashirika wafadhili  zozote mbili (1x2=2)
  4. . Ni vipi fasihi ya Kiswahili ilivyopata nafasi katika utetezi huu? (alama 2)
   • Fasihi ya Kiswahili ni chombo muhimu na chenye uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko katika jamii
  5. Je, ni silaha ipi itamwezesha mtoto wa kike kujihami dhidi ya ubaguzi huu. (alama 1)
   • Elimu/Kuelimisha
  6. Taja wafadhili wawili wa Daktari Momanyi. (alama 2)
   • Shirika la OOSREA
   • Shirika la Fullbright 2006
  7. Idadi kubwa ya wavulana ikilinganishwa na wasichana shuleni inasababishwa na nini? (alama 2)
   • Imani za kijamii na kitamaduni
  8. Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika makala haya. (alama 3)
   1. Utafiti - uchunguzi/ udadisi
   2. Uana - Jinsia
   3. Sera - mpango maalum wa kufanyia jambo
 2. UFUPISHO (ALAMA 15)
  Soma makala haya  kisha ujibu maswali yanayofuatia

  Mwelekeo wa utoaji mafunzo kwa mwalimu wa shule za sekondari nchini unazua mjadala.  Hatua katika Nyanja hizi zinaonekana kuchukuliwa bila kutilia maanani utabiri wa idadi katika siku za usoni.

  Hapo miaka ya tisini, walimu wengi waliohitimu katika shahada za digrii na diploma hawakuegemea upande wa hesabati, sayansi na lugha (kingereza na Kiswahili). Hivyo kukazuka kampeni za chini kwa chini katika vyuo vya nchi ambapo walimu – wanafunzi walihimizwa kusomea Hesabati, Sayansi na lugha.  Hili lilionekana kuwa suluhu kwa wakati ule kwani punde idadi ya walimu hawa iliyokuwa imepungua ilionekana kuongezeka.  Ni wakati huu ambapo walimu wa masomo haya walipewa marupurupu maalum maarufu kwa jina “special allowance” kwenye mishahara yao.

  Idara za Dini, Historia na masomo mengine husika zilipuuzwa na idadi ya wanafunzi waliojisajili hapa kupunguka kabisa.  Wanafunzi katika idara hizi walionekana kutokuwa na matumaini ya kuajiriwa kwani wenzao waliokwisha hitimu walikuwa wengi kupindukia.

  Hali hii ilidumishwa na miaka ya karibuni imeshuhudia tatizo lingine tofauti;  uhaba wa walimu wa Dini na Historia na ongezeko kubwa la walimu wa Hesabati, Sayansi na lugha. Dalili zake ni ukweli kwamba shule nyingi hazina walimu wa kutosha katika Dini na Historia na zinapotangaza nafasi hizi kuwa wazi, hakuna wanaojitokeza kuzichukua. Miongoni mwa walimu waliohitimu na wanaosaka nafasi za kazi, asilimia kubwa zaidi ni wa Hesabati, Sayansi na lugha. Swali ni ‘je, kwa nini mambo yabadilike haraka jinsi hii?’

  Lawama zote zafaa kurudikiwa wizara ya Elimu hasa idara zinazohusika na tarakimu na utoaji wa mafunzo kwa elimu hasa idara zinazohusika na tarakimu na utoaji wa mafunzo kwa walimu.  Kwa kufuata njia za kitaalamu, inawezekana kukadiria idadi ya walimu watakaohitajika katika masomo mbalimbali kwa kipindi cha miaka hamsini au hata zaidi. Maafisa katika idara hizi wafaa kuwajibika na kutoa mwelekeo dhabiti ili kuiepushia nchi matatizo kama haya.
  1. Fupisha aya ya kwanza na ya pili kwa maneno 50. (alama 6, mtiriko 1)
   • Mwelekeo wa mafunzo ya walimu wa sekondari wazua mjadala
   • Mahitaji ya baadaye ya walimu hayatiliwi maanani
   • Miakani ya tisini, waliohitimu hawakutegemea masomo ya hisibati, sayansi na lugha
   • Hivyo kampeni zikawa za kuhimiza walimu kusomea masomo hayo
   • Ilikuwa suluhu ya muda kwani walimu waliohitajika waliongezeka
   • Waalimu hawa walipewa nyongeza katika mishahara yao (Hoja 6x1=6)
  2. Ni hoja zipi muhimu zinazojitokeza katika aya tatu hadi ya mwisho. (alama 7, mtiririko 1)
   • Idadi ya waliosomea masomo haya mengine ilipunguka
   • Walionekana kutokuwa na matumaini ya kuajiriwa
   • Hali hii iliendelea na tatizo lingine likachipuka
   • Walimu wa Dini na Historia waliadimika
   • Walimu wa Sayansi, Hisisbati na Lugha wakaongezeka na kukosa kazi
   • Wizara ya elimu kulaumiwa kwa kutokadiria idadi ya walimu watakaohitajika
   • Maafisa wapaswa kutoa mwelekeo ili kuepuka matatizo haya (Hoja 7x1=7)
 3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1. Taja mifano miwili ya sauti za mdomo – meno. (alama 3)
   1. /f/
   2. /v/
  2. Taja irabu mbili za juu. (alama 2)
   1. /i/
   2. /u/
  3. Tambua aina za nomino katika sentensi hizi. (alama 2)
   1. Abdi alijiunga na halaiki ya watu.
    • Abdi - Nomino ya pekee
    • halaiki ya watu - Nomino ya jamii/makundi
   2. Kupigwa kwake kulisababishwa na ujeuri wake.
    • Kupigwa - Nomino ya kitenzi jina/kitenzi-nomino
    • ujeuri - Nomino dhahania
  4. Andika ukubwa na wingi wa sentensi hii. (alama 2)
   Sahani hii imevunjwa na mtoto huyu.
   • Majisahani haya yamevunjwa namajitoto/matoto haya.
  5. Andika kinyume cha sentensi hii. (alama 2)
   Mama hushona nguo ikapendeza.
   • Mama hushonoa nguo ikachukiza
  6. Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mawili ya neno. (alama 2)
   Mchanga
   • Mtoto mchanga alichezea mchanga wa kujenegea nyumba.
    (mtahini ahakiki jibu la mtahiniwa)
  7. Tenganisha silabi katika neno. (alama 2)
   Ghadhabishwa
   • Gha-dha-bi-shwa
  8. Andika sentensi hizi upya ukitumia visawe vya maneno yaliyopigwa msitari. (alama 2)
   1. Ole Matope alishtuka alipomwona nyati kichakani.
    • Ole matope alishangaa/alimaka alipomwona mbogo kichakani.
   2. Wanafunzi wako karibu kurudi shuleni baada ya gonjwa la korona kudhibitishwa.
    • Wanagenzi wako karibu kurudi skulini baada ya gonjwa la korona kudhibitishwa
  9. Je, ni nini maana ya mofimu ? (alama 1)
   • Mofimu ni kipashio kidogo cha neno chenye maana ya kisarufi
  10. Onyesha na uainishe mofimu katika neno hili. (alama 3)
   Tuliwapikisha
   • Tu- Watenda nafsi ya kwanza wingi
   • li - wakati
   • wa - watendewa/ shamirisho, nafsi ya tatu/ pili wingi
   • pik - mzizi wa kitenzi
   • ish - mnyambuliko kauli ya kutendesha
   • a - kiishio/ kimalizio
  11. Changanua sentensi hii kwa njia ya matawi. (alama 3)
   Mkoba mkubwa mweusi ulipotea jana.
   SwaF42023T1Ansk
  12. Tambua shamrisho katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
   Mhunzi alimjengea mkulima jembe kwa chuma.
   • mkulima - shamirisho kitondo
   • jembe - shamirisho kipozi
   • chuma - shamirisho ala
  13. Anika sentensi ifuatayo katika usemi halisi. (alama 2)
   Mama aliambia Juma asitoke nje ya nyumba baada ya yeye kwenda sokoni.
   • Mama alimwambia Juma," Usitoke nje ya nyumba baada ya mimi kwenda sokoni.
  14. Andika sentensi hizi katika minyambuliko iliyo mabanoni. (alama 2)
   1. Mama alimfanya mtoto ale. (kutendesha)
    • Mama alimlisha mtoto
   2. Maria alifagia chumba vizuri. (kitendewa)
    • Chumba kilifagiliwa vizuri na Maria
  15. Kanusha sentensi ifuatayo. (alama 2)
   Angeenda sokoni angenunua nyanya nyingi.
   • Asingeenda sokoni asingenunua nyanya nyingi
  16. Andika wingi wa sentensi hizi. (alama 2)
   1. Ubawa wa ndege huyo ulivunjika akitua.
    • Mbawa za ndege hao zilivunjika wakitua
   2. Sonara yule alitengeneza pambo zuri.
    • Masonara wale walitengeneza mapambo mazuri
  17. Namino hizi ni za ngeli gani ? (alama 2)
   1. Asali
    • I-I
   2. Mkeka
    • U-I
  18. Ina maana gani kusema kuwa mtu alikubali jambo ‘shingo upande’. (alama 1)
   • Kukubali bila kuwa na uhakika
   • Kukubali kwa kusitasita
  19. Kamilisha methali hizi. (alama 2)
   1. Mwenye shibe hamjui mwenywe njaa
   2. Usikate kanzu kabla ya mwana kuzaliwa
  20. Sahihisha sentensi hii. (alama 1)
   Chakula  tulizokula zilitushibisha.
   • Chakula tulichokula kilitushibisha
 4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
  Halooo! Wapi hapo …………….
  Una …….Unasikia …………. (Anasikiliza kwa makini)
  Aaaaa! Kamishna Herderson.
  Ok! Ok! Ha! Hatoboi.
  Ningekwambia but….. Atoe chai. 

  1. Tambua rejesta hii ya lugha. (alama 1)
   • Mazungumzo ya simu
  2. Andika sifa zozote tano za sajili hii. (alama 5)
   • Utohozi k.m kamishna
   • mdokezo k.m una...
   • Lugha mseto/ kuchanganya ndimi OK
   • Lugha ya mkato
   • Sentensi fupifupi
   • misimu mf. hatoboi  (zozote 5x1=5)
  3. Ni nani dhima ya lugha ? (alama 4)
   • Mawasiliano
   • Huleta umoja - kuunganisha watu
   • Huziba tofauti zilizoko kati ya jamii tofauti
   • Hukuza mila na tamaduni za jamii
   • Hutambulisha watu kutoka jamii mbalimbali
   • Huleta maendeleo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kisayansi
   • Huwezesha kazi kufanyika kwa pamoja na kunufaisha jamii nzima
   • Hutumiwa kusambaza habari katika vyombo vya habari
   • Hutumika kufunzia shuleni au kama somo.   (Hoja zozote 4x1=4)

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 4 Term 1 Opener Exams 2023.

Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students

Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest