0 votes
1.0k views
in Isimu Jamii by

Haya ng’ara … Ng’ara leo! Nguo motomoto. Ng’ara leo kwa bei rahisi. Hamsini hamsini shati. Kuona ni bure. Bure kwa bure. Shika mwenyewe ujionee. Bei nafuu. Bei ya starehe. Haya, haya. Usikose mwanangu! Hamsa! Hamsa! Fifty!Hamsa! Fifty! Hamsa na nyingine.

  1. Bainisha sajili ya mazungumzo haya. 
  2. Eleza sifa nane za sajili hii kwa kurejelea kifungu hiki. 

4 Answers

0 votes
by
  1. Hii ni sajili ya biashara ya kunadi au kutangaza bidhaa (nguo) sokoni au barabarani. Msamiati uliotumika ni msamiata  maalaum wa biashara ya sokoni. Kwa mfano shati, bei, hamsa na fifty.
  2.  
    1. Sajili hii hutumia msamiati maalum wa biashara ili kurejelea shughuli zinazoendelezwa pale. Kwa mfano, shati, nguo, hamsini, bei, hamsa na fifty.
    2. Matumizi ya chuku ili kuonyesha ubora wa bidhaa zao. Kwa mfano, kuona ni bure, bure kwa bure, bei ya starehe, nguo motomoto.
    3. Urudiaji ili kusisitiza ubora wa bidhaa zake na kumshawishi mteja kununua. Kwa ng’ara, haya haya.
    4. Matumizi ya misimu ya biashara ili aeleweke katika muktadha huo wa kibiashara. Kwa mfano nguo motomoto, hamsa, ng’ara.
    5. Lugha shawishi ili kuwavuta wateja wao kununua bidha . kwa mfano: shika mwenyewe ujionee, usikose mwanangu, bei nafuu.
    6. Kauli huwa fupifupi hasa wakati wa kujadiliana bei kwa sababu muuzaji na mnunuzi hawataki kuchoshana au kuna wateja wengine wa kuhudumiwa. Kwa mfano, kuona ni bure , bei nafuu. Tangazo hili kwa jumla ni fupi.
    7. Lugha huwa nyepesi au sahili ili iweze kueleweka na watu wenye viwango vyote vya elimu. Kifungu hiki kinaeleweka bila tatizo lolote.
    8. Kuchanganya ndimi ili  kuwanasa wateja wote na kuwaonyesha ukaribu (ukuruba) kwa kuzungumza lugha nayodhani wateja wanailewa zaidi. Mbinu hii huwafanya wateja anaowazungumzia kumpelea yeye muuzaji na kununua bidhaa zake. Kwa mfano: fifity, fifty au hamsa fifty.
0 votes
by
Sajili ya sioni

0 votes
by
1) matumizi ya sentensi Fupi fupi.2) utohozi kama hamsini hamsini shati bure. 3)kuchanganya Ndimi kama hamsa fifty

0 votes
by
1Sajili ya biashara
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...