Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Eagle II Joint 2021 Mock Exams

Share via Whatsapp

MAAGIZO

 1. Jibu maswali mawili
 2. Swali la kwanza ni la lazima
 3. Kisha chagua swali jingine kutoka hayo matatu yaliyosalia
 4. Kila insha isipungue maneno 400
 5. Kila insha ina alama 20.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE

SWALI

JUMLA

TUZO

1

20

 

 

20

 

JUMLA

40

 MASWALI

 1. Andika tahariri kwa gazeti la kioo ukieleza njia za kukabiliana na joto la kisiasa ambalo limekuwa likipanda nchini.
 2. Sekta ya uchukuzi wa Bodaboda ni sarafu,ina pande mbili. Jadili.
 3. Tunga kisa kitakachodhihirisha ukweli wa methali ,Pwagu hupata pwaguzi.
 4. Andika insha itakayochukua mwanzo ufuatao.
  Ukumbi wa mahakama ulikuwa umejaa watu furifuri. Mshtakiwa alikuwa ameinamisha uso wake. Hatima ya kesi iliyomkabili ilifahamika tu na hakimu. Punde…


MWONGOZO WA KISWAHILI

 1. Insha hii ni ya tahariri
  Sura ya tahariri ijitokeze
  • Jina la gazeti
  • Siku na tarehe ya tahariri kutokea gazetini
  • Jina la mhariri
  • Mada
  • Mwili wa tahariri unaobeba maudhui
   MAUDHUI
  • Kuhamasisha umma kuhusu athari za uchochezi.
  • Kuripoti wanasiasa au watu wachochezi.
  • Kuipa nguvu tume ya uwiano na maridhiano. ( NCIC)
  • Wanasiasa wachochezi wazuiwe kuwania viti vya uongozi.
  • Ugavi sawa wa rasilimali
  • Kuipa nguvu ziadi ugatuzi/ magatuzi/ kuongezea rasisimali
  • Kuongeza maafisa wa kitengo cha upelelezi na jinai/ kuwafunza mbinu mpya za upelelezi.
 2.                            
  • Hasara
   • ajali nyingi barabarani.
   • Vijana wengi kuacha shule ili kuendesha Bodaboda.
   • Unatumiwa na wahalifu kutekeleza uhalifu.
   • Migogoro ya kifamilia ambampo vijana wengine hulazimisha wazazi kuuza shamba au kutumia mali ya familia kununua pikipiki.
   • Umezorotesha maadili,k,m wasichana wa shule kuhadaiwa na waendeshaji pikipiki
   • Umesababisha magonjwa kama vile ugonjwa wa pumu n.k
  • Faida
   • Umerahisisha usafiri.
   • Umeleta ajira
   • Umeongeza ukusanyaji wa ushuru nchini.
   • Umerahisisha biashara k.m kusafirisha bidhaa sokoni.
   • Umerahisisha shughuli za utawala na usalama.
 3. Maana
  • Pwagu – mwizi
  • Pwaguzi – mwizi mkubwa
  • Maana
   • mtu anayejiona ni mjanja kuliko wengine huweza akapata mtu mwingine aliye mjanja kumshinda.
   • Hutumika kwa watu wanaojiona bora zaidi kuliko wengine.
   • Mtahiniwa aandike kisa au visa kuthibitisha ukweli wa methali
   • Kisa au visa vionyeshe mtu mjanja kukutana na aliye mjanja zaidi
   • Mtahiniwa azungumzie pande zote mbili
   • Aweze kuanzia upande wowote
 4. Ni insha ya mdokezo
  Kazi ya mtahiniwa ianze kwa maneno aliyopewa.
  Insha ya mwanafunzi yaweza kuchukua mikondo ifuatayo:
  • Jaji akate kesi na kumpa mshtakiwa kifungo cha miaka mingi korokoroni. Hali hii iwafadhaishe waliohudhuria mahakama.
  • Uamuzi wa jaji ukose kumpata mshukiwa na makosa, hivyo kumwacha huru.Walio katika ukumbi washerehekee kwa shangwe na nderemo.
  • Baada ya uamuzi wa hakimu ,mtahiniwa atumie mbinu rejeshi kueleza kilichokuwa kimetendeka hapo awali hadi mshtakiwa akajipata kizimbani.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Eagle II Joint 2021 Mock Exams.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest