KISWAHILI PAPER 1 - KCSE 2019 MARANDA MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp

Swali la kwanza ni la lazima

 1. Wewe ni mtaalamu wa masuala ya haki za watoto. Andika mahojiano baina ya kona mwanahabari kuhusu kutekelezwa kwa motto wakiume katika jamii
 2. Jadili nafasi ya ushauri na sala katika shule za Upili ili kudumisha nidhani
 3. Andika kisa kitakacho dhirihisha maana ya methali hii. Mwenye kovu usidhani kapoa
 4. Tunga kisa kinacho anza na maneno yafuatayo.
  Nilijaribu kuuinua mguu wangu uliojaa maumivu kutokana na jeraha.


MARKING SCHEME

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA KARATASI YA KWANZA PP1

 1. Haya ni mahojiano Mwanafunzi azingatie mtindo wa tamthilia kama vile:
  • Mwanafunzi :
  • Mwanahabari :
  • Azingatiemada
  • Jinsi mtoto wakiume alivyotekelezwa (kunyimwa nafasi za kazi, kutoshughulikiwa ipasavyo nyumbani, kutoshauriwa vyema, kukosa wa kuiga)
  • Hitimisho
   - Aeleza hatua ambazo zinastahili kuchukuliwa na jamii        
   - Wazazi
  • Wanahabari
 1. Swali la kujadili
  Kuwe na kichwa
  Kuonyesha umuhimu wa ushauri na saha shuleni
  Kuwaelekeza wanafunzi
 1. Mwenye kovu usidhani kapoa
  Maana ya methali hii ni kuwa mtu aliye na kidondo kilicho poa usimfikirie kuwa amepona kabisa. Methali hii huambiwa mtu anayemwamini sana Fulani aliyekuwa mbaya hapo awali.
  Mwanafunzi atoe kisa kinacho anana maneno au Mwanafunzi aandike kisa kuhusu mhusika mbaya ambaye haaminiki kwa maana watu hukumbuka huyo ubaya wake na mara nyingi hufikiriwa kuwa yungali mbaya. Pia mwanafunzi anaweza kutunga kisa kuhusu mtu aliyekumbana na hali ngumu maishani iliyosahaulika na wengine lakini kwake inaendelea kumwathiri.
 1. Kisa kionyeshe alivyopata jeraha (atumie mbinu rejeshi) na akiendeleze kisa bila kuongeza maneno kwenye kianzio au kuongeza maneno.
  VIWANGO MBALIMBALI
  D- (D YA CHINI) MAKI 1-2
  • Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile
  • Kujitungia swali tofauti na kulijibu
  • Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya ndimi
  • Kunakili swali au maswali na kuyakariri
  • Kunakili swali au kichwa tu

   D WASTANI MAKI 4-­5
  • Mtiririko wa mawazo haupo
  • Mtahini wa amepotoka kimaudhui
  • Matumizi ya lugha ni hafifu mno
  • Kuna makosa mengi ya kila aina

   D+ (D YA JUU) MAKI 4-5
  • Insha huwa na makosa mengi ya kila aina, Lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha
  • Hoja hazikuelezwa kikamilifu/mada haikukazwa vilivyo
  • Mtahiniwa hana uhakkika wa matumizi ya lugha
  • Mtahiniwa hujirudia rudia
  • Insha itakayo zingatia sura lakini ikose maudhui ikaridiwe hapa
  • Insha ya urefu wa robo yaani, isiyozidi maneno 174 isipite kiwango hiki.

   C- (C YA CHINI) MAKI 6-7
  • Mtahiniwa anashida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake
  • Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo
  • mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, yahijai na ya msamiati na insha haieleweki kwa urahisi

   C WASTANI MAKI 8
  • Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafiru
  • Dhana tofauti hazijitokezi kwa wazi mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha
  • Mtiririrko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa
  • Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu
  • Ana shida ya uakifishaji
  • Anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati lakini bado insha inaeleweka

   C+ (C YA JUU) MAKI 9-10
  • Ana wasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini bado insha inaeleweka
  • Dhana tofauti zimejitokeza japo kwa njia hafifu
  • Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa
  • Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu
  • Ana shida ya uafikishaji
  • Kuna makosa ya sarufi ya msamiati na hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo
  • Insha ya kiwango cha nusu yaani maneno 175-274 isizidi kiwango hiki

   B- (B YA CHINI) MAKI 11-12
  • Ana wasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofauti akizingatia mada
  • Ana mtiririko mzuri wa mawazo
  • Anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia
  • Makosa yana dhihirika/ nikiasi

   B (B YA CHINI) MAKI 13
  • Anathirihisha hali ya kuimudu lugha
  • Mawazo yake yanthihirika akizigatia mada
  • Ana teuana kutumia mifano michahe ya misamiati mwafaka
  • Sanja yake ni mzuri
  • makosa ni machache

   B+ (B YA JUU) MAKI 14-15
  • Mawazo yake yanadhiririka na anajieleza waziwazi
  • anawasilisha ujumbe kwa njia inayovutiana kwa urahisi akizingatia mada
  • Ana mchanganyiko mzuri wa misamiati unaovutia
  • sarufi yake ni nzuri
  • Uakifishaji wake wa sentensi ni mzuri
  • makosa ni machache ya hapa na pale
  • Insha ya urefu wa robo tatu, yaani maneno 274-374, isipite kiwango hiki.

   A- (A YA CHINI) MAKI 16-17
  • Anadhirihisha ukomavu wa lugha
  • Mawazo yake yana dhihirika na anaishughulikia mada
  • Ana mtiririko mzuri wa mawazo
  • Msamiati wake ni mzuri na unavutia
  • Sarufi yake ni nzuri
  • Makosa ni machache yasikusudiwa

   A WASTANI MAKI 18
  • Anawasilisha ujumbe vizuri kulingana na mada
  • Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato
  • Anatoa hoja zilizokomaa
  • Anatumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia zaidi
  • Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi
  • Makosa ni nadra kupatikana

   A+ (A YA JUU) 19-20
  • Mawazo yanadhirihika zaidi na mada imeshughuliwa vilivyo
  • Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato
  • Hoja zake zimekomaa na zina shawishi 
  • Msamiati wake ni wa hali ya juu na unavutia zaidi
  • Sarufi yake ni nzuri zaidi
  • Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi, kiufundi
  • Makosa yote kwa jumla hayazidi matano

   ALAMA ZA KUSAHIHISHA
  • Hupigwa chini ya sehemu ambapo kosa la sarufi limetokea kwa mara ya kwanza tu
  • Hupigwa chini ya sehemu au neon ambapo kosa la hijai limetokeza kwa mara ya kwanza tu
  • Hutumiwa kuonyesha hoja inapokamilika pambazo ni kushoto
  • Hutumiwa kuonyesha kuacha kwa neon/maneno
  • Hutumiwa kuonyesha msamiati bora. Alama hii huitwa juu ya neon lenyewe
  • Hutumiwa kuonyesha msamiati usiofaa. Alama hutiwa juu ya neno lenyewe. Kila ukurasa uwe na alama ya chini katikati ili kudhibitisha kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo
  • Baada ya kutoa tuzo, lazima mtahinia andike udhaifu wa mtahiniwa

   Mfano wa kutuza:
   Robotatu
   C 08/20
   Udhaifu
   Urefu
   Maudhui
   Hijai
   Sarufi

Download KISWAHILI PAPER 1 - KCSE 2019 MARANDA MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest