Kiswahili Paper 3 Questions - Baringo North Joint Evaluation Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

MAAGIZO

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani; Riwaya Hadithi fupi,Tamthilia na Ushairi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Majibu yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili

SEHEMU A : FASIHI SIMULIZI  LAZIMA (ALAMA 20)

  1.      
    1. Jadili sifa zozote nne za mtambaji bora. (alama 4)
    2. Fafanua hasara zozote nne za miviga. (alama 4)
    3. Jadili hatua tano zinazofuatwa wakati wa utafiti. (alama 5)
    4. Tofautisha istilahi zifuatazo za Fasihi Simulizi. (alama 3)
      1. Matambiko
      2. pembezi
      3. Misimu
    5. Eleza sifa nne za maapizo. (alama 4)

SEHEMU B: RIWAYA
ASSUMPTA MATEI: CHOZI LA HERI
Jibu swali la 2 au la 3

  1. Mwandishi amejadili kwa kina maudhui ya mapuuza. Thibitisha . (alama 20)
    Au
  2. Maisha yangu yalijaa shubiri tangu utotoni.
    1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
    2. Fafanua mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 4)
    3. Jadili jinsi mwandishi amesawiri suala la ukatili. (alama 12)

SEHEMU C: HADITHI FUPI
Chokocho na Kayanda(Wah)Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
Jibu swali la 4 au la 5

  1. Jadili maudhui yaliyoonyeshwa kwenye mabano kutoka hadithi zifuatazo.(alama 20)
    1. Tumbo Lisiloshiba (utabaka)
    2. Masharti ya Kisasa (Unyumba)
    3. Mkubwa (Ufisadi )
    4. Mwalimu Mstaafu (Elimu)
      au
  2. Tulipokutana Tena
    1. Jadili istilahi za lugha zinazojitokeza katika kifungu hiki. (alama 4)
      ‘Bogoa gani huyo?’ Kazu alibadilisha toni ya sauti na mng’aro wa sura yake. Alikuwa tayari kajaa huzuni ingawa hadithi yenyewe alikuwa haifahamu vizuri. Usoni pake ulisimama unyeti na juu ya ngozi ya uso wake huruma zilijitokeza. Ndivyo alivyo Kazu kila siku. Anaweza kubadilika mara moja kama uso wa mtoto mchanga.
    2. Jadili umuhimu wa Bi Sinai katika hadithi hii. (alama 8)
    3.  ‘Jijini ni kuzuri. Kuna majumba makubwa, utapanda magari mazuri mazuri ya marafiki zetu, utakula vyakula vitamu na kupewa nguo za fahari. Utapelekwa shule kusoma na kuandika.‘ Kwa Bogoa , maneno haya ya babake ni kinaya. Thibitisha kwa hoja nane. (alama 8)

SEHEMU D: TAMTHILIA
KIGOGO PAULINE KEA

Jibu swali la 6 au la 7

  1.        
    1. Jadili dhamira ya mwandishi wa Tamthilia ya Kigogo. (alama 10)
    2. Fafanua jinsi Ujenzi wa jamii mpya umeshughulikiwa na mwandishi. (alama 10)
      au
  2. Kutia kwa kulia na kutoa kwa kushoto.
    1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
    2. Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika. (alama 2)
    3. Fafanua sifa nne za msemaji wa maneno haya. (alama 4)
    4. Jadili mbinu hasi za uongozi katika Tamthilia. (alama 10)

SEHEMU E: USHAIRI (Alama 20)

  1. SOMA SHAIRI KISHA UJIBU MASWALI.
    1.  Sidhani ni kichekesho, kesho kuwepo sidhani
      Vilivyoko ni vitisho, viwewe na visirani
      Mimi kupe kwenye josho, la sumu iso imani
      Kesho yangu imeshaliwa.

    2. Kesho yangu imeshaliwa, isibaki hata kitwa
      Kwamba hai nitakuwa, kesho na kesho kutwa
      Hilo haliwezi kuwa, na wakati limepitwa
      Na i wapi kesho yangu?

    3. Sikwambii mtondoo, au ni mtondogoo
      Ajapowika jogoo, kesho sipo ng'oo
      Hata simu za "haloo", hazinipati "haloo"
      Nitaituhumu kesho.

    4. Kesho nitaituhumu, kwa sababu ya hasama
      Hasama ya mahasimu, waliolishana njama
      Kutaka kunihujumu, wanizulie nakama
      Itokapi yangu kesho?

    5. Wa kwanza huyu Ukimwi, daima aniotea
      Kwa dawa huyu hazimwi, haachi kuturingia
      Amekuwa kama zimwi, mtu lisilomjua
      Ati nipangie kesho?!

    6. Nipange yangu matanga, au kujenga nyumba?
      Nipange kung'oa nanga, au shairi kuimba?
      Nipangeni cha kupanga, biashara za mtumba?
      Kesho si ukoo wangu.

    7. Ukimwi nduguze wako, Ebola na Malaria
      Kichomi na sekeneko, mno wajifaragua
      Maadamu wangaliko, vipi kesho kuwazia
      Kesho si ndu yangu mwandani.

    8. Mimi napangia leo, maana kesho sijui
      Usafiri nifanyao, kwenye vyombo anuwai
      Una mikasa kibao, majanga ya kila nui
      Salama yangu i wapi?

    9. I wapi salama yangu, huku wapo wa kijicho
      Ngaa nipatapo changu, waingiwa mpekecho
      Kunipikia majungu, nikikosa changu hicho
      Waso nitakia kesho!

    10. Kesho wasonitakia, watele kama siafu
      Majambazi nasinzia, tapeli na wazinifu
      Roho yangu wapania, kunipeleka kwa ufu
      Nipewe jina "Hayati"

      MASWALI
      1. Ujumbe wa shairi hili unakatisha tamaa. Thibitisha. (4)
      2. Hili ni shairi la aina gani? (1)
      3. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (4).
      4. Eleza mbinu nne za lugha zilizotumiwa. (4)
      5. Andika bahari kwa kuzingatia vigezo; (2).
        Mizani
        Vina
      6. Onyesho jinsi mshairi alivyotumia idhini yake ya kishairi. (2).
      7. Taja; (3)
        Toni
        Nafsi - neni
        Nafsi- nenewa.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions - Baringo North Joint Evaluation Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?