Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2023

Share via Whatsapp
MASWALI
UFAHAMU (Alama 15)\
 1. Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
  Nilianza kusikia habari za ugoniwa wa ukimwi mnamo mwaka wa 1984. Wakati huo nilikuwa nimemaliza masomo yangu ya kidato cha sita na kujiunga ia chuo cha walimu kilichoko wilayani Nyeri kiitwacho Kagumo. Nilihofu sana maradhi hayo hasa nilipowaona walioambukizwa wakikondeana mthili ya ng’onda. Baada ya waathiriwa kufariki, jamaa zao hawakuruhusiwa kuwazika. Wizara ya afya ilitoa amri kali kuwa wale wore waliofariki kutokana na maradhi ya ukimwi wazikwe na kikundi maalum cha madaktari ma wauguzi wa hospitali za wilayani. Kulikuwa na kasisi mmoja tuliyehusiana kiukoo aliyefariki kutokana na maradhi ya ukimwi. Sisi hatukuruhusiwa hata kumsongea karibu marehemu alipoletwa nyumbani.
  Madaktari na wauguzi walivalia majoho meupe ungedhani ni malaika. Mikononi walivaa glovu nyeupe ambazo zilitutisha machoni.
  Mara nyingi nimeshangazwa na athari za ugonjwa huu. Inasemekana kuwa kuna njia kadha za usambazaji wa ugonjwa wa ukimwi. Njia moja ni kuhusika katika kitendo cha mapenzi na mtu ambaye ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo. Njia nyingine nimeelezwa kuwa ni kwa kutumia kwa pamoja vifaa vyenye makali na mtu aliyeambukizwa virusi vya ukimwi. Inasemekana kuwa kugusa damu ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo pia kunaweza kukutia mashakani.
  Mama mja mzito aliyeambukizwa ugonjwa huu anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni anapojifungua na hati baadaye anapomnyonyesha mtoto wake mchanga. Kisha kuna kupokea damu kutoka kwa mtu ambaye tayari ameambukizwa virusi hivyo. Yote hayo yanachangia pakubwa katika kututumbukiza kwenye janga hili la ukimwi.
  Lakini nimewahi kusikia watu wakisema kuwa ukimwi si maradhi. Yaani ni  upungufu tu wa kinga ya kukabiliana na magoniwa katika mwili wa binadamu. Maadamu ukiweza kuimarisha kinga ya magonjwa katika mwili wako basi unaweza kuishi kwa miaka ma mikaka. Anachohitajika mtu ni apate chakula na lishe bora, afanye mazoezi ya kutosha, na kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi na watu wenine ambao huenda wakamwambukiza aina tofauti tofauti za virusi vya ukimwi. Hayo yakifanyika mwathiriwa huwa na matumaini ya kuishi kwa muda mrefu kwani hatazidiwa na maradhi hayo na mwishowe kwenda jongomeo. Kuna haja kubwa ya kujilinda na kuepukana kabisa na janga hili lililotuzingira. Wengi tayari wameshapoteza roho zao. Wengine walioambukizwa wanaugua mahospitalini ma na majumbani mwao kisirisiri. Mungu atujalie heri na shari, kwani utafiti wote ambao umefanywa kuhusu tiba ya uwele huu haujafua dafu hata kidogo. Hata hivyo Mola hamtupi mja wake.
  Maswali 
  1. Ipe habari hii anwani ifaayo. (alama 1)
  2. Kwa nini mwandishi ana hofu sana ya maradhi ya ukimwi? (alama 2)
  3. Hapo awali watu waliwachukulia vipi walioambukizwa maradhi ya Ukimwi? (al 2)
  4. Eleza njia mbalimbali zinazomfanya mtu kuambukizwa maradhi ya ukimwi. (al3)
  5. Je, tunawezaje kuepukana na janga hili la ukimwi? (alama 2)
  6. Eleza maana ya vifungu hivi vya maneno kama vilivyotumika katika taarifa. (alama 5)
   1. Wauguzi ………………………………………………..…
   2. Makali………………………………………………………
   3. Virusi…………,….…………………………………………
   4. Uwele…………………….…………………………………
   5. Janga…………………………………………………………
 2. MUHTASARI
  Soma kifungu kifuatacho kwa makini kisha jibu maswali.
  Sayansi ya lugha kwa mujibu wa matumizi yake katika jamii ni taaluma mpya sana katika silabasi ya somo la Kiswahili kwa shule za Sekondari. Taaluma hii mpya imeibuka na kuibua hali ya taharuki si kwa wanafunzi, si kwa walimu na si kwa washikadau wote wa kitengo maalum cha kukuza lugha nchini.
  Wanapoulizwa sababu ya taharuki yao, jibu huwa ni moja, “Kuku mgeni hakosi kamba mguuni”Jambo la kimsingi ni kuwa mahuluki hutumia lugha katika shughuli ainati.Aidha ni dhahiri shahiri kwamba katika shughuli hizi kuna matumizi ya lugha — ama maneno kwa sauti au ishara kama zile za vipofu na viziwi.
  Lugha itumiwapo katika shughuli au taaluma fulani mahsusi, huwa pana msamiati fulani wa kipekee unaotawala katika shughuli hiyo. Istilahi hizi ndizo huunda sajili. Mathalani, katika taaluma ya zaraa kuna istilahi kama vile kulima, kupalilia, kuchimba makoongo, kuandaa weu, kupiga matuta, miche, mbegu, mbolea, jembe, koleo, mundu, mifugo, mazao na istilahi nyinginezo.
  Msamiati kama huu ndio huunda istilahi za sajili ya zaraa. Mbali na zaraa, kuna sajili nyingine kama sajili ya matangazo ya mpira utibabu, mazungumzo ya watoto wa mitaani; biashara, sheria na mahakama, dini ya Kikristo, Kiislamu na ya Kihindu na sajili nyinginezo.
  Waama, bila lugha matendo yote ya wanadamu yangegonga mwamba na kudorora. Je, viongozi wangetawala vipi? Wafanya biashara wangenadi vipi bidhaa zao? Walimu wangefunzaje’? Bila shaka jibu ni moja tu: ingekuwa vigumu sana.
  Hivyo basi lugha ni chombo muhimu sana. Katika maisha ya waja. Shime kila mtu, tuendeleze lugha yetu ya Kiswahili. Tusiwe wendaguu kwani makofi hayalii ila kwa viganja viwili.
  1. Fupisha aya tatu za mwanzo kwa maneno yasiyozidi 60. (Alama 7)
   Matayarisho
   Jibu
  2. Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno yasiyozidi 40. (alama 8)
   Matayarisho
   Jibu
 3. MATUMIZI YA LUGHA  
  1. Toa sita bainifu za sauti /h/ (alama 2)
  2. Tumia neno “hadi”  kama kihusishi cha (al.2)
   1. Wakati
   2. Mahali
  3. Onyesha matumizi mawili ya parandesi katika sentensi (alama 2)
  4. Tunga sentensi  mbili kuonyesha matumizi tofauti ya
   1. – ki –
   2. – po - (alama 2)
  5. Unda nomino ukitumia mizizi ifuatayo; (alama 2)
   1. – f –
   2. – l –
  6. Kanusha
   Sisi ndisi wakulima (alama 2)
  7. Andika kwa msemo wa tarifa
   Askari: Ulikuwa unaelekea wapi uliposhambuliwa?
   Jirani: nilikuwa nikienda sokoni jana. (alama 2)
  8.  
   1. Eleza dhana ya shamirisho (alama 1)
   2. Onyesha aina tofauti za shamirisho katika sentensi hii. (alama 2)
    Ali alimnunulia Asha viatu kwa pesa zake
  9. Andika sentensi ifuatayo kwa udogo / wingi (alama 2)
   Mtoto mkaidi aliiba kitabu cha mwenzake.
  10. Bainisha virai katika sentensi ifuatayo (alama 3)
   mtoto wake aliketi kando ya barabara asubuhi sana
  11.  
   1. Nini maana ya kiima? (alama 2)
   2. Onyesha kiima katika sentensi ifuatayo (alama 2)
    watoto walisafiria basi
  12. Changanua sentensi kwa kutumia jedwali (alama 4)
   Wachezaji vikapu watakaofanikiwa katika mechi hiyo watatuzwa medali.
  13. Tunga sentensi yenye muundo wa:-
   kiima, kiarifu, yambwa tendwa, yambwa tendewa na yambwa ala      (alama2)
  14. Bainisha matumizi ya “ni” katika sentensi zifuatazo.             (alama 2)
   1. Ondokeni
   2. Kiptoo ni mwinzi sugu.
  15. Huku ukitoa mifano, eleza maana ya silabi funge (alama 2)
  16. Yakinisha katika nafsi ya tatu wingi (alama 2)
   Sijasafiri kwenda Marekani (alama 2)
 4. ISIMU JAMII (alama 10)
  1. Eleza sababu zozote sita zinazochangia kufa kwa lugha (alama 6)
  2. Taja mambo yoyote manne yanayofanywa na serikali yetu kuimarisha lugha ya Kiswahili (alama 4)


MARKING SCHEME

 1.  
  1. Anwani
   • Hatari za ugonjwa wa Ukimwi.
    (alama 1x1 =1) (anwani isizidI maneno 6)
  2. Hofu
   • Kukonda sana kwa waathiriwa.
    Awali waliofariki kutokana na ukimwi hawakuwa wakizikwa na jamaa zao|
    Alama 2 x 1 = 2
  3.  
   • Awali watu waliwaona wagonjwa hao kama waasi au wahalifu waliojiletea balaa.
   • Walistahili kuepukwa kabisa kwa hofu ya kuwaambukiza wengine viini vya maradhi ya ukimwi.
  4.  
   • Kuhusika katika ngono na mtu aliyeambukizwa virusi vya ukimwi.
   • Athari ya kuwa na wapenzi wengine.
   • Matumizi ya vifaa vyenye makali na watu wenye virusi vya ukimwi.
   • Mama mtu aweza kuzambaza viini hivyo kwa mtoto wake wakati anapojifungua na kumnyonyesha.
   • Mtu anapotiwa damu yenye virusi vya ukimwi huambukizwa mara moja.   (zozote 3x1 = 3)
  5.  
   • Kutofanya mapenzi kiholela bila kutumia kinga yoyote.
   • Kutoshirikiana na watu wanaougua ugonjwa huu katika matumizi ya vifaa vyenye makali.
   • Kuwa waaminifu na kumcha Mwenyezi Mungu.   (alama 2x1 = 2)
  6.  
   1. Wauguzi – wanaowahudumia na kuwaangalia vizuri wagonjwa katika hospitali au zahanati.
   2. Makali – sehemu ya kifaa k.m kisu inayoweza kukata.
   3. Virusi – viini vinavyosababisha ugonjwa kama ukimwi.
   4. Ndwele – ugonjwa, maradhi
   5. Janga – balaa, shida, tabu, matata.
 2. MWONGOZO (MUHTASARI)
  1.  
   • Sayansi ya lugha ni taaluma mpya katika silibasi ya lugha kwa shule za sekondari
   • Taaluma hii imeibuka na kuibua hali ya taharuki kwa washika dau wote.
   • Kwa sababu kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
   • Mahaluki hutumia lugha katika shughuli ainati.
   • Kuna matumizi ya lugha, sauti au ishara.
   • Lugha itumikayo huwa pana msamiati wa kipekee unaotawala katika shughuli hiyo.
   • Istilahi hizi huunda sajili mbalimbali.
  2. Mbali na zaraa kuna matangazo ya mpira, utabibu, biashara, watoto, sheria na mahakama,dini (kikristo), kiislamu, kihindu.
   • Bila lugha, shughuli zingekwama.
   • Lugha ni muhimu maishani.
   • Kila mtu ajitahidi kuendeleza lugha ya Kiswahili.
   • Tushirikiane ili tufaulu.
 3. Matumizi ya lugha
  1.  
   • Kikwamizo
   • Siguuna / hafifu
   • Hutamkiwakooni / glota (2 x 1 = 2)
  2.  
   1. Tulicheza hadi adhuhuri
   2. Wezi wailinikimbiza hadi nyumbani mwangu (2 x 1 = 2)
  3.  
   1. Kutoa  maelezo zaidi kuhusu neno au maneno yaliyotangulia.
   2. Hutumika kufungia nambari au herufi za kuorodhesha.
    Mf. (a), (b), (c)
    (i), (ii), (iii)
   3. Hutumika katika mahojiano, mazungumzo au maandishi ya kitamthilia kufungia ufafanuzi. (zozote 2 x 1 = alama 2)
  4.  
   1. ki 
    • Ukilia nitakupiga – masharti
    • Kijino changu kinauma – udogo
    • Kiatu kitashonwa – ngeli (2 x 1 = 2)
   2. po
    • Pavumapo usipachezee – mahali
    • Alipowasili tuliondoka – wakati
  5.  
   1. –f-
    • kifo / vifo
    • mfu / wafu
   2. – l –
    • Mlo
    • Chakula (2 x 1 = 2)
    • Kula
  6. Sisi sio wakulima (1x2 = 2)
  7. Askari alimuuliza jirani alikuwa akielekea wapi aliposhambuliwa naye jirani akamjibu kuwa alikuwa akienda sokoni siku hiyo jioni.(4 x ½ = 2)
  8.  
   1. Ni nomino inayoathiriwa na kitenzi (mtendwa, mtendewa)   (1 x 1 = 1)
   2.  
    • Asha – Kitondo
    • Viatu – kipozi
    • Pesa – ala (zozote 2 x 1 = 2)
  9. Vitoto vikaidi viliiba vijitabu vya wenzao (1x2 = 2)
  10.  
   • Kirai Nomino – mtoto wake
   • Kirai kihusishi – kando ya barabara
   • Kiraikielezi – asubuhi sana (3x1 = alama 3)
  11.  
   1. Ni sehemu katika setensi yenye nomino (1 x 2 = 2)
   2. Watoto (1 x 2 = 2)
  12.                                                                                                          S
                           KN                                   KT 
              N        V                                  S            T      N
     Wachezaji   vikapu   wakifanikiwa katika mechi hiyo   watatuzwa   medali 
   (8 x ½ = 4)
  13. Mama alipika chakula cha mjomba kwa sufuria (3 x 1 = 3)
       l          l                   l              l                   l
   Kiima  Kiarifu    yambwa    yambwa           ala
                            Tendwa      tendewa
  14.  
   1. Kuamrisha
   2. Kitenzi kishirikishi kipungufu (2 x 1 = 2)
  15. Silabi funge huishia kwa konsonati
   mfano: ma-k-ta-ba (2 x 1= 2)
  16. Wanasafiri kwenda marekani (1x2 = 2)
 4.  
  1. ISIMU JAMII
   • Kutoungwa mkono na tasisi mbalimbali k.v elimu dini.
   • Hadhi – lugha ambazo hazina  hadhi huishia kufa.
   • Ndoa za mseto.
   • Kuhama kwa watu – katika sehemu moja hadi nyingine.
   • Athari za elimu
   • Sababu za kisiasa.
   • Uchache wa wazungumzaji.
   • Maendeleo na ubunifu wa viwanda (6x1= 6)
  2.  
   • Kiswahili kufanywa lugha ya taifa / Rasmi
   • Katiba kupitisha Kiswahili kuwa lugha rasm inchini.
   • Kiswahili kuwa somo la lazima shule za upili na msingi.
   • Vyombo vya mawasiliano kutumia lugha ya Kiswahili.
   • Vitabu vingi kuchapishwa kwa lugha ya Kiswahili.
   • Shughuli za bunge kuendelezwa kwa lugha ya Kiswahili.          (4 x 1 = alama  4)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest