Tuesday, 07 September 2021 13:39

Kiswahili Activities - Grade 5 End Term 1 Exam 2021 SET 2

Share via Whatsapp

COMPETENCY BASED CURICULUM
GREDI YA 5, MWISHO WA MUHULA WA 1
SHUGHULI ZA KISWAHILI
JINA....................................................SHULE............................................

ZOEZI 1: KUSOMA KWA UFAHAMU
Soma kifungu kifuatacho kisha uyjibu swali la 1 hadi la 7

Mipango yote ya sherehe ya kuzaliwa kwa baba yangu ilikuwa imepangwa ikapangika.Ilikuwa siku ya tatu ya juma. Baba alikuwa akikamilisha miaka thelathini na tisa. Yeye hakuwa amekula chumvi nyingi kama alivyokuwa babaye Meishisana.

Mapochopocho ya vyakula mbalimbali yalikuwa yakinukia mezani na hata mekoni. Vyakula kama vile pilau, biriani , maandazi na vibanzi vilivutia sana machoni pa wageni watano waalikwa. Nilishangaa nilipomwona Bwana Kauleni akidondokwa na mate kwa sababu ya kuitamani keki yenyewe. Watu wengine ambao sikuwatambua kwa majina yao, walikuwa wameketi kitako sebuleni huku wamejipamba kweli kweli. Bila shaka wote walijawa na tabasamu nyusoni pao. Keki yenyewe ilikuwa tamu kama halua. Mimi mwenyewe nilihusika kwa kuwakaribisha marafiki zangu kwenye viti baada ya kuvipanga.

Maswali

  1. Je, kisa hiki kinahusu sherehe ya nani? 
    ________________________________
  2. Sherehe yenyewe ilikuwa siku gani ya juma?
    ________________________________
  3. Mwandishi alitumia maneno, "hakuwa amekula chumvi nyingi." Je, hii inamaanisha nini ?
    ________________________________________________________________
  4. Wageni walikuwa wameketi kitako. Pigia mstari kielezi katika sentensi hii.
    ________________________________
  5. Je, sherehe hii ilihudhuriwa na wageni wangapi waalikwa?
    ________________________________
  6. Taja jina la babuye mwandishi.
    ________________________________
  7. Kifungu ulichokisoma kinahusu nini?
    ________________________________

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 8 hadi la 14.

    Mwaka huu ulipoanza, sote tulifurahi kurudi katika shule yetu. Shule hiyo inajulikana kama Mematele. Ina wanafunzi elfu moja na mia mbili na mabasi sita. Mabasi yote ya shule hiyo yamepakwa rangi ya manjano.
    Tulipowasili shuleni, tuliingia madarasani na kuketi kwenye viti vyetu. Mwalimu mmoja ambaye tulimpenda sana alingia darasani na kutuamkua, " Hamjambo wanafunzi " Nasi tukajibu, "Hatujambo
    mwalimu Matunda. Shikamoo"

    Kengele ilipopigwa tulielekea gwarideni Tulisimama wima tulipokuwa tukiimba wimbo wa taifa. Baadaye mwalimu alitukagua endapo kucha zetu zilikuwa safi. Mwalimu wetu alitushauri tuwe tukinywa maji mengi kila siku ili tuwe na afya njema.

    MASWALI
  8. Malizia sentensi hii
    Mwaka huu ulipoanza sote tulifurahi 
    ________________________________
  9. Mwandishi husomea katika skuli gani?
    ________________________________
  10. Shule ya mwandishi ina wanafunzi wangapi?
    ________________________________
  11. Mabasi ya shule katika nchi hii ya msimulizi yamepakwa rangl gani?
    ________________________________________________________________
  12. Salamu hamjambo hujibiwa hatujambo je, masalheri hujibiwa aje?
    ________________________________
  13. Ni nani aliwashauri wanagenzi kunywa maji mengi?
    ________________________________
  14. Kwa nini wanafunzi walishauriwa kunywa maji mengi?
    ________________________________

ZOEZI II:SARUFI

  1. Teua salamu ambayo haijaambatanishwa ipasavyo.
    Habari ya jioni.... njema
    Kwa heri..... ya kuonana
    Alamsiki.... aleikum salaam
    Makiwa .... unayo
  2. Je, kati ya maneno haya katika kamusi, ni neno gani litakuwa la pili?
    Muhubiri, Muhutasari, Muhula, Mtihani, Mshtakiwa ________________________________
  3. Mstatili huu una maneno matano ya nomino za vitenzi-jina. Je, ni neno lipi halifai kuwa hapa?
    [Kulala, Kukimbia, Kalia, Kusoma, kutibiwa]
    ________________________________

    Andika kwa wingi.
  4. Mtoto aliacha dawati lake shuleni.
    ________________________________
  5. Mwalimu wangu huja mapema shuleni
    ________________________________

    Chagua neno lifaalo kujaza nafasi.
  6. Matata ___________nyanya samaki. (alibeba, alimbebea, alimbeba)
  7. Tulienda sokoni ___________tununue matunda. (ili, kwa sababu).

  8. Kamilisha methali hii. Asiyekujua ___________{akuthanini, hakuthamini, hakudhamini}
  9. Ni sentensi gani haijakanushwa vyema?
    Tunaenda sokoni Hatuendi sokoni
    Mama yangu amechelewa  Mama yangu hachelewi 
    Walionana mwaka jana Hawakuonana mwaka jana.
    Juma ni mwanafunzi hodari  Juma si mwanafunzi hodari
  10. Nomino,"jua, lepe, jasho, joto na giza," hupatikana katika ngeli ya ___________
  11. Andika sentensi hii katika hali ya ukubwa
    Mtoto wake anasoma _________________________________
  12. Je, sentensi hii iko katika wakati gani?______________________
    Mlinzi mwenyewe analilinda rinda la mama.
  13. ______________________(Karamu ,Ghulamu, Kalamu) ya arusi ilikuwa ya kupendeza sana.
  14. Siku hiyo ___________(pipi,vivi, bibi) arusi alivaa gauni jeupe pe pe pe.
    Jaza mianya iliyoachwa kwa maneno yafaayo kutoka kwenye mabano (Shule, mwiko, vitunguuu,, sabuni)
  15. Mama alipokuwa akisonga ugali alitumia______________________
  16. Idadi ya wanafunzi katika ___________yetu ni elfu mbili.

INSHA
Andika insha kuhusu: MWALIMU NIMPENDAYE

MAAKIZO

  1. Sherehe ya kuzaliwa ya baba( ya mwandishi)
  2. siku ya tatu
  3. Hakuwa mzee sana
  4. kitako
  5. watano
  6. Meishisana
  7. sherehe ya siku ya kuzaliwa
  8. kurudi katika shule yetu
  9. Mematele
  10. elfu moja mia mbili
  11. manjano
  12. aheri
  13. mwalimu
  14. wawe na afya njema
  15. alamsiki
  16. mtihani
  17. kalia
  18. watoto waliacha madawati yao shuleni
  19. walimu wetu huja mapema shuleni
  20. alimbebea
  21. ili
  22. hakudhamini
  23. mama yangu amechelewa
  24. LI-YA
  25. jitoto lake linasoma
  26. wakati uliopo
  27. karamu
  28. bibi
  29. mwiko
  30. shule
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Activities - Grade 5 End Term 1 Exam 2021 SET 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students