- Nomino Kutokana na Mzizi wa Kitenzi
- Kitenzi Kutokana na Mzizi wa Nomino
- Nomino Kutokana na Mzizi wa Nomino
- Nomino Kutokana na Mzizi wa Kivumishi
- Kivumishi Kutokana na Mzizi wa Nomino
- Kitenzi Kutokana na Mzizi wa Kivumishi
- Kivumishi Kutokana na Mzizi wa Kitenzi
- Kitenzi Kutokana na Kielezi

Nomino Kutokana na Mzizi wa Kitenzi
- danganya-kudanganya, mdanganyifu,udanganyifu
- soma-kusoma, masomo,msomi,usomaji
- unda-kuunda, muundaji,uundaji,muundo
- funika-kufunika, kifuniko, mfunikaji, ufunikaji

Kitenzi Kutokana na Mzizi wa Nomino
- mlo-kula
- mlevi-kulewa, kulevuka
- mwimbaji-kuimba
- fikra-kufikiri
- malezi-kulea
- fumbo-kufumba, kufumbua

Nomino Kutokana na Mzizi wa Nomino
- mwimbaji-kuimba, wimbo, uimbaji, kiimbo
- mchezo-kucheza, uchezaji, mchezaji
- ulaghai-kulaghai, mlaghai
- hesabu-kuhesabu,uhesabu
- mdhalimu- kudhulumu, dhuluma, udhalimu

Nomino Kutokana na Mzizi wa Kivumishi
- -refu-mrefu, urefu, urefushaji
- - baya-mbaya, ubaya
- -zuri-mzuri, uzuri
- -kali-mkali, ukali
- -eupe-mweupe,weupe

Kivumishi Kutokana na Mzizi wa Nomino
- ujinga -jinga
- werevu -erevu
- mzuri -zuri
- mpumbavu -pumbavu
- mpyoro -pyoro

Kitenzi Kutokana na Mzizi wa Kivumishi
- haramu-kuharamisha, kuharamika
- halali-kuhalalisha, kuhalalika
- -fupi-kufupisha, kufupika
- bora-kuboresha, kuboreka
-refu-kurefusha, kurefuka - sahihi-kusahihisha, kusahihika
- -sikivu-kusikia
- -danganyifu-kudanganya

Kivumishi Kutokana na Mzizi wa Kitenzi
- dunisha - duni
- Haramisha - haramu
- fupisha -fupi
- sahilisha -sahili
- tukuka -tukufu
- fahamu -fahamivu
- teua -teule
- nyamaza -nyamavu
- ongoka -ongofu
- sahihisha -sahihi
- danganya -danganyifu

Kitenzi Kutokana na Kielezi
- haraka-harakisha
- zaidi-zidisha
- bidii-bidiisha
- hima-himiza
Download Uundaji wa maneno - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates