Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - KCSE Prediction Papers 2022

Share via Whatsapp

Maagizo kwa watahiniwa

 • Jibu maswali yote kwa karatasi hii.


Maswali

 1. UFAHAMU: (Alama 15)
  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
            Mateso ya wanawakiwa ni swala la kijamii linalofaa kutazamwa  kwa darubini kali. Hata hivyo  wanaoathirika zaidi ni watoto ambao bado wako katika umri unaohitaji kulelewa na kupewa mahitaji ya msingi kama mavazi, elimu na mengine anuwai. Hali ya kuachwa na wazazi imekuwa ikizikumba jamii tangu enzi za mababu na kila itokeapo wanajamii huipokea kwa mitazamo  tofauti tofauti, hivyo kuwafanya wanawakiwa  kuathirika sana.
          Baadhi ya jamii zina Imani ya kijadi pamwe na mila zilizochakaa zinazozifanya kuamini kuwa baadhi ya vifo hutokana na laana. Wengine huchukulia kuwa mwendazake ameondolewa na ulozi. Imani kama hizi huifanya jamii kuwatia  watoto walioachwa katika mkumbo ule ule hivyo kuwaangalia kwa macho yasiyo ya kawaida. Hili husababisha dhana gande. Hali hii husababisha  kuwachukulia watoto kama wanaotoka katika kizazi kilicholaaniwa. Jamii basi hukosa kuwapa watoto hawa  stahiki yao. Hata wanapojitahidi kuiwania nafasi yao, waliowazunguka  huwavunja mioyo. Jitihada zao huishia kuwa si chochote kwa kuwa jamii inawatazama kama waliolaaniwa.
            Punde baada ya mzazi mmoja ama wote wawili waendapo wasikorudi, inatarajiwa kwamba aliyeachiwa mtoto, awe mzazi wake, mwanafamilia  au jirani awajibike na kumtunza mwanamkiwa. Kunao kadha wa kadha wanaowajibika--ninawavulia kofia. Hata hivyo wengi hutekeleza jukumu hili walilopewa na Muumba. Si ajabu basi kuona kuwa idadi ya watoto wanaozurura  mitaani inazidi kuongezeka kila uchao. Ukichunguza utakuta kuwa wengi wa watoto hawa ni waliopotelewa na wazazi wao. Inakera zaidi kugundua kuwa baadhi ya watoto hawa wana mzazi mmoja aliyemzaa na kumwachia mwenzake mzigo wa ulezi,aliyeachiwa  ana jukumu la kumpa mwanawe mahitaji ya msingi. Machoni pa Jalali kila anayepuuza wajibu huu ana hukumu yake siku ya kiama!
            Ni haki ya kila mtoto kupata elimu. Katika katiba ya Kenya, mathalan, elimu ya msingi, yaani kuanzia shule ya chekechea hadi kidato cha nne ni ya lazima. Tangu hapo hata hivyo  jamii zimekuwa zikiwanyima wanawakiwa wengi elimu. Kwamba kunao wachache  wanaowaelimisha baadhi ya wanawakiwa, ni kweli. Hata hivyo, wengi hukosa hata wa kuwapeleka  katika shule ya chekechea, hivyo kuishia kutojua hata kuandika majina yao. Mfikirie mtu katika karne ya 21 asiyejua kusoma wala kuandika! Nani ajuaye huenda huyo mwanamkiwa asiyepelekwa shuleni ndiye angalikuwa  profesa, daktari, mwalimu, rubani au msomi mtajika na mtaalamu wa uwanja  muhimu katika jamii!
            Kila mtoto ana haki ya kulelewa hadi kufikia utu uzima kabla ya kupewa majukumu mazito. Katika katiba ya Kenya, utu uzima, ulio umri wa kuanza kufanya kazi huanzia miaka 18. Wanaohakikisha  watoto hawa wametimiza utu uzima kabla ya kufanyishwa gange ngumu wanafaa pongezi. Hata hivyo wanawakiwa wamekuwa wakitumiwa na wengi kama punda wa huduma. Wanaaila wengine huwachukua wanawakiwa kwa machozi mengi wazazi wao waagapo  na kuapa kuwahifadhi  na kuwatunza wana wale wa ndugu zao, kumbe ni machozi ya simba  kumlilia swara! Hata kabla ya mwili wa mzazi mhusika kuliwa na viwavi, mateso kwa mtoto yule huanza, akawa ndiye afanyaye kazi zote ngumu. Utakuta watoto wao wamekaa kama sultan bin jerehe  huku mwanamkiwa yule akiwapikia, kuwafulia nguo, kudeki karibu hata awaoshe miili! Kazi kama zile za shokoa huwa za sulubu na aghalabu husindikizwa  kwa matusi yasiyoandikika.
            Baadhi ya waja walionyimwa huruma huwahadaa wanawakiwa na kuwapeleka ng’ambo  wakitumia vyambo, kuwa wakifika kule watapata kazi za kifahari. Maskini wale huishia kushikwa shokoa, wakawa watumwa katika nyumba za waajiri wao bila namna ya kujinasua. Wengine huishia kutumiwa  kama watumwa wa ‘kimapenzi’ katika madanguro, miili yao ikawa ya kuuziwa makahaba waroho wasiojali utu. Kujinasua kule huwa sawa na  kujitahidi kuokoa ukuni uliokwishageuka jivu, maadamu wanawakiwa  aghalabu hukosa watu wenye mioyo ya huruma ya kuwashughulikia. Wengi huitumia methali ‘ Mwana wa ndugu kirugu mjukuu mwanangwa’ kuwapuzilia mbali wanawakiwa ambao hukimbiliwa tu wabinafsi hawa wanapofaidika wenyewe.
  1. Ipe anwani hii mwafaka. (alama 1)
  2. Eleza dhana ya mwanamkiwa kwa mujibu wa kifungu. (alama 2)
  3. Eleza Imani za kijadi kuhusiana na wanawakiwa.(alama 2)
  4. Jadili masaibu yanayowakumba  wanawakiwa. (alama 4)
  5. Eleza haki mbili za kikatiba zilizokiukwa kuhusiana  na wanawakiwa. (alama 4)
  6. Eleza maana ya msamiati ufuatao kulingana na kifungu.    (Alama 2)
   1. inakera………………………………………………………………………………………….
   2. majukumu……………………………………………………………………………………….
 2. UFUPISHO(Alama 15)
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
  Kule kuukubali ukristo kulimaanisha kuuasi uafrika pamoja na utamaduni wake. Kulimaanisha pia kuikataa miko na matambiko ambayo yalikuwa yanatuunganisha; kulimaanisha kuyakubali maisha na tabia za aina fulani kutoka bara uropa. Wamisheni walikuwa wameshambulia maisha ya jamiii zetu na kushtumu mila na desturi za waafrika kama vile nyimbo na densi za kuvutia miungu mbali mbali; mambo ambayo yalitokana na misimamo yao kuhusu Imani kama hizi.
  Kwa sababu hii, nchini Kenya kwa mfano, huku Wafrika wakinyang’anywa mashamba na raslimali nyingine zilizotokana na jasho lao, wamisheni nao walinyang’anywa roho zao. Hivyo basi mwili na roho ya mwafrika ilikatwakatwa  kwa ahadi ya mazuri ya mbinguni uropa.
  Elimu haikuwa jawabu kwa nyoyo za Waafrika zilizokuwa na njaa kwani ilitukuza maadili ya kikristo ambayo yalikuwa yamedinda kushtumu kudhulumiwa kwa mwafrika- kimwili na kiakili.Elimu ya kwanza aliyopata mwafrika ilikuwa ya kumwezesha kuisoma Biblia ili aweze kutekeleza majukumu rahisi kama msaidizi wa wamisheni. Ndipo baadaye elimu ikaanza kuchukuliwa kama kigezo muhimu cha kujipatia kazi nzuri, kuwa na mali na hivyo kuishi maisha mazuri, ingawa katika mfumo wa maisha ya huko Uropa. Mwafrika aliyekuwa amesoma na mkristo alikuwa tayari amejitenga na asili na utamaduni wake. Uhasama kati ya wakenya na makanisa ya wamisheni; kuanzishwa kwa makanisa yenye misingi yake katika uafrika pamoja na masuala ya kidini ya vuguvugu la Mau Mau, yote yalikuwa mazao ya uhasama wa kitamaduni ulioasisiwa na haja ya wamisheni ya kumbadili mwafrika. Makanisa mbali mbali yaliyoanza yakiwa na uhusiano wa wamisheni na baadaye kujitenga yalijaribu kuanzisha mfumo wa maombi na elimu ambao ulikuwa sambamba  na uliohusiana na matamanio ya jamii ya kiafrika huku yakijumuisha baadhi ya tamaduni za kiafrika katika kuabudu na maisha ya kila siku.
  Siku hizi, kanisa nchini Kenya ni zao la wamisheni kutoka uropa. Wamisheni walikuwa sehemu ya mchakato wa historia yetu-yani majilio ya wakoloni , au kwa maneno mengine wamisheni, masetla na wazungu wengine walikuwa maajenti wa ukoloni. Imewahi kusemekana kuwa wanabiashara na masetla kutoka Ulaya walifuata miongozo iliyotolewa na wamisheni.
  Katika maeneo mengine barani Afrika, uongozi wa kisiasa uliasisiwa kutokana na ombi au shinikizo la wamisheni kutoka nchi ya wakoloni.
  1. Bila kupoteza maana, fupisha aya tatu za kwanza. (maneno 100-110)    (alama 10,  2 za utiririko)
   Matayarisho
   Nakala safi
  2. Dondoa mambo muhimu yanayojitokeza katika aya mbili  za mwisho.     (maneno 50-55) (alama 5,  1ya utiririko)
   Matayarisho
   Nakala safi.
 3. MATUMIZI YA LUGHA  (ALAMA 40)
  1.      
   1. Eleza maana ya sauti mwambatano. (alama 2)
   2. Ainisha kitamkwa /l/ kwa kuzingatia kigezo cha hali ya glota. (alama 1)
   3. Tofautisha  irabu katika neno ;  pindu (alama 2)
  2. Badilisha nomino ‘zawadi ‘ iwe kitenzi kwa kuitungia sentensi.(alama 1)
  3. Iandike sentensi ifuatayo kwa wingi.(alama 2)
   Jumba lili hili ulionalo lilijengwa mwaka wa  1930.
  4. Tumia kirejeshi ‘ji’ katika sentensi ili kutoa dhana zifuatazo; (alama 2)
   1. Mazoea
   2. Kirejeshi
  5. Onyesha muundo wa  (alama 2)
   1. Silabi ya kwanza katika neno: ng’ambo 
   2. Silabi ya pili katika neno: mchezo
  6. Ichoree vielelezo matawi sentensi
   Tuliwakataza lakini hawakutusikia (alama 4)
  7. Kuza sentensi ifuatayo kwa wingi.(alama 2)
   Mbwa mweusi amemuuma mtoto.
  8. Badilisha kitenzi kisaidizi kilicho kwenye sentensi ifuatayo kiwe kishirikishi.  (alama 1)
   Mvule alikuwa akilala  bwenini
  9. Jaza pengo kwa kivumishi mwafaka kutoka kwa kitenzi kilichopigiwa mstari. (alama 1)
   Mkimbizi yule ……………………………….aliyetoroka kwao amekamatwa.
  10. Tunga sentensi moja moja kuonyesha matumizi ya viambishi kama vielezi kuonyesha;  (alama 2)
   1. mahali
   2. wakati
  11. Andika upya sentensi zifuatazo kwa kufuata maagizo.                                                           
   1. Mchezaji huyu anachezea timu ya  Bandari.  (Anza kwa kiashiria kisisitizi) (alama 2)
   2. Paka alimla panya jana jioni. (kutendwa) (alama 2)
  12. Kanusha sentensi ifuatayo. (alama 2)
   Baba alikasirika akatuchapa na kutunyima chakula.
  13. Geuza sentensi ifuatayo iwe katika usemi halisi. (alama 3)
   Baba alisema kwamba wangejenga nyumba nyingine pale mwaka ambao ungefuata.
  14. Bainisha virai katika sentensi ; (alama 3)
   Ombogo alimtaka kulipa deni lote.
  15. Ni nini maana ya shamirisho kipozi? (alama 2)
  16. Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo ;   (alama 2)
   Wenyewe wanavipenda kwa dhati.
  17. Yapange majina yafuatayo katika ngeli zake. (alama 2)
   1. Sukari…………………………………………………………………………………………...
   2. Huzuni………………………………………………………………………………………….
 4. ISIMUJAMII (ALAMA 10)
  Fafanua sifa kumi za sajili ya shuleni.                                


  Mwongozo wa Kusahihishia.

 1.        
  1. Mwanamkiwa / Masaibu anayopitia mwanamkiwa. (alama 1/0)
  2. Mtoto aliyefiwa wazazi wake wote ; yatima.( alama 2/0)                                                     
  3. Vifo vya wazazi wao vilitokana na laana au ulozi(alama 2/0)
  4.        
   • Kunyimwa elimu
   • Kufanyishwa kazi ngumu  na wale wanaowalea
   • Kuhadaiwa na kupelekwa ng’ambo bila hiari
   • Kutumiwa kama watumwa wa kimapenzi katika madanguro ( zozote 4x1=4)
  5.      
   • Haki ya elimu
   • Kulelewa hadi kufikia utu uzima kabla ya kupewa majukumu mazito
   • Kutofanyishwa kazi za shokoa (alama 2x2=4)
  6.      
   1. Inaudhi/ inasinya
   2. wajibu
 2. UFUPISHO
  1.      
   • Kuukubali ukristo kulimaanisha kuasi uafrika pamoja na utamaduni wake.
   • Nchini Kenya, Waafrika walinyang’anywa mashamba na raslimali nyingine zilizotokana na jasho lao
   • Waamishenari waliwanyang’anya waafrika roho zao/  mwili na roho ya mwafrika ilikatwakatwa  kwa  ahadi ya mazuri ya kule uropa.
   • Elimu haikuwa jawabu la njaa
   • Elimu ilitukuza maadili ya kikristo yaliyodinda kushtumu kudhulumiwa kwa mwaafrika
   • Elimu ya kwanza ilimwezesha mwaafrika kuisoma Biblia ili aweze kuwa msaidizi wa Wamisheni
   • Baadaye elimu ikaanza kuchukuliwa kama kigezo cha kujipatia kazi nzuri, kuwa na mali na maisha mazuri kwa mfumo wa uropa.
   • Makanisa mengine yaliyojumuisha tamaduni za kiafrika yalianzishwa na kusababisha uhasama kati yao na Wamishenari.
    Hoja 8x1= 8
  2.      
   • Kanisa nchini Kenya ni zao la Wamisheni kutoka Uropa 
   • Wamisheni, masetla na wazungu wengine walikuwa maajenti wa ukoloni
   • Wanabiashara na masetla kutoka ulaya walifuata miongozo iliyotolewa na wamisheni
   • Katika maeneo mengine Afrika, uongozi wa kisiasa uliasisiwa kutokana na ombi au shinikizo la  wamisheni kutoka nchi ya wakoloni 
    Hoja 4x1=4
 3. MATUMIZI YA LUGHA.
  1.    
   1.    
    • Sauti mbili au Zaidi zinazotamkwa kama sauti moja. K.m /tw/                  (alama 2/0)
    • sauti ambayo huundwa kwa konsonanti mbili au tatu zinazotamkwa kama sauti moja. Km /ndw/  
   2. sauti sighuna      alama 1/0)
   3. /i/ ni irabu inapotamkwa mdomo hutandazika
    Hutamkiwa sehemu ya mbele kinywani
    /u/ hutamkwa mdomo ukiwa umeviringika
    Hutamkiwa sehemu ya nyuma kinywani     (alama 2x1=2)
  2. Alizawidiwa  juzi.    Asiandike zawadiwa.           (alama 1/0)
  3. Majumba yaya haya myaonayo yalijengwa mwaka wa 1930    (alama 2/0)
  4.      
   1. Mchoraji yule ni hodari   (alama 1x1=1)
    Uchoraji/ uchezaji
   2. Wamejifurahisha   (alam 1x1=1)
  5. ng’a---- KI
   che----KI
  6.        
  7. Majibwa  meusi yameyauma matoto
  8. Mvule alikuwa bwenini.
  9. Mkimbizi yule mtoro aliyetoroka kwao amekamatwa.
  10.        
   1. Ameenda sokoni
    Alitualika alikohamia/ alipohamia/ alimohamia
   2. Tutasherehekea tutakapopata matokeo mazuri
    Alalapo hukoroma
  11. Yuyu huyu/ Yuyo huyo anachezea timu ya bandari
   Panya aliliwa nap aka jana jioni
  12. Baba hakukasirika, akatuchapa wala kutunyima chakula
   Baba hakukasirika, hakutuchapa na kutunyima chakula
   Baba hakukasirika na hakutuchapa wala kutunyima chakula
   Baba hakukasirika wala kutuchapa na kutunyima chakula
  13. Baba alisema, ‘Tutajenga nyumba nyingine hapa mwaka ujao.’
  14. Ombogo-  KN
   alimtaka kulipa-KT
   deni lote  KV
  15. Mtendwa au kitendwa katika sentensi
   Nomino inayopokea thari za kitenzi kwa njia ya moja kwa moja
  16. Wenyewe –Kiima
   kwa dhati---chagizo
  17. sukari  I-I,   I-ZI
   Huzuni   I-I
 4. ISIMUJAMII
  1. Lugha rasmi kv Kiingereza au Kiswahili hutumika.
  2. Lugha sanifu kv Kiingereza au Kiswahili hutumika
  3. Kuhamisha msimbo- Kiingereza na Kiswahili
  4. Kuchanganya msimbo-kiingereza na Kiswahili 
  5. utohozi  k.m picha
  6. msamiati wa kimasomo. Km mitihani
  7. Lugha nyenyekevu/ upole/ adabu-  mwanafunzi kwa mwalimu
  8. Lugha amrishi/ agizi/ kali
  9. Lugha shawishi
  10. Maswali na majibu
  11. Sentensi ndefu ndefu
  12. Kauli zisizokamilika/ Kukatizana kauli
  13. Lugha ya kimafumbo/ tamathali za usemi
  14. Lugha nyepesi/ rahisi kueleweka
  15. lugha chapwa/ legevu
  16. Lugha changamfu
  17. Lugha himizi/ matumaini
  18. Takriri/ uradidi
  19. Viziada lugha/ ishara
   zozote    10x1=10
   Afafanue hoja au atolee mfano ndipon atuzwe  alama 1.
   Adhabu-   

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - KCSE Prediction Papers 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest