KISWAHILI PAPER 1 - 2019 LAINAKU JOINT MOCK EVALUATION EXAMINATION

Share via Whatsapp
Download PDF for future reference Get on Whatsapp for 50/-

INSHA

Maagizo

 1. Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni yalazima
 2. Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia
 3. Kila insha isipungue maneno 400
 4. Kila insha ina alama 20
 5. Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili
 1. Lazima
  Andaa mahojiano kati ya mtangazaji katika idhaa ya Redio Miale na mtaalamu wa
  Ushauri nasaha kuhusu vyanzo vya kuporomoka kwa maadili miongoni mwa vijana.
 1. Tamasha za muziki, michezo na shughuli nyinginezo nje ya darasa huwapotezea wanafunzi wakati adimu wa masomo na zafaa kupigwa marufuku. Jadili.
 1. Samaki mkunje angali mbichi
 1. Andika insha itakayo chukua mwanzo ufuatao.
  Ukumbi wa mahakama ulikuwa umejaa watu furifuri. Mshtakiwa alikuwa ameinamisha uso wake. Hatima ya kesi iliyomkabili ilifahamika tu na hakimu. Punde…

MARKING SCHEME

 1. Ni insha ya mahojiano
  Vipengele vya kimuundo vizingatiwe;
  1. Anwani/kichwa cha kipekee- kidhihirishe yafuatayo:
   • Mahojiano kati ya….
   • Mhoji na mhojiwa
   • Suala linalojadiliwa
  2. Mtindo wa tamthilia au majibizano uzingatiwe
  3. Mtahiniwa atumie lugha hai kuandika insha yake- yaani taswira ya mhoji na mhojiwa ibainike.
  4. Utungo wake ubainishe sehemu zifuatazo:
   1. Utangulizi
    Maamkizi na makaribisho
   2. Mwili
    Tanbihi: kilahojaayayake.
   3. Hitimisho
    Shukrani kwa mhojiwa/mhoji kwa kumwalika mhojiwa katika stesheni ya habari.
    Kuagana.

    Baadhi ya hoja
    1. Shinikizo kutoka kwa wenzao
    2. Wafanyabiashara laghai wanaoshiriki uuzaji wa dawa za kulevya
    3. Matumizi ya vileo
    4. Malezi yasiyofaa/wazazi kutelekeza wajibu wao
    5. Kukosa vielelezo
    6. Athari za teknolojia ya kisasa
    7. Kuvunjika kwa asasi za kuendeleza maadili
    8. Tamaa ya anasa na starehe
    9. Hamu ya utambuzi

     Tuza hoja zozote nyingine zenye kuafiki swali.
 1. Ni inshayamjadala
  Kuunga
  1. Huchukua muda mwingi wa mazoezi na maandalizi
  2. Wanapoambukizwa tabia hii, wanajipata wakifukuzwa kutoka shuleni.
  3. Suala hili huathiri pakubwa ratiba ya masomo ya wanafunzi wengine wasioshiriki katika shughuli hii kutokana na kelele na sauti za waliokuja kushindana.

   Kupinga
   1. Hutoa burudani/ kuwaburudisha wanafunzi.
   2. Ni njia ya kuwatuza wanafunzi kwa vyeti na aina nyinginezo za zawadi.
    Tanbihi:         Tuza hoja nyinginezo mwafaka.
 1. Utungo wake ulenge kuonyesha umuhimu wa kumrekebisha / kumpa malezi mazuri mwana kutoka utotoni.
 2. Ni insha ya mdokezo
  Kazi ya mtahiniwa ianze kwa maneno aliyopewa.
  Insha ya mwanafunzi yaweza kuchukua mikondo ifuatayo:
  • Jaji akate kesi na kumpa mshtakiwa kifungo cha miaka mingi korokoroni. Hali hii iwafadhaishe waliohudhuria mahakama.
  • Uamuzi wa jaji ukose kumpata mshukiwa na makosa, hivyo kumwacha huru. Walio katika ukumbi wa sherehekee kwa shangwe na nderemo.

Download KISWAHILI PAPER 1 - 2019 LAINAKU JOINT MOCK EVALUATION EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-

Join our whatsapp group for latest updates
Read 1403 times Last modified on Wednesday, 25 March 2020 07:17
Print PDF for future reference