Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lanjet Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO KWA MTAHINIWA:

 • Karatasi hii ina maswali manne.
 • Jibu maswali mawili pekee. Kila swali lina alama ishirini.
 • Swali la kwanza ni la lazima.
 • Chagua swali lingine lolote moja kutoka yale matatu yaliyosalia.
 1. Wewe ni mwanahabari mtajika nchini. Umepata fursa ya kumhoji Waziri wa Afya kuhusu njia mbalimbali za kukabiliana na maradhi yasiyo na tiba. Andika mahojiano yenu.
 2. Eleza njia mbalimbali zinazofaa kuchukuliwa na serikali katika kukabiliana na migogoro ya kifamilia nchini.
 3. Andika insha inayoafiki methali: Asiyejua faida ya mwangaza aingie gizani.
 4. Tunga kisa kitakachoanza kwa maneno yafuatayo:
  Hospitali ilionekana kumetameta kwa wingi wa watu...


MARKING SCHEME

Swali la Kwanza

 1. Wanasayansi wana kazi kubwa kuendelea na uvumbuzi wao ili kupata tiba.
 2. Serikali inahitaji kutenga pesa kiasi kikubwa kusaidia wakati wa majanga kama Korona.
 3. Serikali kuhifadhi chakula kingi kuepusha wananchi dhidi ya magonjwa.
 4. Wananchi kuelimishwa jinsi ya kujikinga dhidi ya magonjwa haya.
 5. Binadamu wafaa kushirikiana ili kupigana na magonjwa haya (kifedha na kiteknolojia).
 6. Binadamu kufanya mazoezi ili kupigana na baadhi ya magonjwa haya.
 7. Wanadamu kutumia chakula chenye virutubishi mwafaka ili kupigana na magonjwa haya.
 8. Wanadamu kudumisha usafi.
 9. Wanadamu kufuata sheria za kukabiliana na magonjwa haya.
 10. Serikali kujenga vituo vingi vya afya ili kushughilikia janga lichipukapo.

Swali la pili

 1. Kuweka sheria madhubuti kulinda kila mtu katika familia.
 2. Kuweka adhabu kali kwa wavunjao sheria kuhusu familia.
 3. Wanadamu kuelimishwa kuhusu umuhimu wa kuhifadhi amani katika familia.
 4. Sera madhubuti za kulinda ndoa ziwekwe na serikali.
 5. Sera madhubuti za kulinda haki za watoto.
 6. Sera madhubuti ziwekwe kulinda ugavi mwafaka wa ardhi.
 7. Mashirika tofauti yaidhinishwe kushughulikia watoto, wanawake na wanaume.
 8. Sheria kali kuwekwa kwa wanaoharibu ndoa za watu wengine.
 9. Serikali kutowapa wafanyakazi uhamisho kiholela ili wanafamilia wawe na mshikamano mwema.
 10. Wanandoa wafanyao kazi sehemu mbalimbali kupewa nafasi na waajiri wao ili wapate kuonana.

Swali la Tatu

Mtahiniwa aelewe maana ya methali.

Kisa cha mtahiniwa kionyeshe mapuuza kuhusu jambo, kitu au mtu fulani. Baada ya mtu yule kuondoka, umuhimu wake uweze kutambulika.

Swali la Nne

Mtahiniwa atunge kisa cha kusisimua na sharti mwanzoni atumie maneno aliyopewa.


Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lanjet Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest