Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Bondo Mocks 2021 Exams

Share via Whatsapp

MASWALI

SEHEMU A: TAMTHILIA
Pauline Kea: Kigogo

 1. “Kubali pendekezo letu la kufungwa kwa soko… huoni hii ni fursa nzuri ya kulipiza kisasi? Najua umekuwa ukimmezea mate…’’
  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
  2. Bainisha vipengele  viwili vya kimtindo katika dondoo hili.(alama 4)
  3. Kufungwa kwa soko ni ukatili. Mbali na ukatili huu, toa mifano mingine ya ukatili kwenye tamthilia. (alama 6)
  4. Msemaji wa maneno haya ni mshauri mbaya. Thibitisha kauli hiyo  kwa kurejelea mifano yoyote sita  katika tamthilia ya Kigogo (alama 6)

SEHEMU B : RIWAYA
Assumpta K. Matei: Chozi la heri
Jibu swali la 2 au la 3

 1. “Je, mtu husahau sinema za kweli anazoona maishani? ”
  1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake (alama 4)
  2. Bainisha vipengele  viwili vya kimtindo katika dondoo hili. (alama 4)
  3. Kwa kutumia hoja kumi na  mbili, eleza namna  Wahafidhina mbalimbali walivyoona sinema za kweli maishani mwao.(alama 12)
 2.    
  1. Jadili umuhimu wa mandhari katika kuijenga riwaya hii kwa kurejelea Msitu wa mamba. (alama 10) 
  2. Fafanua maudhui ya ubaguzi wa kijinsia   ya kike kwa mujibu wa Chozi la Heri. (alama 10) 

SEHEMU C: HADITHI FUPI
A. Chokocho Na D. Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
Jibu swali la 4 au la 5

 1. “…………… Ningeondoka …. mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.”
  1. Eleza muktadha wa maneno haya (alama 4)
  2. Onyesha vile Kinaya kinavyojitokeza katika dondoo hili(alama 2)
  3. “Kinaya kimetumika kwingine katika hadithi husika. Thibitisha kwa kutumia hoja tisa  (alama 9)
  4. Eleza  umuhimu wa msemaji katika hadithi hii (alama 5)           
 2.      
  1. Eleza namna maudhui ya ndoa yalivyosawiriwa katika hadithi ya Masharti ya Kisasa. (alama 13)  
  2. Kwa kurejelea hadithi ya Shibe inatumaliza, eleza namna maudhui ya ufisadi yanavyojitokeza. (alama 7)

SEHEMU D: USHAIRI
Jibu swali la 6 au la 7

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. 
  Vijana wetu hawa tumaini wamepungua 
  Wamebaki kujinywea vidawa
  Na vinywa vyao havikosi
  Mioshi kufuka. 
  Wamebaki kujinamia suruale zikidondoka
  Kama kuku wa kidimu
  Utadhani ndio waliowazaa wazee  wao
  Wamebaki kuiba na nyinyi kuwacheka
  Wamebaki kuomba na nyinyi kuwacheka
  Wamebaki walipokuwa jana na na nyinyi mbele mwaenda.
  Mtakapofika ukingoni na pembeni kuitwa 
  Nahodha watakuwa hawakusalia
  Taifa litagonga ule mwamba mkubwa
  Akose kijana aliyejasirika kulikwamua!
  1. Lipe  shairi hili anwani  mwafaka (alama 2)
  2. Shairi hili lina ujumbe gani kwa hadhira (alama 2)
  3. Fafanua kwa kutolea mifano mbinu mbili zilizojitokeza kwenye utungo (alama 4)
  4. Tolea mifano matumizi mawili ya mishata (alama 2)
  5. Tambua nafsi neni na nafsi nenewa katika shairi (alama 2)
  6. Fafanua toni ya malenga (alama 2)
  7. Tasnifu ya malenga ni ipi  (alama  2)
  8. Eleza uhuru wa mshairi katika utungo (alama. 2)
  9. Toa maana ya vifungu kama vilivyotumiwa (alama. 2)
   1. Nahodha watakuwa hawakusalia 
   2. Taifa  litagonga mwamba mkubwa
 2. Soma shairi kisha ujibu maswali
  Lau kama ingakuwa, madhali tuna uhuru
  Watu kodi kutotowa, na kuifanya kufuru
  Vije nchi ingakuwa, taifa bila ndururu
  Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
  Hivi taifa kumea, na kuendelea mbele
  Kwamba hajitegemea, haliwatege’I wale
  Yataka kujitolea, ushuru bila kelele
  Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
  Wafanyikazi wa umma, mfano mwema walimu
  Wauguzi mahashuma, daktari wahadimu
  Bila hizi darahima, vipi wangalihudumu?
  Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru.
  Si vyema kuombamba, kwa wageni kila mara
  Huwa twajifunga kamba, na kujitia izara
  Adha zinapotukumba, kujitegemea bora
  Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru.
  Miradi ya maendeleo, yahitaji darahima
  Nd tufike upeo, ulio dunia nzima
  Wadogo na wenye vyeo, bila kodi tutakwama
  Taifa halingakuwa, bilashi ushuru.
  Ushuru si kwa wanyonge , wasokuwa na uwezo
  Watozwe hata wabunge, na wengine wenye nazo
  Yeyote asijitenge, kodi akalipa bezo
  Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
  Kwetu kutoa ushuru, ndiko kujitegemea
  Pasiwepo na udhuru, usio wa kulea
  Huwa ni kama kiguru, asenao kutembea
  Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
  1. Lipe shairi anwani mwafaka? (alama 1)
  2. Weka shairi hili katika bahari mbili tofauti.(alama 2)
  3. Eleza muundo wa ubeti wa tatu. (alama 3)
  4. Fafanua uhuru wa mshairi(alama 3)
  5. Andika ubeti wa sita katika lugha tutumbi. (alama 4)
  6. Taja nafsi nenewa katika shairi hili.  (alama 2)
  7. Tambua toni la shairi hili.(alama 1)
  8. Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano.(alama 2)
  9. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ilivyotumika katika shairi. (alama 2)
   1. Twajifunga kamba
   2. Bezo

SEHEMU E:FASIHI SIMULIZI

 1. Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.
  Asiyemjua mjua alionwe atamjua
  Namjuza kwa sifa zake alizokuwa nazo
  Alisimika ufalme uliosifiwa
  Akawa shujaa asiyetishwa
  1. Tambua kipera hiki (alama 1)
  2. Fafanua sifa tano za kipera hiki (alama 5)
  3. Tambua aina ya miviga katika jamii ya kisasa (alama 3)
  4. Fafanua njia za kuimarisha fasihi simulizi katika ulimwengu wa kisasa. (alama 5)
  5. Kwa kurejelea vigezo vitatu onyesha umuhimu wa fani katika kufanikisha usimulizi wa hadithi za fasihi simulizi. (alama 6)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.        
  1.        
   1. Maneno haya ni ya sauti ya mzee Kenga 
   2. mawazoni mwa Majoka. 
   3. Haya yanatendeka katika ofisi ya Mzee Majoka 
   4. wakati Husda na Ashua wanapigana.
   5. Majoka anakumbuka ushauri wa Kenga wa jinsi ya kumnasa Ashua kwa kusababisha fujo baina yake na Husda.
  2. Swali balagha – huoni ni fursa nzuri ya kulipiza kisasi?
   Nahau – kummezea mate; kumtamani
  3.        
   1. Kumwaga kemikali na taka sokoni licha ya kuwa wananchi wanakaa na kufanyia biashara zao katika soko. 
   2. Kuwatumia wahuni kunyamazisha wapinzani. Mzee Kenga anakutana na Wahuni chini ya mbuyu ambao baadaye wanamwumiza Tunu. 
   3. Kuruhusu dawa za kulevya na wanafunzi ambao wanakuwa makabeji
   4. Kuwaua wapinzani, kama vile vijana watano walioandamana
   5. Kuwatumia polisi kuwaua na kurushia waandamanaji risasi na vitoa machozi.
   6. Kuwanyima wafanyakazi haki, kama vile walimu na wauguzi wanaongezewa asilimia ndogo ya mshahara kasha kupandisha kodi.
   7. Utawala kuruhusu uuzaji wa pombe haramu kinyume na katiba, ambao umesababisha vifo na kufanya watu kuwa vipofu.
   8. Kufungulia biashara ya ukataji miti ilhai watu wanategemea miti hiyo kuboresha mazingira.
   9. Kufunga kituo cha runinga ya Mzalendo kwa kuonyesha mkutano wa Tunu na wapinzani wengine wa utawala.
   10. Utawala kutumia vyombo vya dola kuwafukuza watu wanaoenda sokoni na kuweka ulinzi mkali licha ya kuwa ulikuwa uwanja wa umma.
   11. Kuwarushia wakazi vijikaratasi vyenye ujumbe hasimu wakitakikana wapahame mahali ambapo wamekuwa wakiishi kwa muda wote wa uhai wao. 
  4.      
   1. Kenga anamshauri Majoka amwalike Ashua na Husda ili patashika itokee, naye Majoka apate jinsi atakavyolipiza kisasi kwa Sudi kwa kukataa kuchonga kinyago.
   2. Anamshauri Majoka atangaze kuwa maandamano ni haramu kisha anawamuru maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi dhidi ya umma unaondoa maandamano.
   3. Majoka anakataa Suala la polisi kutumia nguvu zaidi lakini Kenga anamwambia “Acha moyo wa huruma….. Siasa na hisia haziivi kwenye chungu kimoja ndugu yangu.
   4. Anakubali pendekezo la Majoka la kufunga Runinga ya Mzalendo kwa kupeperusha matangazo ya mkutano moja kwa moja.
   5. Kenga alihusika katika kupanga mauaji ya Jabali kwani Majoka anamsifu kwa kupanga hilo na hata wanapigishana Konzi
   6. Anaibua pendekezo la kumuua Chopi kwa kutofuata maagizo ya kumuua Tunu akisema, “Nafikiri Chopi lazima aende safari.”
   7. Anamwambia Majoka kuwa si kweli kwamba watu watampigia Tunu kura na kusema, “Tunu hawezi kupigiwa hata!”
   8. Anapendekea kukusanya kodi ya juu na kukataa kuitumia vyema na kwa njia halali k.v. kutoa taka.            
 2.        
  1.      
   1. Haya ni mawazo ya Umulkheri, 
   2. Akiwa darasani katika shule ya upili ya Tangamano
   3. Kila mara mwalimu Dhahabu alimkumbusha Umu arejeshe mawazo darasani.
   4. Hata hivyo ilimwia vigumu kusahau yaloyopita maishani mwake.   4x1
  2.      
   1. Taswira – sinema za kweli anazoona mtu
   2. Swali  balagha – je, mtu  husahau..?
  3. Mwanafunzi anatarajiwa kujadili namna wahusika walivyoleta aibu mbalimbali riwayani.
   1. Umu kuwapoteza wazazi wake na Sauna kuiba umbu wake. Hakuweza kuwatunza alivyoahidi.
   2. Masaibu ya Kairu, alivyosombwa na nduguze na wazazi hadi kambini, mamake pia kukosa samaki wa kuuza
   3. Mwanaheri na Lime/ Kaizari kutorokewa na mama yao Subira.
   4. Mabarobaro kuwabaka mabinti wa Kaizari na kuipaka mashizi familia hiyo
   5. Zohali kupata ujauzito na kufukuzwa shuleni.
   6. Mamake Chandachema kumtelekeza na kuishia kumwacha pweke ili kulelewa na bibi yake.
   7. Tenge kuwaleta wanawake wengine chumbani mbele ya watoto na Chandachema Bi, Kimai alipokuwa shambani.
   8. Neema na Mwangemi wanajitahidi kupata mtoto lakini hawafanikiwi na wanaishia kumpanga Mwaliko.
   9. Wafuasi wa Mwanzi kupinga ushindi wa Mwekevu mwishowe yeye ndiye anayechukua uongozi.
   10. Kaizari anajitahidi kuzuia wahuni wasiwabake binti zake lakini wanamzidi nguvu na kuwabaka.
   11. Lunga anajitahidi kumrithia na kumpendeza mkewe Naomi lakini hatimaye anamtoroka na kumwachia Watoto
   12. Annette kupuuza ushauri wa Kiriri asiende ughaibuni lakini anampuuza na kuhamia huko.
   13. Kiriri anawasihi wanawe warudi nyumbani lakini waliendelea kuishi ughaibuni hata baada ya kukamilisha masomo yao.
   14. Ndoa ya Pete inapingwana nyanyake.
   15. Mamake Kipanga kukataa kumwambia babake halisi baada ya aliyemdhania kuwa babake kumkana lakini mamake hakumwambia.
   16. Nyumba za mabwanyenye wa Tononoka zinabomolewa hata baada ya kutoa hongo ili zao zisibomolewe.
   17. Naomi alimtoroka Lunga kwa sababu ya umaskini lakini anaishia kuteseka zaidi na baadaye kufa
   18. Amize Lucia wanajizatiti kupinga ndoa yake.
   19. Wanaume kumtusi Mwekevu anapojitosa siasani ili kumvunja moyo lakini anavumilia mpaka anachaguliwa kuwa kiongozi wa Wahafidhina.
   20. Pete anakunywa dawa ya kuua panya ili afe lakini anapelekwa katika kituo cha afya cha Mwanzo Mpya na kuendelea kuishi.
   21. Pete anajaribu kuavya mimba ya mtoto wake wa pili na wa tatu. 
 3. Chozi la Heri
  1. Umuhimu wa msitu wa mamba- mambo tunapata kujua tu kupitia mandhari haya.
   1. Msitu wa Mamba ulikuwa na usawa wa watu – daktari maarufu Ridhaa,Kaizari, Selume na wengineo
   2. Dhiki ya kisaikolojia iliyowapata wakimbizi – Kaizari na aila yake na waliyoyapata, Subira kukatwana mabarobaro.
   3. Suala la ubakaji – Mwanaheri na Lime, 
   4. Njaa na kupigania vyakula – milolongo mirefu, Ridhaa kula mzizimwitu, aliyekuwa waziri wa fedha kung’ang’ania hasa uji.
   5. Ushindi wa Bi. Mwekevu – alivyostahimili vitisho na matusi kutoka kwa wanaume/ maelezo ya Bi. Shali
   6. Visima vya maji vilivyochimbwa na Mwekevu alipokuwa mkurugenzi.
   7. Wimbi la mabadiliko lilifika katika jamii. Mwekevu apewe nafasi ya kuongoza
   8. Taharuki ilitanda nchini. Vyombo vya dola vilitumwa kudumisha usalama.
   9. Misafara ya Wahafidhina waliohama kwao bila kujua waendako.
   10. Vita vya baada ya uchaguzi – mizoga ya watu, magofu ya majumba n.k
   11. Usimulizi wa tetei, namna wanaume walivyotumikishwa na kiongozi wa kiimla wa kike
   12. Ulawiti wa wanaume na hakuna anayewatetea 
   13. Uporaji wa mali, magari kuchomwa moto, nk – Hitman/ kijana muuaji 
   14. Unafiki katika upigaji kura kwa wasiojua kusoma- alama x kwa Kiboko ikiwa humtaki
   15. Ahadihewa walizopewa vijana – ubalozi, attache
   16. Matumizi ya misala  - sandarusi kisha misala kuchimbwa
   17. Misaada ya shirika la makazi bora - mzee Kaumu, Bw. Kute kupata mara tatu zaidi Indhari  - mambo tunayojua tu kupitia kwa msitu wa mamba 
  2. Jadili ubaguzi  wa kijinsia
   1. Jamaa za Kangata kupinga elimu ya mabinti zake
   2. Kimbaumbau kumdhulumu Naomi anapokataa kujihusisha kimapenzi naye.
   3. Mwimo Msubili kutotaka kukutana na mwanamke asubuhi kwa madai kuwa ni Mkosi.
   4. Lime na Mwanaheri kunajisiwa na vijana wahuni.
   5. Bwana Maya anamdhulumu mamake Sauna kwa mapigo na matusi aulizapo swali lolote lile.
   6. Kuuzwa kwa Pete kwa Fungo ili wazazi wake wapate pesa za kuwaelimisha ndugu zake watano wa kiume.
   7. Pete anabakwa na mlevi anapolewa chakari
   8. Mamake Zohari kuridhia kila asemalo mumewe na kushidwa kumtetea anapopata himila.
   9. Mamake Mwangeke aliwahi kumwonya kulia kama msichana. Hii ni ishara kuwa jamii yamwona mwanamke kama mnyonge.
   10. Mwanzi anakataa kukubali matokeo ya uchaguzi madhali anashindwa na mwanamke, Mwekevu.
   11. Wahafidhina kuamini kwamba mtoto wa kiume ndiye pekee anayestahili kuwa mrithi wa mali ya babake. 
   12. Ushindi wa Mwekevu unaonekana kama kutoheshimiwa kwa mwanaume.
   13. Mwekevu kusingiziwa wizi wa kura anapomshida Mwanzi.
   14. Kutishwa, kutusiwa na hata kutengwa kwa Mwekevu anapojitosa katika siasa zilizoaminiwa kuwa ni za wanaume
   15. Fungo anamharibia Pete maisha anapomwoa kisha kumfukuza anapojifungua mtoto.
   16. Mwanamke kuonekana kama mnyonge anayestahili kulia akabiliwapo na vizingiti au changamoto maishani. Mwanaume hafai kulia
    Kadiria hoja za mwanafunzi zozote
 4. Ndoto ya Mashaka
  1.         
   1. Maneno ya  Mashaka .
   2. Katika ndoto .
   3. Yumo chumbani mwake.
   4. Anaota kuhusu kurudi kwa ua lake baada ya kupotea kwa karne moja.
  2. Tambua na ueleze mbinu ya lugha iliyotumiwa katika dondoo.
   1. Tashihisi -  dunia kunikunjulia mikono kunifariji baada ya kunicharaza …
   2. Nahau – kunikunjulia mikono yaani , Baraka
   3. Taswira – kunicharaza fimbo
  3. Eleza jinsi dunia ilimcharaza fimbo msemaji kwakutolea hoja kumi na nne. (al.13x1)
   1. Mamake Mashaka kufariki punde tu baada ya kumkopoa.
   2. Babake pia anafariki punde tu baada ya mamake.
   3. Kuambulia mama mlezi maskini.
   4. Kuanza kufanya kazi za kijungu jiko kujikimu yeye na mama mlezi.
   5. Licha ya bidii yao mara kwa mara walikosa ikamlazimu Kidebe kutumia akiba yake.
   6. Kufiwa na mama mlezi.
   7. Kufungishwa ndoa ya mkeka na Mzee Rubeya.
   8. Kudharauliwa na wazazi wa Waridi kwa sababu ya umasikini wake.
   9. Kuishi katika mtaa duni.
   10. Chumba chake ni duni  - kinavuja paa inyeshapo.
   11. Alikosa samani  chumbani – hana meza,viti,kitanda wala godoro.
   12. Kazi ya usiku.
   13. M shahara duni .
   14. Kukopoa pacha mara tatu.
   15. Kulazimika kuomba nafasi ya malazi ya wana kwa jirani.
   16. Mazingira yenye harufu mbaya ya chooni.
   17. Mke na wana kumkimbia. Zozote 13x1
 5.      
  1.      
   1. Msemaji ni Bogoa Bakari
   2. Kwa kina Sebu, Kazu na wake zao
   3. Katika klabu ya Pogopogo.
   4. Bogoa  na Sebu rafiki yake wa zamani walipokutana baada ya miaka 40
  2. Usimulizi wa Bogoa unatujuvya mambo yafuatayo;
   1. Ulitima wa wazazi wa Bogoa – sabuni kuwa kitu cha anasa
   2. Uhaba wa maji kijijini mwao
   3. Ajira ya watoto – kuchoma maandazi na kuuza shuleni
   4. Kuuzw na wazazi wake kwa familia ya Bi. Sinai kule jijini
   5. Mapenzi ya dhati  kwa watoto wao – kukataa kwenda mjijini
   6. Kunyimwa nafasi ya kusoma kama mtoto. Alifunzwa na Sebu
   7. Kunyimwa nafasi ya kucheza na wenzake
   8. Ukiukaji wa haki ya kutibiwa. Alichomwa na mafuta ya maandazi
   9. Talanta ya usonara na uchezaji dansi.
  3. Shibe inatumaliza
   1. Mzee Mambo hafanyi kazi wizarani ilhali analipwa mshahara mkubwa kuliko Sasa na Mbura wanaofanya kazi wizarani
   2. Mambo anatumia runinga ya taifa inayofaa kuufahamisha umma masuala ya taifa lao kwa maslahi yake. Anaitumia kupeperusha sherehe inauofahamika nyumbani kwake.
   3. Mambo anaifilisi serikali kwa kutumia pesa za serikali kugharamia sherehe zake binafsi. DJ na wenzake wanalipwa mabilioni ya pesa za serikali kwa kusimamia sherehe hii.
   4. DJ anaipunja serikali kwa kutumia mtaji wa bohari kuu ya dawa za serikali kufungua duka lake la dawa.
   5. DJ anaifilisi serikali kwa kupokea huduma za maji, umeme na matibabu bure ilhali wananchi maskini wanazilipia.
   6. Wafanyakazi wa umma wanaibia serikali saa za kazi. Sasa na Mbura wanahudhuria sherehe zilizofanyika kwa Mambo siku nzima ilhali walipaswa kuwa kazini.
   7. Mzee Mambo anatumia magari ya serikali kwa maslahi yake binafsi. Kwa mfano, anayatumia kusomba maji, chakula, kuwaleta jamaa wa Mambo shereheni na mapambo. 
   8. Sasa na Mbura wanaofanya kazi wizarani zisizotambulika – mipango na mipangilio.
 6.      
  1.      
   1. Vijana
   2. Usasa   ataje na aeleze au anukuu mfano 01 
   3. Jinamizi la jamii Hakiki
  2. Vijana wanapotoka hasa kwa mihadarati na mitindo ya kisasa. 
   Vijana wamekengeuka na kuonyesha tabia  hasi k.v wizi n.k (1x2)
  3.      
   1. Taswira – uharibifu unaotazamiwa hasa katika aya ya mwisho k.v Mtakapofika ukingoni ….. taifa litagonga mwamba mkubwa., Pia ubeti / wanavyolewa, mioshi kufuka, nguo zadondoka. 
   2. Takriri – wamebaki n.k 
   3. Kinaya / kejeli – ubeti 2 (Vijana ndio nguvu za jamii lakini kwa mujibu wa shairi, hao ni mzigo.
    • Wamebaki kuomba na nyinyi kuwacheka 
    • Wamebaki walipokuwa jana na nyinyi mbele mwaenda 
    • Utadhani ndio waliowazaa wao. 
    • Nahau – Gonga mwamba  
     Hakiki – mbinu na mfano
  4. Mishata
   …. Kama kuku wa kidimu … na vileo vya mauti mtakapofika ukingoni na pembeni kuitwa…
  5. Nafsi neni – Mtu mzee / mhakiki wa mambo / msahuri/ mzazi anayetambua mabadiliko katika vijana / mkaguzi
   Nafsi nenewa  umma ndio wanaelezwa hatari
   Viongozi  waliomo vijana
  6. Toni – Ya kutamauka (ubeti wa mwisho)
   Kutahadharisha (1x2) Ataje na kueleza.
  7. Tasnifu – sawa na funzo.
   1. Kurekebisha mambo kabla yaharibike 
   2. Tusiposhughulikia tatizo la vijana, taifa litagonga mwamba mkubwa. (1x2)
  8. Kubananga sarufi
   …… tumaini wamepungua – wamepungua tumaini 
   Nahodha watakuwa hawakusalia – Hawatakuwa wamesalia Nahodha 
   Tabdila : Suruale – suruali (2x1)
  9.      
   1. Tutakosa kuwa na viongozi/ waelekezi/ watu wa kuigwa
   2. Taifa litaangamia 2x1
 7. USHAIRI
  1. Lipe shairi hili anwani mwafaka
   Taifa ni ushuru / ushuru      (1x1  =  1 )
  2. Weka shairi hili katika bahari mbili tofauti (al. 2) 
   Mathnawi – lina vipande viwili katika kila mshororo
   Ukaraguni – vina vya kati na vya mwisho vinatofautiana    ( 2 x 1 =  2 )
  3. Eleza muudno wa ubeti wa tatu (al. 3 )
   • Lina mishororo mine
   • Lina vipande viwili katika kila mshororo
   • Lina mizani kumi na sita katia kila mshororo
  4. Fafanua uhuru wa mshairi (al. 3)
   • utohozi – kodi
   • Inkisari – haliwatege’I, wasokuwa
   • Kuboranga sarufi – watu kodi kutotowa
  5. Andika ubeti wa sita katika lugha tutumbi (al. 4 )
  6. Mshairi anaeleza kuwa kutoa ushuru si kwa wanyonge wasiokuwa na uwezo ila kwa wabunge na wengine wenye uwezo ni vyema kila mtu ajihusishe katika kulipa kodi, ili taifa likuwa na liendelee kwani haliwezi pasipo ushuru
  7. Taja nafsi nenewa katika shairi hili (al. 2 )
   Wananchi
  8. Tambua toni la shairi hili (al 1 )
   Kuhimiza / kushauri
  9. Eleza ujumbe unaojitokeza inahitaji pesa
   • Miradi ya maendeleo inahitaji pesa
   • Wadogo na wenye vyeo washirikishwe katika utoaji kodi   
    (2 x  1  =  2)
  10. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ilivyotumika katika shairi
   • Twajifunga kamba – kujizatiti
   • Bezo – dharau
 8.      
  1. tambua kipera hiki
   tendi / tenzi
  2. fafanua sifa tano za kipera hiki
   1. huwa na masimulizi yanayotolewa kishairi
   2. hutoa wasifu wa shujaa
   3. huwa na matumizi ya chuku
   4. ni masimulizi refu
   5. husimulia matukio ya kihistoria
  3. Tambua aina ya miviga katika jamii ya kisasa (al 3 )
   1. Sherehe za mazishi
   2. Sherehe za harusi
   3. Kuapishwa / kutawazwa kwa kiongozi
  4.      
   1. Matumizi ya tamasha za muziki ya kitamadhuni katika shule, vyuo na mashirika mbalimbali – katika ngazi ya kitaifa na kimataifa
   2. Kushirikisha fasihi simulizi katika sherehe za harusi, jandoni, mazishi na matambiko katika jamii mbalimbali
   3. Kuimarisha na kusisitiza vipindi vya redio na runinga katika vituo vyetu stesheni zetu
   4. Kuimarisha michezo ya kuigiza, mashairi, na nyimbo kupitia redio, runinga na shughuli nyingi za kitaifa
   5. Kuimarisha utafiti wa Nyanja/vipera mbalimbali ya fasihi simulizi
   6. Kusisitiza tamasha za utamaduni zinazoendelezwa na kila jamii
   7. Uimarishaji wa ujenzi wa makabathi yatakayosaidia katika kuhifadhi na kuendeleza baadhi ya vitengo vya fasihi simulizi
   8. Kusisitiza matumizi ya lugha ya mama kwa vizazi vipya ili viweze kunghamua kwa urahisi thamani ya fasihi simulizi
   9. Kutilia maana uchongaji na uchoraji wa vinyango na sanamu cinazosisitiza utamaduni na destruri za jamii mbalimbali
   10. Matumizi ya vitabu, takilishi na kanda za video kuhifadhi baadhi ya vipera vya fasihi simulizi
  5. Kwa kurejelea vigezo vine, onyehsa umuhimu wa fani katika kufanikisha usimulizi wa hadithi za Fasihi simulizi (al. 8)
   1. Ploti – ni mfuatano wa matukio katika hadithi huwa na mwanzo unaotambulisha hadithi, mwili unatoa ujumbe / habari kuu na mwisho unaotoa utatuzi wa mgogoro uliopo
   2. Mandhari – ni masingira ya mahali, wakati na hali inayozunguka tukio – huwezesha utendaji / tukio / kisa
   3. Wahusika – viumbe vinavyotenda katika hadithi.  Huwasilisha vyumbe kwa hadhira
   4. Lugha – maneno yanayotumiwa na wahusika kuwasilisha ujumbe

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Bondo Mocks 2021 Exams.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest