Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 Term 1 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp

Instructions

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani: Riwaya, Ushairi na Tamthilia.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.

SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI

  1. Lazima.
    Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.Maulana alikuwa amewatunukia mapenzi si haba.Makazi yao yalikuwa yamepambwa yakapambika.Walitegemea matunda mbalimbali yaliyokuwa baharini kama mapera, matomoko matikitimaji na kadhalika.

    Siku moja usiku wa manane, maji yakaanza kupwa.Ndovu aliathirika zaidi. Alijaribu kuinama majini lakini hakuweza . Alimwita sungura amsaidie lakini sungura alikuwa ametoweka. Ndovu aliamua kwenda kumtafuta sungura. Alimtafuta hadi msituni lakini hakumpata. Alihofia kurudi baharini na hadi wa leo yumo msituni.
    Maswali
    1. Tambua utanzu na kijipera chake. (al.2)
    2. Taja fomyula zingine mbili za kutanguliza kifungu hiki. (al.2)
    3. Eleza umuhimu wa kijipera hiki. (al.5)
    4. Eleza sifa za kifungu hiki. (al.5)
    5. Eleza umuhimu wa fomyula:
      1. Kutanguliza (al.3)
      2. Kuhitimisha (al.3)

SEHEMU B: TAMTHILIA
Pauline Kea: Kigogo

  1.  “Kubali pendekezo letu la kufungwa kwa soko… huoni hii ni fursa nzuri ya kulipiza kisasi? Najua umekuwa ukimmezea mate…’’
    1. Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
    2. Bainisha vipengele viwili vya kimtindo katika dondoo hili. (alama 4)
    3. Kufungwa kwa soko ni ukatili. Mbali na ukatili huu, toa mifano mingine ya ukatili kwenye tamthilia. (alama 6)
    4. Msemaji wa maneno haya ni mshauri mbaya. Thibitisha kauli hiyo kwa kurejelea mifano yoyote sita katika tamthilia ya Kigogo (alama 6)
      Au
  2. “Wananchi katika mataifa ya Afrika wanakumbwa na tatizo la uongozi mbaya.” Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa mujibu wa Tamthilia. (alama 20)

SEHEMU YA C: RIWAYA
Assumpta K. Matei: Chozi la Heri

  1. Kipi kinachowavuta raia kuhamia ughaibuni? Angeuliza nafsi yake pale ambapo mzigo wa simanzi na ukiwa ulipokilemea kifua chake. Je, ni huo mshahara mnono unaowageuza kuwa watumwa wa kufanya kazi kidindia ati kwa kudai kuwa nchi za ughaibuni ni twenty-four-hour economies?
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
    2. Huku ukitolea mifano maridhawa, fafanua mbinu nne za kimtindo zinazojitikeza katika dondoo hili (Alama 4)
    3. Eleza changamoto inayomkumba msemaji katika dondoo hili. (Alama 2)
    4. Fafanua jinsi maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili yameshughulikiwa kwingineko riwayani. (Alama 4)
    5. Fafanua umuhimu wa mandhari katika kuijenga riwaya hii kwa kurejelea Msitu wa Mamba (Alama 8)

      Au
  2. Eleza jinsi maudhui ya ufisadi yalivyoshughulikiwa katika riwaya ya Chozi la Heri. (al 20)

SEHEMU D: USHAIRI

  1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

    KAMA SODOMA!
    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Haihitaji makini, kwa mwenye macho mazima
    Utaona walakini, mradi ukitizama
    Wanazini hadharani, wana kwa watu wazima
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini.

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Wanazini hadharani, wana kwa watu wazima
    Wanatafuna maini, vijana na kina mama
    Hawana haya nyusoni, wameharamisha wema
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini.

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Hawana haya nyusoni, wameharamisha wema
    Baba na binti ndani, wanacheza lelemama
    Marijali wa mbioni, kujipagaza umama
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini.

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Marijali wa mbioni, kujipagaza umama
    Wameikataa dini, toka tumboni mwa mama
    Wadai Wataliani, watajirisha mapema
    Yafanana na sodoma, mji yetu kwa yakini.

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Wadai ufirauni, watajirisha mapema
    Hivyo mambo ya kigeni, yametunukiwa dhima
    Uwaonapo fuoni, nusu uchi wa mnyama
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini.

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Uwaonapo fuoni, nusu uchi wa mnyama
    Watu hawana imani, umezidi uhasama
    Na viongozi wa dini, kuabudu darahima
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini.

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama sodoma!
    Na viongozi wa dini, kuabudu darahima
    Wamekeuka yamini, kati yao na Rahima
    Wamemuasi Manani, na kusahau kiyama
    Yafanana na sodoma, miji yetu kwa yakini.

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Wamemuasi manani, na kusahau kiyama
    Ya Illahi tuauni, tuwe watu maamuma
    Tukue katika dini, siku zetu za uzima
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini.

    Maswali
    1. Bainisha bahari ya shairi hili ukijikita katika ruwaza zifuatazo (alama3)
      1. Mishororo
      2. Maneno
      3. Vina
    2. Eleza muundo wa shairi hili (alama4)
    3. Bainisha mbinu zifuatazo za kimtindo katika shairi hili (alama3)
      1. Tashbihi
      2. Taswira
      3. Tasfida
    4. Eleza toni ya shairi hili (alama1)
    5. Bainisha nafsi nenewa katika shairi hili (alama1)\
    6. Fafanua dhamira ya mtunzi wa shairi hili (alama2)
    7. Andika ubeti watatu kwa lugha tutumbi (alama4)
    8. Fafanua maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa na mshairi (alama2)
      1. Manani
      2. Marijali

        Au
  2. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Maendeleo ya umma
    Sio vitu maghalani
    Kama tele vimesaki
    Lakini havishikiki
    Ama havikamatiki
    Bei juu

    Maendeleo ya umma
    Sio vitu gulioni
    Kuviona madukani
    Kuvishika mikononi
    Na huku wavitamani
    Kama tama ya fisi
    Kuvipata ng’o

    Maendeleo ya umma
    Sio vitu shubakani
    Dhiki ni kwa mafakiri
    Nafuu kwa mafakiri
    Ni wao tu washitiri
    Huo ni uistimari
    Lo! Warudia

    Maendeleo ya umma
    Ni vitu kumilikiwa
    Na wanyonge kupatiwa
    Kwa bei kuzingatiwa
    Bila ya kudhulumiwa
    Na hata kuhadaiwa
    Hiyo ni haki.

    Maendeleo ya umma
    Dola kudhibiti vitu
    Vijapo nchini mwetu
    Na kuwauzia watu
    Toka nguo na sapatu
    Pasibakishiwe na kitu
    Huo usawa.

    Maendeleo ya umma
    Watu kuwa na kauli
    Katika zao shughuli
    Vikaoni kujadili
    Na mwisho kuyakubali
    Maamuzi halali
    Udikteta la.

    Maendeleo ya umma
    Watu kuwa waungwana
    Vijakazi na watwana
    Nchini kuwa hakuna
    Wote kuheshimiana
    Wazee hata vijana.
    Maswali
    1. Eleza dhamira ya shairi hili. (al.2)
    2. Baininsha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (al.2)
    3. Eleza umuhimu wa usambamba katika shairi hili. (al.2)
    4. Onyesha jinsi maendeleo ya umma yalivyo kinaya. (al.2)
    5. Eleza mambo ambayo mshairi anachukulia kuwa maendelo halisi ya umma. (al.4)
    6. Tambua matumizi ya mistari mishata kwa kutolea mifano. (al.2)
    7. Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (al.1)
    8. Fafanua toni ya shairi hili. (al.1)
    9. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (al.4)


MARKING SCHEME

SEHEMU A : FASIHI SIMULIZI (Lazima)
  1.  
    1.  
      • Utanzu – Hadithi      (1x1)
      • Kipera – Ngano za usuli   (1x1)
    2.  
      1. Fanani : paukwa
        Hadhira : pakawa
      2. Fanani : Hadithi! Hadithi
        Hadhira : Hadithi njoo
    3.  
      1. Huburudisha wanajamii husika
      2. Huelekeza wanajamii husika
      3. Huelimisha wanajamii husika
      4. Huhifadhira huziona ya jamii husika
      5. Huonya wanajamii wa jamii husika
      6. Hujenga ushirikiano wa jamii husika
      7. Hujenga kumbukumbu ya wanajamii.   zozote (5x1)
    4.  
      1. Huhusisha wahusika wanyama
      2. Wanyama hupewa tabia za binadamu
      3. Huwa na ucheshi mwingi
      4. Hutoa matumaini kwa wanyonge kwamba mwishowe watakuwa washindi
      5. Hutoa maadili na kuonya kwa njia ya kuchekesha isiyoumiza. Zozote 5x1
    5.  
      1. Umuhimu wa fomyula ya kutanguliza
        • Humtambulisha mtambaji
        • Huvuta makini ya hadhira
        • Hutoa hadhira kutoka ulimwengu halisi hadi wa ubunifu
        • Hutofautisha kipera cha hadithi na vipera vingine
        • Huashiria mwanzo wa hadithi
        • Hushirikisha mtambaji na hadhira. zozote 3x1
      2. FOMYULA YA KUHITIMISHA
        • Hupisha shughuli nyinginezo
        • Huashiria mwisho wa hadithi
        • Hutoa funzo kwa hadithi
        • Humpisha mtambaji mwingine
        • Hupumzisha hadhira
        • Hutoa hadhira kutoka ulimwengu wa hadithi hadi ulimwengu halisi. Zozote 3x1

SEHEMU B:TAMTHILIA YA KIGOGO ( PAULINE KEA)

SWALI LA PILI 

  1.  
    1. Maneno haya ni ya sauti ya mzee Kenga 
    2. mawazoni mwa Majoka. 
    3. Haya yanatendeka katika ofisi ya Mzee Majoka 
    4. wakati Husda na Ashua wanapigana.
    5. Majoka anakumbuka ushauri wa Kenga wa jinsi ya kumnasa Ashua kwa kusababisha fujo baina yake na Husda.                                     
  2.  
    • Swali balagha – huoni ni fursa nzuri ya kulipiza kisasi?
    • Nahau – kummezea mate; kumtamani                                                     
  3.  
    1. Kumwaga kemikali na taka sokoni licha ya kuwa wananchi wanakaa na kufanyia biashara zao katika soko.
    2. Kuwatumia wahuni kunyamazisha wapinzani. Mzee Kenga anakutana na Wahuni chini ya mbuyu ambao baadaye wanamwumiza Tunu.
    3. Kuruhusu dawa za kulevya na wanafunzi ambao wanakuwa makabeji
    4. Kuwaua wapinzani, kama vile vijana watano walioandamana
    5. Kuwatumia polisi kuwaua na kurushia waandamanaji risasi na vitoa machozi.
    6. Kuwanyima wafanyakazi haki, kama vile walimu na wauguzi wanaongezewa asilimia ndogo ya mshahara kasha kupandisha kodi.
    7. Utawala kuruhusu uuzaji wa pombe haramu kinyume na katiba, ambao umesababisha vifo na kufanya watu kuwa vipofu.
    8. Kufungulia biashara ya ukataji miti ilhai watu wanategemea miti hiyo kuboresha mazingira.
    9. Kufunga kituo cha runinga ya Mzalendo kwa kuonyesha mkutano wa Tunu na wapinzani wengine wa utawala.
    10. Utawala kutumia vyombo vya dola kuwafukuza watu wanaoenda sokoni na kuweka ulinzi mkali licha ya kuwa ulikuwa uwanja wa umma.
    11. Kuwarushia wakazi vijikaratasi vyenye ujumbe hasimu wakitakikana wapahame mahali ambapo wamekuwa wakiishi kwa muda wote wa uhai wao.
  4.  
    1. Kenga anamshauri Majoka amwalike Ashua na Husda ili patashika itokee, naye Majoka apate jinsi atakavyolipiza kisasi kwa Sudi kwa kukataa kuchonga kinyago.
    2. Anamshauri Majoka atangaze kuwa maandamano ni haramu kisha anawamuru maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi dhidi ya umma unaondoa maandamano.
    3. Majoka anakataa Suala la polisi kutumia nguvu zaidi lakini Kenga anamwambia “Acha moyo wa huruma….. Siasa na hisia haziivi kwenye chungu kimoja ndugu yangu.
    4. Anakubali pendekezo la Majoka la kufunga Runinga ya Mzalendo kwa kupeperusha matangazo ya mkutano moja kwa moja.
    5. Kenga alihusika katika kupanga mauaji ya Jabali kwani Majoka anamsifu kwa kupanga hilo na hata wanapigishana Konzi
    6. Anaibua pendekezo la kumuua Chopi kwa kutofuata maagizo ya kumuua Tunu akisema, “Nafikiri Chopi lazima aende safari.”
    7. Anamwambia Majoka kuwa si kweli kwamba watu watampigia Tunu kura na kusema, “Tunu hawezi kupigiwa hata!”
    8. Anapendekea kukusanya kodi ya juu na kukataa kuitumia vyema na kwa njia halali k.v. kutoa taka.                                                            6x1

SWALI LA 3 - KIGOGO

  • Unyakuzi wa mali ya umma – Majoka anaamua kulifunga Soko la Chapakazi ili kujenga hoteli ya kifahari.
  • Ubinafsi – Majoka anavibomoa vibanda vya Wanasagamoyo na kupanga kujenga hoteli yake ya kifahari.
  • Utepetevu/ukosefu wa uwajibikaji – wananchi wanalipa kodi lakini wanakosa huduma kusafishiwa soko na huduma za maji taka.
  • Vitisho – Majoka anatisha kumfuta Kingi kazi
  • Viongozi wamekosa maadili ya kikazi – Majoka anamrai Ashua mkewe Sudi ili aendeleze ufuska naye.
  • Kuwatesa wapinzani – Tunu na Sudi wanateswa lakini wanaendelea kupigania mageuzi
  • Kuvunja sheria – Majoka anampa Mamapima kibali cha kuuza pombe haramu ambayo ni kinyume na katiba
  • Wizi wa kura –Majoka anasema kuwa hata wasipompa kura atashinda
  • Ubaguzi katika utoaji wa kandarasi  - kandarasi ya kuoka keki inatolewa kwa Asiya ambaye ni mke wa Boza
  • Matumizi mabaya ya pesa za umma – pesa zinatumiwa katika shughuli za kuchonga vinyago
  • Utawala wa kiimla na wa kutojali – Wanasagamoyo hawana usemi wowote; Majoka anasema kuwa atajenga hoteli watu wapende wasipende
  • Mauaji ya kikatili – watu wasio na hatia wanauawa; Jabali 
  • Kuzwazulia watu wasio na hatia  - Ashua anazuiliwa na Majoka bila kosa lolote
  • Wanasagamoyo wanakabiliwa na unyonyaji – bei ya chakula kwenye kioski cha kampuni imepanda maradufu tangu soko lilipofungwa
  • Kuwanyima wanasagamoyo haki ya kaundamana – wanaharamisha maandamano
  • Unasaba – Majoka anamwajiri Kenga ambaye ni binamuye kama mshauri wake mkuu
  • Viongozi wanatumia nafasi zao kuwaangamiza vijana  - matumizi ya dawa za kulevya – wanfunzi katika shule ya Majoka Academy wadungana sumu ya nyoka
  • Utapeli  - Kuwaongezea  walimu mshahara na wauguzi na kuongeza kodi
  • Kurithisha uongozi – Majoka anapanga kutambulisha Ngao Junior kuwa kiongozi mpya mpya badala ya Wanasagamoyo kumchagua kiongozi wao
  • Kuruhusu biashara ya ukataji wa miti.
  • Matumizi mabaya ya vyombo vya dola – polisi wanatumiwa kuwatawanya waandamanaji.

SEHEMU C:  RIWAYA YA CHOZI LA HERI (ASSUMPTA K MATEI)

SWALI LA NNE

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili  (Alama 4)
    • Haya ni mawazo ya Kiriri akiwa nyumbani kwake kabla ya kifo chake. Alikuwa anasumbuka kwa kuachwa na jamaa yake. Alikuwa ameachwa na mkewe ,Annette na wanawe ambao sasa walikuwa ughaibuni na walikataa kurudi nchini alikokuwa Kiriri hata baada yake kuwarai.
  2. Huku ukitolea mifano maridhawa, fafanua mbinu nne za kifasihi zinazojitikeza katika dondoo hili                                (Alama 4)
    • Maswali ya balagha/mubalagha -Kipi kinachowavuta kuhamia ughaibuni?
      -.....nchi za ughaibuni ni    twenty-four-hour economies?
    • Sitiari -mzigo wa simanzi kurejelea huzuni aliokuwa nao Kiriri kwa kuachwa na jamaa yake.
      -Mshahara mnono-kurejelea mshahara mkubwa.
    • Uhaishaji/tashihisi- mzigo wa simanzi ulipokilemea kifua chake.
    • Kuchanganya ndimi- twenty-four-hour economies.
  3. Eleza changamoto inayomkumba msemaji katika dondoo hili (Alama 2)
    • Ukiwa/upweke- Kiriri aliachwa na mkewe Annette na wanawe ambao sasa walikuwa ughaibuni.
  4. Fafanua jinsi maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili yameshughulikiwa kwingineko riwayani.    (Alama 4)
    Maudhui ya upweke/ukiwa
    • Lunga anaachwa na mkewe
    • Umu anachwa na kijakazi
    • Umu anaachwa na watoto wao wakembe ;Dick na mwaliko waliouzwa na kijakazi.
    • Umu anaachwa na babake,Lunga anapoaga dunia hata baada ya Mamake kumwacha babake alipokuwa akilala.
    • Ridhaa anaachwa na mwanawe Tila,Mkewe ,Terry na pia mkaza mwanawe na mjukuwe.
    • Selume anaondoka nyumbani kwa katika Msitu wa Heri baada ya kushutumiwa na jamii ya mumewe.
    • Mwangemi anawapoteza Mkewe na mwanawe. Hata anapokuwa katika nyumba yake kando ya bahari,anawawaza.  (Hoja 4×1)
  5. Fafanua umuhimu wa mandhari katika kuijenga riwaya hii kwa kurejelea Msitu wa Mamba.  (Alama 8)
    • Ukosefu wa vyoo
    • Ukosefu wa malazi/malazi
    • Ukosefu wa chakula
    • Ukosefu wa maji safi
    • Upweke
    • Magonjwa kama vile kipindupindu
    • Uharibifu wa mazingira(Lunga na wakaaji wengine katika Msitu wa Mamba kukata miti ili kuendeleza kilimo.
    • Ukimbizi wa ndani kwa ndani.                         (Hoja 4×1)

SWALI LA TANO

Eleza jinsi maudhui ya ufisadi yalivyoshughulikiwa katika riwaya ya Chozi la Heri.
 
  • Nyumba za maskini zinapobomolewa Tononokeni, mabwanyenye wanaanza kutoa milungula ili nyumba zao zisibomolewa.
  • viongozi wanapowapoka raia ardhi zao, raia walalamikapo hupozwa roho kwa kuambiwa kuwa kumeundwa tume za kuchunguza kashfa hizo.
  • wakati wa uchaguzi, wanasiasa wanawahonga raia ili wawachague.  Papa aliwahonga kwa pesa na unga.
  • Hazina ya Jitegemee inalenga kuwafaidi vijana wa taifa la Wahafidhina lakini ukabila na unasaba unapoliandama hawanufaiki.
  • nyumba zinazolengwa kupewa maskini katika mtaa duni wa Sombera zinachukuliwa na viongozi baada ya ujenzi kukamilika.
  • familia ya Bwana kute inajigawa na kuwa familia tatu ili wapate msaada mwingi kuliko wakimbizi wengine.
  • Serikali inabomoa majengo ya raia katika mtaa wa Tononokeni na Zari bila kuwafidia. 
  • raia wanaiba mafuta ya lori ili wawauzie madereva wa wakubwa au walinda usalama ili wayauze kwingine.
  • madereva wa wakubwa wanafyonza mafuta kwa mirija na kuwauzia wenye magari ya kibinafsi.
  • askari wananunua mafuta ambayo yameibiwa na kuyauza kwingine.
  • matapei wanawauzia wananchi wenzao ardhi ya makaburi bila kujali
  • raia matapeli wanauza ardhi zao mara mbili kwa watu wawili tofauti na kutoa hati miliki mbili halali na bandia
  • viongozi wananyakua ardhi iliyotengewa upanzi wa chakula na kujenga nyumba zao mf. Madhabahu kwenye mlima wa Nasibu yalinyakuliwa ili kujenga hoteli za kitalii.
  • vigogo wanauza mahindi yanayotolewa na mataifa ya nje kama msaada.
  • vigogo wanawalazimisha wataalamu wa maswala ya lishe kuidhinisha uuzaji wa mahindi yaliyoharibika.
  • viongozi wanapasua mbao na kuchoma makaa katika msitu wa mamba baada ya msitu huo kupigwa marufuku.
  • viongozi wanahamisha wakimbizi kutoka msitu wa Mamba na kuanza kuvuna mahindi yaliyopandwa na wakimbizi badala ya kuwaruhusu kuyavuna kabla ya kuwaondoa.
  • Baada ya Fumba kumpachika mimba mwanafunzi wake, aliachishwa kazi kwa muda kisha akahamishwa kwingine hivyo kumsababishia Rehema kutopata haki yake.
  • Baadhi ya walinda usalama wanashirikiana na wahalifu ili wagawane mali iliyoibiwa.
  • Magari ya vigogo hayaondolewi barabarani na askari licha ya kuwa mabovu.
  • Buda anawahonga askari wanapoenda nyumbani kwake kumtia mbaroni.(biashara ya ulanguzi wa mihadarati)      (Zozote 20x1=10)
SEHEMU YA D:USHAIRI
 
  1. SHAIRI LA KWANZA
    1. Bainisha bahari ya shairi hili ukijikita katika ruwaza zifuatazo (alama3)
      1. Mishororo
        • Takhmisa –mishororo tano
      2. Maneno
        • Pindu-utao, mshororo wa mwisho wa ubeti unafanywa ukwapa wa mshororo wa kwanza ubeti unaofuata
        • Kikwamba – Neno/ukwapi wa mshororo wa kwanza kila ubeti ni lile/yale yale
      3. Vina – mtiririko 
        • Vina vyote, vya ndani vina urari (ni) aidha vina vya nche vina urari (ma)
    2. Eleza muundo wa shairi hili (alama4)
      • Beti nane
      • Mishororo 5 kila ubeti
      • Bipande viwili kila mshororo
      • Mizani kumi na sita kila mshororo
      • Vina vya ukwapi ni ‘ni’ na  vya utao ni ‘ma’
      • Lina kibwagizo
    3. Bainisha mbinu zifuatazo za kimtindo  katika shairi hili (alama3)
      1. Tashbihi – kidogo kama Sodom!
      2. Taswira-uwaonapo fuoni, nusu uchi wa mnyama
      3. Tasfida-wanatafuna maini (kushiriki ngano)
    4. Eleza toni ya shairi hili (alama1)
      • Kukashifu/kusuta/kushauri
    5. Bainisha nafsi nenewa katika shairi hili (alama1)
      • Wanajamii
    6. Fafanua dhamira ya mtunzi wa shairi hili (alama2)
      • Kukashifu utovu wa maadili katika jamii/mijini
      • Kuonyesha uozo uliopo mijini
    7. Andika ubeti watatu kwa lugha tutumbi (alama4)
      • Hakika, miji yetu imekuwa kama Sodoma.
      • Watu hawana haya kwani wametupilia mbali maadhili
      • Baba na binti zao hishiriki mapenzi wasichana wadog kuwa waja wazito. Miji yetu inafanana na Sodoma.
    8. Fafanua maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa na mshairi (alama2)
      1. Manani – Mola/Mungu
      2. Marijali - wasichana /mabinti
  2. .SHAIRI LA PILI
    1. Eleza dhamira ya shairi hili.              (al.2)
      • Anadhamiria kuonyesha wanyonge wanastahili usawa na haki – na wanyonge kupatiwa kwa bei kuzingatiwa bila kudhulumiwa – ubeti wa 4
    2. Baininsha tamathali mbili za usemi katika shairi hili.              al.2)
      • Tashbihi – ni kama la moto, wavitamani kama tama ya fisi
      • Takriri – Maendeleo  ya umma
      • Nidaa – Lo!
    3. Eleza umuhimu tatu wa usambamba katika shairi hili.        (al.2)
      • Maendeleo ya umma (urudiaji wa fungu) – kusisitiza ujumbe
      • Urudiaji wa silabi …..ni, ki – kuleta ridhimu
      • Urudiaji wa neno.
    4. Onyesha jinsi maendeleo ya umma ulivyo kinaya.             (al.2)
      • Ni kinaya kuwa tuna vitu tele lakini bei I juu
      • Ni kinaya kuviona  vitu madukani  lakini kuvipata ng’o
    5. Eleza mambo ambayo mshairi nachukulia kuwa maendelo halisi ya umma.                  (al.4)
      • Vitu kumilikiwa  na wanyone kupiwa.
      • Bei kuzingatiwa bila kudhulumiwa
      • Dola kudhibiti vitu vijapo nchini mwetu.
      • Watu kuwa na kauli katika shughulika zao.
      • Watu kuwa waungwana.
    6. Tambua matumizi ya mstari mishata kwa kutolea mifano.                 (al.2)
      • Mishororo ambayo si toshelezi katka shairi
      • Maendeleo ya umma
    7. Bainisha  nafsi neni katika shairi hili.                (al.1)
      • Ni mzalendo/mwananchi-nchini mwet ubeti 5
      • Mtetezi wa haki – ubeti 4
    8. Fafanua toni ya shairi hili.                                  (al.1)
      • Kuhamasisha
      • Kuzindua
    9. Andika ubeti wanne kwa lugha nathari.               (al.4)
      • Maendeleo ya umma ni kutafuta  vitu na kuwauzia wanyonge kwa bei nafuu pasi  na kunyanyasua wala kudanganywa na hivyo kulinda haki zao            
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 Term 1 Opener Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest