Kiswahili Paper 3 Questions with No Answers - Maseno Mock Exams 2020/2021

Share via Whatsapp

Kenya Certificate of Secondary Education
102/3- KISWAHILI -Karatasi ya 3
(FASIHI)
Muda: Saa - 2 ½

Maagizo

 1. Jibu maswali manne pekee.
 2. Swali la kwanza ni la lazima.
 3. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani: Riwaya, Hadithi Fupi, Ushairi na Fasihi Simulizi..
 4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
 5. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
 6. Majibu yote sharti yaandikwe kwenye nafasi ulizoachiwa kwenye kijitabu hiki cha maswali.

SEHEMU A: TAMTHILIA

P. Kea: Kigogo

 1. Lazima
  “Ama ale hizo falsafa zake! Udongo haubishani na mfinyazi...Kigogo hachezewi; watafuta maangamizi!”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Bainisha mbinu nne za kimtindo kwenye dondoo hili. (alama 4)
  3. Huku ukitoa hoja kumi na mbili, thibitisha kuwa kumchezea kigogo ni kutafuta maangamizi. (alama 12)

SEHEMU B: RIWAYA

A. Matei: Chozi la Heri

Jibu swali 2 au 3

 1. “… kile ambacho raia wanahitaji ni mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi na sera zenyewe za uongozi. Na naona awamu hii,…wingu la mabadiliko limetanda.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (alama 6)
  3. Huku ukitoa hoja kumi, dhihirisha kuwa wingu la mabadiliko limetanda katika jamii ya Wahafidhina. (alama 10)
 2.  
  1. Wanawake katika riwaya ya Chozi la Heri ni vyombo vikuu vya ukiukaji wa haki za kibinadamu. Thibitisha. (alama 10)
  2. Huku ukitoa mifano kumi, onyesha namna mwandishi wa riwaya ya Chozi
   La Heri ametumia mbinu rejeshi kuendeleza maudhui. (alama 10)

SEHEMU C: HADITHI FUPI

Jibu swali 4 au 5

A. Chokocho na D. Kayanda (Wah): Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine

 1.  
  1. Salma Omar Hamad: Shibe Inatumaliza.
   “Ndugu yangu kula kunatumaliza.’’
   “Kunatumaliza au tunakumaliza?’’
   1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 5)
   2. Eleza namna “kula” kunaimaliza jamii ya hadithi hii . (alama 5)
  2. Ali Abdulla Ali: Ndoto Ya Mashaka
   “Nimechoka hata naradua kufa kuliko kuishi. Hadi lini mashaka haya ya kutengenezwa?”
   1. Fafanua umuhimu wa msemaji wa kauli hii katika kuendeleza hadithi hii. (alama 5)
   2. Fafanua kwa hoja tano mambo yanayopelekea msemaji kuradua kufa kuliko kuishi. (alama 5)
 2. Mohammed Khelef Ghassany : Mame Bakari
  “Aliendelea kububujikwa na machozi kila alipoyafikiri yaliyompata na yatakayompata miezi si mingi ijayo.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Fafanua mambo ambayo mrejelewa alifikiri yangempata miezi si mingi ijayo. (alama 6)
  3. Eleza namna maudhui ya elimu yanajitokeza katika hadithi zifuatazo
   1. Mwalimu Mstaafu (alama 5)
   2. Mtihani wa Maisha (alama 5)

SEHEMU D: USHAIRI

Jibu swali 6 au 7

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

  Jicho, tavumiliaje, kwa hayo uyaonayo?
  Kicho, utasubirije, maonevu yapitayo?
  Kwacho, lijalo nalije, nimechoka vumiliyo
  Naandika!

  Moyo, unao timbuko, maudhi tusikiayo
  Nayo, visa na mauko, wanyonge yawakutayo
  Kwayo, sina zuiliko, natoa niyahisiyo
  Naandika!

  Hawa, wanotulimiya, dhiki wavumiliayo
  Hawa, mamiya mamiya, na mali wazalishayo
  Hawa, ndo wanoumiya, na maafa wakutayo
  Naandika!

  Hawa, sioni wengine, kwao liko angamiyo
  Hawa, huwapa unene, watukufu wenye nayo
  Hawa, bado ni wavune, Kwa shida waikutayo
  Naandika!

  Bado, wawapo mabwana, wenye pupa na kamiyo
  Bado, tofauti sana, kwa pato na mengineyo
  Bado, tuling’owe shina, ulaji pia na choyo
  Naandika!
  1. Huku ukitoa hoja sita, eleza mambo ambayo yanamsukuma mshairi kuandika shairi hili. (alama 6)
  2. Eleza bahari zinazojitokeza katika shairi hili ukizingatia vigezo vifuatavyo; (alama 3)
   1. Idadi ya vipande katika mishororo
   2. Idadi ya mizani katika mishororo
   3. Mpangilio wa vina katika beti
  3. Changanua muundo wa shairi hili. (alama 4)
  4. Eleza toni katika shairi hili (alama 2)
  5. Fafanua kwa kutoa mifano mitatu mbinu ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. (alama 3)
  6. Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 2)
 2. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

  Jua la mashariki limezibwa
  Na mchweo ya magharibi
  Tukabaki kUhesabu siku
  Na kila sekunde inayopita
  Ikilifyatua shaka jipya
  Ambalo bado kidogo
  Litakuwa limeliua tumaini
  Na sumu yake kulipuka hadharani
  Ulimwengu ushuhudie.

  Ni upeo wa sayansi:
  Waundapo silaha
  Mabomu ya masafa ya mbali
  Yanayomwaya yake mimweso
  Na kutudonoa
  Kama yule jogoo
  Wa radi.

  Ni upeo wa uhayawani:
  Tuundapo silaha
  Mabomu ya masafa ya karibu
  Au zana za kukingia wao jogoo
  Asitudonoe na kututia mautuni
  Katika yetu ardhi
  Walipoishi na kuzikwa wetu wahenga.

  Ni udikteta sisi kuongozana bibaya
  Ni udikteta viongozi kuwauwa wapinzani
  Ni unyama watu kupigwa watu risasi
  Ni unyama wananchi kuteswa
        Lakini
  Ni demokrasia wao kutuvamia
  Na yetu ardhi kukalia
  Ni demokrasia kuwaua viongozi wetu
  Pamoja na wananchi kwa yao makombora
  Yenye kiu ya damu yetu.

  Ni haki kutukatia mifereji ya maji
  Tukanyauka na kujifia kama vipando
  Katika majira magumu ya ukame?
  Ni utu kuwatesa watoto wetu
  Waliojisabilia kuipigania nchi katika ushinde
  Katika ardhi hii tulopawa
  Naye Mola Moliwa?

  Lakini fahamuni:
  Tofauti kati ya hadithi fupi na ndefu
  Ni kuwa ndefu huchukua mrefu wakati kuisha
  Na ile fupi huchukua muda mfupi
  Zote lakini zina miisho
  Na hii nayo ipo siku
  Ukingoni itafika
  Hatimaye watoto wetu wapate tena
  Jioni kuitamani
  Jioni isiyo na mimweso
  Mimweso ya kutishia wao uhai
  Na mingurumo na mirindimo
  Ya kutangaza yao maangamizo!

  Najua sitakuwepo hili kulishuhudia
  Lakini kwangu itakuwa si kitu
  Muhimu ni wajukuu wafahamishwe
  Kuwa hapa nilipita na kushuhudia
  Binadamu akiutekeleza unyama
  Alipoupindua juu chini, nje ndani
  Kama funzo la demokrasia
  Kwa ulimwengu kipofu!

  Maswali
  1. Huku ukitoa hoja sita, dhihirisha kuwa jamii ya nafsineni imekandamizwa. (alama 6)
  2. Toa mfano mmoja mmoja wa mitindo ifuatayo kwenye shairi. (alama 4)
   1. Usambamba
   2. Taswira
   3. Tashibihi
   4. tashihisi
  3. Toa mifano ya idhini zifuatazo za kishairi. (alama 2)
   1. Kuboronga sarufi
   2. Tabdila
  4. Tambua nafsineni katika shairi hili. (alama 1)
  5. Andika ubeti wa tano katika lugha tutumbi. (alama 4)
  6. Eleza toni ya mshairi katika shairi hili. (alama 1)
  7. Eleza matumaini ya mshairi katika shairi hili. (alama 2)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

 1.  
  1. Eleza maana ya miviga katika Fasihi Simulizi. (alama 2)
  2. Fafanua sifa tano za miviga. (alama 5)
  3. Wewe ni mwigizaji wa michezo ya jukwaani. Eleza mambo matano ambayo utazingatia ili kufanikisha uigizaji wako. (alama 5)
  4. Unanuia kutumia mbinu ya maandishi kukusanya na kuhifadhi habari kuhusu miviga ya tohara.
   1. Eleza manufaa ya kutumia mbinu hii. (alama 4)
   2. Eleza udhaifu wa kutumia mbinu hii. (alama 4)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions with No Answers - Maseno Mock Exams 2020/2021.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest