Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Pavement Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ina alama 20.
  • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  • Insha zote sharti ziandikwe katika kijitabu cha majibu ulichopewa.
  1. Lazima.
    Wewe ni mhariri wa gazeti la ‘Pevuka’. Andika tahariri kuhusu kiini cha mauaji katika ndoa na hatua za kukabiliana na janga hili.
  2. Janga la Korona limeathiri jamii kwa chanya na hasi. Jadili.
  3. Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
  4. Endeleza kisa hiki.
    “Nisamehe baba.Nilipotoshwa.Sitarudia kitendo kama hiki cha kufedhehesha tena. Sitakaidi tena makanyo yako. Nilijikuta nimepiga magoti mbele ya babangu


MARKING SCHEME

  1.  
    1. Kichwa :Jina la gazeti, tarehe na mada chini ya kichwa.
    2. Utangulizi :Ufafanuzi mfupi wa mada.
    3. Mwili :Maelezo kamili ya maudhui.
    4. Hitimisho :
      1. jina la kampuni inayomiliki gazeti.
      2. majina ya wahariri na vyeo vyao.
        Maudhui:
        Sababu za mauaji katika ndoa.

        1. Tamaa ya mali.
        2. Mfadhaiko wa moyo/msongo wa kimawazo.
        3. Matumizi ya dawa za kulevya.
        4. Ukosefu wa ushauri nasaha.
        5. Ukosefu wa uaminifu katika ndoa.
        6. Wanandoa kutelekeza majukumu ya kinyumba.
        7. Ubadhirifu.
        8. Dini/ushirikina/Imani potovu za kidini.
        9. Kutotimiza/kutoshughulikia mahitaji ya kimsingi ya familia kama lishe, makazi, karo na kadhalika.
        10. Taasubi ya kiume/kike/utamaduni.
          Suluhisho
          1. Ushauri nasaha.
          2. Kuelimisha jamii kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto katika ndoa.
          3. Kuimarisha demokrasia katika kitendo cha familia.
          4. Kuimarisha hali ya kiuchumi kwa wanandoa.
          5. Hatua kali za kisheria kwa wanaotekeleza unyama huu.
          6. Kukabiliana na dawa za kulevya.
          7. Viongozi wa kidini kuwajibikia majukumu ya kuelekeza wanajamii.
  2. Hili ni swali la mjadala.
    Mtahiniwa ataje hoja za kuunga na kupinga kuunga.
    Hasara/Athari hasi
    1. Shule zilifungwa ili kukabiliana na hali hii.
    2. Watu walifariki.
    3. Hoteli zilifungwa ili kukabiliana na ugonjwa huu.
    4. Usafiri uliathirika kwani baadhi ya maeneo yalipigwa marufuku.
    5. Watu walipoteza kazi kwani wengi wao ajira zao zilifungwa.
    6. Msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ulishuhudiwa.
    7. Mikutano ya hadhara ilipigwa marufuko.
    8. Uhuru wa kuabudu uliathirika kwani maabadi yalifungwa kwa muda.
    9. Amri ya kutotoka usiku ili kukabiliana na ugonjwa huu iliwekwa.
    10. Kalenda ya Elimu ilibadilika kwani wanafunzi walikaa sana nyumbani.
    11. Unyanyapaa ulishuhudiwa kwa kutengwa kwa wale waliokuwa na ugonjwa huo.
    12. Mwingiliano na uhusiano wa wanajamii uliathirika kwa amri ya kutosalimiana kwa mikono na kutokusanyika kila mara.
      Faida/mazuri

      1. Teknolijia iliweza kuimarika
      2. Watu walijifunza njia badala za kufanya kazi
      3. Wazazi na watoto walipata nafasi nzuri ya kutangamana na wengine
      4. Sekta ya Afya iliweza kuimarika kwani ilibidi hospitali zikarabatiwe na zingine kujengwa upya
      5. Juhudi za utafiti zilichacha ili kutafuta tiba/Chanjo
      6. Biashara kama vile kuuza barakoa zilichacha
      7. Usafi uliimarika hasa kwa ushauri wa kunawa mikono
      8. Mashirika ya kibinadamu yaliweza kuonyesha mchango wao kwa kuwasaidia wale walioathirika.
      9. Wanafunzi na walimu walipata nafasi ya kupumzika
      10. Talanta zilikuzwa kwani wengi walitumia muda wa kutofanya kazi kupalilia vipawa vyao.
        Tanbihi
        • Mtahini ahakika hoja za wanafunzi.
        • Mtahiniwa lazima aonyeshe pande zote mbili.
        • Atoe msimamo wake.
        • Akishughulikia upande mmoja atunzwe. (x/10)
  3.  
    1. Mtahiniwa alenge maana kuwa anayefanya jambo la kuumiza wengi huenda akaumiza mtu wao.
    2. Alenge kuonyesha si vyema kufanya jambo la kuumiza wengi.
    3. Aonyeshe pande mbili za methali.
    4. Akionyesha upande mmoja atunzwe. x/10.
    5. Akipotoka kimaudhui asitunzwe Zaidi ya 2/20.
  4.  
    1. Kisa kionyeshe kuwa alikuwa amekanywa akakaidi.
    2. Aonyeshe kuwa alipotoshwa.
    3. Asipotumia mbinu rejeshi amepotoka na asituzwe Zaidi ya alama tatu.
    4. Asipoonyesha kuwa alikuwa amekanywa amepotoshwa na sababu za kutokwa na damu amepungukiwa na asipishe alama kumi.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Pavement Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest