Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - KCSE Prediction Papers 2022

Share via Whatsapp

Maagizo kwa watahiniwa

 • Andika insha mbili
 • Swali la kwanza ni la lazima.
 • Kisha chagua insha nyingine moja kwa tatu zilizosalia.
 • Insha isipungue maneno 400


Maswali

 1. Umepata tangazo la nafasi ya kazi ya uhariri katika shirika la uchapichaji wa vitabu vya fasihi kwenye gazeti la Taifa Leo.
  Andika barua ya kuomba nafasi hii na uambatanishe wasifukazi wako kwa maelezo zaidi. (alama 20)
 2. Utelekezaji wa mtoto wa kiume nchini ni janga kuu. Jadili. (ALAMA 20)
 3. Andika insha inayoafikiana na methali Baniani mbaya kiatu chake dawa.
 4. Andika insha itakayomalizia kwa maneno yafuatayo:
  ................................Hapo ndipo iliponibainikia kuwa nilikuwa nikiogelea baharini pekee kinyume na wenzangu wote. (alama 20)


    

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

   Mwongozo Wa Kusahisha

 1. Umepata tangazo la nafasi ya kazi ya uhariri katika shirika la uchapichaji wa vitabu vya fasihi kwenye gazeti la Taifa Leo.
  Andika barua ya kuomba nafasi hii nauambatanishe wasifu kazi wako kwa maelezo zaildi. (alama 20)
  1. Muundo wa barua rasmi - yenye anwani 2
   1. Ina anwani ya kwanza: - Mwandishi –mtahiniwa abunianwaniyake – Iwewima. (alama 1)
   2. Tarehe – Chini ya anwuani ya kwanza (alama ½)
   3. Anwani ya pili Mwandikiwa – mkurugenzi washirika la uchapishaji (alama 1)
   4. Mtajo /mada – KUH/MINT/YAH:KUOMBA KAZI YA UHARIRI (alama 2)
   5. Mwili wa barua -
    1. utangulizi - Asili ya habari kuhusu nafasi ya kazi - tangazo
    2. Maelezo ya kibinafsi kwa kifupi
    3. Ufaafu wake kwa hiyo nafasi (alama 4)
    4. Maelekezo kwa wasifu kazi kwa maelezo zaidi.
   6. Hitimisho - Sahihi ya mwandishi, jina na cheo kama anacho. (alama 1)
  2. Wasifu kazi / Tawasifu kazi
   1. Haari za kibinbafsi
    • Jina
    • Jinsia
    • Umri/Tarehe ya kuzaliwa
    • Ndoa – ameolewa au la /Hadhi
    • Anwani – Barua pepe, Meme/webu nambari ya simu
    • Dini
    • Lugha uzijuazo
   2. Elimu – Orodha ya shule - Aanze kwa kiwango cha juu zaidi na kumaliza shule ya msingi
    Ataje hadhi na jina la taasisi, kipindi cha wakati, cheti alichohitimu. (alama 2)
   3. Tajriba - Ujuzi wa kikazo / maarifa. Ataje tajiri mbali yonayo katika utendaji kazi anayoitomba.. Ujuzi alionao uonyeshe shirika au kampuni alipofanya kazi. (alama 2)
   4. Ufanisi - Ataje na aeleze ufanisi wake. (alama 1)
   5. Uraibu - Ataje mambo abayo anapenda kufanya wakati wa ziada au anapokuwa hayumo kazini. K.M kusoma, kusaidia jamii n.k (alama 1)
   6. Wadhamini/ Warejelewa wawili au zaidi.
    Habari zifuatazo kuhusu wadhamini zitolewe.
    • Wawe wawili au watatu
    • Jina/majina
    • Vyeo/Taaluma / kazi
    • Anwani
    • Nambari ya simu
    • Kipepesi (alama 2)
 2. Utelekezaji wa mtoto wa kiume nchini ni janga kuu. Jadili

  Kuko sawa elekezi
  Kuwachwa kujikidhi pekee
  Kutopigiwa debe kama msichaa
  Kutwi kwa majukumu angali machanga
  Kutowajari wana mashirika ya ufadhili
  Vyama vya kupigania mvulana kutowajibika
  Kunyimwa nafasi ya masomo
  Kukosa mashirika ya utafiti kuhusu wavulana.

  Janga
  Anaacha masomo
  Anaingilia dawa za kulevya na anasa
  Anaunganana na vikundi vya ugaidi
  Wanakosa sahadhi ya mwanamume
  Kuchangia kuporomoka kwa misingi ya kifamilia
  Kukosa viongozi wa kesho.

  TANBIHI
  1. Lazima aonyeshe pande mbili asipoatuzwe nusu ya alama
  2. Kuwe nakichwa au mada
  3. Atimize maneno kati 350 – 400
  4. Kadiria hoja nyinginezo.
 3. Andika insha inayoafikiana na methali Boniani mbaya kiatu chake dawa.
  Maana
  Kiatu cha baiani ni kitu au kundi la watu ambalo limechukiwa au kudharauliwa.
  Dawa: Kitu husika huenda kikwa ndicho jibu au jawabu au suluhisho kwa tatizo Fulani maishan9 mwa mtu au katika jamii.
  Mtahiniwa anaweza kutumia methali nyingine zenye maana sawa kama;
  • Matango na matikiti ndio maponya jaa
  • Wembamba wa reli gari moshi hupita
  • Nyumba nzuri si mlango fungus uingie
   Utuzaji
   1. Pande zote za methali zishughulikiwe. Anayeshughulikia upande moja asipite alama C 08/20
   2. Anayekosa kulenga katika kisa chake amepotoka kimaudhui alama D 03/20
  • Andika insha itakayomalizia kwa maneno yafuatayo:
   ................................Hapo ndipo iliponibainikia kuwa nilikuwa nikiogelea bahariuni pekee kinyume na wenzangu wote. (alama 20)

Mwongozo

 1. Mtahiniwa ahitimishe insha yake kwa maneno aliyopewa
 2. Kisa chake kifungamane na mawazo ya kauli aliyopewa.
 3. Kisa kidhihirishe tukio ambalo halikufahamika na mhusika.
 4. Mtahiniwa atumie nafsi ya kwanz umoja
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - KCSE Prediction Papers 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest